katika ari ya mwaka mpya mambo mapya, nafufua mjadala wa uraia wa nchi mbili. nakaribisha maoni juu ya hili, ukizingatia kwamba bongo hakuna kitu kama hicho. kwa upande wangu mie naminya kwa sasa kwani sijaona hasara ya kubaki homu wala faida ya kuzamia...
aidha, wale mlioamua kuzamia, ukiacha faida ya mali, hali zenu zikoje tofauti na sie huku? hivi (semeni ukweli) mmekacha shida zilizopo nchini ama majumbani kwenu? wadau mliozamia huko tuwaiteje; wakimbizi wa kisiasa, kiuchumi, kimaisha? je huu usemi kwamba iwe mashariki ama magharibi, nyumbani ndo bora unawaingiaje vichwani?
Mungu ibariki tanzania na watu wake...
naomba kuwasilisha
Urai wa nchi mbili mheshimiwa michuzi kwa maoni yangu si mbaya kuwa nao. sio wote wamezamia au kukumbia nchi ni katika hali ya kutafuta maisha wapo ambao wameendelea kiasi fulani na wapo ambao wamechoka hata kurudi nyumbani wanaona sooooo.Wengine wamejifanya wakimbizi wakizania watapata neema huku lakini hamna kitu na sasa wanashindwa kurudi nyumbani kwani wametupa passport zao.Wengine wanasoma na njia rahisi ya kusoma kama huna kipato ni kuchukua uraia wa huku ughaibuni hivyo wengi wanatumia shotcut kwani fees ya shule baba kama sio raia nikiama tupu na system yao ya vikadi vya kuingilia darasani usipolipa mlango haufunguki kazi kweli kweli.kwamimi binafsi nyumbani kuzuri ukifanya kazi na kujituma sio kama ughaibuni.
ReplyDeleteNi kweli kabisa bwana Michuzi nakubaliana na wewe shida zipo popote duniani isipokuwa zinatofautiana kwa uzito. Na hata kama sisi tulio huku tukirudi huko sidhani kama ndugu Michuzi nikianzisha Kafoto point kama cha kwako hapo utafurahia sasa ili kukwepa taabu za aina hiyo ni bora sisi tulioko huku tubaki huku na if possible tuwe na uraia wa nchi mbili ili tusije banana hapo besides hata kama huku kuna shida lakini unaweza amka asubuhi kutafuta kibarua ukapata bila shida yoyote na hakuna mgao wa umeme wala maji sio kwamba naikandia nchi yangu lakini shida zake nyingi ni za kujitakia sasa kama naweza kuepuka japo kidogo kwanini nisizamie bwana Michuzi. Uraia wa nchi mbili sidhani kama ni tatizo hii inatuwezesha tusiukane uraia wa nchi yetu nzuri Tanzania ili tuweze kusaidia pale inapobidi sio kwa mali kwani hakuna nchi yenye mali kama Tanzania, hata mawazo tu. Kwa hiyo bwana Michuzi mimi naunga mkono kuwili
ReplyDeleteToa pumba hapa. Ungekua umeshawahi kuishi nje ya nchi ndio ungeelewa hili jambo. Kutembea nchi nyingi haina maana unaelewa system ya uhamiaji. Kwani kuishi nchi nyingine lazima mtu awe na jina? Hao wahindi ambao wanadual citizenship unawaitaje? Kama unataka kujadili hili kwanza do your home work na uelewe nini maana ya uhamiaji na nini maana ya dual citizenship. Waulize india na Nigeria nini wanachofaidika na raia wao kuwa na dual citizenship. Waulize kwa nini wasouth wanataka in 2010 kila African America anayetaka kuwa citizen wa nchi yao atakaribishwa. Nakuheshimu sana lakini hapa umechemsha. I hope utapost my comment otherwise utasoma na uelimike. Manake sometime unachemsha sana tu. Wewe unatumwa na kijiji nini?
ReplyDeleteKaka michuzi nakushukuru sana katika kutoa mada hiihapa katika hii kasi mpya ari mpya.
ReplyDeletePili kaka michuzi mimi ninakusupport kwa upande waliyoacha au kukimbia Tzwamekimbia hali ya maisha wala siyo siasa wala vita.
Maana huku Ughaibuni nilipo kuna elfu wa watu ni tz hapa,wakidaiwamekimbia vita na maisha ya shida Tanzania kwa kusingizia wametoka nchi ya UGANDA,RWANDA,BURUNDI,haswa wengi wanajitetea wametoka SOMALIA kwa kuwa kuna asilimia kumbwa na waislamu kwa kubadilisha majina.
Kama unavyosema kaka michuzi ni kweli kukaa home ni bora kuliko maisha wanayoishi kwa hawa watu wanaotaka uraia nchi mbili.
Kwa kweli wanaisha maisha ya dhiki sana na manyanyaso hali ya juu,jina etu yupo Ulaya hakuna mtu anaweza kumuona shunguli anazofanya hapo.
Wengi waliyopata hii furasa angalau wamepewa hizo passport nyekundu ukiwauliza umefanyia nini hii passport tangu umepata?hana jibu la kusoma unakuta mtuu anaisha kufanya kazi za kishenzi tuu wakati ana haki ya kusoma bure kama raia wa nchi aliyejilipulia kwa kudai ni mkimbizi lakini hakuna kitu wamebaki nina mkoba mwekundu bwana na tende na halua tuu.
Kwa maoni yangu ni afadhali niwe mtumwa katika nchi yangu Tanzania maana najua kama sikula jasho langu kwa kudhulumiwa basi wataifaidi watoto wangu au wajukuu wangu badala ya kuicha huku.
Maana piga ua,karagaza chini,Tupa koko beach liwa na mambo kuna siku tuu utarudi Tz kukuta uliyowaacha wamefika mbali na kushangaa.
Swali utarudi na nini?umefaidika nini?ulichokimbilia umekipata?
Sio watu wote walio nje wamekimbia. Watu wako nje kwa sababu mbali mbali. Inaweza kuwa ki-elimu, au kikazi, au vyote. Pia neno kuzamia lisitumike mahali ambapo si pake. Mtu aliyekwenda nje kwa kuomba na kupewa visa, si mzamiaji. Mtu anayekwenda nje kwa kudandia meli, na kupona kutupwa baharini, huyo ndio mzamiaji, kwa sababu hajaenda kihalali. Nyumbani ni nyumbani, hata kuwe vipi. Lakini kama viongozi, na serikali za huko nyumbani haziweki mazingira ya kuridhisha kwa watu kurudi kuishi, kwa nini wasibaki nje? Kama mtu akiwa nje anaweza kufanya kazi akalipwa zaidi ya Tsh.35 million kwa mwaka, wakati kwa kazi ile ile angelipwa laki 3, au 4 akiwa Tanzania, kwa nini arudi. Tena huyo anayelipwa Tsh.35 million kwa mwaka, kwa standard za U.S. sio mshahara mkubwa. Kwa sababu kuna watu hapa U.S. wanapokea mpaka Tsh.1 billion kwa mwaka. Kwa nini mtu arudi Tanzania wakati akituma zawadi kwa ndugu zake, pale EMS wanalipishwa tax zaidi ya thamani ya zawadi, mpaka watu wengine wanaacha zawadi zao zinaozea pale EMS. Mtu akileta vitu alivyokuwa akitumia nje, pale bandarini watoza kodi hawaamini price list iliyokuja na bill of lading, badala yake wanapiga hesabu zao wenyewe(basing on what?)alafu wakikupa hiyo figure ya tax, unatamani kukimbia. Kwa mtindo huo wa kukomoana(by TRA) na wengineo, hatutaendelea ng'o, na watu watazidi kubaki nje na kuja kusalimu tu, au kupiga simu basi. Kwa mawazo yangu binafsi, ni bora nitafute uraia huku niliko, kuliko kurudi Tanzania ambako nitaishia kugombana na watu wavivu wasiotaka kufanya kazi, lakini wa kwanza kupokea mshahara. Nitakuwa naenda Tanzania kusalimu tu, unless system yote imebadilika, na rushwa na ujambazi vimeisha.
ReplyDeletekaka michuzi naomba sana huu mjadala uufute na hata nisingependa kuusikia, maana that shows how much r not patriotic these days, yaani sitaki kusikia kitu kama dual citizenship, kama unataka kuwa mbongo halisi kuwa otherwise ukane uraia wa bongo lakini mchezo wa kuwa huku na huku hatutaki !! please delete this post michuzi
ReplyDeleteDunia ya leo ni dunia ya Utandawazi, siyo lazima Watanzania wote waliosoma waishi Tanzania ili waweze kutumia elimu yao na pia kujitafutia maisha mazuri wao na familia zao.
ReplyDeleteLeo tuna wasomi chungu nzima ambao wanasaga lami, je kuna kosa gani hawa kama watapata kazi nchi za nje ili kujiingizia riziki na pia kutumia elimu yao kwa faida yao na wale watakaowajiri?
Tanzania ni nchi ambayo miaka ya uongozi wa Hayati Baba wa Taifa (Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi-AMIN) ilisomesha wasomi wengi, lakini walikuwa hawatumiwi ipasavyo na wakati mwingine hawakupewa vitendea kazi ili kuongeza ufanisi wao. Ilikuwa si ajabu kukuta MATX na hii mpaka leo bado inatokea (mfano makaburu wa TANESCO) wakilipwa pesa chungu nzima pamoja na kuwa kisomo na uzoefu wao ni mdogo ukilinganisha na Wabongo. Hii inaashiria matatizo makubwa kwamba viongozi wetu bado wanadhani kwamba wazungu kutokana na ngozi yao ni watendaji wazuri hata kama kuna ushahidi tosha wa kuipinga dhana hiyo.
Wabongo wakaamua kujitafutia riziki katika nchi za nje, na walio wengi wanafanya vizuri sana.
Pamoja na kuwa wako nje wanafuatilia kwa karibu mambo yote yanayotokea nyumbani na wanasaidia kwa hali na mali kuinua viwango vya maisha vya ndugu, jamaa na marafiki. Na siku zote huiombea Tanzania mambo mema.
Muda si mrefu walio wngi wanaweza kutaka kuwekeza Tanzania, kwa maoni yangu sioni sababu ya kutoruhusiwa kuwekeza kama Watanzania. Wengine wanaweza kutaka kuja kuajiriwa Tanzania na kutumia uzoefu walioupata nchi za nje ili kuimarisha ufanisi wa huko watakakoajiriwa, pia hapa sioni sababu ya kutoajiriwa kama Watanzania.
Nchi nyingi za Afrika kama vile Ghana, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi n.k. zimeona faida kubwa ya kuruhusu wananchi wao kuwa na uraia wa nchi mbili. Ndio maana nchi zote hizo ama zimesharuhusu ama ziko mbioni kuruhusu uraia wa nchi mbili. Viongozi wetu hawafanyi kitu mpaka nao wawe wanafaidika kwa njia moja au nyingine. Hivyo kwa kuwa wawe wanaona hawafaidiki na hili la uraia wa nchi mbili wameamua kutolipa kipaumbele. Muda si mrefu watoto wao ambao wengi wao wanasoma nje wataanza kuchukua uraia wa huko waliko, hapo ndipo Viongozi wetu wataona umuhimu wa uraia wa nchi mbili, kwani nao watakuwa wanafaidikia kupitia kwa watoto wao.
China mapato yao ya fedha za kigeni asilimia kubwa inatokana na Wachina wanaoishi nje, hili pia linawezekana Tanzania na katika nchi nyingine za Kiafrika.
Inafurahisha kuona utaratibu uliowekwa sasa hivi na Viongozi wa awamu ya nne ya kukutana na Watanzania wanaoishi nje kila wanapokuwa nje ya nchi. Hili ni jambo zuri sana na lazima lidumishwe kwani linasaidia kuwaonyesha viongozi wetu kwamba Watanzania wanaoishi nje si majasusi wala wasaliti.
Tuachane na fikra za mwaka 47 kwamba Watanzania walio nje ni majasusi au wasaliti. Hawa wapo nje ili kutafuta ajira ambazo ni za shida Tanzania, kuongeza vipato vyao kwa faida yao wenyewe na familia zao na pia kusaidia Tanzania kwa njia moja au nyingine.
Mwisho kabisa katika hili la uraia wa nchi mbili si vibaya pia uongozi wa awamu ya nne kupata mawazo toka nchi nyingine nilizozitaja hapo juu ili kujua kulikoni mpaka nchi hizi zimeamua kuruhusu uraia wa nchi mbili ama ziko mbioni kufanya hivyo.
Michuzi ,
ReplyDeleteAcha kejeli za kitoto una maana gani unaposema watu wamezamia ? Unajua maana ya kuzamia wewe ? Kama unataka kupata maoni ya watu basi waulize kiustaarabu na sio kukebehi watu !
Napata shida Michuzi kukuelewa...una maana gani unaposema 'kuzamia'?Kwasababu hakuna mtu aliyekimbia nchi...kwenda nje ya nchi kusoma kwa sababu ya uhaba wa nafasi katika vyuo vikuu Tanzania,unakosea unaposema huko ni kuzamia.
ReplyDeleteUnapowaita watu ambao wanakuja nyumbani kutembea na kurudi kuishi walikochagua kuishi maisha yao ni kuwatukana unapowaita wamezamia...it's an abuse'incase kama hujui.Ningekushauri uwe makini unapochagua maneno ya kutumia unapoamua kuandika habari.Ethics of journalism ni pamoja kuheshimu wengine.
Elimu bora,mali,international exposure,kazi nzuri(more Tanzanians graduate from recognized universities nowdays),kuishi bila hofu ya vibaka wanaoingia baa na machine gun kukwapua chupi za watu,na mengine mengi tu Michuzi amabayo wadau wengine watakueleza.
Again,chagua maneno ya kutumia...hakuan ukimbizi unapokwenda kutafuta elimu.Ulipoondoka kijijini kwenu kuja Dar ama kwenda shule kokote ulipokwenda...umekuwa mkimbizi wa maisha ama elimu???
Kuna tofauti kubwa ya maisha ya Ulaya na bongo.Taja wewe tofauti hizo...si umekuja States?Kuna watu wanatengeneza hela nzuri kwa siku amabayo inaweza kuendesha Daily News.Kuna tofauti nyingi nyingi mno Bro.Hata hivyo kama ulivyosema nyumbani ni nyumbani bila kujali uko pembe gani ya dunia.Home is where u find true love.Bado hakuna hasara kurudi huko kufurahia dola na paunds licha ya ubabaishaji,unafiki na kila aina ya uozo wa viongozi wetu.Mungu Ibariki Tanzania,Mungu tubariki watanzania.
Hii dhana ya uraia wa nchi mbili (dual citizenship) ni tata sana, na inategemea unaegemea upande upi. Nafikiri kila upande una haki ya kupendekeza na kukata dhana ya hiyo kutokana mbalimbali nategemea baadhi ya wadau watachangia. Natumai baadhi ya wadau watatoa maoni na kupendekeza namna gani wanafikiria kuhusu dhana ya nchi mbili
ReplyDeleteNimeona lazima kusema machache kwenye hili suala manake ni muda umefika kuzungumzia waziwazi. Kuna wa-tz wengi walio nje wanaoipenda tz kuliko wa-tz walioko nchini. Wengi walio nje wana ujuzi wa aina nyingi wanaotaka kuuleta tz lakini wanashindwa kwa kuwa inabidi waache shughuli zao zenye faida kubwa nje ya nchi. Mataifa mengi makubwa yanaruhusu uraia zaidi ma mmoja (canada mfano). Watanzania walio nje wataweza kuwekeza bongo na kusaidia uchumi kama ilivyo kwenye nchi za wenzetu. Kama nilivyosema, walio nje wazalendo kama walio nchini.. kama sio zaidi
ReplyDeleteMICHUZI HUU NI MJADARA MZURI LABDANINGEANZA KWA KUONGEA UPANDE WANGU MIMI NINAYE ISHI KWA GEORGE. KWA KUWA NINA VIPANDE HALALI VYA KUISHI NA KUTOKA HUMU INCHINI. NINAVYO ONA MIMI NI KAMA WEWE ULIYE KULIA KIJIJINI NA MAISHA YAKO KUAMUA KUISHI NA KUJIJENGA HAPO DAR, NIKO HUKU LAKINI NIMEJENGA TZ NA NINAKUJA LIKIZO WAKATI NINAPOKUWA NA NAFASI, HAYA NI MAMBO YA GLOBALIZATION YOU DUMMY! KUNA WAZUNGU WAHINDI WARABU WENGI HUWAAMBII KITU KUHUSU BONGO HAWATAKI KURUDI KWAO, SASA DAMMY LIKE YOU CAN ARGUE THIS POINT. HAPA UGAIBUNI NI SEHEMU TU YA KAZI BUT WE ALL LOVE TZ AND WE PRAY FOR ALL OF YOU MSIKUMBWE NA UDITOPILE, WE LOVE YOU ALL SASA KWANI UKIWA NA URAIA WA NCHI MBILI KUNA UBAYA GANI? ONLY DUMMY PEOPLE WILL THINK LIKE YOU. ETI WAKIMBIZI!! ANYWAY IT IS JUST THE MATTER OF EDUCATION, THE STUFF YOU ARE POSTING TO THIS BLOG IS JUST SIMPLIFYING YOUR LEVEL OF EDUCATION AND UNDERSTANGING THAT IS IT! i LIKE YOU AS A PERSON BUT I GUESS YOU ARE SO DUMN IN BRAIN AND REASONING! SORRY UKWELI UNAUMA!!
ReplyDeleteMimi binafsi siafiki URAIA wa nchi 2.Na ninaamini kuwa kuna wa2 wengi tu haswa wenye asili ya bara ASIA wana uraia wa nchi 2 (India-Tanzania) au (Tanzania na UK) au (Canada na Tanzania) sasa ikiwa ndiyo halali c itakuwa balaa... kwanza wataajaa huku... Tembelea ktk hoteli mbali*2 utawakuta mpaka wafagiaji kutoka huko... Sitaki EA community sitaki Muungano wa TZ na Zanzibar na wala ctaki URAIA wa NCHI 2.
ReplyDeleteMtu mwenye uraia wa nchi zaidi ya moja hana tatizo sababu.Mfano India na Ethiopia utaratibu wao ni huu:Mtu anayeomba uraia wa nchi mbili
ReplyDelete1.Haruhusiwi kupiga kura wala kupigiwa kura au kugombea uongozi katika serikali au chama cha siasa
2.Hawezi kuwa mbunge au kiongozi wa kuteuliwa kuongoza serikali,bunge au mahakama.
3.Hawezi kuajiriwa serikalini
4.Hawezi ajiriwa jeshini
5.Hapewi hati za kusafiria ya nchi zote.Anapewa moja anakoomba uraia wa pili,au wa tatu hapewi passport.
Kwa hiyo sana sana ni kama mwekezaji mzawa anayechuma mataifa mengine na kuwekeza kwako.
Uraia wa nchi mbili muhimu watoto waliozaliwa na wazazi wa wenye uraia nchi tofauti wanapata shida sana.Mfano baba mmarekani mama mtanzania.Na unakuta kila mmoja hataki kuacha uraia wake.Sasa watoto unakuta wanahaha kwa baba wanakutaka na kwa mama wanakutaka.Wasaidieni jamani.
Pili kuna watu si kwamba wanapenda kuomba uraia nje lakini ukiomba ndipo unaweza pata kazi nzuri zaidi ambazo ni raia wa nchi hizo tu ndio waweza pewa vinginevyo ukiwa si raia huwezi pata.Lakini unakuta mtu moyo wake uko Tanzania na hataki kuacha uraia.Lakini ili achume kule analazimika aombe uraia nje ya nchi.Hawa wako wengi wafikiriwe pia.
Tatu ni kujenga uwezo wa nchi kiuchumi.Wahindi raia mfano wa nchi hii ni daraja la biashara za India kuingia Tanzania,Raia waarabu walioko humu nchini ni daraja la biashara kutoka uarabuni.Biashara toka uarabuni au uhindini zinafikia kwa waarabu na wahindi ndipo ziwaendee waswahili.Unapokuwa na Raia wako wenye uraia wako nchi ingine wale watu wanakuwa daraja la maslahi yako kibiashara,kiuchumi,kiusalama, kiulinzi n.k Hivyo uraia wa nchi mbili au zaidi ni muhimu sana.
Mwisho hata tujikaushe tujifanye hatutaki ukweli ni kwamba wenzetu waarabu na wahindi ni raia wa uhindini na uarabuni vilevile.Hata wakwambie sisi ni watanzania tu basi unajua ni uwongo wa mchana.wanafaidika na India/Uarabuni na Tanzania vilevile.Kwa nini mzawa tu (Ngozi nyeusi kama mkaa) abanwe wakati wengine wanafaidika huku na huku?
Naomba tujaribu. Tuache woga kama tutaiona sera hiyo haitufai tutaifuta mbeleni. Tuanze angalau na watu wachache tuone kama tunafaidika au la.Kama Raisi alivyosema katika hotuba zake Ukiogopa wasanii na vibaka au wajanja hutakuja kufanya lolote la maana.tujaribu tuone.
koloboi@yahoo.com
Michuzi
ReplyDeleteNakupongeza sana kwa uvumilivu mkubwa unaouonyesha kwamba licha ya baadhi ya watu kukusoa kwa lugha nzito na sometimes zenye kebehi,dharau na kutia hasira kwa namna fulani,bado umeendelea kuyaweka hewani maoni yao.
Unaonyesha ukomovu wa hali ya juu.Watu wengi hawapendi kukosolewa;na mioyo yao huumia sana sana wanapopewa 'laivu'.Hujisikia kama wamejeruhiwa na wakati mwingine hutamani ardhi ipasuke!
lakini pia kwa mara ya kwanza kabisa nakupongeza kwa kiswahili fasaha na mantashau ulichotumia kuwasilisha mjadala wako.Mara kadhaa nimekuwa najiuliza namna unavyoandika habari zako kama kweli umekwenda shule ya uandishi wa habari...ama pengine ni aina ya ya mwalimu aliyekufundisha.Well hongera kwa hili zuri ulilolifanya.Endelea kuanika hewani maoni ya watu without getting personal.
Iam watching brother.You are just a good guy.
Wanzania Wenzangu,
ReplyDeleteNamshukuru alianziasha majadala huu. Nafikiri suala hili tuliangalie kwa undani zaidi na tujifunze kutoka kwa mataifa mengine ni kwa nini yanaruhusu uraia wa nchi mbili na kwa nini baadhi ya mataifa hayaruhusu uraia wa nchi mbili.
Nafikiri tujiulize maswali wenyewe kabla hatujatoa maoni. Je kuwa na uraia wa nchi mbili utaleta manufaa gani kwa watanzania waishio nje ya nchi, waliopo nyumbani na kwa nchi yetu na je jamii yetu ya wanzania itanufaika au itapata hasara gani.
Mimi ninafikiri suala na kubaki nyumbani au kwenda nje ya nchi tulipe uhuru wa kila mtu kuamua.
Nyumbani ni nyumbani hakuna anayepinga! Maisha ya ughaibuni ni bora kuliko nyumbani, kama kuna anayepinga anyooshe kidole! Nyumbani hakuna amani, fullstop! Swali la kujiuliza ni je, wote walio nje wanaokumbuka kusaidia kuboresha maisha ya nyumbani walikotoka?
ReplyDeleteWaite wakimbizi wa kiuchumi, kisiasa, kimaisha, whatever lakini maisha yao ni bora mara 100 kuliko watu waliobakia huko nyumbani. Ni kweli kakimbia shida za TZ, sio siri! Muite mkimbizi ukitaka! Lakini jiulize aliyebaki hapo kafanya nini cha maana.? Asukume mkokoteni, akauze chips Kariakoo? au awe konda wa daladala?
Nchi imekuwa gizani miezi mingapi, rushwa, ujambazi, mishahara kiduchu, watu hawana amani! Wanafunzi masikini ya Mungu wanafaulu vizuri form six, lakini chuo kikuu hawawezi kujilipia, bodi ya mikopo inafanyakazi kisanii. Waende wapi hawa vijana kama sio kuzamia mamtoni. Wakati mwingine sio kwa kupenda, ila mfumo wa maisha, yakichangiwa na sera mbovu za serikali yetu,wanalazimika kukimbia nchi. Tunawaachia Makaburu wa Tanzania one na makampuni ya kuchimba madini, Richmondi, Wahindi, IPTL, songas, wawatumikishe, sio ndo mnafurahi? Na wanasiasa wa TZ waliowageuza wapiga kura kuwa jembe lao la kulimia. Wanakula nchi na wawekezaji wazungu na wahindi, wala hawawajali watanzania wenzao wa hali ya chini.
Wakenya wanaingia kwa wingi na Masters zao na wanaajiriwa katika kampuni nyingi za kigeni. Unajua idadi ya wakenya na waganda wanaomaliza vyuo vikuu kila mwaka? Ni zaidi ya mara tatu ya Tanzania! Jamani inauma! Halafu serikali wala haishtuki, ndio kwanza inatoa kipaumbele katika masuala mengine!
Kifupi ni kwamba, watanzania walioko mamtoni unaweza kuwaita jina lolote unaloweza kuwaita, lakini hao unawaita wachovu wana hali bora kuliko wachovu waliobaki bongo. Hata kama hajasaidia chochote nyumbani kwao lakini maisha yake mwenyewe anayamudu bila kumtegemea mtu yoyote na anaishi nyumba inayoitwa nyumba, umeme, maji, balanced diet anapata, hakuna hofu ya ujambazi, unalala mlango wazi mpaka asubuhi! Nyumbani huko nani anapata huduma kama hizo kama sio matajiri tu, yaani wanasiasa, na hao wawekezaji?
Nyumbani ni kokote unapoamua kuishi. Kuna nchi ilikua moja na sasa zimetengana
ReplyDeleteMichuzi huku hamna mtanzania mkimbizi kwa vile TZ ni nchi ya amani haina vita. Kisiasa sijui kama wapo na kama wapo sio wengi. Kwa hiyo kuita watu wakimbizi sio vizuri. Hivi na wewe unajiita mkimbizi??? Kwasababu ninauhakika wewe sio mzaramo sasa sijui Dar unafanya nini?? Ulimwengu umekua mdogo siku hizi.
ReplyDeleteSioni ugumu wa hili jambo kwa vile penye nia pana njia. Wahindi ninaowajua hapa marekani Kwa vile hawataki kulipa dola $5000 wote wanachofanya ni kuwa Mume anakua citizen na mke anakua just a green card holder and vice versa. Kwa hiyo mke anafaidi manufaa ya uraia kwa kupitia mume wake na huko india mume anakubalika kupitia uaraia wa mke. Sasa kama ni kuinverst hela nchi nyingine sio tatizo ni akili ya mtu tu.
Tanzania inatakiwa kujua tu ni kiasi gani watu wanatoa nje ya nchi per year. Au kuweka masharti makubwa iwadiscourage hao waarabu ambao watataka kupeleka hela nje ya nchi. US wanakuruhusu tu lakini how much for real you can take out of the country per year? You have to declaire more than $10,000? It is not easy na hela yote pia ni taxable money. Kwa hiyo hapo inakuwa double taxation.
Na sijui ni wazawa wangapi ambao ni raia wa nchi nyingine watakaonufaika na hili processau au wata take advantage ya hii process.
Mwisho ni heri niwe huku mniite mnachotaka na niwenze kujitunza, nakuja kusalimu na kupiga simu na nikipata kidogo nawasaidia huko kuliko niwe hapo niishie kuwa mzigo kwa watu wengine. Kila siku nitumie dollar basi..Ni watu wangapi wakubwa tu above 21 years of age. Wanakaa kwa baba na mama mpaka leo hapo Dar.Sisi wakimbizi unaotuita tunakula jasho letu, tunavaa jasho leu, tunalala mahali tunapaita kwetu na tunatunza watoto wetu wenyewe. Wengi hapa wanatoa comment still wanatumia computer ya baba......... Kama unataka mjadala weka "NI UMRI GANI MTU ANATAKIWA AANZE KUJITEGEMEA ATOKE NYUMBANI KWA BABA NA MAMA? It is too much let us love each other tutaendelea. TZ kuna big gap btn watu wanaoishi nje ya nchi na wale wanaoishi nchini. wanafikiri sisi hatupendi nchi yetu au tumekimbia. Kumbe wangejua tunawasaidia sana tu. Kwa vile siajabu ningekua bongo ningechukua kazi yake.
Michuzi huku hamna mtanzania mkimbizi kwa vile TZ ni nchi ya amani haina vita. Kisiasa sijui kama wapo na kama wapo sio wengi. Kwa hiyo kuita watu wakimbizi sio vizuri. Hivi na wewe unajiita mkimbizi au mzamiaji? Kwasababu sidhani kama wewe ni mzaramo sasa sijui Dar unafanya nini? Ulimwengu umekua mdogo siku hizi.
ReplyDeleteSioni ugumu wa hili jambo kwa vile penye nia pana njia. Wahindi ninaowajua hapa marekani wao wanaruhusiwa lakini wengi wao hawataki kulipa dola $5000 za kuomba uraia tena huko India. Wengi wanachofanya ni kuwa Mume anakua citizen wa USA na mke anakua just a green card holder and vice versa. Kwa hiyo mke anafaidi manufaa ya uraia kwa kupitia mume wake na huko india mume anakubalika kupitia uaraia wa mke. Sasa kama ni kuinverst hela nchi nyingine sio tatizo ni akili ya mtu tu.
Tanzania inatakiwa kujua tu ni kiasi gani watu wanatoa nje ya nchi per year. Au kuweka masharti makubwa yatakayo wadiscourage hao waarabu ambao watataka kutoa hela nje ya nchi.
Hizi nchi kubwa zinakuruhusu tu lakini how much for real you can take out of the country per year? You have to declaire ukitoa au ukipokea more than $10,000 per year? So how many years? It is not easy otherwise uwe willing to be taxed and that will be double taxation sasa.
Na sijui ni watanzania wangapi ambao ni raia wa nchi nyingine watakaonufaika na hili processau au wata take advantage ya hii process.
Mwisho ni heri niwe huku mniite mnachotaka lakini ninamaisha yangu.
Ni watu wangapi wakubwa tu above 21 years of age. Wanakaa kwa baba na mama mpaka leo hapo Dar. Sisi mnaotuita wakimbizi, mara tunabeba mabox tu tunakula jasho letu, tunavaa jasho leu, tunalala mahali tunapaita kwetu, tunatunza watoto wetu tunakuja kuwasalimu.
Na wengi manaotoa commet huku tunasaidia sana tu sijaona hata mtu ameniambia leo nakutumia hela ni kila siku nitumie dola nitumie dola.
Na wengi hapa wanatoa comment still wanatumia computer ya baba na mama yao sis tunawaita majina yeyote?
Kama unataka mjadala kuhusu real life weka "NI UMRI GANI MTU ANATAKIWA AANZE KUJITEGEMEA ATOKE NYUMBANI KWA BABA NA MAMA? NANI KWA NINI WATOTO WENU WANATUNZWA SIKU HIZI NA BABU NA BIBI??
It is too much let us love each other tutaendelea kama mataifa mengine. TZ kuna big gap btn watu wanaoishi nje ya nchi na wale wanaoishi nchini. Wengi wanafikiri sisi hatupendi nchi yetu au tupo tu huku for leisure. Kumbe wangejua tunawasaidia sana tu hata wao. Wengine siajabu ningekua bongo ningechukua kazi yake.
Jamami GIVE US LOVE....PEASE
Acheni fujo na uraia. Mtu kama anataka kuwa raia wa nchi mbili shauri yake, kwa kufanya hivyo je anafanya kosa gani? Nadhani viongozo wa nchi yetu wanaguswa sana kibnafi na tatizo hilo. Watoto wao ambo wengi wnaishi au wanasoma ugaibuni wanahitaji dual citizenship ili maisha yao yawe bora zaidi. Acheni washughulikie swala hilo vikamilifu. nchi kadhaa uerope and america wanatumia mtindo huo na hakuna matattizo. Kuishi ugaibuni siyo lazima kuwa mkimbizi
ReplyDeleteUraia wa nchi mbli unakuja tu muda si mrefu maana Vingunge wana watoto wao chungu nzima ambap wanakimbizana na makaratasi huko waliko ili wapate uraia.
ReplyDeleteMadiplomat wa Kitanzania ambao walijaliwa kupata watoto nje ya nchi hasa Ulaya ya Magharibi, Canada na Marekani huwashauri watoto wao wakishafika miaka 18 kuchangamkia uraia wa nchi hizo kwa kuonyesha kwamba wao ni wazaliwa wa huko na ushahidi ni Birth Certificate. Madiplomat wengine Wakitanzania ambao watoto wao walizaliwa bongo mara wamalizapo muda wao katika nchi za magharibi watoto wao huukana udiplomat na kuanza kufukuzia makaratasi yatayowawezesha kuupata uraia wa nchi wanazoishi.
Kwa maoni yangu sidhani kama itachukua muda mrefu kabla ya hili kuruhusiwa.
Kwa wale ambao hawajawahi kuwa Watanzania ni lazima kuwa na utaratibu wa kuomba uraia. Kwanza wapate ukazi wa kudumu (permanent resident) kama watatimiza masharti yote yaliyowekwa, pili ili waweze kupata uraia wa Tanzania ni lazima waishi Tanzania kwa kipindi cha miaka 6 au 7 mfululizo, hawajawahi kufanya makosa yoyote na wanaajira au biashara zinazoeleweka.
Kaka Michuzi uraia wa nchi mbili unakuja tu mtake msitake, kuwakana Watanzania wanaoishi nje hakuna maisha marefu, leo mnamuona Obama, Mkenya ambaye labda atagombea nafasi ya Urais Marekani hebu niambie ni akili kweli kumnyima uraia wa Kenya Obama eti kwa sababu ana uraia wa Marekani!? Miaka michache ijayo si ajabu kumsikia mbongo ana nafasi kubwa katika mojawapo ya nchi za magharibi, kumkana mtu kama huyu ni kosa kubwa sana kwa maendeleo ya nchi yetu.
Mwisho napenda kukushukuru sana kwa kuanzisha mjadala huu.
Suala la uraia wa nchi mbili lina faida na hasara zake. Lakini nionavyo mimi faida ni nyingi kuliko hasara. Kwa kuongezea faida zilizotajwa na wanablog hapo juu, kwa wale wanaofuatilia masuala ya uchumi duniani, waangalia recent development ya uchumi wa Pakistan yamesaidiwa na nini. Kifupi uchumi wao umekuwa kwa takriban 8% P.A. kutokana na wawekezaji wa Kipakistan waishio nje ya Pakistan wenye dual citizenship.
ReplyDeletePia ieleweke kuwa wengi wa waTZ waendao nje at least wana elimu au ufahamu fulani kwa hiyo kumpoteza mtu kama huyu na kizazi chake ni hasara kwa taifa na ni faida kwa nchi anayopata uraia. Kimsingi ni ngumu kuuacha uraia wa nchi ya dunia ya kwanza ambapo ana uhakika wa usalama wake, afya yake na elimu yake hata kama ataukana ule wa dunia ya tatu. Kwa hiyo, hakuna ubaya kuwa na uraia wa nchi mbili afterall ataegemea zaidi kule alikotoka ambako ana social ties (ndugu wengi, jamaa, na marafiki.)
East West nyumbani ni best, na wa TZ walioko nje watarudi, lakini watakataa kuendelea na usanii wa nyumbani.
ReplyDeleteKizazi hiki kinapiga kelele, kinalalamikia usanii na hali mbaya ya maisha ya mtanzania, lakini hakitakimbia forever, kitarudi na kubadilisha mambo.
Faida kubwa ya kutembea nje ni kwamba unagundua masha bora yanawezekana. Unagundua kwamba si haki wanafunzi(tena wachache) walioko vyuoni wanaandamana kila siku kwa kukosa huduma kutoka serikalini(serikali ambayo imeundwa na baba zao na mama zao!). Unagundua kwamba sio kawaida kukosa maji, kukosa umeme, kukosa waalimu, kukosa barabara, kulipa rushwa kila mahali, kutoheshimiana kwa kutishiana, kudhalilishana kwa nidhamu ya woga. kutotibiwa mpaka ulipe!!
Kama bongo ingekuwa mbaya, hao wazungu,wahindi na waarabu, wachina, n.k walioko TZ wangeondoka. Bongo si mbaya, ila kwa wa TZ wengi, wale mafukara wasio na nafasi katika jamii,ni mateso makubwa nchini kwao wenyewe. Ughaibuni hakuna mtumwa, kila mtu atafanya kazi, na kila mtu atakula jasho lake!!
Ndugu Michuzi, nashukuru kupata fursa hii kuchangia mada hii.Naona imewagusa watu wengi mno na wengi wao wamejibu kwa hasira kwani jinsi ulivyoulizia hili suala unaonekana kuwa na kejeli kinamna kwa wabongo wenzio.
ReplyDeleteUraia wa nchi mbili kwa anaetaka sio jambo baya hata kidogo, mbali ya kumfaidisha aliokua anao pia inachingia kwenye maendeleo ya nchi. Issa Michuzi weye utaona vipi hasara ya kukaa Bongo wakati wewe unawafadhili wanaokubeba!! na utaona vipi faida ya kuzamia ilhali hujawahi kuzamia?
Ndugu yangu walioko nje ya nchi sio watoto wa kajamba nani tu, huku wapo festi klasi mpaka sie akina thedi klasi. Huku kuna wabongo wenye kufanya kazi kuanzia Ikulu mpaka machinga. Hivi Bwana Issa hebu tuambie kweli unataka turudi bongo, tuje tufanye shughuli gani? hebu fikiria hapo bongo kama kungekuwa na vifotopoint kama hamsini Michuzi angekuwa wapi? je! kweli angeandika mada kama hii!? wewe huoni kuja kwetu huku kumeisaidia nchi kupunguza tatizo la ajira? J.K anakubaliana na mimi kwenye hilo. Je! unafahamu kwamba senti chache tunazotuma huko zinachangia kwenye pato la serikali la fedha za kigeni? uliza wadau Benki kuu watakutoa tongotongo. Faida za wabongo kuwa nchi za watu ni nyingi kuliko kubaki hapo Bongo. Angalia hili suala katika ngazi ya kitaifa na sio kwa kuangalia watu wawili watatu ambao unawajua wewe.
Acha utani Issa, unataka kunambia huoni tofauti ya maisha ya bongo na ughaibuni???!!! kama wengi waliotangulia ninakwambia kwamba mbongo mlala hoi wa ughaibuni ni sawa na tajiri wa hapo bongo.Mwenye kufanyakazi ughaibuni ana uhakika wa milo mitatu tofauti na mfanyakazi wa bongo.
Bwana Michuzi acha kuwadhihaki wabongo wenzetu hapo bongo eti kwa sababu wewe neema imekutembelea.
Kuishi huku sio ukimbizi mie naita ni uamuzi. Hatujakimbia bongo isipokuwa sisi ni wabongo wenye kuipenda nchi yetu kuliko hata wewe ndio maana tukaamua kuisaidia nchi kupunguza tatizo la ajira pia kupunguza mzigo wa kusomesha wabongo nk.
Tunajua nyumbani ni bongo na ndio maana tukilala usingizi wa milele tunarudi kulala nyumbani.
Kumalizia Ndugu Issa kunafaida kubwa hususani kwa nchi kuruhusu raia wake kuwa na uraia wa nchi mbili kwani wale unaowaita wakimbizi watapata changamoto ya kurudi nyumbani kuwekeza aidha kwa kutumia elimu na ujuzi waliopata nchi za watu au itafungua milango kwa wabongo kufanya biashara na serikali pamoja na wabongo wenzao,kumbuka mchango wa pato la fedha za kigenin.k.
Maisha ya wabongo nchi za nje ni bomba huwezi kulinganisha na wabongo wengi hapo bongo na wewe umo ndani. ukiacha wapemba hakuna mbongo mkimbizi, watu wameamua kuisaidia serikali kutatua matatizo ya ajira na elimu. mwisho kumbuka kuishi nje haina maana kwamba huipendi bongo.
Michuzi umetumwa nini?
ReplyDeleteRais au Waziri Mkuu akitembelea nchi mojawapo za ugaibuni zilizo na Watanzania, kama kuna ofisi ya ubalozi, watanzania wa mji wa matembezi wanatafutwa ili wakutane na Rais au Waziri Mkuu wao. Wakina mama hupiga vigelegele kwa fujo endapo Rais na mke wake au Waziri mkuu na mke wake wanapojitokeza kukutana na Watanzania hao.
Mara nyingi Rais au waziri Mkuu hufurahi sana kuwaona Watanzania wengi namna hiyo wakimlaki kuliko kulakiwa na kukutana na maafisa wa kibalozi na Watanzania watano tu.
Sio kila Mtanzania ana bahati ya kufanikiwa ugenini. Lakini mara nyingine hata yule ambaye hakufanikiwa anaweza at least kumpelekea rafiki yake kachupi, kasinika, kakofia ama kafulana ka FUBU, ambako si feki (na vizawadi vinginenvyo vidogo na vikubwa). Cha maana ni kwamba hao Watanzania wasio na uwezo mkubwa, at least wanaikumbuka nchi yao na kutoa hivyo vizawadi.
Turudi kwa walio nyumbani. Mapesa yaliyowekwa kwenye benki za nje (kulingana na takwimu za Benki Kuu ya Tanzania, kama alivyonukuliwa miaka miwili hivi Gavana Bilali) ni ziadi ya fedha zilizowekwa katika mabenki nchini!!!!!!!!!!!!!!
Wa nyumbani wanatorosha, wanaiba, wanapora (nyingize zikiwa za 10 mpaka 12% kutokana na tenda za umma...Kama mwenye kutapata tenda za namna hiyo akisema ushuru ni mkubwa, Watanzania watia saini makubaliano ya tenda hizo wanasema: Pandisha bei...mwisho inakuwa Tanzania ndiyo inawapa Watanzania hao 10 -12%), na kuziweka katika mabenki ya nchi za nje ama kununua property ugaibuni. Pesa za namna hiyo zimenunua majumba nchi za nje!!!!!!!!!Pesa za namna hiyo haziwekwi Tanzania zinabakia ng'ambo!
Sasa ni nani aipendaye Tanzania kuliko mwingine..wa ugaibuni au wa nchini!
Michuzi, ninakuomba kwa dhati uweke mjadala mpya wa namna hii kuhusu wakubwa, vigogo, wezi, waporaji wa mali ya umma wa nchini wenye maakaunti nchi za nje ili tuujadili. Ukifanya hivyo utakuwa ume-balance uwiano wa kuipenda Tanzania, vingine, mjadala wako utakuwa kama umetumwa!
naomba nami nichangie
ReplyDeletekwa mtazamo wa haraka haraka maoni yanaonesha ughaibuni kumekucha. nimeanza kupata mshawasha wa kutaka kuja. tatizo sijajua kama nikiamua kufanya hivyo niende nchi gani ama mji upi? na kwa sababu gani?
Michuzi, napenda kutabiri: Mwaka huu hautaisha kabla wewe hujaingia Marekani!
ReplyDeleteBwana Michuzi,
ReplyDeletePamoja na kwamba sina uhakika kama lengo lako ni nini hasa kuleta hii hoja, ukweli unabakia palepale Tanzania haiwezi kujitenga na mabadiliko yanayotokea duniani sasa hivi kuhusu swala zima la urahia wa nchi. Watanzania wanasafiri sana sasa hivi wanasafiri na kuamia nchi mbalimbali duniani.Lakini hii haimaanishi kwamba eti kwa sababu wameamua kuishi ughaibuni, ni lazima waonyeshe au kuleta maendeleo nyumbani Tanzania, lazima watakuwa hawana maana yoyote. Sisi tunaoishi huku ni sawa tu na waliobaki nyumbani. Tofauti kubwa ni kwamba nyinyi mliobaki huko, ni watu wapokea rushwa sana na msiojari utu wowote. Watanzania kama raia wengine wa hii "free world" wanaweza kutumia njia nyingi tu ili mradi kufanikisha malengo yao ya kuishi Ughaibuni. Kama watu wataamua "kubadili" dini zao au utaifa ilimradi wapate wanachotaka kuna tatizo gani hapo? Kwani mtu akijifanya msomali au mkristu/mwislamu anapunguziwa nini katika utaifa wake kama Mtanzania halisi?
Although we, Tanzanians who lives abroad sometimes we go through a lot of problems, the truth is Tanzania can't afford to loose us. While we live abroad, majority of us know that we have the resposibility to build our homeland, Tanzania. Different expertise, exposure and other skills of building poor nations like TZ comes from the western world. The more little money everyday people from abroad keep on sending to their families and relatives back home eventually will make a big impact to the economy. But always we have to remember that this impact will not be seen overnight. It will take a time. A new immigrant to get settle in the western world would take about 8-10 years. As the years goes on, changes will be felt in the economy. The Western Union Tanzania has all the data. They should be able to tell us how much money is going to Tanzania every year.
The Kikwete Administration has a role to play on all these. The Government has to set a conducive environment which will allow Tanzanians who needs a passport and other consular related problems be solved in a good way. We need the Government to give priority our problems. If the Government chooses to go it's way and leave us. We will also decide to abandon Tanzania. If they decide to allow us to maitain dual nationality, it will be well and good. The whole thing is like the introduction of "multi party" in Africa.
Michuzi weka mjadala wa hawa wakenya kuutangazia ulimwengu kuwa serengeti ni mali yao na sisi tutakakaa kimya tu,iko wapi serekali na wizara ya utalii jamani?au tumenunuliwa tayari?
ReplyDeleteMjadala huu ni mzuri na kuna mifano ya kuiga ama kutazama e.g. :
ReplyDeleteDual Citizenship for Overseas Indians Considered
The Indian Prime Minister announced new regulations affecting Indians abroad in order to encourage the diaspora to invest in the country. India’s domestic industry raised objections to the possibility of dual citizenship.
In advance of legislation granting Indians abroad dual citizenship, the Indian government announced a Persons of Indian Origin (PIO) card scheme. The cards will provide visa-free entry and a number of educational and financial benefits over such things as property and income earned on dividends. The scheme would also enable overseas Indians to cut through much of the country’s tangle of regulations.
Prime Minister A.B. Vajpayee launched the card scheme while addressing the Global Indian Entrepreneurs Conference in New Delhi. The issue was also raised by the Union Urban Affairs Minister, Ram Jethmalani, at the 18th International Conference of Non Resident Indians in the same city in December. Vajpayee noted that Indians abroad had contributed over $12 billion a year in remittances for the past two years. The Resurgent Bond Issue alone raised $4.2 billion in a matter of weeks (see Traces #3). Members of the diaspora had been calling for dual nationality for a number of years.
The Prime Minister also announced in November that a dual nationality policy would be implemented early in 1999. He also called on Non-Resident Indians (NRI) to invest in India’s new highway network, while Jethmalani asked for assistance in the country’s low-cost housing sector.
These moves are regarded as part of a concerted effort by the BJP government to restore and strengthen links with Non-Resident Indians – objectives which were part of their election manifesto. They envisage not just economic links, following the success of China in tapping the overseas Chinese, but also enhancing ‘social, cultural, emotional and spiritual’ ties. They may involve reviving the NRI Consultative Committee under the chairmanship of the Minister of Finance, Yashwant Sinha. There may be modifications in investment rules and regulations, as well as more involvement of NRI entrepreneurs in advisory positions close to government. Some overseas figures have suggested that NRIs should be nominated to India’s Upper House of parliament.
Opposition to the proposals for dual nationality has come from Indian industry, concerned about the threat of foreign competition if NRI investors are allowed greater access to India’s markets. Among the suspicions directed towards NRIs is the question of their divided loyalty, and whether dual nationality gives too many benefits to residents abroad. Spokesmen for Indian industry question whether the desirability of opening up investment opportunities also requires granting citizenship.
Indian PM launches PIO card scheme to woo Indians abroad, Asia Pulse 12.11.98; PM Vajpayee assures dual nationality, benefits to expat Indians, Agence France Presse 12.11.98; New Delhi pledges greater emphasis on NRIs, Anand Sagar Gulf News 13.11.98; Industry upset over 'dual citizenship', V. Jayanth The Hindu 16.11.98; Tapping the Indian diaspora, The Hindu 23.12.98; 'Govt. considering dual citizenship for NRIs', The Hindu 26.12.98; Private transfers Spectacular turnaround, Harish Damodaran Business Line 9.11.98