mshindi wa shindano la 'ni wapi hapa' ni bimkubwa. naomba tumia barua pepe yangu issamichuzi@gmail.com unielekeze unataka zawadi ya picha gani na nikutumieje. hongera sana. anony sm wa toronto, canada, umepatia ila sema ile kusema 'mimi nafikiri' ambako kumeonesha kusita, kumekula nusu maksi na kumpa bimkubwa ushindi. pole na jaribu tena siku ingine. asanteni pia mlioshiriki. jiandaeni kwa shindano lingene hivi karibuni...
JIBU NI: HAPA NI KARIBU NA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU/SHAURI MOYO, ILALA MCHIKICHINI, MKABARA NA KIWANDA CHA BIA.
KANUNI: ILI KUPATA ZAWADI MSHINDI SHURTI ANITHIBITISHIE
1. KWAMBA NI YEYE (KWA HAPA NI WERWE BIMKUBWA)
2. NAMBA YA SIMU AMA ANUANI YAKE
3. SHINDANO HILI NI KWA WALIO UGHAIBUNI TU
4. UAMUZI WA JOPO LA SHINDANO NI WA MWISHO
aidha, nashukuru kupata barua pepe toka kwa mdau sm wa toronto, kanada, ambaye kakubali kushindwa kiungwana na kuahidi kushiriki tena. asante sm na pongezi kwa moyo huo.
pia nimepokea barua pepe kibao za kukata rufaa dhidi ya kumtangaza bimkubwa kuwa mshindi. nimezipokea na jopo la rufaa linazifanyia kazi huku likiomba maoni zaidi. hivyo, zawadi itatolewa ndani ya siku 10 baada ya kanuni hizo juu kuzingatiwa na kuthibishwa.
vile vile tegemea shindano kama hili mara moja kila baada ya mwezi. hivyo jiandae na shindano la januari 2007 kabla ya jumapili hii.
naomba kuwasilisha katika ari ya mwaka mpya mambo mapya...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Michuzi sasa jibu hapo ni wapi?

    ReplyDelete
  2. Sasa Bwn Michuzi mbona hatujajua hapo ni wapi? HAyo majibu mnapeana kwa siri?

    ReplyDelete
  3. Huyu bwana anahitaji mawazo yenu kuendeleza hii dream yake www.elisaccenter.com

    ReplyDelete
  4. rufaa, huyu bimkubwa kwa maelezo yake anaonekana hayuko ughaibuni. Haiwezekani ukajua hadi radi za daladala zinakokwenda. Na wewe ulitoa shindani kwa watu walioko ughaibuni.

    ReplyDelete
  5. Wewe Anonymous wa 11:47 mbona UNACHEMSHA. Kuwa ughaibuni haimaanishi kuwa huruhusiwi kurdi TZ likizo. Sasa kama bimkubwa alikuja huku likizo mwaka jana juzi hata ule wa 2001 bado hizo route zilikuwepo!!! ONDOA rufaa yako!!

    ReplyDelete
  6. Hello Bw. Michuzi,

    Nimefurahi kwa ushindi. Zawadi ambayo ningependa kupata ni Picha ya Rais wetu jakaya Mrisho Kikwete iwe ni picha ambayo umempiga akiwa pekee yake, a good choice would be ile aliyokuwa akihutubia baraza la UN but any choice would do. It should be a picture that I can put up in a frame.

    Asante sana. na kwa wale wenye wasiwasi kuwa nipo bongo. You are dead wrong. Nipo US, wapo wanaofahamu hilo na ni jambo lililowazi. Kuwa nje haina maana huwezi ukajua mitaa ya nyumbani. Nyumbani ni nyumbani hata juu ya miti ni nyumbani tu.

    ReplyDelete
  7. Bimkubwa!

    Hongera sana. Jopo la majaji la shindano la "wapi hapa" limethibitisha pasina lepe la wasiwasi kwamba wewe waishi ughaibuni, hivyo zawadi ya picha ulochagua ni halali yako.

    Tafadhali fungua email yako ndani ya masaa 24 ili uopkee hiyo zawadi.

    Taarifa: Ile rufaa ya mdau anony wa Tuesday, January 02, 2007 8:27:12 PM inatupiliwa mbali kwani haina joto tena.

    Hongera Bimkubwa na endelea kushiriki kwenye shindano lijalo litalokuja kabla ya Jumapili hii...

    ReplyDelete
  8. Nimekata rufaa kwa bosi wako mpya Mjengwa unatakiwa usitoe zawadi mpaka rufaa isikilizwe.

    ReplyDelete
  9. Wewe anonymous wa 9:33 mbona mchemfu sana, hiyo picha kwa mtu anayefahamu vyema jiji la Dar atakueleza hiyo picha imepigwa maeneo ya makutano ya barabara ya uhuru na mtaa wa shaurimoyo. Na kama m2 unafuatilia kwa karibu mambo yanatokea nyumbani utajua rangi za route mbalimbali za jiji la Mh kandoro. Inaonesha jinsi gani ulivyo mbumbumbumbu na kukaa kote DAR unashindwa kujua ni eneo gani. SM, Toronto, Ontario - Canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...