mwalimu akiongoza matembezi ya kuunga mkono azimio la arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ina maana Teacher na yeye katembea umbali wote huo au yeye kawapokea tu pale Ubungo?Maana mbulu sio mchezo babaake yenyewe tu kuja kuiona Arusha ni kazi kweli halafu sasa hiyo safari ya dar?

    ReplyDelete
  2. Anon wa hapo juu, picha hiyo ya Mwalimu na kundi lake, ni tofauti na iliyotangulia ambapo Mwalimu anawapokea waunga mkono Azimio la Arusha waliotembea kutoka Mbulu hadi Dar es Salaam.

    Hiyo picha ya Mwalimu na kundi lake, inaonyesha sehemu ya safari yake iliyoanzia Kijijini Butiama. Mwalimu alikuwa anatoka Kijijini kurejea Dar es Salaam. Lakini badala ya kuondoka kwa gari, Mwalimu na kundi lake waliamka wamevalia magwanda ya Jeshi la Kujenga Taifa na kuanza kutembea. Umati ulimfuata nyuma kutoka kijijini kuelekea barabara ya kutoka Musoma kwenda Bunda hadi Mwanza.

    Pengine ni wachache tu katika msafara huo waliokuwa na habari kamili kuwa safari hiyo haingekuwa fupi. Msafara ulifuatiwa na magari ya Jeshi yaliyokuwa yamebeba vifaa na mahitaji safarini. Wasindikizaji wengi hawakuwa na habari iliwabidi kuondoka pole pole kadri msafara ulipokiendelea. Mwalimu alikuwa akiwahimiza kuzidi kutembea. Baadhi ya wasindikizaji walidhani safari itaishia mjini Bunda. Waliamua kutomwacha Mwalimu; wakajikuta wamefika mjini Bunda.

    Kutoka Bunda, msafara uliendelea na barabara iendayo Mwanza kupitia Ramadi (mpakani mwa mikoa ya Mara na Mwanza) ambako kulikuwa na magari mengine ya Jeshi na la Kujenga Taifa yakiwangoja.

    Wasafiri walichubuka miguu; Mwalimu pia. Wanajeshi waliwahudumia. Waliozidiwa, waliokolewa na magari ya jeshi. Pamoja na michubuko hiyo, Mwalimu hakukata tamaa; aliendelea kutembea kuelekea Ntuzu, Magu, Nyakato hadi mjini Mwanza. Kutoka Mwanza Mwalimu na watu wake walipanda ndege kurudi Dar es Salaam.

    Wengi mtakumbuka kuwa safari ya mwanzo kabisa ya kuunga mkono Azimio la Arusha kwa kutembea hadi Dar es Salaam, ilifanywa na kundi la vijana kutoka Arusha. Kwa bahati mbaya (kama sikukosea), kiongozi wake (jina limenitoka kichwani) alifia njiani kabla ya kufika Dar es Salaam.

    Matembezi hayo ya Arusha na kifo cha huyo kiongozi, pamoja na matembezi mengineyo ya vijana yaliyokuwa yakipamba moto nchini, viliugusa mno moyo wa Mwalimu kuamua naye kutembea kutoka Butiama hadi mjini Mwanza, kama picha ya pili inavyoonyesha!

    Katika picha hiyo (kama sikukosea ilichukuliwa wakati msafara ukikaribia kuingia mjini Mwanza), mbali na sura ya Mwalimu, kuna sura za watu mashuhuri waliotembea safari hiyo toka mwanzo hadi mwisho.

    Hebu wanaowafahamu, tutajieni!

    ReplyDelete
  3. Teacher amekula buti za kufa mtu na kapelo ya kijeshi! Hapo kweli katoka ki Amiri Jeshi Mkuu!
    Huyu mzee aliitendea mema mengi nchi yetu, mwenyezi Mungu amlaze pema peponi mzee wetu Julius.

    ReplyDelete
  4. Alitembea kutoka Butiama hadi Mwanza. Alitumia kama siku tano hivi. Hata hivyo njia ilikuwa imeandaliwa vilivyo kukiwa na waganga, madawa, vyakula na maji karibu njia yote

    ReplyDelete
  5. Azimio La Arusha lilikuwa tamko rasmi la Chama likielezea ni namna gani nchi itaendelea. Kupitia Azimio hilo na maazimio mengine kama lile la Musoma na Iringa Mwalimu alifanya kazi kubwa ya kumkomboa Mtanzania. Mambo yamedilika sasa baada ya Azimio la Zanzibar. Wakauwa Azimio la Arusha. Hivi hivi tukiona. Mbadala wake ukauwa kila kitu kuanzia huduma za afya hadi elimu. mtoto wa maskini hasomi tena. fukara hatibiwi. Hiyo ndiyo Tanzania Ruksa na BWM. Labda JK atafuata nyayo za JK Nyerere. Anaonyesha anayo nia ya kuwajali wazawa. na hasa hiyo ndiyo sera kuu ya Azimio la Arusha. Mzawa kwanza. Si kuuza nchi kwa bei ya bwerere. Mambo gani haya. Laana ya JKN imwangukie yule anayeiuza nchi kwa mgongo wa ubinafshaji usiowajali wazawa. Mengi alitaka kuinunua Kilimanjaro, wenye nchi wakamzuia. Sasa mnashabikia nini eti kilimanjaro ing'ara. mapato yote yanakwenda kwa huyo muwekezaji. Bongo tunabaki na nini? Nyumba za serikali zote wakubwa wamejigawia. Halafu wanjenga nyingine. Hii ni hesabu gani jamani? Ipo kila sababu ya kurejesha Azimio la Arusha. Au nyote mmemezwa na UTANDAWIZI wa BWM? Angalia Geita, Sharaton sijui inatwaje siku hizi, IPTL, NBC na mengi rukuki. JK tusaidie au tutabaki na Tanzania inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno.

    ReplyDelete
  6. Tatizo Tanzania hatuna discipline ya biashara. We are not business oriented people. Kwa mfano, ni companies/corporations ngapi zilianzishwa wakati wa Nyerere, siku za mwanzo zilionekana kufanya vizuri kibiashara, lakini leo ziko wapi? Mtu kaajiriwa kama receptionist, lakini akifika kazini anabakia akipiga domo siku nzima kwenye simu na shoga zake, wageni wanakuja kazini, hawasikilizi yuko kwenye simu zake private. Pia monopolization ndio iliua kabisa. Hiyo ilitoa mwanya kwa yale makampuni ambayo hayakuwa na mshindani kujifanyia yanayotaka bila kumjali mteja. Kwa mfano, TANESCO,TPTC(Posta na simu), NIC(bima). Haya makampuni yalikuwa yakinyanyasa wateja. Kitu kingine politics ziliingia kwenye biashara. Kwa mfano, ATC flights nyingi ziliahirishwa, kwa sababu tu ndege inapelekwa Dodoma kumchukua Malecela, au Songea kumfuata Kawawa, wakati ndege ilitakiwa ibebe abiria kwenda mahali fulani. Wenzetu wakenya kwa biashara ya ndege wametupita sana, wanakwenda Amsterdam kila siku, na pia ni partners na KLM. Pia rushwa nayo, maana kila mtu anataka ale rushwa, na kuiba haraka ili awe na hela ya ziada pembeni. Bado Tanzania kuna safari ndefu sana kufikia mafanikio ya kibiashara.

    ReplyDelete
  7. Baba Nyerere aliipenda tz na watu wake. Kiini cha azimio la Arusha kilikuwa ni kwa manufaa ya mtanzania. Wazungu walielewa kama mambo yangekwenda sawa kama ilivyotakiwa leo tungekuwa mbali. Wakapiga vita (hasa waingereza na waamerika)............Baba Julius
    (alitujuwa watoto wake tuko wapole na tume zubaa kiasi fulani ukitoa wachaga)... ona sasa biashara kubwa leo ziko mikononi mwa wageni, wageni wanajiruhusu kufanya watakacho tz hata ujambazi..Baba angekuwepo leo pasingetosha....anyway JK inaelekea unapenda watu pia fata nyayo za Baba Julius... mirija imezidi!

    Mungu ibariki tz, viongozi na watu wake.

    ReplyDelete
  8. Mtu huyu hakuwa wa kawaida. Alikuwa mtu mwenye upendo wa hali ya juu kabisa kwa nchi yetu na watu wake. Hakuiba mali ya umma kabisa. Hakuwapenda wala kuwakumbatia mafisadi. Alipenda kuona mtanzania ananeemeka ktk nchi yake. Alikuwa mzalendo namba moja. Bahati mbaya mabepari hawakumpenda wakafanya kila njia kuua jitihada zake. Aliichukua nchi toka kwa wakoloni katika hali mbaya sana: wasomi wachache, miundo mbinu duni achilia mbali mambo muhimu kama elimu,afya n.k. Alikuwa mtu wa haki.

    Naamini TZ inao baadhi ya watu wenye moyo kama wake. Lakini siasa chafu na uongozi hafifu baada yake unashindwa kuwatambua watu hawa na kujenga misingi ambayo itapelekea mapinduzi ya kweli ya kiuchumi hapa kwetu. Siasa yetu na mifumo ya elimu inaruhusu kweli meaningful succession planning kwa viongozi?

    ReplyDelete
  9. ilimchukua muda gani kufika mwanza ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...