hata vijijini madishi yapo. hapa ni mikindani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Heeee hii kali, lakini bwana lazima tukubali MULTICHOICE(DSTV) wamesaidia sana katika maendeleo ya mwafrika na haswa Mtanzania kwani kwasasa tunauwezo wa kuamua mambo tukijipima na Dunia ya kwanza kwani tunaona kila kitu kwenye vipindi mbali mbali vinavyoletwa na DSTV. zamani tulikuwa hatuelewi kitu na kurizika na vitu vidogo kwani tulikuwa hatuwezi kujipima na Dunia ya kwanza, Thanks to DSTV now we can. Jamaa wamefikia mpaka level ya kumuwezesha mwananchi wa kawaida kupata huduma kwa dollas 25 tu kwahiyo mtu unakuwa na choice kutokana na uwezo wako.Nawaomba wana DSTV kwa kupitia supersport waibebe JK 11 ili basi wanetu waweze kuonekana Duniani na kutuingiza katika Ulimwengu wa Soka. Wanablogu ya MICHU tulizungumze hili....

    ReplyDelete
  2. Mahali pazuri sana hapa.

    ReplyDelete
  3. A picturequese place. Remember it when was teaching at Ndanda Sec back in 1978-79.

    ReplyDelete
  4. michuzi hongera kwa kuwa na blogu ya kimataifa. ni wengi tunaifurahia na kujifunza lugha ambazo hatukuziacha tulipoondoka nyumbani.
    mimi pamoja na waungwana wengine hatuchoki kutazama habari motomoto unazotuwekea humu ndani kila siku. unastahili pongezi kwa uchapakazi kwani pamoja na vijisafarisafari vyako umeendelea kuleta burudani. Swali nililonalo leo ni kama kuna uwezekano ukatuwekea website zenye kuhusiana na matangazo ya kuuza nyumba na viwanja. Tunataka kuanza safari za kurudi nyumbani ila hatujajua wapi tutashukia. Kwa niaba ya wenzangu nitashukuru kama utatuwekea site za namna hiyo, ninaamini wanamamtoni wengi watafaidika.

    ReplyDelete
  5. haaaa basi hujaja kwetu Kilosa bwana! Mbona utaduwaa, kwetu ndo uzunguni bwana!!!

    ReplyDelete
  6. Mchuna ngozi Mbeya ahukumiwa kunyongwa
    Na Innocent Ng'oko na Solomon Mwansele, Mbeya
    MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, imemhukumu Obadia Kijalo, adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kupatikana na hatia ya kumuua na kumchuna ngozi mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Ilenje.
    Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Othman Chande ambaye
    alisema mahakama haina adhabu mbadala kwa mtu anayeua kwa kukusudia zaidi ya kupewa adhabu hiyo.
    Jaji Chande aliamuru kielelezo katika kesi hiyo ambacho ni ngozi ya marehemu Ezekia Swila, wapewe wazazi wake kwa ajili ya mazishi.
    Awali, Wakili Ayoub Mwenda wa upande wa Jamhuri, ulidai mbele ya mahakama hiyo kuwa Juni 15, mwaka 1999, katika kijiji cha Ilenje, mwanafunzi huyo aliuawa na kisha mwili wake kuchunwa
    ngozi.
    Mwenda alisema washtakiwa wa mauaji hayo walikuwa ni Kijalo, Anyandwile Mtafya, Edwin Steven (Kifimbo Cheza) na Richard Kajula ambao walikamatwa kuhusiana na mauaji hayo.
    Ilidaiwa watuhumiwa hao walikiri kuhusika na mauaji hayo na kuongeza kwamba washitakiwa watatu katika kesi hiyo walifariki dunia kwa maradhi tofauti wakiwa gerezani ambao ni Mtafya,
    Steven na Kajula.
    Wakili Mwenda aliongeza kuwa mshtakiwa Kijalo aliendelea na kesi hiyo ambayo upande wa utetezi ulikuwa ukiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Simon Mwakolo.
    Upande wa mashtaka ulileta mashahidi tisa na kielelezo cha ngozi ya marehemu.
    Mahakama Kuu ilimuona mshtakiwa kuwa na hatia ya kuua kwa makusudi na hivyo kumtia hatiani.
    Upande wa mashtaka uliomba adhabu kali itolewe kwamshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine ambapo upande wa utetezi uliomba mshtakiwa apewe adhabu ndogo kwa
    sababu amekaa gerezani kwa zaidi ya miaka minane hivyo amejifunza na kujutia kosa lake.

    ReplyDelete
  7. Miroast unikumbusha home kabisa mi ntalia!!

    ReplyDelete
  8. Michuzi ,

    ACHA KUTUKANA MIJI YA WATU NI TANGU LINI MIKINDANI PAKAWA KIJIJINI ?

    ReplyDelete
  9. Ano wa kwanza kabisa hapo juu una hatari. Hivi unadhani TV inakuletea maendelea. Ningekushauri upunguze muda wako wa kuangalia TV na badala yake muda uutumie kwa kazi nyingine kama kusoma vitabu, kufanya mazoezi, kujifunza lugha ya kigeni au kufikiria cha kufanya. TV muda mwingi inapumbaza kwa kukupa mambo kutoka na mlengo wa chombo chenyewe na kwa matangazo ya biashara yanayokutaka uamini bidhaa ni nzuri na unaihitaji wakati huihitaji. Uamuzi ni wako lakini.

    ReplyDelete
  10. BAADHI YA ESTATE AGENCY IN TZ

    ANON WA NNE JUU ULIOOMBA NYUMBA NA VIWANJA BONGO YOU CAN CHECK THE WEBSITES BELOW .... LAKINI MOSTLY NI DAR MY DEAR INAELEKEA TANZANIA NI DAR KWINGINE HAKUJULIKANI AU HAWAJITANGAZI.. KAMA ULIVYOSEMA MICHUZI ATUCHEKIE NA MIJI MINGINE ATUWEKEE MANAKE NI VIZURI TUKAWA NA MALENGO NA NAMNA YA KUYAFIKIA SIO TURUDI NAVIPOUND VYETU ALAFU TUCHEMSHE...

    http://www.my-beach.com/

    http://www.rupiainvestment.net/web/index1.asp

    http://www.prointz.com/

    KILA LAHERI NDUGU

    ReplyDelete
  11. Hii inaonyeshs jinsi gani Watanzania tnavyopenda maendeleo na starehe lakini hali ya uchumi inatutuzuia. Tunajitahidi kadri tuwezavyo kuwa sawa na wengine duniani tunashindwa! Hii ni kwa sababu vigogo wanaiba sana kwa mtindo wa Rushwa na kupeleka pesa nje ya nchi. Angalia sasa, watu wamechoka, nyumba kwisha, lakini wameweza kuweka dish la TSHS 250,000 nyumbani ili waone angalau Ar Arabia au Ar Jazeera!

    Kuna umuhimu wa kuwa kama Kenya. Kule watu wanaiba fedha kule na wanatumiza kuwekeza humo humo ndani ya nchi, tofauti na sisi hapa Bongo! Ukipita Nairobi au Mombasa utakunya majumba yanaitwa KIBAKI FLATS, NJONJO BEACH, ODINGA TRANSPORT. Lakini bongo mbona hakuna MRAMBA COCONUT PLANTATION? Wanapeleka wapi mabilion haya ya RADA?

    ReplyDelete
  12. anonymous wa feb 8 4:25pm nakushukuru sana tena sana kwa kuweka website hii mimi siye niliyeuliza lakin katika tazama tazama yangu kwenye blog hii nimeona hii kitu ni cha maana sana na nimezicheki website hizo bomba hata na mimi nilikuwa nazitafuta niko huku ughaibuni, yani daima ubarikiwe sana tena sana na aliyeuliza pia ameuliza swali jema sana na shukran pia michuzi kwa kuweka katika blog yako wewe ndo mwenyewee michuzi boy babake si mchezo nakufagilia mwanangu kwa sana tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...