jk akiongea na mtendaji mkuu wa marks and spencer Stuart Rose jijini landan leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Huyu jamaa anapenda London huyu duuu!!!!!!!!!!! dizaini alikuwa anakuota sana kabla hajawa president,kila kheri na london,aangalie UK na US huku hakuaminiki,watamuondoa akina osama??????

    ReplyDelete
  2. Hivi Jamani! Kila nnavyosoma magazeti na nnavyotembelea Michuzi.blog, namuona huyu Rais wetu kutwa akiwa nje (kwa raha zake), sijui anapenda kutembea tembea...au yuko bisee tu kwa mafanikio wa nchi. Naombeni jamani mniambie:
    - safari zote hizi zinatusaidia?
    - anatumia pesa zake au ...?

    ReplyDelete
  3. Kikwete hoyeeeeeeeee!
    Kaona kuwa kuna kaka mmoja alisema kuwa madada zetu wanavaa nguo za CHINA. Hivyo anataka Marks spencer wawekeze DAR, kisha tutanunua nguo kwa kubadilisha na NANZI.

    ReplyDelete
  4. Atumie hela zake kasema nani? Toka lini kiongozi wa kiafrica akatumia hela zake? hela zinazotumika ni za serikali na offcourse atakuambia anasafiri kusaidia nchi. kazi kwenu wa tanzania ndio baba wa Taifa huyo. I guess hakuna kwa kukimbilia kama wahenga walivyosema mtoto wa nyani ni nyani, na unaruka majivu kukanyaga moto. i tought big of JK! na nilifurahi alivyochaguliwa urais lakini sasa i don't have a single respect for him, and unfortunatley he is our next president for the next 10 years.

    ReplyDelete
  5. Hivi Ukerewe hawaondoagi ombaomba kuwarudisha makwao/Dodoma?

    ReplyDelete
  6. Jk kaka,tunakuheshimu!tunaomba umuachie na Dakta Shein naye japo visafari vichache.Huchoki kaka we!?

    ReplyDelete
  7. Watu wamesema mengi,kuhusu Kingunge na Viongozi wengi waliopita na waliokuwepo madarakani.Mi binafsi naona ukweli upo palepale,hata msemeje nyie manotetea huu uozo wa viongozi wetu nchi ina amani sawa,lakini nchi ni maskini pia????. Mi nahisi nyie manaotetea viongozi hawa mnamahusiano nao,na kwa kifupi mnafaidika na wizi wanaoufanya kwenye maliz za uma,ivo hamuwezi wapinga hata siku moja.Watu wanamsifia Nyerere,kwa mambo mengi,wakati wake nchi ilikuwa na amani,nchi ilikuwa inaongoza kwa kuwa na watu wanaojua kusoma na kuandika katika sub saharani africa,rushwa ilikuwa katika kiwango cha chini kabisa,viongozi walitambua miiko ya uongozi. Sio leo watu hajui hata miiko ya uongozi,wameingia wameuza madini yetu,wamesaini mikataba ya ajabu,inayotuleta matatizo kila siku,nawakiondoka madarakani ni matajiri kuliko hata mwaziri wanaotoka katika nchi zinanozotoa misaada. Ebu angalia nchi kama Ghana,mabazo zilipishana na Tanzania miaka 4,kupata uhuru zikowapi sasa???zimetuacha mbali mno.Halafu mnasema eti sisi tumeifanyia Tanzania,kumbuka hawa watu wameanza kuongoza kupitia wakiwa na umri wa kuanzia miaka 20 kwenda juu,napaka sasa wapo madarakani karibu miaka 40,na hakuna cha maana,Jerry Lawrings wa Ghana ameoongoza kwa miaka mingapi nasasa Ghana ipo wapi???ndio maana tunasema hawana jipya waachie nchi yetu,tuiongoze nasisi. Sanasana wanachofanya ni kuchukua pesa kujenga majumba ya kifahari,kuwaanzishia watoto makampuni ambayo yanapewa tenda za serikali kupitia vifua vya baba zao,nani asiye jua habari za Mkapa na mwanae,nani asiyejua Kingunge na mwanae, nani asiyejua habari za akina Kigoda,na wengine wengi,zote awamu hizi kingunge ni mshauri,je Nyerere angeamua kufanya hivo familia yake ingekuwa wapi,ukizingatia ameongoza kwa miaka 24,acheni kutufanya mazuzu bwana,hamna hoja hapa,hata nchi zilizopitia vita zinamaendeleo kuliko sisi???nyie mnasema wanawunza amani,sasa tunapenda amani,lakini pia na maendeleo,nchi inanuka rushwa,na Kikwete anasema nawajua,eti anawapa muda wajirekebishe.Sisi tuanamachungu sana na nchi yetu kuliko nyie mnafaidi pesa za ndugu zenu wanaoibia nchi,nadhani mnalitambua hilo,na mnajua ipo siku mwisho wenu utafika, na mungu atawaadhibu kwa matendo yenu hata vijukuu vyenu.

    ReplyDelete
  8. Tangia Kikwete awe Rais wa Tanzania kuna mjadala ya kuwa Rais anasafiri sana nje,ni sahihi Rais amesafiri nje kuliko hata ziara za Mikoani,Kuna wanaosema Rais anapenda sana kusafiri,lakini tusiwe watu kuzungumza bila kutafakari kwa nini Rais anasafiri sana nje.
    Kwanza Rais Kikwete alishapata kuwa waziri wa mambo ya nje wa muda wa miaka kumi,kama kusafiri nje amesafiri sana sana aniujua sana dunia wala haitaji kusafiri nje kwa kuwa amekuwa Rais,hili lieleweke,Kikwete kuwa waziri wa mambo ya nje kumempa ujuzi sana na siasa za kimataifa,Rais anapo kwenda nje ya nchi kuomba wafanya biashara wakubwa wawekeze nchini mwake ni tofauti na kumtuma waziri,maana hao wafanya biashara kila siku hukutana na mawaziri kutokana nchi mbali mbali wameshazoea hilo,lakini wanapo kutana na Rais wa nchi huwapa moyo na mwamko wa kuwekeza.
    Pia kukutana na viongozi wa nchi tajiri kuomba misaada ya kimaendeleo kwa Tanzania,mawaziri wa nchi nyingi maskini kila siku wapo katika nchi hizo wakiomba misaada lakini ngazi ya viongozi ni wachache.
    Rais ameligundua hilo na kuona ili Tanzania ipate wawekezaji wengi na misaada mingi ni vizuri kama rais mwenyewe akailishughulikia kuliko kutuma mawaziri na kupigwa kalenda na wakubwa.
    Rais ni mtu mwelewa ana washauri na wengi waelewa anajua anachokifanya hawezi eti aende nchi ya nje aketembee akijirusha atakuwa rais wa ajabu sana.

    ReplyDelete
  9. sawa tunakubali hayomasafali yako lakini muachie kidogo namakamu wako yeye kila siku kwenye matembezi ya mshikamano akisafili arusha au znz tuna kubali unatafuta wawekjezaji lakini kazi ni ushilikiano sheni mechaguliwa pamoja muachie nayeye kidogo.

    ReplyDelete
  10. watanzania zaidi ya 99% hawana uswezo wa kununua nguo za mark & spencer sasa rais wetu anaongea naye nini???????
    mheshimiwa mjomba ukienda msibani aliyefiwa utamjua,atakuwa avaa......!!! sikufundishi mjomba hizo ni salamu zangu kwako

    ReplyDelete
  11. Tukumbukeni kwamba Jk alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa mda mrefu sasa bado anamazoea na ile kazi yake ya zamani ( habits die hard). Tumpeni mda kidogo, nadhani hatimaye atakumbuka kwamba yeye sasa ni rais wa nchi

    ReplyDelete
  12. ...JK nafikiri kuomba misaada as one of your policy is a very bad idea...naomba ukae home upigane na rushwa maana ndio inaturudisha nyuma na wala sio hiyo misaada....na usisahau kulazimisha pato kubwa la taifa liende kujenga barabara,umeme na mfumo mzuri wa elimu hayo mengine utaona yanabadilika tuu

    ReplyDelete
  13. Michuzi! asante kwa photos za Rais wetu akiwa nchi zaz nje kila siku.

    Je kuna uwezo wa kupata information, inayoonyesha ni nini kinampeleka nchi za nje kila siku? na anachofanya kuna matunda ndani yake?

    Kitu ni kwamba Itabidi labda uombe diary yake toka huko state house tuone ni siku ngapi anakaa nchini? ni siku ngapi anatumia akitembelea nchi za nje? na ni shilingi ngapi pesa za serikali wanatumia kila trip incl. expenses?

    Alikuwa UK last month, ameenda tena this month? Nani ni Waziri wa Finance maana safari hii ya feb kwa nini hawakufanya hayo last month? Na huyo Mama Kikwete na Kuonana na Cherie Blair y hawakuonana last month hapo kwa balozi?

    Mie nimekasirika kuona kuwa Kikwete amekuja kuwa Rais anayesafiri sana na kutokaa nchini. Lowassa yeye anasaidia katika safari gani?

    Maraisi wengi wa nchi zingine huwa hawasafiri sana kwenda hata hiyo LONDON etc kila dakika 3.

    Naomba mtu amwambie Jakaya Kikwete ajielezeeeeeeee, hiyo kutafuta wafanyabiashara ameshakaa chini kuangalia tangu apate uraisi na campaign yake hiyo wangapi wameingia, na kwanini bado anatafuta watu or ni kwamba hajapata or hawaji? labda wanaogopa RUSHWA as yeye RAIS anaonyesha mfano mbaya kila siku hewani wow holiday. Akae atulie matatizo Tanzania bado ni mengi sana na mie ni mkeleketwa ambaye nilikuwa nimefurahia yeye kuingia ila sasa najiuliza tumeleta a YOUNG one kula life?

    Pia nimesahau kuuliza Kikwete anasafiri kwenda Mikoani? Ipi ameshaenda? Amesaidia or ongeza nini huko? Anaenda kila mwezi pia?

    OOOhhhhhhhh anaangalia income ya watanzania kuiongeza? anaongelea nini juu ya poverty? or yeye ni furaha kuona new buildings za maofisi za foreigners ambao hata tax hawalipi miaka 4 ya mwanzo na wananchi hawafaidiki hata maduka yakifunguliwa ni ya bei kaliiiiiiiii

    aaaaggghhh kikwete nina mengi ya kuongea till next time

    NB kama kuna website ya wananchi kupost maoni to RAIS ipost please.

    ReplyDelete
  14. wacha tuone mwisho wake!

    ReplyDelete
  15. Jamani mambo ya "Stop over" hayo akisubiri direct flight kwenda bongo si ametokea Sitokihomu hamna direct flight kurudi bongo ndio maana JK yuko Ukerewe nadhani. Mmmh lakini siku mbona nyingi hata kama ni stop over tangu last week nasikia yupo hapa Ukerewe.

    ReplyDelete
  16. Hivi kwani hakuna direct flight kutoka sitokihomu michuzi?

    ReplyDelete
  17. Stuart Rose (MD wa M& S), aliwahi Kuishi Tanzania alivyo kuwa mdogo, hata alivyopata kazi yake M&S alitoa ahadi kwamba kama akifanikiwa kukuza mauzo ya M&S na bei ya hisa za M&S, na hivi kupata bonus..yeye atoa hii bonus kama mchango katika shule moja Tanzania..na hivi naamini miezi michache iliyopita ilitimiza ahadi hii..bonus ilikuwa kiasi zaidi ya £500,000/=.
    PK

    ReplyDelete
  18. Hata kama JK akipata misaada mara saba mara sabini kama hakuna usimamizi wa hiyo misaada ni bure kabisa. Kwanza mbona hatujui misaada iliyotolewa kununua chakula, idadi yake hatuijui na mchanganuo wake hatuujui. Na hawa wazungu ni bure kabisa, tangia waaanze kutusaidia hamna mtu ambaye yuko serious na kuuliza hiyo misaada kama imeelekezwa kwenye malengo yake. Haiwezekani mfanyakazi wa serikali ukajenga nyumba yenye thamani ya zaidi ya bilioni moja. Ni kwasababu huna uchungu na pesa unayotumia.

    Na hawa wazungu wengi wanatoa misaada ili nao wafaidike kama sio kuleta raia wao ambao ni unemployed kwao ili wakafanye kazi bongo lakini ukimwuliza anachokifanya hajui bali wabongo ndo wanamwandalia kila kitu. Sasa utategemea nini, mtu kama huyo amekuja kufanya nini.

    Tulishakosa moyo wa kitaifa kwani kiongozi akimaliza muda wake bila kufanya chochote watu wanamcheka kuwa yule bure kabisa muda wote kapoteza tu. Lakini nafikiri itafika wakati watz wataamka na kutambua wanavyofanyiwa na kudanganywa na maneno matamu, basi shughuli yake itakuwa pevu--SIKU ZINAKARIBIA.

    ReplyDelete
  19. Bongo nako jua limezidi

    kuna ubaya gani JK akisafiri? baraza la mawaziri wako 40 sasa shida yenu ni nini jamaa kashazoea mara yuko SELFRIDGES mara yuko HARRODS

    at least hana zile skendo za kutuibia mapesa mengi huyu yeye anpenda kuvaa na kusapoti Arsenal na wenye wivu watunyonge

    Naogopa sana kiongozi ambaye hasafiri lakini akiondoka madara kani unashangaa jamaa kumbe ana nyuma 3 CAPE TOWN!

    Bora ku dela na huyu mzaramo mara mia

    ReplyDelete
  20. Huyu jamma anatakiwa akae nyumbani sio kila mara nje tu, hakuna cha maana hapo anachofanya, wawekezaji wenyewe wakipata chance kuwekeza huku wanaleta na watu wao kutoka huko, utakuta katoto kadogo labda kamemaliza shule juzi juzi born in 1983/4/5/6 eti anaajiriwa alafu mbaya zaidi anatake home salary ya ajabu wewe uko pale more than 10 yrs unaambulia zero, what the hell are these labour and immigration people doing?? inauma sana, amkeni jamani tunaingiliwa vibaya, check on these people coming to be employed wana profession yeyote mayayi matupu tena viza.!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...