makande bado yako kwa wingi bongo. mdau wa ughaibuni unakumbuka lini mara ya mwisho kula msosi kama huu?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Aaaah Michuzi si unajua kuwa,msahau kwao ni mtumwa?Huku nako makande yapo ukiyataka au kuyatamani.Ni jana tu nimekula makande ya nazi,ingawa nazi yenyewe ilikuwa ya kopo.

    ReplyDelete
  2. YEE TONIII NETHIMAN JE CHA OKADHEE IKI MICHUZI ETHIMAN JE HENA MAKANDE SEHEMU YOYOTHE AHA AMERIKA AMBU HE MADUKA YA VHAA SPANISHI HENA MAHINDI YALIYOKOBOLEWA.
    USINIKUMBUSHE ILBORU UKANIACHA NINALIA KITEI(WALI NYAMA),KANDE(MAKANDE),KICHUI(UGALI MAHARAGE).
    BINO(MUSHI) NA MZULU(MEDUKENYA) NINAWASHUKURU KWA UONGOZI WENU JAPO WAKATI ULE TULISUGUANA KIDOGO.MTUI ULITUHARIBIA SHULE YETU MAARUFU TZ.

    ReplyDelete
  3. AISEE MICHUZI WE ACHA TU NATAMANI SANA HAYO MAKANDE MARA YA MWISHO NILIKULA MWAKA 2003, HEBU FIKIRIA.

    ReplyDelete
  4. Michuzi unisiambie mambo ya lifti vale yanaleta makande kwenye harusi.Maana hiyo picha inaonekana ni mnuso wa nguvu huo.Soon itakuwa ugali na mahargwe kwenye harusi ukiingia ungonjwa wa mahindi yasiyosagwa kuwa unga.Tuombe Mungu.

    ReplyDelete
  5. Sikujua tooth pick nazo chakula cha kuwekwa kwa sahani. Usinikumbushe housegirl wangu nilimkuta anapiga watoto wangu, kuuliza kisa? Wanamaliza tooth pick, wakichukua wakazitumia hawakumbuki kuzirudisha!

    ReplyDelete
  6. Du mzee michuzi , mimi mara ya mwisho kule kande ilikua 2003, alafu babake yalikua yamepikwa na mpare mmoja hivi, kande limechanganywa na iliki pamoja na nazi, dah! yule mtoto!, tulikombea kila kitu. Dah niya miss kinoma!

    ReplyDelete
  7. Washkaji hayo makande ni kama manjonjo tu ya traditional food zetu kwenye harusi hiyo ambayo ilifanyika malaika house - Cine club na bwana harusi upande ni mpare, wanayeishi na biharusi wake UK. Harusi ilifana!!!!

    ReplyDelete
  8. Michu, Majuu pumzi yako tu kila kitu kipo hata nazi za kukuna kama ukiwa na mbuzi. Of course thanks to immigrants.

    ReplyDelete
  9. Sasa huyo mtoto umemficha ili tusijue kwamba yeye ndo amekula kande nyingi?
    Muweke basi tumwone mrembo huyo akibugia kande

    ReplyDelete
  10. Hizo toothpicks inaonekana ni za kuchukulia matunda na keki hapo. Kazi kwenu!!

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi una roho mbaya wewe. Ndio nini kutumanisha. Mara ya mwisho nilikula makande ilikuwa ni enzi za boarding school Makumira, Arusha. Hahah. Those were the days.

    ReplyDelete
  12. Mtoa Maoni: Anonymous wa saa Monday, February 26, 2007 1:41:00 PM, wewe ni kama housegelo wako! (CHEKA)!

    Tooth picks hizo si za kuchokonoa TU kile kilichoingia na kung'ang'ania menoni!

    Wakati mwingine hutumika kama uma, kwa mfano, kutunga vipande pande vya jibini, vipande vya mayai ya kuchemshwa, vipande pande vya maini ya kuku au ng'ombe yaliyokaangwa ama kuokwa, kadhalika.

    Natumaini hapo pichani tooth picks hizo zinatumika kwa ajili ya vipande vya watermelon kuliko kuvikamata na mikono ama uma! Hakuna ubaya wa kuziweka hapo.

    Watu wengine hula na mikono michafu. Kwa hiyo, tooth picks hizo ni level moja kubwa ya usafi, kiafya.

    ReplyDelete
  13. Aloo avae avae !!!!
    Thela wee !!

    ReplyDelete
  14. thats my Favourite food, boding niliyala hadi basi japo hata hayakuwa yakiungwa vizuri, unajua kuna makande ya njugu pia, wee it taste so nice, makande yangekuwa yanaiva haraka kama wali au ugali yangeipata, but anyway ni chakula cha hamu so huwezi kula kila siku kwani tumbo nalo likijibu inakuwa balaa,

    ila michuzi usiwaringishie watu wa majuu hayo makande kwani nasikia huko vyakula vya nyumbani viko vya kumwaga, nina mafiki huko hasa uk, wanasema maduka ya wahindi na warabu hata tesco na sainsbury, n.k,kuna vyakula vya kiafrica, pia kaona hata unga wa bakhresa toka dar, so kwa mambo ya msosi hawamiss sana,

    kazi njema michuzi

    NB: watu mliosoma shule za moshi mnakumbuka 'makukulu' ni matamu pia, ni kama kande ila mahindi hayakobolewi pia yantiwa magadi, haluuuuuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...