Home
Unlabelled
kp
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
mpachike kingo au lodi lofa pia ktuwekee picha za akina jangala, pwaga na pwaguzi mzee kipara, jongo na onyango
ReplyDeleteKP Mimi naomba nikusaidie kuhusu hili tukio lilotokea siku ya jana kama sio mtu niliosahau Kuhusu kile kikaragosi cha Kuhusu TAASISI ZA KIJAMII MOJA . Mi nadhani ni kweli kabisa inabidi tuanze kupiga Kurunzi huu upande mwingine wa Shilingi kwani mi kuna mambo fulani yanafanyika binafsi yananipa maswali na moja ni hili lilojitokeza hili la matangazo ya wenzetu. Sitaki kuitetea serikali kwamba hakuna wabadhirifu kama wanavyoitwa, ila najiuliza hivi vyama vyetu vya kiraia ni visafi? Hivi tummuuliza huyu mtu wa HAKIELIMU haya matangazo alitengeneza wapi? Je kulitangazwa zabuni ya manunuzi ya kazi Hii? au wanafanyaje wanavyogawa hizi Kazi? Kwani nina wasiwasi na undugunaizesheni au kujuana katika kugawa kazi hizi hasa za USHAURI za Asasi zetu za kiraia. Kama mimi muongo naomba muhusika ajibu hili? Nani anamtengenezea hizi kazi na taratibu gani zimetumika. Kwani tusije tukawa tunaipigia kelele Serikali kumbe na sisi ndo wabadhirifu wakubwa. NAOMBA KUWAKILISHA NA KUFUNGUA MJADALA.
ReplyDeletekaka eeh,najua hii ni out of point lakini naomba utuwekee picha za askari wa jwtz wakiondoka kwenda Lebanon kulinda amani...
ReplyDeleteMimi naona Kp angezungumzia hali ya viongonzi wetu wa kiafika kutopenda kukosolewa, critism kwao, wanaita kejeli na wanachukilia kama dharau, wao badala ya kujibu critism kwa hoja, wanatumia nguvu kumkomoa yule aliye critise. Jamani ukweli ni kwamaba elimu iko kwenye matatizo makubwa mno, watu hawaoni hilo, lakini kwa tathmini yangu binafsi mimi nahisi kuwa pamoja na elimu yetu kutoenda na wakati, inashindwa kutuaandaa watanzania tuweze kuleta maaendeleo ya maana. Kinachotakiwa na serikali kukubali kasoro zilizopo pamoja na critism na kutafuta solutions ambazo zitaweza kubadilisha elimu yetu iwe ya kisasa na bora
ReplyDeleteKipanya,
ReplyDeleteBeba kapu kubwa la kubebea kima cha chini cha mshahara kilichopendekezwa!! maana hizo laki 3.5 hutaweza kuzinyanyua kipanya!!!
procurement act ya mwaka 2004 inaelezea taratibu za manunuzi ya bidhaa na hudumu kwa idara na asasi za serikali.hata hivyo sheria hiyo haizihusu asasi zisizo za serikali wala makampuni binafsi.hivyo basi HAKIELIMU hawalazimiki kutangaza zabuni wanapohitaji kufanya manunuzi.
ReplyDeleteKipanya weka hoja za rais kusafiri kila leo....atulie amuachie na Karume safari zingine na Shein na waziri wa mambo ya nje...
ReplyDeleteAnon02/08-9:06am,
ReplyDeleteWewe anon mimi nahisi unafanya kazi ktk ofisi ya waziri mkuu kama sio ofisi ya raisi.
Hawa haki elimu wametoa vipi hayo matangazo yao hiyo ni biashara yao for as long as they do not use our tax payers' money, I could care less. Sasa basi hii serikali ambayo inatumia pesa yetu, ambayo sisi ndio waajiri wake ndio tunalia nayo. Mimi hapa naadika kwa uchungu kwani mama yangu ni mwalimu wa shule ya msingi (mikoani-vijijini) na hayo yalioandikwa yamemkuta na yanaendelea kumkuta. kwanza kuna kipi cha kuisifia hiyo serikali? Hakielimu-kazeni mwendo na kwanza waziri mkuu hamtamkuta ofisini kwake kwani atakuwa amekwenda airport either kupokea au kumuaga raisi.
Hivi nataka kuuliza huko Brazil Stars wamekwenda bila mwandishi wa habari. Maana hatujui kama wanajifua au wanajirusha tu na vimwana. Tanzania hebu tuache ushamba hebu tupeni habari, picha au hata matokeo. Ushamba huu halafu mnataka misaada.
ReplyDeletesi washamba kivipi, ni jukumu la vyombo vya habari kusafiri au kutafuta habari eg CNN au BBC correspondent. Mashirika yetu ya habari hayana uwezo wa kumpeleka mwindishi kwa kipindi hicho cha mazoezi. Trust me ingekuwa timu ya brazil ipo kambi bongo hata Skysports wangekuwa na mwakilishi wao. We ndo mshamba !
ReplyDeleteKipanya ungejeuza shilling upande mwingine kidogo kwa sasa. Hebu jaribu kuangalia raia wa Tz nao kidogo. Nini wanachangia kufanya nchi iwe ilivyo sasa hivi.
ReplyDeleteKwa maoni yangu ukiangalia tu hawa almost Millioni moja wa huku kwenye blog ya michuzi. Wengi wao ni majungu tu na malalamishi. Hamna mwenye kuangalia picha akaona atleast kitu kimoja kizuri. Kila kitu ni kibaya kwao....Nadhani mind zetu kila siku zinaona a glass is half empty and never half full at all.
Hatutaendelea kama kilichoko machoni kwetu ni kibaya na kukosoana tu. Watu watakua wanaogopa kuwa wabunifu kwa kuogopa kuwa lolote watakalojaribu kufaya lisipokua 100% perfect wabongo hawatalala na watasemaje sana.
Ukitembelea blog za wakenya... wana kiswahili kibaya sana, wana english mbaya tu. Sio wote wanaojua kingereza fasaha. Lakini sijaona watu wanasoma na kuanza kumkandia yule anayechapia kiswahili au kingereza. Wao wanajali ni ujumbe gani ulioko. Kwa watanzania wamekalia kupoteza muda kumkosoa mtu anayechapia kiswahili au anayechapia kingereza. Wakati hawajui huyo anayeandika kiswahili amejifunzia wapi au huyo anayechapia kingereza mwalimu wake alikua ni nani na elimu yake ni gani.
Watanzania tunatakiwa tubadilike kidogo na tuwe na mawazo ya kuona things in a positive side kidogo. Hamna jema machoni kwa mbongo kabisa.....
Inasikitisha na inatia aibu....perhaps we need to change kwa vile majungu bila lolote la maana hayatatufikisha popote
Natofautianna na ndugu yangu Masoud Kipanya katika makala ifuatayo iliyochapwa kwenye Rai ya leo.
ReplyDelete" Nani Anai-DhiHaki Elimu Yetu?
Katuni ya Masoud Kipanya
Mwandishi,
Maggid Mjengwa, Soma zaidi; http://mjengwa.blogspot.com
Kipanya,
ReplyDeleteNaomba uizungumzie ndege "Jet" ya kikwete kwani inasifika afrika kwa " pollute"kuharibu mazingizira kutokana na safari zisizoisha ...
Kipanya ,
ReplyDeleteTafadhali zungumzia sula la kuuzwa nyumba o'bay na jinsi ambavyo zoezi zima lilivofanyika , pia guzia kuhusu wasichana warembo wasio wafanyakazi wa serikali walivyouziwa hizo nyumba pia na baadhi ya viongozi wa chama tawala walivyouziwa hizo nyumba pia
asante sana KP .
Wewe Kp utakosaje chakusema wakati kuna ma-issues kibao yanayokera kama wizi bandarini, tra kusamehe makampuni kodi na wawekezaji bila mpangilio, rushwa, pcb wanakula hela za watanzania hamna wanachokifanya ukilinganisha na mamilioni wanayotafuna wao kama mshahara na marupurupu, watu wanalishwa chips zinazopikwa na mafuta ya transformer, wizi wa vifaa vya magari bandarini, viongozi wala rushwa na wabovu bado wanakumbatiwa katika ngazi mbali mbali za serikali, ACHA KULALA KIPANYA.
ReplyDeletewww.majira.co.tz
ReplyDeleteImetolewa mara ya mwisho: 09.02.2007 0203 EAT
•
Stars yagoma kufungwa Brazili
* Yatoka sare 1-1 na Boavista
Na Benny Kisaka, Rio de Janeiro
TIMU ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) juzi ilitoka sare ya bao 1-1 na timu ya Ligi Kuu ya Brazili, Boavista katika mchezo wa kirafiki uliotawaliwa na ufundi mwingi na kasi uliofanyika kwenye Uwanja wa Portugues Carioca unaomilikiwa na timu hiyo.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilikuwa 0-0, lakini kipindi cha pili kocha wa Stars, Marcio Maximo aliwapumzisha Salum Swed, Shaaban Nditi na Abdi Kassim na nafasi zao kuchukuliwa na Dickson Daudi, Nadir 'Haroub Cannavaro' na Amir Maftah.
Stars ilijikuta ikipachikwa bao dakika ya 52 lililofungwa kiufundi na Douglas Silva kwa mpira wa adhabu aliopiga umbali wa mita 40 uliogonga nguzo ya chini na kumzunguka kipa Ivo Mapunda na kujaa wavuni. Mfungaji huyo aliyekuwa akiisumbua ngome ya Stars, amepata kuzichezea timu za Lo Gremio, Sport na Flamengo.
Goli hilo lilimfanya Maximo aliyesimama dakika zote 60 za mchezo kufanya mabadiliko. Aliwatoa Gaudance Mwaikimba na Mecky Maxime na kuwaingiza Ibrahim Mwaipopo na Jerry Tegete.
Mabadiliko hayo yalizaa matunda dakika ya 58 ambapo pasi ndefu ya Nizar Khalfan ilimkuta Said Maulid aliyewachomoka mabeki wa Boavista na kumlamba chenga kipa na kufunga kwa mguu wa kushoto akiwa katika 'impossible angle'.
Mchezo huo uliochezwa dakika 60 kutokana na mpangilio wake, haukutangazwa jijini Rio de Janeiro ili watazamaji wahudhurie, lakini Maximo alisema anachozingatia ni kupata mafunzo na si matokeo ya mchezo hata kama wangefungwa. Boavista katika mchezo wa mwishoni mwa wiki wa Ligi Kuu ya Brazili ilifungwa bao 1-0 na Fluminense.
Mchezaji anayetawala katika vyombo vya habari Tanzania kutokana na mustakabali wa usajili, Athumani Idd ndiye aliyeng'ara zaidi katika mchezo huo akicheza kama Mbrazili kutokana na kutulia, kutoa pasi za uhakika, chenga na jinsi alivyokuwa akikaba. Mwingine aliyecheza vizuri ni Nizar Khalfan. Wote walicheza safu ya kiungo.
Baada ya mchezo huo, Maximo alisema wachezaji wake karibu wote walikuwa makini kwa dakika zote za mchezo na walicheza zaidi soka badala ya kubutua, walisikiliza vyema maagizo yake.
"Tumekuja kujifunza soka, tupo tayari kwa matokeo yoyote katika mechi zetu za majaribio," alisema Maximo aliyeonekana kufurahishwa na kiwango walichoonesha wachezaji wa Stars katika mchezo huo.
Kocha wa Boavista ambaye ni mchezaji nguli wa zamani wa timu ya Botafogo na timu ya taifa ya Brazili miaka ya 1980,
Gaucho alisema Stars kuja hapa inapata uzoefu wa soka la kiwango cha juu cha Brazili.
Gaucho aliyekuwa beki wa kati akicheza pamoja na Zico, alisema Stars wameonesha kupiga hatua endapo dhamira yao wataiendeleza kwa kasi waliyonayo.
Maximo alimtambulisha kocha huyo kuwa ni miongoni mwa makocha wa viwango vya juu Brazili na amepata kuwa kocha wake mkuu, wakati huo Maximo akiwa mmoja wa wasaidizi katika benchi la ufundi la Botafogo anayoishabikia.
Aliyepata kuwa kocha wa Simba, Neider dos Santos alisema hakutarajia kuona Stars ikicheza hivyo au kutoka sare na timu ya Ligi Kuu Brazili.
"Hiki hakikuwa kiwango cha Stars, wamecheza vizuri sana na hii inaleta picha nyingine katika kiwango cha soka Tanzania, nimevutiwa wanavyojipanga, wanacheza kwa kasi na kujiamini ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa majaribio.
"Sikutarajia kama wangetoka sare na hii wakiwa hawajatimia, hakuna Victor Costa wala Henry Joseph ambao wapo kikosi cha kwanza, wanastahili pongezi," alisema Dos Santos aliyekuwa mmoja wa mashabiki wachache waliohudhuria mchezo huo.
Kabla ya mchezo kuanza Dos Santos alisalimiana na wachezaji wote wa Stars ambayo mchezo mwingine wa majaribio itacheza Jumanne dhidi ya timu nyingine ya Ligi Kuu ya Nova Iguazu (Nova Iguacu).
Stars ilipangwa hivi: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Mecky Maxime/Ibrahim Mwaipopo, Hamis Yusuf, Salum Swed/Dickson Daudi, Shaaban Nditi/Nadir Haroub, Said Maulid, Athuman Idd, Gaudence Mwaikimba/Jerry Tegete, Nizar Khalfan na Abdi Kassim/Amir Maftah.
MZEE WA BARE.