
malkia wa taarabu aliepata mafunzo toka kwa malenga siti binti saadi, bi. kidude baraka, akiwasili ngome kongwe tayari kwa sauti za busara mwaka juzi.
nabandika insha hii fupi ya picha kumuenzi bi. kidude ambaye amepeperusha sana bendera ya bongo nje ya nchi kwa miongo kibao, na hadi sasa ambapo ana umri wa zaidi ya miaka 80 anaendeleza libeneke, ingawa nasikia afya yake safari hii kidogo inasumbuasumbua...
kesho tamasha la nnne la sauti za busara linazinduliwa rasmi na waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. muhammad seif khatibu na zaidi ya vikundi 40 toka ndani na nje ya nchi vitatumbuiza wiki nzima hapo ngome kongwe.
filamu ya bi. kidude inatarajiwa kufungua dimba la tamasha hili ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa biashara ya utalii visiwani na bongo nzima kwa ujumla.
tamasha hili litafungwa rasmi huko kendwa beach siku ya wapendanao kwa burudani ya usiku kucha katika kukazia ule usemi wa waandaaji wa 'hakuna kulalaaaaaaa!'
kiingilio ni bure kati ya saa 12 jioni hadi saa 2 usiku ambapo baada ya hapo inabidi utoe kitu kidogo. panapo majaaliwa nategemea kuwa huko wiki nzima hivyo stei tyuund...
kwa khabari zaidi bofya www.busaramusic.com
NAOMBA KUELIMISHWA HUYU NANI, MIE NIKO CANADA.
ReplyDeleteNA NI KABILA GANI,:? MNYAMWEZI NINI, ANA SURA MBAYA HIYO.
Tuekee basi kavideo clip kidogo ka huyu malkia. Inaelekea watu wanafaidi sana. Sasa hata sauti au kitu kidogo. Kam vile ulivyotuwekea jiji la musoma sijui mwanza kule wakila samaki wasio na minofu vile basi nadhani unaelewa ninachoomabapoa basi
ReplyDeletenatanguliza shukurani kwa yote unayotuwekea huku.....
Duh! Ila mbaya sio utani. Mbona hana viatu?
ReplyDeleteSELEBRITE WETU HAPO NDO KAPOZI ANAPITA KWENYE RED KAPETI TIHIII TEHEHEEEEE.... KEEP UP GOOD WORK BI KIDUDE...
ReplyDeleteLOVE YAAA YIP YIP YIPPPPPPP HUREEEE
INASIKITISHA SANA KUMWONA HUYU BIBI YETU AKIWA KATIKA HALI HII. Hao wanao andaa hayo matamasha nafikiri wanaangalia kujaza mifuko yao na sioni kama watakuwa wa msaada sana kwa huyu bibi. Wakati kukiwa na function ndio wanatafuta hawa mabibi lakini baada ya hapo ni kwaheri. Utashangaa anachokifaidi kwenye hili tamasha/busara.
ReplyDeleteNYI MNAOSEMASEMA MAMBO YASIOELEWEKA! hivi nyie hamjui vibibi kama hivi shauri yenu kama hamjavimba midomo.
ReplyDeletehuyo anaitwa BI KIDUDE
ReplyDeletenaona michuzi blog yako imejaa watindiga
sasa fanya mipango kesho uposti picha ya SHAABAN ROBERT
utaona watakavyo kuuuliza hivi ni nanii eeeh?
Nilipokuwa kijana nilipata kuwa na mpenzi wa Kiingereza mwenye asili ya Kiyahudi. Moja ya fasili alizonipa ambayo mpaka leo naikumbuka ni fasili ya neno la Kiingereza CUTE. Fasili yake iliyonipa: Cute means ugly but interesting!
ReplyDeleteBi Kidude anafanana na ile fasili aliyonipa mpenzi wangu wa ujanani!
Masalaamia.