jk akiwa na wadau wa boston pamoja na hasheem thabeet mwaka ulopita. chini kuna mdau kaniletea ujumbe wenye usongo na link kibao juu ya hasheem. ikumbukwe jk alipoongea na hasheem akimshauri sana aweke masomo mbele na mchezo na mengine yafuatie. nafurahi kuona dogo amefuata ushauri huo na kurejea skuli na kuendelea na kitabu. hongera sana hasheem. na wala usikatishwe tamaa na maneno ya watu - maji ya moto hayachomi nyumba!!!!


Hii habari ya "National Hero" ndio naisikia sasa. Kila mtu anamzungumzia Hasheem Thabeet ni kweli ama zugazuga tu ndio tumzungumzie kama ninavyofanya hapa?
Kwenye blogu ya Michuzi na group discussion ya TanzAlt wanamtukana Hashim mpaka unajiuliza ni wivu ama ni kweli wanamfahamu kwa ubaya hivi? Watoe basi wazo la kumshauri arekebike, wapi!
Tz kuna watu wana haka ka mtindo kachafu sana na kakupinga kwa nguvu zote ka watu wenye roho kutu na mbaya wa kuoneana wivu wa kizembe na kuzibiana na kupakana matope pale wanapoona mtu anapong'ara na kufanikiwa. Sijui (tuna?)wana matatizo gani.
Ndio sababu mojawapo kati ya nyingi ya kwanini (hatu?) hawandelei. Ukitaka kumwona pichani ni mrefu kuliko wote, tizama: http://www.uconnhooplegends.com/images_mensteam06-07/TeamPicture.jpg



Wasalaam, Subi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Michuzi huyo mshikaji aliyevaa kakhi suruali na shati msikaji wangu wa siku nyingi Feruz tuwasiliane kaka tuwasiliane ndugu yangu maana tangu mitaa ya Ada estate mpaka chuo tumesoma pamoja enzi hizo siku kibao. wasalimie Boston

    ReplyDelete
  2. Hakuna mtu anayewaza wala kumzungumzia Hasheem. Kafanya nini la maana kuwa National Hero wa Tanzania? au labda sababu alikutana na Kikwete ambaye kashindwa kuendesha nchi. Huyu jamaa anasoma kwa kutumia Student Viza, kitu ambacho kinamuweka mguu mmoja ndani/nje. Kuna wabongo wengi ughaibuni wamesoma na wana nyadhifa kubwa kubwa. Itakuwa Hasheem!

    ReplyDelete
  3. Nimesoma mambo ya Hasheem ktk mtandao uliotoa. Sasa Subi usisumbuke sana, unachohitaji ni kujikumbusha ile methali isemayo "Nabii hapendwi ................."

    Wabilah Tawfiq!!

    ReplyDelete
  4. UAMUZI MZURI HASHEEM,
    MWAKA KESHO BEI YAKO KULE NBA ITAKUWA JUU ZAIDI. JIJENGE KWANZA KIMCHEZO, HUWEZI JUA BWANA UNAWEZA KUWA NO 1. PICK!!
    BRAVO!!!

    HAYO MANENO YA WENYE ROHO YA KUTU USIYASIKILIZE

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli wewe mdau uliyetoa hii Hoja ya watu kumponda Hasheem umenena tena kwa sauti ya busara. Yaani sisi wabongo sijui tumelogwa, yaani mtu akifika Mamtoni basi ndiyo anajiona amemaliza na kuona wengine hawana nyimbo. Mimi niko hapa ulaya naona wenzetu kutoka kama Nigeria walivyo na ushirikiano na kuanzisha makampuni mbalimbali yakuhakikisha wanasaidiana na kuisaidia nchi yao. Lakini sisi Watanzania ukifika ulaya kilichopo ni kuchonga tu kama tulivyorithishwa, yaani mpaka inakera. Kuna vijana wengi sana TZ kwa sasa wanaweza kucheza mpira Ulaya, ila hakuna connections,hakuna hata Mtanzania aliyejitokeza na kuwasaidia hao wenzetu kama watu wa Nigeria. Kwa kweli jamani watazanzia tuache roho mbaya, hivi tuna roho za aina gani, huu utanzania tunaolingia uko wapi. Mimi nilikuja hapa Ulaya kusoma mwaka jana, nilikutana na watanzania cha ajabu walinikimbia mpaka leo hatuonani, ni kitu ambacho ninashangaa mpaka leo, kwanini wananipiga chenga, badala ya kunisaidia na ugen wangu, ikabidi wakimbizi wanaishi huku wa kutoka Rwanda na Congo ndiyo wawe wenyeji wangu. Kwa kweli inasikitisha sana.

    by GAZ

    ReplyDelete
  6. There can be only one Subi to write this!!!
    Much love from London
    John K

    ReplyDelete
  7. Wee annon wa 4:55,watanzania wanasaidiana ila wengi tunaangali unayemsadia anakuhusu vipi?huwezi saidia mtu ambae humjui eti kwa kuwa ni mtanzania tu,WHY,kwa sababu wengi wenu mkisaidiwa ndo baadae wajanja kuliko hata aliewasaidia ndo maana watu wengine wanaingia mitini kwa nini ujitafutie matatizo na mtu ambae humjui eti kwa kuwa ni mtanzania?Wanigria wanasaidiana kwa kucheck huyu ni Ibo,yoruba,fulani kwa sababu they have something in common hawasaidiani eti kwa kuwa wote wanigeria nooooo.

    ReplyDelete
  8. watu wanaongelea mambo ya hasheem,we unaongelea mambo ya kukimbiwa? ulikuja nani?kama sio peke yako,times is money jali yalokuleta kila mtu na mzigo wake,waache kufanya mambo yao wakuangalie wewe? wapi kwenu wewe? ndo ulijue jiji Aloooooooooo!

    ReplyDelete
  9. Watanzania na watu weusi wamejaa wivu. Hatutaki kuona moja wetu ana endelea. Mwacheni kijana wa watu!

    ReplyDelete
  10. Jamani, mbona tunapoteza muda kuwasaga watu bila sababu. Tunabidi kuwapa moyo wenzetu wanapofanya jambo la kuletea sifa nchi yetu. Tuwache ulibukeni na wivu usio na maana. Nyie mnaosaga wenzenu, je umeshafanya lipi la maana la nyie kupewa sifa? Grow up you Tanzanians, and stop being a ignorant. Huyu kijana anakwenda shule na kucheza basket ball. Niko sure nyie mnao sanga hata shule hamuendi. So stop your mambo jambo and focus on something positive. Hasheem, Aluta continua. Keep up the good work. Focus with your goals. Forget about the ignorants.

    ReplyDelete
  11. Kumradhi wajameni ni Hasheem Thabeet au Hashim Thabit? au ndio ku americanise mambo ya kina Rasheed, Jamaal, Shareef?? anyway ni majina ya kiarabu tu bado, bottom line.

    ReplyDelete
  12. We anonymous wa 28 April 8:45, hizo ndizo tunazosema ni roho mbaya, huyo bwana naamini alipokuja kusoma huku hakutegemea kupata msaada wa aina yoyote kwa watanzania atakaokutana nao, lakini ukienda ugenini kwa hali ya kawaida ukikutana na watu wa kwenu bila kujali kwamba ulikuwa unawafahamu toka TZ ni jambo la furaha na kufahisha, msitegemee kwamba mtu kutoka TZ aizoee Ulaya kwa mudamfupi, lazima ategemee wenyeji wake kumuelekeza. Sasa kama wenyeji wenyewe ndiyo wenye akili kama yako basi ndiyo hiyo roho ya kwanini. Nafikiri hata huyo dada aliyefariki Ugerumani, alikuwa na urafiki na watu wa Kenya kwa sababu ya roho za ajabu kama hizi. Bila kujali umetokea upande gani wa Tanzania ukija huku lazima tukusaidie. Msiwe na roho za kutu bwana.

    Rahma (Ukraine)

    ReplyDelete
  13. Hasheem, Hasheem, tushamchoka bwana michuzi, trip hii tutafutie akina emolo bwana Ah!

    ReplyDelete
  14. Nakusoma George (GAZ). Pole sana. Umemwona nduguyo Chris Mwakapyusa? hapo?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2007

    Eee bwanaee hii ya leo kali, we anonymous 30 April 2:54 sikutegemea kama ungegundua jina langu. Anyway hakuna shida, Chris namuona tu mwenyewe kanuna ka nini. Mimi napatikana kwa gzumba@gmail.com naomba tuwasiliane.

    GAZ

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2007

    kwanza huyu dude siye mtanzania kabisa hatuna mtu ngongoti kama huyu acheni zenu nyie kutu changanya vichwa vitu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 02, 2007

    Huyo GAZ nimekaa naye ulaya bahili kama nini.Eti alifika ukimwambia mchangie mfano kulipia chumba hataki anasema yeye mgeni tumpe nafasi ajijenge kwanza kwani sisi wengine tulikuja huku Ulaya kuja kujibomoa? Kazoea kula kulala Tanzania akifikiri na huku Ulaya tutamwendekeza nyoooo! Huku haendekezwi mtu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 16, 2008

    Hi ka'Michu. Mi mdau wako mkuu niko ughaibuni. Nimesikia mengi kuhusu m'Tz mwenzetu Hasheem Thabeet. Please tunaomba utukusanyie habari zake uzipublish. We are so interested in him. Please usibanie this is important.
    We appreciate your work! Keep it up and may God be with you!
    HT.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 16, 2008

    ka michuzi mbona habari za hasheem unazibania? Please bring us more about him.(his news and pictures). We are so proud of him. Please ombi usiliweke kapuni.
    mshabiki.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 16, 2008

    Ka michu mbona hasheem thabeet umempoteza? hujambandika kwenye blog yako siku nyingi! kulikoni?
    mkereketwa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 16, 2008

    Hallo michuzi. can you give us more about hasheem thabeet plz! i am so excited about him. I hope ombi langu limepokelewa na litatendewa kazi. i trust you.
    bye!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 16, 2008

    Hasheem Kapotelea wapi sku hizi. Usibanie watu bwana.
    faza celeb.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 16, 2008

    Bro michu, we want more about hasheem thabeet. what is he doing now? did he enter the draft. We need to know more about the guy. He's my no 1 fan. plz publish news and picha zake.
    pkz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...