kuna madau aliye ughaibuni kaomba nimtundikie hapa maoni yake.
mambo vipi?
aisee nashindwa kuweka commects kwenye blog yako kwa muda sasa. nikisign in napata msg kuwa password is incorrect na nikitaka kutuma kama anonymous pia zinakataa.leo nilikuwa najaribu kuweka ujumbe kwenye picha ya tangazo walilowekeana the so called wasomi wa mlimani juu ya mgomo wao.nimeshindwa kuvumilia bila kuwasilisha feelings zangu hizi.kwa kweli hili swala linanisikitisha sana.kama inawezekana naomba nining'inizie comment hii.
hawa watoto ni wafupi sana wa mawazo.mwandishi wa huu upuuzi inaelekea nyumbani kwao mambo safi,yeye mwenyewe anasema "tutaenda kujisomea kwa raha nyumbani"hajui kuwa kuna wenzake kuja chuo ni njia muafaka ya kukimbia shida za nyumbani.huu upuuzi sijui utaisha lini kwenye vyuo vyetu.samahanini kwa lugha yangu imebidi niitumie tu kwa sababu nimekasirika sana na nisipoandika lugha kali labda nitavunja kioo cha hii computer kuondoa hasira.mimi najua wanafunzi kibao waliomaliza form six wanafundisha mjini tuition kujipatia kipato wao wako chuo kikuu wanashindwa kuimprovise???kwa hali hii hata wakisomeshwa hawana manufaa yoyote kwa taifa.
otherwise mambo hapa bomba tu.naendelea kuisikilizia mitandao uliyo jikoni.
cheers.


Wanaosema huku majuu migomo haipo wasome hapa! Too much mabox hata hamjui yanayotekea kwenye academics!!
ReplyDeletehttp://en.wikipedia.org/wiki/2005_Quebec_student_strike
http://www.wsws.org/articles/2003/oct2003/uni-o22.shtml
http://www.haaretz.com/hasen/spages/846646.html
http://www.boston.com/news/world/europe/articles/2006/03/23/french_student_strike_shows_deep_worries_over_jobs/
sasa tatizo ni hao watoto wafupi wa mawazo au huyo mwandishi?
ReplyDeleteHIVI MBONA WATU WANATOA MAONI KWA HASIRA HIVYO? HAO WANAFUNZI WANA JINGINE WALILOWAKOSEA AU NI HILI LA KUGOMA TU? SIAMINI.
ReplyDeleteJE,WOTE TUNAOTOA MAONI HAPA TUMEWAHI KUSOMA MLINANI,MZUMBE,MUHIMBILI,SUA AU UCLAS TUKAONA HALI HALISI YA HUKO VYUONI?
TUNALIJUA PATO LA MTANZANIA WA KAWAIDA(AMBAPO 80% NI WAKULIMA)? GNI per capita: US $340 (World Bank, 2006) -SOURCE:http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/country_profiles/1072330.stm
PIA TUFAHAMU KUWA NCHI HAITAENDELEA KAMA SERIKALI HAITACHUKUA HATUA ZA MAKUSUDI KUWAKOPESHA WANAFUNZI WOTE WASIO NA UWEZO WA KUJILIPIA.WENZETU KENYA WANALIPIWA 60%(BUREEE) NA SERIKALI NA WANAKOPESHWA ASILIMIA 40%.
WATANZANIA WANADAI TU WAKOPESHWE 100%KAMILI (SIO BURE KAMA 60% BURE WALIPIWAZO WAKENYA NA SERIKALI YAO).KIKWETE ALIAHIDI ATAFANYA HIVYO BY THIS APRIL ILA KIMYA KIMEENDELEA;NAHISI ALIKUWA ANATAKA WAFANYE MITIHANI WAENDE TEACHING PRACTICAL/PRACTICAL TRAINING BILA AHADI KUTIMIZWA ILA KUTENGENEZA "PRECEDENT" YA KUWAKANDAMIZA WANAFUNZI KWA MIAKA IJAYO.
SIJUI TUNAELEKEA WAPI JAMANI.MIMI NINA MASTERS YANGU NA NAKULA MAISHA TU HAPA U.K(NA NAJUA WENGI TULIOKO HUKU UGHAIBUNI TUNA ELIMU ZETU NZURI,PESA AU KAZI) LAKINI TUNAWAFIKIRIA VP HAWA VIJANA WETU AMBAO NDIO WAJENZI WA NCHI WA KESHO? ELIMU ZETU PEKE YETU ZITAWEZA KUISAIDIA NCHI KUONDOKANA NA UMASKINI? AU HATUPENDI WENGINE WASOME KAMA SISI?
TUACHE UBINAFSI KTK KUTOA MAONI NA TUANGALIE MASLAHI YA NCHI YA BAADAE.HIVI KAMA MZAZI ANASHINDWA KULIPA GHARAMA ZA KUMPELEKA MTOTO A-LEVEL(ADA TSH 70,000 NA GHRAMA ZINGINE YAWEZA KUWA KAMA 200,000 KWA MWAKA) ATAWEZA VIPI GHAFLA KUMUDU 40% YA ADA YA CHUO KIKUU AMBAPO KWA BAADHI YA KOZI SIO CHINI YA 1,000,000?
NAWAPA POLE HAO NDUGU ZANGU NA INANIUMA KWAMBA TUNAENDA KUMEZWA KTK EAST AFRICAN FEDERATION NA WENZETU WENYE POPULATION NDOGO ILA WANA WASOMI WENGI.NAJIULIZA PIA,HIVI NIKIFURAHIA HAO WANAFUNZI KURUDISHWA NYUMBANI AU KUFUKUZWA KABISA CHUO NITAFAIDIKA VIPI?
NAHOFU NKIRUDI NA BMW YANGU NA MALI ZINGINE HOME HAO WANAOSHINDWA KUSOMA KWA KUKOSA ADA WANAWEZA KUNIPORA-NAHISI WANAWEZA KUGEUKA MAJAMBAZI AU MAGAIDI.LAKINI NISIPORUDI HOME SI NINA JAMAA ZANGU KIBAO NYUMBANI,HAWATATHIRIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KWA KUISHI KTK NCHI YA WATU MAMILIONI WASIO NA ELIMU?
WENZETU WADAI WAKOPESHWE PESA ZAO(WANAZOLIPA KODI MABALIMBALI IKIWEMO V.A.T 20%)NA SIO WAPEWE UPENDELEO AU BURE NA SERIKALI.
WACHA NIENDE ZANGU KIBARUANI SASA NISAKE POUND.POLENI WANAVYUO WA TZ.
NAOMBA KUWAKILISHA;NI MTIZAMO TU-MASELA TUSIJENGE CHUKI NA TUHESHIMIANE!
Ninachoelewa wanafunzi wa UDSM wanaona mbali. Unaposema kuwa kuna watu wanakimbilia university ili kukimbia shida za nyumbani, basi si walipwe asilimia 100 na wasirudishe kwa serikali pia ili waishi kwa raha chuoni. Pia, kama unavyoafiki kuna watoto wa wasio na uwezo, sasa nani atasoma. Kila mtu ana haki ya kusomeshwa bibie. Madeni nchi yetu imefutiwa, hela ziko wapi? Serikali ya kishkaji hii.
ReplyDeleteDuh hii kazi kweli kweli sasa wa wa sokoine nao wamefukuzwa wacha warudi home wakaoshe vyombo
ReplyDeleteSikubaliani na maoni uchwara na pumba za huyo boss aligomewa kulogin. I think hata PC yake iligundua uchafu aliotaka kuandika ndo maana ikawa inamkatalia. Sijui kama anajua kuna wanafunzi wangapi wanatoka Dar au mijini na wangapi wanatoka vijijini ambako hakuna hata hizo primary za kutoa tution. The issue here ni kwamba hakuna source of income vijijini ambako majority we are coming from. Am very sorry to the poor Tanzanians.
ReplyDeleteMisupu watu wakikutumia uchafu kama huu wa jamaa MDAU wako usituwekee hapa.mimi hapana mwelewa kabisa huyu mdau wako ipo taka nini!! hii ndo ili nduu iposema "mtaka cha uvunguni nyenyua matanda".
ReplyDeleteMimi kama mpita njia nafikiri wanafunzi wa Mlimani wanaona mbali wanaona vitu vilivyopigiwa kelele miaka ya tisini ikashindikana. Tanzania inaelekea kufutika katika ramani ya dunia. Bila elimu, wakati watu wanawekeza kwenye siasa mnafikiri tutafika wapi? Kuwekeza kwenye Rushwa, Ukimwi, magonjwa mbali mbali hata technologia hakutakuewa na maana kama watu hawana elimu.
ReplyDeleteLeo hii hata na wawekezaji wanaogopa kuwekeza katika nchi ambazo elimu yao ni duni. Ndio maana wewe uliyeko ugaibuni utapata shida kuleta mwekezaji wa maana Tanzania, labda kama ni wa kufagia barabara. Uliza kama unataka kumpeleka Kenya, South Africa kamwe hautapata shida.
Nilitegemea leo hata wabunge watoe msimamo mkali sana katika suala zima la Elimu, lakini kama mbunge mmoja alivyoseama juzi juzi nafikiri hakutakuwa na kitu cha maana.
Boss aliyeshindwa kulogiin nafikiri kwa wale wanadini na wanasaikologia wanaweza kujua tatizo lake
Vyuo Vikuu...ni ubabe tu!
ReplyDelete2007-04-18 16:07:02
Na Waandishi Wetu, Jijini
Baada ya Serikali kuamua kuwatimulia mbali wanafunzi wote wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vitivo vyake hadi hapo watakapowatangazia baadaye, hali ya ubabe imeendelea kushika nafasi yake ambapo sasa, wanafunzi nao wamecharuka na kuamua kujipanga kivingine kuhusiana na hatma yao.
Madenti hao ambao hadi jana saa 12:00 jioni walitakiwa wasionekane kwenye maeneo ya chuo, wamepanga kukutana leo ili kujifua upya.
Taarifa za awali zinasema katika kikao hicho, wanafunzi hao wataamua ama kujibu mapigo ya Serikali au kusalimu amri mbele ya uamuzi huo mzito.
Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini, TAIROSE, Bw. Bruno Mingo, amesema viongozi wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Dar watakutana leo ili kutoa uamuzi wao kuhusiana na kitendo cha Serikali kuwasimamisha masomo.
``Tutajadiliana leo kwa pamoja kuhusiana na hatua ya kuwasimamisha kwa muda usiojulikana wenzetu,`` akasema Bw. Mingo.
Amesema hatua ya kukutana kwa pamoja inatokana na vyuo vyote kuguswa na maslahi yaliyosababisha kugoma kwa wanafunzi hao kabla ya Serikali kuwatimua.
``Sisi bado tunaendelea kuingia darasani lakini kikao cha leo ndio kitatoa msimamo kama mgomo uwe wa nchi nzima ama la,``akasema Mwenyekiti huyo.
Amesema vyuo vitavyoshiriki katika majadiliano hayo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo kikuu kishiriki cha Sayansi na Tiba (MUCHS), Chuo Kikuu kishiriki cha Usanifu wa Majengo (UCLAS), Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni.
Vingine ni Aghakan , Dk. Kairuki, IMTU, Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere,Taasisi ya Uhasibu Nchini (TIA) na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Nchini.
Jana, baada ya wanafunzi kugomea asilimia arobaini wanayotakiwa kutoa kwa ajili ya kugharamia masomo yao na kisha Serikali kupitia uongozi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam kutoa uamuzi wa kuwatimua hadi watakapotangaziwa, hali ilikuwa ya mshikemshike kwa wanafunzi wote waliokuwa hosteli.
Katika kampasi kuu ya Mlimani, wanafunzi walionekana kwa makundi wakifungasha mizigo yao `fasta-fasta` na kuondoka eneo hilo ili kukwepa tishio la kutembezewa virungu na mabomu ya machozi toka kwa askari wa FFU.
Hali ilikuwa hivyo pia katika hosteli za Mabibo na kwingineko ambapo ilipofika mishale ya saa 12:00, wengi walikuwa tayari wameshatimua na kwenda kujibanza majumbani kwao, kwa marafiki, ndugu na jamaa.
Baadaye, taarifa zinasema askari wa kutuliza ghasia, FFU, walitinga na kukagua huku na huko hadi wakati wa giza totoro, wakiangalia kama madenti hao wametii agizo la kuondoka kwenye `anga` za Chuo.
Ukiachana na Block F ambalo hukaliwa na wanafunzi wa shahada za juu na pia wanafunzi wageni, majengo mengine ya kuanzia Block A hadi E pale Mabibo yalikuwa hayana tena wanafunzi hao ambao wengi walishatimua zao.
Wakati akitoa uamuzi wa kuwatimua wanafunzi hao jana, Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema hatua hiyo inatokana na uamuzi wa bodi ya chuo ambayo ilitoa muda kwa wanafunzi kuacha mgomo na kurejea madarasani lakini wakakaidi.
Vyuo hivyo ni kampasi ya Mlimani, UCLAS, DUCE, MUCE, Chuo kishiriki cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, IJMC.
Wanafunzi hao wanapinga kulipa asilimia 40 ya ada ambayo wanatakiwa kuchangia, wakitaka Serikali iwakopeshe kwa asilimia 100 kwa sababu wengi wao wanatoka katika familia masikini na kamwe hawawezi kujigharimia kiasi hicho.
Wakati huohuo, baadhi ya wanasiasda wa upinzani nchini wamelaani vikali hatua ya Serikali katika kuwatimua wanafunzi hao na kudai kwamba wako mbioni kuiburuza Serikali kortini.
Wakizungumza na Alasiri leo asubuhi, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia amesema kitendo hicho cha kufunga chuo na kuwapa wanafunzi muda wa kuondoka ni cha uvunjwaji wa haki za binadamu.
Akasema pia kitendo cha wanafunzi hao kutimuliwa huku wakiwa na hoja za msingi kwenye madai yao ni unyama na ukatili mkubwa.
Amesema wanafunzi hao kukusanyika kwenye ukumbi wao wa Nkurumah na kubadilishana mawazo ni haki yao ya kikatiba na wala hawakuvunja sheria yeyote.
``Wanafunzi hao wanayo haki yao ya kikatiba ya kubadilishana mawazo. Hawakuvunja sheria yoyote kwa kukusanyika pale Nkrumah... lakini hatua ya Serikali ya kufunga chuo na kuwapa muda waondoke huku wakijua baadhi yao hawana ndugu Jijini Dar es Salaam ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,`` akasema Bw. Mbatia.
Aidha amesema kuwa tangu jana usiku amekuwa akiwasiliana na wanasheria mbalimbali ili kuona uwezekano wa kuiburuza Serikali kortini ili iache manyanyaso hayo na kutekeleza madai ya msingi ya wanafunzi.
``Serikali isifikiri kwa kufunga vyuo hivyo inawakomoa wanafunzi, wanaoumia ni wananchi ambao ndio walipakodi, nawasihi wawarejeshe chuoni haraka, `` akasema Bw. Mbatia.
Naye Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augustino Lyatonga Mrema, ameeleza masikitiko yake kufuatia uamuzi wa Serikali kuvifunga vyuo hivyo, akisema hakuna utawala bora unaozingatia sheria.
``Mimi niliwahi kusema wakati wa kampeni kwamba CCM hawana tofauti, kazi inayofanyika hivi sasa ni kuonyesha umma kwamba CCM hawataki kukosolewa,`` amesema Bw. Mrema.
Bw. Mrema amesema madai ya wanafunzi ni ya msingi na wala hakukuwa na sababu ya kuwatimua, akisema kwamba madai yao ni sehemu tu ya ahadi ambazo Serikali ya awamu ya nne ilizitoa kwa wananchi.
``Nimesikitishwa sana, juzi juzi nimewaona wanafunzi hao wakiimbishwa wimbo wa CCM, sasa leo urafiki huo umekwisha na sasa wanafukuzwa, au sio chuo hiki ambacho Rais Jakaya Kikwete amewapa ahadi hiyo yeye mwenyewe,`` amesema Bw. Mrema.
SOURCE: Alasiri
Mi nadhani wale wote mnaowalaani wanafunzi hamjawahi kusoma huku mkiwa na njaa, Ni ngumu mno, hakiingii kitu kichwani. Leo sitaongelea overspending ya serikali yetu kwenye masuala yasiyo na lazima Ila ni aibu kubwa kwa wanafunzi kuhahidiwa fedha ndogo halafu KIMYAAA kama vile ahadi haikutolewa! Kwanini uongozi wa chuo usimpigie simu J.K kuhusu ahadi yake kabla ya kufukuza wanafunzi? Hawa watoto hata nauli ya kuondoka hapo chuoni hawana. Sijawahi kusikia per diem za viongozi wa serikali zikicheleweshwa. Wabunge wetu nao wanatia aibu na huruma, inaonyesha wazi kwamba wao wapo tu kwa ajili ya mlo wao tuu. Hii njaa hii!
ReplyDeleteMimi nashindwa kuwaelewa jamaa wanaokandia mgomo wa UDSM. Bila kujali uwezo wa mzazi au mwanafunzi kiuchumi, serikali inajukumu la kumsomesha kila mtanzania anayefaulu kujiunga na degree ya kwanza. Hiki ni kitu ambacho hata viongozi wenyewe walipata na ndiyo maana wale wa masters wanajisomesha na hawafukuzwa. Hivyo jamani kokote huko mliko "Tanzania inawajibu wa kuwasomesha hawa vijana bila kujali uwezo (maskini au tajiri) familia ya mwanafunzi." Kwa maana hiyo mgomo ni halali kama kulikuwa kuna ubabaishaji wa kutekeleza makubaliano "Solidariry is the power for the underpreveleged"
ReplyDeleteZumba's
mbona kila mtu anammwagia lawama JK,swala la bajeti ya nchi ni swala la bunge.wakati makadirio ya matumizi ya wizara ya elimu ya juu inapitishwa vijana hawa walikuwa wapi?mbona walikaa kimya tu ikapitishwa.mabadiliko yoyote wanayotaka sasa kikatiba inabidi yasubiri bajeti ya mwakani.
ReplyDeletemimi ndio nilioandika hii comment.sasa nimefanikiwa kupost moja kwa moja.haikuwa haja yangu kumsumbua michuzi,ila swala hili nimeshindwa kulivumilia.watu wanaandika hoja kama serikali ni lazima iwawezeshe wananchi kusoma elimu ya juu kwa asilimia 100.tujiulize maswali ya msingi:je serikali inapaswa kuwawezesha wanafunzi wa ngazi ya chuo kikuu peke yao?je serikali inapaswa kuwezesha wananchi katia sekta ya elimu tu?ukweli ni kwamba resources ziko limited na tunapaswa kuzigawanya katika hali inayofaa.kuna anayeweza kutaja any social group nchini ambalo linaridhika na huduma linayopewa na serikali.sasa tujiulize,iwapo kila atakayeona hajaridhishwa basi aanzishe boycot.nchi itakuwa wapi?halafu lazima tukumbuke kuwa migomo kwenye vyuo vyetu ni tabia ambayo ni kama ugonjwa sugu.sio tu kwa ajili ya kukopeshwa ada,hawa hata wangepewa ada wangekuja na sababu nyingine ya kugoma.nakumbuka kuna kipindi wanafunzi wa SUA walialikwa kwenye semina ya wiki mbili,wiki moja ilipoisha tu wakagomea semina.can you imagine!hii migomo tusiwe tunaichekea na kuitetea,tabia hii ndio iliyosababisha watu kupoteza maisha muhimbili kwa sababu kuna mtu anataka alipwe milioni!!!halafu kuna kudanganyana baina ya hawa wanfunzi eti solidarity,hiki ni kichekesho tu.solidarity ya kweli ingekuwepo wale wanaoweza kujilipia ada wasingeenda kuomba mkopo ili wasio na uwezo ndio wakopeshwe.kuna wanafunzi wangapi walikuwa wanalipa ada kubwa zaidi sekondari kuliko hiyo ya chuo na bado wanaomba mkopo na kugoma.nchi haiwezi kujengwa kwa tabia za kilafi na kibinafsi,nchi inajengwa na kizazi kilichokuwa tayari kutaabika kwa ajili ya vizazi vijavyo.zemarcopolo
ReplyDeleteTAFADHARI SANA KAKA MICHUZI, CHONDE CHONDE, MAONI YA KIJINGA KAMA YA HUYU JAMAA ALIYEJIITA ZUMBA'S EBU YASIPATE NAFASI KWENYE MAIN PAGE YABAKIE KWENYE KURASA YA MAONI. ATATUKANWA SANA HUYU, MIMI BINAFSI SIKUJUA KAMA KUNA MITANZANIA MIVIVU YA KUFIKIRIA KAMA ZUMBA'S. YAANI PAMOJA NA WATU WENGI KUTOA MAONI YA MAANA YEYE AMENG'ANG'ANA NA KUWAPONDA WANAFUNZI WALIOGOMA. HIVI HAWA WAZAZI WANAOSHINDWA HATA KUNUNUA MBOLEA KWA AJILI YA KILIMO WATAWEZA KUCHANGIA ELIMU YA JUU. SI AFADHARI WAWAAMBIE WACHANGIE ELIMU YA SECONDARI KULIKO CHUO KIKUU. KWANZA KINACHOOMBWA NI MKOPO, JAMANI HATA HILI NI GUMU KWA WATU KAMA ZUMBA'S. An advice to people to Zumbas...SHUT YOUR BEAK IF YOU BRAIN IMPAIRMENT.
ReplyDeleteWe anonymous wa april 18, 10:41:00 ninakuomba kabla ya kukurupuka kutoa maoni ujaribu kusoma na kuelewa kilichoandikwa. Hivyo pitia tena ujumbe nilioandika halafu uone sehemu gani nimeponda mgomo siyo kuropoka tu, Nyamafuuuuuu
ReplyDeleteZumba's
Wee mshamba mtunzi wa huu ujumbe wa kugomewa kutoa comment au Anony wa Wednesday, April 18, 2007 8:10:00 PM Jaribu kutofautisha kati ya maharade na nyama! Jamaa hawajagoma kwaajili ya pesa ya kula bali kwaajili ya ADA. Kama kweli uko ughaibuni basi utakuwa unaosha matako ya hao wazee.naamini kabisa wewe shule kwako ni kituo cha polisi.naomba kujua jina lako au contact yako nikupe shule.
ReplyDeleteZEMARCOPOLO wewe ndo mbumbumbu wa kwanza Tanzania. Umezamia meli nini huko? Angalia!!!
ReplyDeleteAnony aliyeanzisha mada hii ningependa kujua kiwango chake cha elimu nina imani kuna uwezekano kikawa cha chini sana.
ReplyDeleteNingeomba siku nyingine atunze mawazo yako make ni mepesi mno.
Anony aliyeanzisha mada hii ningependa kujua kiwango chake cha elimu nina imani kuna uwezekano kikawa cha chini sana.
ReplyDeleteNingeomba siku nyingine atunze mawazo yako make ni mepesi mno.
Wee Anony wa Wednesday, April 18, 2007 8:10:00 PM naona umechanganya kati Zumba's na Zemarcopolo. Aliyezoza pumba ni Zemarcopolo, zumba's anampinga zemarcopolo. Naungana na na Zumba's na Msemaukweli katika hili.
ReplyDeleteHoja ya kuwa ughaibuni inanikera!
ReplyDeleteMichuzi kuabudu hao walioughaibuni unanikera!
UDSM kugoma wakati wa Mitihani mnanikera!Nahisi kuna MAZUZU huwa hayajajiandaa na UE basi ndio yanatafuta kisingizio yanaanzisha migomo.Kwani migomo ndio njia pekee ya kutatua mambo?
Serikali ya Tanzania kukurupukia mambo inanikera!Hio Bodi ya mikopo ni KERO tupu!
Watawala wa UDSM kwa kufungafunga chuo kikuu kama CHOO cha kulipia mnanikera!Kuna nchi marais huwa wanapata urais kwa maandamano ya wanafunzi,sijui ni kwa akina Sohato...
Kitafika kizazi ambacho hakiogopa hao FFU,sijui itakuaje?
Wee MKUU WA UDSM hembu ona aibu japo ukagombee UBUNGE kwa huna taaluma/utashi/akili/uwezo wa kuongoza taasisi kubwa kama hiyo!TOKA MZEE,bungeni kutakufaa,kwani kuna kazi gani zaidi ya kulipwa posho kwa kazi ya KUSINZIA!!!???
mimi nadhani kama kuna mtu ana hoja ya kutetea mgomo aitoe na sio kuexpress emotions tu.upeo mfupi wa mawazo ndio uliosababisha maafa katika nchi nyingi tu,matokeo yake ni majuto na wakati mwingine hata wakati wa kujuta unakosekana.hili tatizo linaweza likazaa tatizo kubwa kuliko ushabiki mnaoushangilia.i see nothing but public hysteria in this boycot and this behaviour is immature.kuna watu wanataka kutishana kwa kudoubt viwango vya elimu vya watoa maoni,cha msingi nionavyo mimi ni kutoa maoni yanayoelezea fikra zako na sio kutishana na viwango vya elimu.zemarcopolo
ReplyDelete