sokomoko la kuondoka mlimani kabla ya mstari mfu jana....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kikwete asilete mambo ya udikteta sasa...elimu yetu bado ni duni saaaana...hao ni watoto wa kunigotiate nao tu....makinda bado.
    sio watu wa kushindana nao....
    This is unfair!!!

    ReplyDelete
  2. Akitoa msimamo wa wanachuo, Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi (wa UDSM), Julius Mtatiro, alisema mgomo huo utaendelea hadi serikali itakapotoa tamko la kuondolewa kwa uchangiaji huo.

    "Hapa tulipo baadhi yetu wanakwenda kuanza mafunzo kwa vitendo Juni 3 na wameanza kulipwa pungufu, hali inayodhihirisha kwamba madai yetu hayajafanyiwa kazi," alisema Mtatiro.

    Kwa mujibu wa Mtatiro wanafunzi hao wameanza kulipwa sh. 3,600 kwa siku badala ya sh. 6,000 ikiwa ni fedha za malipo ya mafunzo kwa vitendo.

    Alisema hawawezi kusubiri hadi Agosti wakati tayari wanafunzi wameanza kwenda katika maeneo yakiwemo mikoani kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

    Kuhusu hatua yao ya kugoma, Mtatiro alisema pamoja na kwamba ni kosa kulingana na sheria za chuo, wamelazimika kufanya hivyo kudai haki zao.
    "Tunafahamu kugoma ni kosa lakini sisi hatumwagi damu...mgomo wetu ni wa kisomi wa kugomea masomo," alisema Mtatiro.

    Kutoka Morogoro, Mwandishi Latifa Ganzel, anaripoti kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Sokoine Cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro nao waliingia katika mgomo wakidai kupatiwa majibu ya barua yao walioiandikia Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kuhusiana na uchangiaji wa asilimia 40.

    Katika barua hiyo, wanafunzi hao walitaka kuondolewa kwa uchangiaji huo kwa kuwa hawana uwezo.
    Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Sheria katika chuo hicho, Lumanyika Joson, alisema wameamua kutoingia darasani ili wapate muafaka wa barua yao walioandika tangu Februari ya kutaka kuondolewa kwa asilimia 40.

    "Tumeandika barua hiyo na kupeleka uongozi wa SUA lakini hadi sasa hatujapatiwa jibu, tumeamua kugoma hadi tutakapopatiwa majibu ya barua yetu," alisema.
    Alisema kuwa wao ni wadau wa mikopo ya vyuo vikuu hivyo hawapaswi kuwekewa masharti magumu kama hayo kwani hiyo mikopo watatakiwa kurejesha mara wamalizapo chuo.

    Alisema kikubwa kinachowatatiza ni kulipwa sh. 3,600 badala ya sh.6,000 kwa siku kwa ajili ya kujikimu wanapokuwa katika mafunzo ya vitendo.
    "Hiki kiasi ni kidogo ukilinganisha na matumizi ya mwanafunzi akiwa katika mafunzo hayo, katika barua yetu tuliyoandikia wizara tumeomba pia hilo liangaliwe upya, tunahitaji kiasi cha sh. 10,000 kwa siku ili itosheleze mahitaji wakati wa mazoezi hayo.

    Naye Naibu Waziri wa Sheria SUA, Victor Byanjweli alisema iwango hicho hakiwezi kumsaidia mtoto wa mkulima kupata elimu ya juu kwa kuwa wazazi wengi ni wakulima wenye kipato cha chini.

    "Kama hata ada ya sh. 20,000 ya sekondari za serikali mkulima huyo anashindwa leo hii sh. 800,000 ataweza?," alihoji.
    Alisema kuwa hali hiyo itasababisha wanafunzi wachache kupata elimu hiyo na wanyonge kushindwa kutokana na kipato chao duni.

    source: www.uhuru.info/kitaifa.htm

    ReplyDelete
  3. Duh! Hii inanikumbusha wanafunzi walivyofukuzwa huko UDSM 1987? (huenda niemkosea mwaka). Ilikuwa ule mgomo uliongozwa na akina Bazigiza.

    Wanafunzi walitumuliwa na maFFU. Wengi waliondoka kwa mguu. Heri hao wanaondoka na magari. MaForeign Student walibakia campus kwa mshangao huko vyuo vyao na ubalozi zao zilihangaika wafanye nini nao.

    Lakini serikali lazima itizame madai ya hao wanafunzi. Kwa wanaokumbuka enzi za Mwalimu watu walisomeshwa na serikali na hata kulipwa posho. Wanafunzi wengine waliweza kusomesha wadogo zao na hizo posho. Posho zikapunguzwa na mwisho kufutwa na ikawa shida. Tatizo ni wanafunzi wengi si kama wakati ule.

    Sasa kuna kulipia masomo, chakula malazi. Lazima ukikumbuka enzi zile utasema Mmmm! Waliotangulia walifaidi, wanafunzi wa siku hizi wamepunjwa. Lakini ni 2007 na siyo 1960's/70's/80's.

    ReplyDelete
  4. JUZI HAPA NILIONA KWENYE MAGAZETI KIKWETE ANA WAPONGEZA WATOTO WA KIDATO CHA SITA NA CHA NNE KWA KUFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YAO. LEO HUYO HUYO KIKWETE ANA WATUMIA POLISI KUWAFUKUZA CHUONI. WHAT IS THIS? HII NI MESSAGE GANI ANATUMA KWA WATOTO WALIOPO KATIKA SHULE ZA SECONDARY. VIONGOZI WETU HAWATUMII AKILI KABISA..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...