TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete kuhutubia mkutano wa Ajira.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa viongozi wa Afrika wanaotarajiwa kuhutubia mkutano wa 11 wa kanda ya Afrika wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuzungumzia maendeleo na kutoa muelekeo wa ajira barani Afrika, utakaoanza Addis Ababa, Ethiopia tarehe 23 April, 2007.
Mkutano huu wa Shirika la Kazi Duniani hufanyika kila baada ya miaka minne na kukusanya baadhi ya viongozi kutoka nchi 53 barani. Rais ataondoka Kesho Jumapili tarehe 22 April, 2007 kuelekea Addis Ababa kuhudhuria mkutano huo.
Katika kikao kilichofanyika Ouagadougou, Burkina Faso, Septemba 2004, kuhusu Ajira na Kuondoa Umaskini viongozi wa Afrika waliohudhuria kikao hicho waliahidi na kuweka dhahiri kutoa kipaumbele kwenye kutengeneza ajira ili iwe kitovu na lengo kuu katika sera za kiuchumi na kijamii katika ngazi ya nchi, kanda na barani kwa ujumla kwa nia ya kuondoa umaskini na kuboresha hali za maisha ya watu.
Tangu kutolewa kwa mapendekezo hayo, kukuza ajira zenye tija katika mazingira yenye hadhi kumepewa kipaumbele siyo kwa nchi na barani tu bali imekuwa lengo la kimataifa.
Mkutano huu wa 11 wa Viongozi utalenga na kuainisha hatua zinazohitajika kufuatwa na kuchukuliwa na nchi wanachama, ILO na wenza wao katika maendeleo kwa miaka ijayo, ili kuhakikisha kuwa shabaha hii ya kuwa na mazingira ya kazi yenye hadhi na tija inafanikiwa na kutendeka barani, ili kuweza kupata njia muafaka ya kupunguza umaskini kwa njia zinazokubalika.
Katika mkutano huo viongozi watajadili ripoti mbalimbali zitakazotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa ILO ambazo zitaelezea jinsi ILO ilivyofanya kazi na nchi wanachama, hasa nchi za Afrika na ripoti yenye kuelezea malengo halisi ya dunia na Afrika, kuainisha sera na mifano halisi ambayo ni muhimu kutekelezwa katika ajira zenye hadhi.
Mkutano pia utashuhudia ripoti za ILO zikitolewa mkutanoni zinazoelezea mifano kadhaa kuonyesha juhudi katika ajira zenye hadhi barani na pia kuonyesha muelekeo, muhtasari na mchanganuo wa hali ya ajira barani. Rais atarejea nchini tarehe 25 April, 07.
Imetolewa na ikulu,
April 21, 07

KWA WALIOUGHAIBUNI UNAWEZA KUFUATILIA MECHI YA YANGA NA ESPERENCE LIVE KATIKA WEBSITE YA ESPERENCE. (e-s-tunis.com). Nenda LIVE
ReplyDeleteWAZEE NGOMA BADO NI NGUMU. HALF TIME SIJUI KAMA TUNAWEZA KUSHINDA NNE!!
ReplyDeleteJk hana dili lolote hata Ahutubie nini!1 nchi ishamshinda bado mapemaa kazi yake kucheka cheka tu sijui ana ugonjwa gani....
ReplyDelete