Ustaadh Issa,

Habari za kazi bwana. Asante kwa updates unazotupatia ktk blog yako. Kweli unaipenda kazi yako, una kipaji na unakubalika.

Kwa heshima na taadhima nakuomba uibandike hii kwenye blog yako.

Kuhusu hili sakata linaloendelea la wanafunzi wa UDSM baada ya kusoma maoni ya wadau kadhaa nimepata wazo. Naona kuna umuhimu wa kuanzisha chombo kinachojitegemea kwa ajili ya kuwasaidia wanavyuo kupata ushauri usioelemea upande wowote kunapokuwa na msuguano kama huu wa kuchangia 40%. Nasema hivi kwa sababu:

1. Endapo wanachuo watakubali kulipa hiyo 40% kama walivyoamriwa wataonekana ni wapuuzi na wanapotezea watu muda kwa mgomo wao
2. Endapo hawatakubali kulipa (ambayo ni vigumu ku-organize msimamo huo kwa sasa baada ya kuwa wametawanya) then serikali itashikilia msimamo wa kufunga chuo ili tu kuwaonesha wanafunzi kuwa hawawezi kushindana na serikali.

Sasa basi ni muhimu kuwasaidia wanafunzi kufanya maamuzi ya busara next time wanapokuwa katika mtafaruku wowote kama huu. kwa ufupi vyombo vilivyopo sasa kushughulikia misuguano kama hii vinaelemea upande fulani.

Mfano DARUSO ni chombo cha wanafunzi na kinaelemea upande wa wanafunzi (ambao ndio wanawaweka madarakani). Utawala wa Chuo Kikuu, Wizara ya Elimu ya Juu na Bodi ya Mikopo ni vyombo vya Serikali na vinaelemea upande wa serikali (ambayo ndio inawalipa mishahara).

Kwa hiyo idea ni kwamba kuwe na kikundi cha watu binafsi (kama NGO) ambayo itachangisha fedha toka kwa wananchi, wanafunzi, utawala wa vyuo na vyanzo vingine ambavyo vitakubalika kwa kanuni ya kutoelemeza kikundi upande wowote ambacho kitaratibu utafutaji wa ukweli na kuchapisha mambo yote kwenye mtandao.

Kuna wadau wamependekeza serikali kujitoa kabisa katika suala zima la kuwalipia wanavyuo. Wadau wa aina hii naona watapinga hili wazo. Lakini kwa vile serikali imeshaunda bodi ya mikopo ni ishara kuwa serikali itaendelea kujihusisha na kulipia wanavyuo kwa miaka kadhaa ijayo (sina uhakika hapa kuwa mandate ya Bodi ya Mikopo itamalizika lini. nafikiri kwa sasa haijawekewa mwisho na ikionekana umuhimu wake umekwisha bila shaka itavyunjwa ndani ya muda mfupi kama ilivyoanzishwa)

Naona hii itawasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu kupata taarifa sahihi kuhusu nini cha kufanya kunapokuwa na msuguano kati yao na serikali.

Naomba kuwakilisha.


Fredrick Mboma (Mdau aliyeko Bongo)
fredmboma@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hili wazo ni zuri, lakini naona hakuna haja ya kuwa na chombo kingine cha kutatua migogoro kama hii. Kinachotakiwa ni kwamba hiyo bodi ya mikopo iliyopo iwe inatoa msimamo mapema, yaani kabla ya mwanafunzi hajajiunga na chuo ijulikane kwamba ufadhiri atakaopata ni muda gani na uta-cover vitu gani (ie fee, accod. allowance etc). Kutokana na kesi hii ya kugoma inaonekana bodi haikuweka wazi kwa wanafunzi kwamba itawalipia kiasi gani, italipa mpaka lini na wanafunzi watachangia kiasi gani. Katika mikataba kama hii kila kitu kinatakiwa kuwekwa wazi siyo kufanya mambo nusunusu. Chombo kipo ila kiwe wazi. Kwa hili naamini mwanafunzi kabla hajajiunga na chuo atajua nini cha kufanya na udhamini wa namna gani atapata kuliko kumuita mtu chuoni halafu katikati ya safari (masomo) unabadilisha TOR. Nakumbuka enzi zetu tunasoma ilikuwa hivyo hivyo, unaambiwa mkataba ni mwaka mmoja, baada ya hapo utatakiwa kujaza mkataba mwingine, lakini tangu nilianza chuo hadi nahitimu sikuwahi kujaza huo mkataba mwingine. Yaani mambo yalikuwa kinguvu nguvu hivi hivi.

    Zumba's

    ReplyDelete
  2. 1)Wazo la kuanzisha chombo huria kutoa mikopo ni zuri lakini matatizo yatabaki pale pale kama wanafunzi hawataelimishwa nini kinawezekana. Mfano kama hicho chombo kipya kitakuwa na uwezo wa 70% je wanafunzi si watagoma tena??
    2) Naomba kueleimishwa juu ya huu mgomo-je hii 40% ilikuwepo kwenye makubaliano au ni kitu kipya?? Je Serikali iliwahi kutoa ahadi ya kuongeza mikopo mpaka 100%??
    3)Inabidi jamani tuelewe kuwa wanafunzi wa elimu ya juu wamekuwa wengi mno (kuliko enzi za Nyerere), inabidi kuwekwe mikakati mbadala ya kukabili ongezeko hili la wanafunzi.

    ReplyDelete
  3. Huyo aliependekeza kuwa serikali ijitoe kulipa wanafunzi--aache kuongea kama kuku alitoka kutaga maya mawili kwa wakati mmoja. Mimi serikali imenisaidia hadi form six tu sasa nina masters nimelipa na kazi ya kubeba mabox. Kwanza tuelewe moja, serikali ni sisi ndio tumeiweka madarakani sio yenywe ndio imetuweka sisi madarakani.
    Kwa maana hiyo basi seri kali haina pesa wala mali yeyote ile, male na pesa ni yetu sisi watanzania 35mil, kwa maana hiyo:kama tunataka wanafunzi walipiwe inabiidi tuileweshe seshe hii so called serikali kwa njia moja au nyingine.
    Mkisema kwamba serikali isilipe--kwahiyo watoto wa walala hoi, wakulima (ambao ndio wanatoa asilimia kubwa ya hiyo pesa tunayogombea) hawatasoma--hata hapa marekani kuna watu wanapewa grants-wanalipiwa kila kitu kutokana na kipimo cha uwezo wao.
    huyo Kiwete nani kamlipia shule, huyo Makapi -- na so called viongozi wengine wametoa wapi pesa ya kulipia hizo degree zao za siasa walizo nazo tena wengine wamenunuwa---Pesa hiyo hiyo wanayo sema haipo---wanaitumia kulipia watoto wao kusoma huku marekani na nchi zingine----huyu mjinga mwenye dgree ya kilimo anasoma huku marekani hivi sasa nani anamlipia?
    Tuwaambie kwa sauti moja kuwa hiyo pesa wanayotumia kwenda kutembea nnje kila siku--hiyo pesa wanayo tumia kununuwa magari ya kifahari, hiyo pesa wanayojeangea majumba makubwa ya kifahari, na hiyo pesa walioipata baada ya kuuziana nyumba zetu ndio walipie hiyo 40%----kiwete akae akielewa pia "people who have lost all hpoe have no fear"---fidi fosi haita saidia wala hiyo Radar haita saidia---mimi leo ni mmoja naandika hii lakini ninauhakika kuna wengi wanaoteseka---
    La mwisho, Kiwete, waambie so called mawaziri wako kama wanataka maghari ya kifakhari yanayo endena na hadhi yao basi waache uwaziri wafanye kazi binafsi wanunuwe yao, sisi watanzania ambao ndio tunanunuwa na kulipia gharama zote za hayo magari, hatuna uwezo huo--tuna mambo mengi ya mhimu ya kufanya. kuna watoto washule wana kaa chini, kuna shule hazina vyoo--kuna walimu na watumishi wengine wa chini hawajalipwa mishara, the internal debt needs to be paid up---waambie mawaziri wako kuwa sisi mabosi wako wewe Kiwete nido tumekutuma uwaambie hivyo---kwa nini watu tuishi nchi za watu kama wakimbizi wakati kwetu kupo.

    ReplyDelete
  4. Mkereketwa, wanafunzi waliiahidiwa mkopo kwa 100%. Ukumbuke ni kipindi ambacho JK alikuwa anaomba kura za uraisi kwa hiyo asingeruhusu Bodi kuchafua mambo. Ktk sakata hili kauli aliyotoa JK ni kwamba "wanavyuo watafikiriwa ktk bajeti ijayo". kwa hiyo kwa ufupi mwaka huu wameumia. Ila naona wengi wanahimizana kwa sms kukomaa na kutolipa hiyo 40% kama UDSM na serikali ilivyoamuru

    ReplyDelete
  5. Anony baada ya mkereketwa nashukuru kwa mawazo endelevu. Mkereketwa ni juzi tu serikali imewalipia ada hata masters ukitaka hata kwenda marekani ulikuwa unapata asilimia yoyote unayotaka haya mabadiliko ni baada ya wazee kupata madili ya kuwa ofisini.

    Siasa za tanzania zitatumaliza tu. Watu tumeamua kuwa matapeli tu. Tunaongea mengi tunatenda machache. Kuna anayesema wanachuo wamekuwa wengi mno na kulinganisha kipindi cha nyerere na kipindi hiki, mimi nafikiri pia pesa zimekuwa nyingi mno. Allowance ya mbunge wa sasa na waziri wa sasa na wakati wa nyerere ni tosha kuonyesha kuwa hatuna haja ya kulinganisha kipindi hiki na baba wa taifa aliyewapa watu akiri na sasa wanageuka watu.

    Waliambiwa wanakopa kujenga barabara hatuna budi kukopa kwa ajili ya elimu na kuweka utaratibu mbadala wa kurudisha hizo pesa. Serikali inashindwa nini kutambua wananchi wake na kuwasomesha pia kuwa kuweka taratibu za kukusanya hizo pesa.

    Nafikiri tanzania ni kati ya nchi chache duniani zisizoweza tambua raia wake.Tunaomba watawala wasione wanakula na kuishi vizuri wakadhani kuwa hao ndio watanzania, watanzania wenye nchi kawaangalie vijijini.

    Tanzania siyo dar es salaam mjini na mwanza mjini na Arusha. Kwa mfano baadhi ya mikoa zamani watu tulisoma kwa wazazi kuuza kahawa, sasa sijui hata kama mabwana shamba wako tayari kwenda huko vijijini.

    tafuteni njia, kopeni kama barabara tuwasomeshe watu waelimike watengeneze nchi yetu, watoto wenu tu hawatatosha kujenga tanzania

    ReplyDelete
  6. Wadau, Nawapongeza kwa mjadala endelevu ambao ndio tunapaswa kuufanya humu. Naomba kwanza nianze kwa kuwashauri wadau wenzangu walio nje ya Tanzania wakumbuke walikotoka kabla ya kutoa maoni yao. Inasikitisha sana unapolinganisha malipo ya elimu ya Marekani na Tanzania. Kuna mdau mmoja kwenye maoni fulani humu alisema yeye hizo shilingi 800,000 wanazotakiwa kulipa wanachuo, yeye analipia (1 credit hour)kwa hiyo akawashangaa wanafunzi wa chuo kikuu kwa kugoma baada ya kutakiwa kulipa asilimia 40. Naomba tukumbuke kuwa hali halisi ya watanzania, ndiyo inafanya watu walalamike wanapotakiwa kuchangia huduma. Kwa mfano, huyo jamaa anayejilipia shule Marekani, ni kwa vile hali ya maisha inamruhusu kufanya hivyo. Yani kuna kazi inayoweza kumpatia hizo 800,000. Sasa tunaporudi kule kwetu Kimanzichana, Nangurukuru, Machame na kadhalika, hizo nafasi walau za kubeba maboksi hazipo.

    Naamini moja kwa moja kuwa kama hizo kazi zingekuwepo, wanafunzi wangefanya wajisomeshe. Kwa hiyo jamani tunapochangia, tuelewe kuwa hawa jamaa wanafanya hivyo kwa vile hali halisi ya maisha imewabana na hawana njia mbadala ya kuwafanya wamalize masomo yao salama.

    Kwa vile sisi tumepata nafasi ya kusoma na hata kutoka nje ya nchi, nadhani tumeona namna nyingi ambazo zinatumika kusaidia kuendeleza elimu. Huu sasa ni wakati muafaka kwetu kuonesha uzalendo wetu kwa nchi yetu kwa kutoa mawazo yanayojenga na si kulaumu na kutukana.

    Sasa turudi kwenye suala la msingi. Ni kweli nchi yetu inaendelea na ni ukweli usiopingika kuwa idadi ya wanafunzi inaongezeka vyuo vikuu, lakini hili halijatokea kwa ajali kwa kuwa walichaguliwa na ndio mana idadi ikaongezeka. NA hili linatokana na sababu kuwa elimu ni muhimu sana ili nchi iendelee. Sasa basi nini kifanyike ili kutatua tatizo na kama ikiwezekana tuongeze idadi ya wanaopata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu? Hilo ndio twapaswa kulifikiria, naamini njia zipo na zipo ndani ya uwezo wa nchi yetu.

    Serikali inapowataka wanafunzi wasio na ajira wala chanzo chochote cha kipato wajilipie asilimia 40 ya masomo, ni kama baba mwenye mtoto wa miaka 10 anapomtaka mtoto wake achangie gharama za chakula cha kila siku, eti kwa sababu yeye (Baba) amekuwa akichangia kwa kipindi choote hadi mmiaka 10. Ni wazi kuwa mtoto atalia tu ili baba aone huruma na abadili msimamo kwani mtoto hana pa kupata chakula zaidi ya kwa baba. Wanafunzi wa chuo kikuu wengi ni watoto wa wakulima ambao kwao shilingi laki moja ni kitendawaili kisicho na jibu.

    Sasa basi, ninini kifanyike ili hili tatizo liondoke? Nadhani jambo la kwanza ni kuelewa kuwa wanafunzi hawawezi kujilipia kwani uchumi wa nchi na mifumo ya maisha haijawapa uwezo wa kufanya hivyo. LAKINI, ili tuendelee, tunahitaji wataalamu katika nyanja zote za maisha, tena wataalamu wa ndani ambao wataiingizia serikali yetu pato na kuendeleza nchi yetu. Mara nyingi tumekuwa tukiagiza wataalamu toka nje kuja kusaidia katika mashirika ya umma, tunaishia kuwalipa fedha nyingi sana ambazo haziturudii hata kidogo, wengine ndio huduma zao hata hazikidhi haja sana sana zinatupa hasara...mifano mnaijua sihitaji kuitaja humu.

    Kwa sababu hiyo basi, serikali haina budi kutoa kipaumbele kwanza kwenye swala la elimu kwani ukichambua kwa makini ndio chanzo cha maendeleo yote. Hivi kama tunakopa kwaajili ya kujenga barabara, kwanini tuone aibu kukopa ili kuelimisha watanzania watakaosaidia kuingiza fedha za kulipa mikopo hiyo baadaye?

    PILI, kusaidia kupunguza makali ya maisha kwa wanafunzi na kuwafanya wachangamke zaidi, kuna kitu hapa Marekani kinaitwa WORK- STUDY PROGRAM, ni mpango ambao unamfanya mwanafunzi afanye kazi ndogo ndogo za chuoni au hata kwenye mashirika na makampuni mengine ya binafsi. Inawezekana wanafunzi wakafanya kazi na kulipwa kwa masaa, hivyo, migahawa ya vyuo, maduka na hata baadhi ya kazi ambazo si za kiutawala sana zikafanywa na wanafunzi. Gharama ambazo zingetumika kuwalipa wafanya kazi wengine, zinawalipa wanafunzi na kuwapunguzia makali ya maisha.

    Jambo hili litawafanya pia wanafunzi kuthamini kazi yoyote hivyo kuchangamkia fursa za maendeleo zilizosheheni nchini mara baada ya kumaliza masomo yao. Nilipofika marekani kwa mara ya kwanza nilishangaa baada ya kuona kazi zote zinafanywa na wanafunzi bila aibu. Wanapakua vwakula migahawani, wnafyeka nyasi za bustani wanauza maduka na kadhalika.

    Serikali au hata uongozi wa vyuo unaweza kuzungumza na wamiliki wa makampuni makubwa Tanzania ili wasaidie maendeleo ya elimu ya juu kwa njia moja au nyingine. Njia mojawapo ikiwa ni kuajiri wanafunzi kwa saa ambazo wanakuwa hawaana vipindi. Hivyo wanafunzi wa uhandisi wafanye kwenye makampuni yanayoshughulika na fani yao, waalimu wapewe fursa ya kufundisha na kadhalika. Hali kadhalika, waalimu wa vyuo vikuu nao watoe ushirikiano kwa wanafunzi wanapokuwa wanafanya kazi ili mradi tu kazi isiathiri maendeleo ya mwanafunzi darasani.
    Nadhani hili litasaidia hata kuongeza kasi ya utendaji kazi, Masaa ya kufanya kazi yaongezeke, watu wafanye kazi hata usiku kama kuna uwezekano.

    Watanzania tunabezwa siku zote kuwa ni nchi inayoendelea lakini saa zetu za kazi ni chache na hata hizo chache ufanisi na heshima kazini pia bado sio vya kuridhisha.

    Hivyo basi, badala ya kulaumu na kuweka vitisho na sheria zisizotekelezeka ambazo zitazaa mgawanyiko usio na sababu, hebu tuangalie uwezekano wa kutafuta suluhisho la kudumu. Inawezekana kama kila mtu atawajibika kwa nafasi yake.

    Mwisho kabisa, kwa ndugu zangu wanafunzi wa vyuo na watanzania wengine, tujenge tabia ya kupenda na kuheshimu kazi. Ni kweli huenda kazi nyingine zikaonekana kama zinadhalilisha, Hii imetokana na hali tuliyojengewa na wakoloni kuwa sisi tukishasoma tunapaswa kufanya kazi za ofisini tu na zile nyingine hazitufai. Hii ni sumu iliyopandikizwa kwenye mawazo yetu kutupumbaza. Mbona wenyewe wanafanya! Utakuta mzee ana PhD Lakini anapalilia bustani yake, anachukua tenda za kusafisha maofisi. Wasipokuwepo watu wa kumsaidia anafanya mwenyewe bila kujali jamii itasemaje. Matokeo yake maendeleo ya nchi yanaenda kwa kasi ya ajabu na mgogoro wa ukosefu wa ajira unapungua kila siku kwani watu wanafanya ubunifu na kutengeneza ajira na si kuomba ajira tu. Tanzania itajengwa na mimi na wewe, na hakuna sehemu yoyote inayoonesha kuwa kazi ya wwaliosoma ni ile ya kukaa ofisini tu.

    Nawashukuru kwa kusoma

    ReplyDelete
  7. kwa ujumla hakuna hoja ya kutuweka macho usiku kucha kuchangia. ...sijui kwa nini watanzania mpaka leo mnadhani serikali inatakiwa ilipie elimu ya juu. hakuna nchi inayoendeshwa hivyo. Tunashukuru kwa kile serikali imetoa kwa wanafunzi, ni kweli mahitaji ni makubwa kwao, lakini hilo ni tatizo la jamii. Harambee kwa ajili ya elimu zitasaidia zaidi ya ya michango ya harusi mpaka makazini. AMKENI !

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli hapo kuna watu wanataka ziada.Na ni asilimia kuwa wanataka ziada.

    Kwani si kila mtu analipa kodi Tanzania.Kwa kila mzazi anayelipa kodi mtoto wake anastaili kupata mkopo.

    Wewe angalia magari yale walivyojipanga msululu ni ya wanafunzi sasa una gari then unashindwa kulipa ada????

    Huko ndio kuwaibia walala hoi.Kila mtu mwizi tu bwana.Na wewe mwanafunzi acha kuuibia serikali.Hiyo mikopo mtalipa????Unataka mkopo wa serikali kununulia vitu vya anasa.

    JK rekebisha sheria za mkopo kila mtu anahitaji kukopa.Ukishindwa dumisha huduma muhimu kwa umma mengine yote yatajipa.

    ReplyDelete
  9. We anony wa Sunday, April 22, 2007 8:01:00 AM Acha kufikiri mama mwenda wazimu na usiongee vitu usivyovijua. Magari yaliyojipanga hapo ni Tax ambazo watu wamelazimika kukodi baada ya kutimuliwa kibabe na serikali.
    Hivi watu wengine mnaoongea humu mlimaliza hata darasa la saba kweli? Mjitu unajiita eti ni Mdau halafu unang'ang'ana eti JK kaza uzi hao jamaa walipe.

    JAMANI FIKIRI KABLA YA KUONGEA. MANENO YAKO YANAAKISI UWEZO WAKO WA KUFIKIRI, HEBU MSITUONESHE UTAAHIRA WENU HUMU. KAMA MMEPATA NAFASI YA KUCHAMBISHA WAZEE HUKO MAREKANI ENDELEENI NA MSIANZE KUTUKANA HOVYO NA KUTOA MAONI YASIYO NA MBELE WALA NYUMA.

    Imenibidi nitumie lugha ya hasira kidogo kwani kuna watu wanajiita wadau wa ughhaibuni wanatutia aibu. Jamani jirekebisheni mnatuaibisha wenzenu

    ReplyDelete
  10. Kilimanjaro wazo lako zuri sana ila napenda kukukumbusha kitu kimoja

    hapo zamani wanafunzi wa UD walikuwa wanafanya kazi ndogo ndogo mitaani za zilikuwa zinawaongezea kipato, lakini kwa makusudi mazima uongozi wa chuo wakakaa wakasema chanzo cha migomo ni wanafunzi wapo idle sana, wakabuni mitaala ya kuwakeep busy the whole day.

    Somo moja likagawanya mara nne ili kumfanya huyu dent awe busy the whole day.

    vipindi vinaanza 7:00am na kuisha 8pm sometimes mpaka 10:00pm. Mwanafunzi anakipindi cha kwanza 7:00am cha pili 1pm na cha mwisho 6:00pm unatarajia atafanya kazi mjini huyu na kama atafanya ujue atakuwa na supplementary kumi au at disco at the end of the year.

    pili graduates wenyewe wanalilia hata part time jobs hakuna, kama huna godfather wewe hata kama una first class ujue utasota tu

    mi nafikiri hapa cha muhimu ni serikali kuanzisha sera maalum kwamba kila graduate akopeshwe 100% na akimaliza apangiwe kazi na serikali afanye huku analipia deni deni likiisha atakuwa tayari na experience anaachia nafasi wengine yeye anatafuta private employment.

    kwa hali hii na wale wazee waliokuwepo toka wakati wa TANU nao wastaafu na kuwaachia vijana nafasi wajenge nchi.

    kinachofanya TZ iwe nyuma siasa zimekuwa kila mahali wakuu wa vyuo, serikalini watendaji wote wanajifanya wakereketwa ili wale kiulaini, polisi nako usiseme, elimu ndio kabisa

    kama kweli tunataka maendeleo na kukuza uchumi basi tuache polics na kung'ang'ania madaraka kama vikongwe wetu wanavyo fanya. wanastafu serikalini warudi kwa kupitia ubunge mawazo yanakuwa yale yale

    nina mengi ila nisiwachoshe. Hii ndio TZ too much talking too litle actions

    ReplyDelete
  11. Hizi siasa za wanafunzi kugoma kukomoa serikali hazijawahi kumsaidia mtu yeyote. Kama mtu unajijua wewe masikini tulia, pokea kilichopo, soma. Ukimaliza ndio utakuwa na jeuri ya kudai mshahara au kujipangia bei yako ya consultancy maana wakati huo utakuwa na soko. Sasa wakati huu wa uanafunzi, huna kitu, uko so vulnerable, ati unagoma, kumtisha nani? Na uanafunzi ni kipindi kifupi tu, kinaisha unaendelea na maisha yako tena yenye nafuu zaidi. Kwa nini wanafunzi wanajiharibia nafasi zao? Ni umbumbumbu, ulimbukeni au ni nini? Hebu chunguzeni wenzenu waliogoma huko nyuma wako wapi na maisha yao yakoje. Ovyo tu! Kugoma shuleni si sawa hata kidogo kwa ulinganisho na kupigania haki, hata kidogo. Mgomaji ama kiongozi wa mgomo wa shuleni hapati credit yoyote mwisho wa mgomo, hata kama wenzie watapata faida fulani kutokana na mgomo aliouongoza. Wapigania haki wengine hupata credit haki ile inapopatikana (mfano wapigania uhuru), lakini wagomaji wa shuleni husahauliwa mara! Mimi siwakumbuki kwa lolote jema wale waliokuwa wanashabikia migomo nilipokuwa chuo kikuu miaka ya 1990. Na hata inapotokea nikikutana nao leo barabarani huwa natafuta njia ya kuwakwepa maana wamechoka vibaya, kila wanayemwona wakimjua wanamwomba hela, na wanatapeli pia! Hali zao ovyo kabisa kuliko hata wale ambao hawakufika hata sekondari! Yale makeke waliyokuwa nayo chuoni ya kuwahimiza na kuwatishia wenzao wagome yote yameyeyuka! Wale maprofesa waliokuwa wanatukanwa bado wapo na wanazidi kula nchi kwa raha zao! Sisi tuliokuwa tunaonekana waoga wa migomo tumemaliza shule salama, tumepata vyeti safi, wala havijaandikwa ati tulikuwa waoga chuoni! Na kwa jinsi transcript zetu zilivyotulia, tumefanya masters na wenzangu wengine wanafanya PhD. Wale wagomaji wengine waliobahatika kusamehewa na kurudi chuoni wamepata pasi mbovumbovu, lakini masikini vyeti vyao havijaandikwa kwamba hizo GPA duni zimetokana na kugoma! Matokeo yake ni kwamba yeyote (e.g prospective employer) atakayeona vyeti hivyo ataelewa hao jamaa ni maselule, akili ndogo, kumbe jamani walikuwa na uwezo wa kufanya vizuri, ni ujinga wa kufuata mkumbo uliwaponza!

    Sasa vijana acheni ujinga, migomo kama hii ya kipuuzi kabisa, haiwasaidii lolote. Yako mambo yanayostahili kugomewa, mkigoma kwa sababu hiyo tutawaunga mkono, lakini kwa hili la safari hii poleni, hili mmelikoroga mtalinywa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...