
jk akisalimana na bi. flora, mjane wa hayati oscar kambona, mmoja wa mawaziri wa kwanza wa tanganyika ambaye ndiye alikuwa mbongo wa kwanza kufanya kazi idhaa ya kiswahili bbc london miaka 50 ilopita. jk aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya utangazji wa idhaa hiyo kwenye hoteli ya kempinski kilimanjaro ambapo wafanyakazi wote wa idhaa hiyo walihudhuria, aliiomba bbc pamoja na idhaa zingine za nje zinazotangaza kwa kiswahili kutoendeleza libeneke la kutangaza mabaya tu ya bara la afrika na kuangalia mazuri mengi yanayofanyika. aliisifia bbc kwa kazi nzuri na pia kueleza furaha yake kwamba bongo ndiyo iliyofungua idhaa hiyo miaka 50 iliyopita kupitia kwa hayati kambona na kuifanya ifikishe wasikilizaji zaidi ya 21 wakati mbongo tido mhando alipohitimisha jubilei yao ya dhahabu. katika hesabu hiyo wasikilizaji milioni 13 ni wa bongo
Mama Kambona aliwahi kuwa Miss Tanzania miaka ya siti. Je, una picha zake za wakati huo?
ReplyDeleteHuyu muungwana anaviasa vyombo vya habari vya nje viache kutangaza mabaya ya afrika na vianze kutangaza mazuri. Hivi kuna mazuri gani wanayoyafanya zaidi ya kutuingizia usiku? Wakipata uongozi wanakuwa arrogant, akina baba haambiliki, wanajua kila kitu.
ReplyDeleteJakaya na Idhaa ya kiswahili ya BBC ni damu damu. Tokea lini wakamsema vibaya? ni wanamtandao wake hao. Tido na wenzake waliongoza kampeni wakimtangaza na kumpamba sana. Kweli walifanikiwa. Jakaya akaingia ikulu. Sasa ameanza kulipa takrima, wanaotoka BBC anawapa mahala pa kujitafunia taratiiiiibu.
ReplyDeleteJakaya inaelekea hajui ni hasa ni kazi ya chombo/vyombo vya habari. si kuburudisha au kuelimisha au kuhabarisha. kazi ni kukosoa, kukemea, kuonya, kuasa, kushauri, kutahadharisha. kazi ni kuwa sauti ya mnyonge asiye na jukwaa kusema linalomkera, lililomsibu. mnyonge asiyekuwa na pesa za kununua hisa za Rai au Nipashe au Mwananchi achilia mbali Uhuru, TVT RTD na Daily News.
Maswali ni mengi kuhusu kauli hii ya Jakaya. Je anataka BBC au DW au VOA wasiohoji kuhusu Richmond? Ujenzi wa barabara umesimama wasiulize kunani? Chuo Kikuu kikifungwa wakae kimya? Bajeti ikiwa ni ya kumkandamiza mnyonge BBC waimbe ndio Mzee? Safari za nje zisizo na matunda BBC iseme mwacheni atanue? Je anataka VOA na DW washangilie utitiri wa mawaziri na serikali kubwa isiyo na ufanisi na kusema hii ndiyo kasi mpya? Au anataka wasiseme au kuandika kuhusu mikataba hewa na kuuzwa kwa raslimali za nchi kiholela? Anataka mazuri yapi yaandikwe au kutangazwa? Amani umoja na mshikamano wa watanzania wanautangaza. Au anataka waseme uchumi unakua ili hali unakufa?...Maswali bado ni mengi. Lakustajabisha na kusikitisha ni kuwa mista misifa bado anataka sifa. Kumbuka waswahili walisema Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
Nakumbusha tena VYOMBO VYA HABARI KAZI YAKE SI KUWA MTUMWA WA MTAWALA.
Muungwana nasaha zako kwa BBC ni kweli tupu...lakini fanyeni basi mambo mazuri hili nao wapate cha kutangaza. Mazuri hakuna ndio maana wanatangaza mabaya hili nao mkono uwende kinywani. Hebu mchomoe Balali hapo BOT and then Zidisha mrabaha wa madini ya kule Nyarugusu kutoka 3% mpaka angalau 25% uone kama hawatatangaza.
ReplyDeleteUSHAURI KWA KAKA JAKAYA WA KIKWETE...!
ReplyDeleteBROTHER JAKAYA HAKO KATUMBO KAMA MIMBA YA MIEZI MINNE ANGALIA OBESITY INAUA HALAKA HAIJALI KAMA WEWE NI MKUU WA NCHI,KAKISUKARI KAKO KATAKUSUMBUA SANA, JARIBU KUANZA UTALATIBU WA TUMAZOEZI KAKA KIKWETE. USINGOJE MPAKA UDONDOKE TENA UWANJA WA TAIFA....! MWILI UNAHITAJI MAZOEZI HILO TUMBO SI DAMPO LA CHAKULA LINAHITAJI MAINTENANCE AMBAYO NI MAZOEZI.
Jk watu wamshauri afanye mazoezi
ReplyDeleteHapo JK katoka kama Katuni vilee, tumbo kubwa nguo zimembana. Watu wa itifaki mpo wapi? Kumwacha Raisi avae nguo kama hivi sio busara. Ona sasa watu wanamwambia Raisi kama ana mimba ya miezi minne na wewe Michuzi unachapisha tu, wakati watu tumeweka komenti za maana na umebania, sijui saa zingine huwa unafikiria nini wewe Issa
ReplyDeleteCha kusikitisha, sijaona mkurugenzi au mratibu hata mmoja wa main BBC baba kutoka London.
ReplyDeleteHawa big bosses walikua wapi, katika sherehe hii muhimu, kuwapa mkono BBC swahili katika kutimiza miaka hamsini.
Je tunatarajia nini hapo baadae kwa BBC..Kuna upgrade yoyote inayoondelea, na inabidi waexpand BUSH house ya miaka hamsini na ? Je kuna utaratibu wowote wa kufanya uratibu au kwenda kwenye maeneo mengine yenye vyombo vya kisasa ?
Hivi ni maswala ambayo tulitaka kusikia toka kwa hawa wakurugenzi wa BBC swahili na wakurugenzi wakuu wa BBC in general.
BBC world service, should go LARGE!! na BBC TV swahili.. Seriously these are fundamental issues should be in core of the decision makings within BBC inc.
Kuna tetesi wanataka kuwa privatised iwe inajenga its own finance to pay its expenses, that the move should be encouraged ili waweze kufight na BSKY B, ITV na wengineo...
Hii yote itaimprove vipindi vyao, ikiwa ndani ya RAdio au TV..The legacy ya kutegemea serikali wapange TV license na kutishia kuzuia pesa.. imeshapita na wakati..
Kama munakumbuka Mkurugenzi mkuu Mr. Greg Dyke aliachia ngazi, ati BBC ina scrutinized the Government ???
Vyombo vya habari lazima viwe independent kutoka kwa Government influence, ni mategemeo yetu will turn private soon rather than later.
By Mchangiaji.