Wizi Mpya wa Simu....
Michuzi,

Kijana mmoja anayesoma katika chuo cha kidini kilichopo huko maeneo ya uwanja wa ndege alipata dhahama inayotia uchungu sana maeneo ya posta. Mkasa wenyewe ulianza hivi.

Kijana huyo alikuwa anasubiri daladala ili awahi kurudi chuoni maeneo ya posta mpya. Mara akatokea mama mwenye heshima hivi ana mtoto ambaye ana dalili za kuumwa. Akamwomba kijana simu yake ili ampigie mumewe pengine kumweleza mtoto mgonjwa. kijana akasema simu ina shilingi 600, mama akamsisitizia kuwa haitotatosha ila anaomba aweke laini yake ya simu na kijana akakubali. Mama akapokea simu akatoa laini ya kijana akaweka laini yake na kupiga na kisha kumrudishia simu kijana. Kijana hakuangalia kama laini iliyowekwa ni yake au la...... Kosa kubwa!!!!!

Mara usafiri wa daladala ukafika kijana akaingia na baada ya kuanza safari abiria mmoja akasikika kaibiwa simu. Kijana aliyekuwa naye, yaonekana ni mwizi mwenziwe, baada ya kutafuta chini ya kiti akashauri wajaribu kuipiga na ndipo simu ya kijana msamaria huyu ikatoa mlio. Wale vijana wakaanza kumpiga kipigo cha mbwa mwizi wakidai kaiba simu na kulazimisha kuichukua kutoka kwa kijana kwa nguvu. Kwa busara za mzee mmoja aliyekuwa ndani ya gari lile walifanikiwa kufika kituo cha polisi na polisi bila kuuliza wala kupokea maelezo ya kijana wakamnyan'ganya kijana simu na kuwapa wale vijana waliodai simu imeibiwa na wakaondoka. Vijana wale walikuwa wakifanya kila wanaloweza kijana yule asijieleze........

Ndipo maskini kijana wa watu akaanza kuwaeleza polisi kilichotokea. Polisi wakabaki mdomo wazi, na kujaribu kumwomba kijana msamaha. Lakini tayari alikuwa na majeraha kichwani na simu yake halali kabisa ikiwa imeibiwa.
Ni hadithi ya kusikitisha ambayo inaweza kumpata kila mtu. Hivyo wenye simu tafadhali tuugundue wizi huu mpya wa simu.

Alamsiki..
Stephen L. Kirama

"It's better to keep your mouth shut and give the impression that you're stupid than to open it and remove all doubt."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2007

    Naomba mnisikilize:
    Maoni yangu yanatiririka kuzingatia kuwa hao jamaa na yule mama ni wakatili mno na kwa vitendo vyao jamaa angeweza kuishia kubebeshwa tairi na kuchomwa. Inawezekana kuwa hiyo ishatokea kupitia watu hao hao. Hao polisi badala ya kutoa macho na kuomba msamaha ingebidi wajaribu kuwafuatilia hao watu kwa kutumia IMEA. Operator yeyote wa simu inabidi awasaidie polisi ili kukomesha maafa yanayoweza mpata mimi na wewe kwa uunwana wetu.
    Pia nchi nyingi sana zinalinda vituo vya polisi kwa kutumia cameras. Yaani yeyote anayefika hapo kituoni anabakia ktk records zao kwa muda say 24 hrs.Kama bongo hiyo haipo tujitahidi kuiweka kwani kuibiwa silaha kunatokea mara nyingi.
    Kijana pole sana: Nilipokuwa bongo last year watu kibao walitumia simu yangu. Labda hawakunifanyia kweli kwani ilikuwa Nokia 3310? Sorry kwa barua ndefu
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2007

    Michuzi, keep up the good work. Hiyo taarifa kuhusu wizi mpya wa simu utasiadia kuokoa watu wengi wsiibiwe simu zao kwa njia hiyo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2007

    NO GOOD DEED GOES UNPUNISHED

    Huku tuliko huombi hata chumvi kwa jirani. mambo hayo ya kuazima na kuomba tushasahau. Unakuta mtu anaflat tire unampita kama humwoni. "you got change to spare" = ombaomba wako wengi tu lakini unawapita kama huwaoni. Hujui wanaloomba ukitoa kiwallet chako wakichungulie wakufwate nyuma wawakuchukulie kila penny iliyo.

    Next time hamna kumpa mtu kama hamna pay phoe then you are doom. Kwa kulivyokua hakuna cell phones ilikuaje????

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2007

    Kuna mdau hapo juu amenishangaza sana, tuache kuwadanganya watu wa nyumbani jamani. Huyu mdau amesema kuwa...I quote "Mambo ya kuazima tumeisha tushasahau" siyo kweli bwana, hapa ninapoishi mimi Washington DC watu wanaomba kutumia simu ya mtu bwana, Jumamosi tu kuna dada mmoja aliniomba kutumia simu yangu kumpigia mtu aje amchukue Silver spring metro station, tuache hivyo jamani. Nashukuru kaka michuzi kwa hiyo taarifa bwana siku hizi kuamini watu ni vigumu...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2007

    Huu ni mtego wa panya kuingia walokuwemo na wasokuwemo. maana sasa hata akija mtu na shida ya halali msaada hauwezi patikana. Mwanamke afriti mkubwa wewe unayetumia mtoto katika wizi wako. Unamfundisha nini huyo taifa la kesho. Kaa mbali unatia kichefu chefu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2007

    huyu ni stephen kirama alopitia Ntungamo major seminary kule Bk au? Kama ndiye please nipe contact zako maana nahisi kama tunafahamiana sana. Pius.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2007

    ndo maana siku hizi watu hawatoi lift.unakuta mama mtu mzima njiani anapunga huku analia,kisha anakwambia kafiwa anawahi msibani,unamwonea huruma hata njia unabadili ili umfikishe kwenye huo msiba kumbe anakupeleka kwenye ambushmaana njiani anasema tusimame hapa mara moja,ghafla mnavamiwa unapigwa na kunyang'anywa gari.yametokea.wahenga walisema wema usizidi uwezo.

    ReplyDelete
  8. duh! hii mbaya sana, lakini tumejifunza kitu, never trust a strenger

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2007

    Tanzania tunaelekea wapi jamni?sisi kijjini kulikua na mtu mmoja tu mwenye gari lakini gari hilo lilikua la kijiji,usiku mama anajifungua tunalenga kwa huyo jamaa,kuna mtoto kazirai tunalenga kwa huyo jamaa,personaly hilo gari la huyo mzee limenisaidia sana siku moja lakini sasahivi mi nafikiri nikiwa na gari langu nilitumieje?maana haikawii kuwa matatizo kwangu,mara kichuma kimemuumiza mtu then ananisue jamani mambo gani haya?Ukafiri umeshatufika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...