NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI,

KWA MASIKITIKO MAKUBWA, KWA NIABA YA UKOO WA MAZARA WAISHIO MAREKANI, TANZANIA NA KWINGINEKO DUNIANI. TUNASIKITIKA KUWAJULISHENI YA KWAMBA BINTI YETU SHEMSHA KENNEDY MAZARA(wa miaka 8). AMBAYE TUMEKUWA TUKIMUUGUZA KWA MUDA MREFU HUKO DALLAS-TEXAS, HATIMAYE MWENYEZI MUNGU AMEAMUA KUMCHUKUA NA KUMPUMZISHA KATIKA MATESO YOTE ALIYOKUWA AKIYAPITIA MCHANA WA LEO WA LEO TAREHE 27/06/2007

SHUKRANI ZA DHATI NA UPENDO, ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI AMBAO KWA KIPINDI CHOTE HICHO WAMEWEZA KUUNGANA NASI KATIKA MAOMBI, KUTUMIA MUDA WAO MWINGI NA FEDHA KATIKA KUSAFIRI ILI KUMSALIMIA MAREHEMU BINTI YETU, BILA KUSAHAU WALE WOTE WALIOWEZA KUTUMIA MUDA WAO KATIKA KUPIGA SIMU AU KUANDIKA EMAIL ILI KUTUFARIJI.

MAZISHI YATAFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI MCHANA, HUKO DENTON-TEXAS, WAKATI WA MCHANA.

WOTE TUKO KATIKA SAFARI HIYO HIYO. ASANTENI NA MUNGU AENDELEE KUWAPA NGUVU KATIKA YOTE MFANYAYO KATIKA DUNIA YETU HII YA KUPITA.

PATROBAH MAZARA(mazarap@yahoo.com)

The late Shemsa, Big Uncle.

Ken Mazara(kenmazara@yahoo.com)

The late Shemsa's Dad

Rehema K Mazara(reymazara@yahoo.com)

The late Shemsa's Mom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2007

    Poleni sana familia ya mzee Mazara,sara zetu ziko na nanyi ktk wakati huu mgumu wa maombolezo.R.I.P shemsha.
    CAL.USA.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana familia ya Mazara. Shemsa sasa ni malaika mbinguni. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2007

    pole sana familia ya Mazara

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2007

    Poleni sana wafiwa.....Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. Amina.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2007

    RIP little angel

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2007

    Rest in Peace!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...