
jamaa akilipiga sop sop wanja letu jipya la neshno stedium. jana jk alilitembelea na kushauri kwamba endapo hautakamilika kabla ya siku ya mechi na msumbiji usifanyiwe haraka kufunguliwa hadi asilimia 15 zilizosalia za ujenzi zikamilike. jk pia alipiga mkwara kwamba matunzo na kuajiri kwa watu wenye ujuzi vipewe kipaumbele ama sivyo watu watatafutana ubaya. jina limebakia lile lile la tanzania national main stadium hadi itapoamuliwa vinginevyo. kuna waliopendekeza uitwe benjamin mkapa kumuenzi aliyewezesha ujengwe, wengine wamependekeza uitwe mwalimu nyerere kumuenzi baba wa taifa na wengine wametaka uitwe jina la rubani wa ndege za kivita alieanguka hapo miaka ya nyuma, kepteni karama
kweli uwanja wa taifa wa neshno stedium unatisha
ReplyDeleteUwanja poa sana huu lakini unatakiwa kuhifadhiwa vizuri, Sasa mtu unaenda kutazama mechi huna wasiwasi hongera wabongo.
ReplyDeleteWacha uitwe hivyo hivyo Tanzania National Stadium na SIO vinginevyooooooo !!!!
ReplyDeleteAISEE MICHUZI UWANJA HUU HAUNA HAJA YA KUPEWA JINA LA MKAPA WALA RAIS YOYOTE KAMA ILIVYO KAWAIDA YA WAAFRIKA. UKIZINGATIA KWAMBA NI UWANJA UNAOWEZA KUTUMIKA KWA MICHEZO MBALIMBALI JINA LITAKALOPENDEZA ZAIDI NI "THE NATIONAL SPORTS STADIUM" AU "THE NATIONAL SPORTS ARENA".
ReplyDeleteMAJINA MENGINE NI VICHEKESHO TU KMA SIYO KIINGEREZA KIBOVU.
Uwanja wa taifa ungepewa jina tofauti kuliko kila kitu kuitwa majina ya watu na viongozi imeshapitwa nawakati.
ReplyDeletetafadhali Michuzi watu waenziwe na ukweli wa Mambo, rubani aliyeanguka hapo kwa jina sikumbuki isipokuwa ni mtoto wa Chief Haroun Msabila Lugusha wa Sikonge, kwa jina la nyumbani Mazwazwa,sasa labda kama siasa zinaingilia lakini ukweli wa mambo ni huo!!
ReplyDeletesio siri dude linapendeza..yaani world class kabisa isipokuwa kuhusu jina sijui Karama ni nani lakini aliyeanguka hapo kama rubani wa Air Force ni Kapteni Mazwaza, mtoto wa Chifu Lugusha wa Sikonge, Unyanyembe, sasa sielewi kama siasa zimeingia hapa kupotesha ukweli, Michuzi saa nyingine inabidi ufanye homework kabla ya statement kama hizi, kuna wanaojua lakini tupo pembeni tu.
ReplyDeletejamani hiyo ni domestic MOA intatumika kukata majani ya uwanja wa taifa. serikali nunueni machine zinazotakiwa kutumika viko kama tractor but vidogo sana hata tfsc watakuwanazo,hiko kitaaribu uwanja tu.hata hivyo nawapa hongera kwa kazi nzuri iliyofanyika uwanja ni mzuri na unavutia cha kufanya sasa tafuteni wadhamini wakubwa ambao wataweza kuendesha stadium.
ReplyDeleteWamekwisha anza tia aibu, hiyo mashine ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani---hata mtu ukitumia akili ya kawaida tu utagundua kuwa HP yake ni ndogo kukata wanja lote hilo---wabongo sijui tuko vipi?
ReplyDeleteUwanja poa lkn huyu dereva mkokoteni mimi simuani hata kidogo ktk kutunza uwanja.
ReplyDeleteTrekta ni trekta tu, hata kama ni dogo!
ReplyDeleteMimi naona hicho ki-MOA kinafaa sana. Ila waongeze idadi yake, kama vitano hivi.
Trrekta, hata kama ni dogo, linaharibu turf!
Aisee Anon wa June 30, 2007 5:22:00 PM EAT
ReplyDeleteHata mimi nimeshangazwa na hiyo Domestic Lawn Mower inayotumika kwa kazi hiyo ya kukata majani uwanja wa kimataifa kama huo. Yaani ina maana serikali imeshindwa kununua better Lawn Mower ambayo inaweza kufanya kazi effectively?? au hadi nazo tupewe msaada na wachina?? Kweli waafrika tuna matatizo. Hii Lawn Mower hata kwa domestic ni ndogo sana na mara nyingi ukiitumia hata majani unakosea kuyakata.
"TANZANIA MAIN NATIONAL STADIUM"??? maana yake ndio nini jamani? kiingereza nacho kigumu kweli!!!!!!
ReplyDeleteKweli kamashine kadogo sana kwa uwanja mkubwa kama huo . Wajitahidi wanunue vile kama vitrekta vitahifadhi hata nguvu za kiume za mkataji .Namna hiyo ukimaliza kufyeka wanja lote hilo namna hiyo ni kasheshe au wakagomboe yale majani bandarini na walipie ushuru kama alivyo agiza JK TFF bwana?
ReplyDeleteHilo jina la uwanja ni zuri ILA kama kweli mamlaka husika ilikuwa inataka kutengeneza pesa ingeuza haki za jina la uwanja kama vile Aseno walivyofanya kule Uingereza. Mwenye uchache mkubwa ndiye angeweza kuweka jina lake katika uwanja huo.
ReplyDeleteNamuunga mkono Raisi Jk kwa kuwaonya wanaoutunza uwanja waajiri watu na lazima wame na vifaa vya kisasa sio kama hicho domestic MOA kinacho katia majani hapo huo ni udhalilishaji.Tafuteni vifaa kama tractor ndogo na wanazijua.Kuweni na upendo na mali za wananchi nyie mlio pewa kumiliki kwa kuupa matunzo.Pia wabongo wame na uchungu na mali mamoja na maendeleo ya nchi kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo ili tz iendelee.Mfano wanaonesha wachezaji wa taifa star.Basi na sisi wangine tuige mfano huu kwa kuongeza juudi katika shughuli zetu na sio kukalia mizinga na rushwa kila mtu.Nchi ni yetu na kila raiya anawajibu wa kujitolea muanga ktk kuijenga kwa hali na mali
ReplyDeletesasa hii noma huyu jamaa hadi amalize uwanja mzima huo mgongo utakuwa umepinda nusu mduara. uwanja mzuri sana next muhimbili.
ReplyDeleteKwanini wasitangaze na zawadi ya watu wakuname huo uwanja wabongo bwana wanapenda sifa zao wenyewe. Huku tuliko kila siku kuna mashindano ya kuuchagua jina la kitu fulani. na watu wanapewa tarehe ya mwisho. wakipata majina wanachuja na kupata jina la maana
ReplyDeleteni raha kuona na sisi tumeanza kusababisha kashkash kwa wapinzani wetu kwa mfano b.faso. eti chama wamejiuzulu kutokana na kipigo kutoka kwa TZ!
ReplyDeletehttp://news.bbc.co.uk/sport1/hi/football/africa/default.stm
kwa kweli kama tuko serious , hi lawm mower ya nyumbani haitakiwi kutumika kukatia huo uwanja, naomba muombe ushauri kwa hao wajenzi au nchi jirani ni machine gani itafaa, kama hiyo tractor etc na sio domestic one.
ReplyDeletelakini mambo yetu yakiwa kama ya siku zote haya tuendele na domestic lawn mower
Kwa kweli hata mimi nadhani serikali na FAT wanatakiwa wanunue mashine ya kukatia majani.
ReplyDeleteDomestic Lawn Tractor ina cost kati ya $1500 mpaka $3000, angalau tununue hiyo. Hi mashine ya kusukuma inatudhalilisha.
Wanja poa sana, matunzo tu .
Anony wa June 30 @ 5:22 pm mie nakuunga mkono kuhusu issue ya kutafuta machine zilizoenda shule kuliko huo mkokoteni anaousukuma huyo mshikaji. Hizo tractor ndogo zinapatikana tena at a very reasonable price na zina range kati ya $1500 hadi $2500. Sasa jamaa wasije wakapiga bao kwa kusema wamenunua hizo trekta kwa $15,000, maana bongo kwa kupigana mabao hatujambo.
ReplyDeleteWalipewa picha ya lawn mower wakachagua the least expensive bila kujua ukweli. Huo ni utani na ndio kuharibu uwanja. na huyo mtu akitoka hapo mgogo umempinda...duh hapo mbeba box anaona kazi yake kama ni yke poa sana. Hat athe cheap tractor lawn mover could do the best job
ReplyDeleteIsijekua mwenye tenda kapewa millioni 15 kununua profession one kaagiza hiyo.
ReplyDeleteJamani hata kabla hawajakabizi hilo liwanja tuwaulize hela za lawn mower yetu tuliowapa ndio hiyo? Manual labor hatutaki tena.
ReplyDeleteWe need a good one
Tusilaumu serikali hilo wanja bado hatujakabidhiwa hivyo wanatumia the cheap cheap one siku wakitupa tutawauliza the good good one iko wapi??? Nadhani ilikua included kwenye contract he he he ehe
Kwanza hao wafanyakazi lazima wawe na uniform,lazima tuheshimu huo uwanja.Naunga mkono watu washindane kuchagua jina la kiwanja..sio lazima liwe la Kiongozi..kila kitu Tz kitakuwa na jina la kiongozi while kuna majina mengi mazuri
ReplyDeleteIangalieni kwa macho na akili hiyo lawn mower! Sio manual, jamani! Kwani hiyo mashini juu ya sehemu ya majembe ni ya nini? Hizo waya kutoka kwenye mashini hadi usukani wa mwendeshaji ni za nini?
ReplyDeleteMwendeshaji anaonekana kana kwamba anasukuma manually. labda hakufundishwa namna ya kuongoza mashini hiyo. Amezoea hizo za manual ndio maana simama ya namna hiyo.
Wengie mnaropoka ropoka tu.
ReplyDeleteNakubaliana na Uwanja wa Nyasi kuwa mashini hiyo si manual! Hiyo mashini ni sawa na hizo zitumikazo katika kula theluji huku kwenye nchi za theluji!
kama alivyosema, trekta linaharibu the turf. Kwa hiyo walioleta hiyo mashini...natumaini ni hao hao waliojenga hilo wanja, walijua!
Cha maana ni kuwa na mashini za namana hoyi kama tano hivi ili kufanya kazi upesi.
Acheni kuropoka. Mwulizeni Michuzi, ambaye ameiona mashini hiyo, kama kweli ni manual!
Jamani Mliotoa maoni kuhusu hiyo mashine hata mimi nawaunga Mkono. Lakini hebu tusipende kulaumu Serikali kwa kila kitu. Ukweli Huu uwanja badoupo chini ya Mkandarasi na Serikali bado hata kukabidhiwa kiwanja. Kwa hiyo kama ni mashine ya Domextic use hilo bado lipomikononi mwa mkandarasi. Inaonyesha kuna wadau wao wanaugonjwa wa kukosoa serikali tuuuuuu. Bila hata ya kufikiria ukweli nani alaumiwe.
ReplyDeleteS.alaikum wadau pls. nijulisheni lini huu uwanja utafungulia rasmi na mimi nipate kuja Bongo, Naishi Muscat na hamu niwepo siku ya kufungua uwanja.
ReplyDeleteMwahahaaaaaaaaaaa, sasa uwanja mkubwa wote huo atamaliza saa ngapi?
ReplyDeleteYaani wanatujengea uwanja kama huo lakini hawana kigari cha kuufyeka?
Kweli tuko Afrika haahhaaaaaa
daim!!! is he gonna finish kweli na usawa huu wa lawn mower ya kukatia back yards?? They better buy big equipment or something!!
ReplyDelete