mdau wa amstedam kaleta changamoto hii sasa hivi na kuwataka waundaji wetu wawe wabunifu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2007

    TPDC introduces gas-powered vehicles

    2007-07-04 09:24:38
    By Felix Andrew

    The Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) has broken new ground by showcasing that vehicles can run cheaply on natural gas instead of expensive petrol and diesel.

    Through the initiative, TPDC hopes that other motor vehicle owners, including institutions would soon choose to convert their automobiles into gas fuelling systems and do away with expensive and environmentally inhospitable fossil fuels.

    The excessive burning of fossil fuels is blamed for carbon dioxide emissions, a greenhouse gas blamed for causing global warming.

    Speaking to this paper on Monday during the on going Dar es Salaam International Trade Fair (DITF), in Dar es Salaam, the TPDC Public Relations Officer, Felix Haule, said TPDC would establish the first natural gas selling centre in Dar es Salaam within this year.

    He said the centre would be located at Ubungo close to Songas gas-to-power generators and would be providing services to customers who would have already converted their vehicles into gas burning systems.

    TPDC has a pool of experts who can play around with the mechanics of engine adaptation.

    One has to part with at least 1m/- to switch some engine parts from fossil based fuelling to gas systems, he said.

    TPDC has already procured two cars running on gas and plans are afoot for adapting its remaining office fleet into gas runners.

    Some of the advantages likely to be obtained by gas-based vehicle owners include savings on fuel consumption and lower price per unit compared to the fossil fuels.

    Cars running on gas are said to have 60 percent reasonable standard of consumption of fuel per distance as compared with those using fossil fuels.

    Again, as of yesterday, while the pump prices of petroleum products had shot up to 1,500/-, the same litre of compressed natural gas (CNG) would be sold at 810/-, according to reliable sources.

    While this technology looks apparently new on Tanzania`s market, some countries like Argentina, India, Egypt, South Africa and Norway had long past adapted to it.

    Meanwhile, TPDC has confirmed that recently discovered natural gas deposits in Mkuranga District, Coast Region would be mined latest three years to come.

    The corporation`s principal geologist George Ngwale, said Mkuranga natural gas deposits which were discovered in January this year would be mined from 2010.

    `At the moment we are in the process of surveying other possible areas until we strike five wells or even more, as this is widely considered to provide economically viable deposits for miners.

    TPDC in collaborating with an exploration company Maurel & Prom would conduct surveys over additional 200 kilometers within Mkuranga District.

    The cost of surveying a single gas well is estimated at between USD10m and 20m.

    * SOURCE: Guardian

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2007

    Hivi Tanzania hatuwezi kuwa na watengeneza bidhaa zikiwemo Boti kama hiyo kama watengenezaji wa bidhaa feki kama India na China ili tuinue Uchumi wetu na kuvipa uwezo viwanda vyetu mahali pa kuanzia kukua?

    Nchi nyingi zilizoendelea duniani zilianza kwa kutengeneza bidhaa feki. Walianza kutengeneza kwa ajili ya soko la ndani baada ya kuona ndani zinakubalika wakaanza kuuza nje ya nchi.Bidhaa feki au za kiwango cha chini ndio msingi wa tekinologia ya viwanda na ukuaji wake duniani pote.

    Niliwahi zungumza na Profesa wa viwanda Kuhusu tamko la Waziri wa Serikali ya Tanzania kuhusu kupiga marufuku bidhaa zinazoitwa feki toka China na India akaangua kicheko akasema mtakalia hayo hayo wenzenu wanasonga mbele kwa kuanzia angalau kutengeneza hizo bidhaa feki ! Akauliza nyie Watanzania bidhaa feki za kwenu ni zipi ambazo angalau mwaweza sema tumemudu kutengeneza hiki! Akasema mnapiga marufuku bidhaa za wahindi na wachina ili muingize za wazungu! Mnachofanya ni kushindanisha wakoloni waletao bidhaa nchini kwenu kuwa yupi bora kuliko mwingine wakati wenyewe mko hoi!

    Lazima wasomi wetu waanze kutengeneza hivyo vitu viitwayo feki wasiogope wala kuona haya labda vitu hivyo view hatari kwa maisha ya watu kama dawa na vyakula.

    Nchi zote zilizokomaa kiviwanda zimeanzia kutengeneza vitu feki vya hali ya chini iwe Japan,Marekani,Ulaya,Singapore,Taiwan,Korea, n.k

    Nchi zote zilizoendelea kiviwanda msingi wake ulianzia kutengeneza bidhaa feki za kiwango cha chini.Kama nchi yako haina viwanda na unataka viwanda vianze kuibuka ruhusu vitu feki vianze kuzalishwa.Wanablog mnaweza nishangaa lakini ndio ukweli.China,India kuna viwanda feki vitengenezavyo bidhaa feki za hali ya chini kila kona,Singapore,Taiwan,Korea kote huko hadithi ni hiyo hiyo.Ukizuia ukuaji wa viwanda vya kutengeneza bidhaa feki unaua ukuaji wa viwanda na hutakuja uone sekta ya viwanda ikikua ndio maana China na India hawataki kukomesha hilo.

    China na India ndiyo zinaongoza sasa hivi duniani kwa utengenezaji na usambazaji vitu feki toka viwanda vyao feki. Na ndizo nchi zinazokuja juu sana kiuchumi na dunia nzima wanawashangaa.Watu dunia nzima wanavihitaji vitu vyao feki kuanzia saa zinazoharibika baada ya mwezi mmoja n.k

    Wachina na wahindi hawaogopi mtu na hawaoni haya hata uwapigie kelele uwaite wafalme wa utengenezaji vitu feki wao wanaziba masikio na wanasonga mbele kitekinologia kwa spidi ya ajabu Sababu hawaogopi kutengeneza na kuvipeleka sokoni hivyo feki nchini kwao na nchi nyingine .Mapato ya mauzo ya vitu feki vyao wanayatumia kujenga viwanda vizuri zaidi vizalishavyo bidhaa nzuri zaidi.

    Naomba serikali ianze kuachia wazalishaji vitu feki kuanzia sufuria,spea,n.k Serikali sana sanaidhibiti tu madawana vyakula lakini iachie
    Isiwafuate wala kuwabana wazalishaji wa bidhaa feki za hali ya chini na ma-copy cats wanaocopy na kumodify vitu na kuviuza kama vyao.

    Nalipongeza Jeshi la Tanzania limeanza kutengeneza magari ya Nyumbu.Nimeyaona yale magari. Nawaomba waanze uzalishaji mkubwa na waanze kuuza mtaani. Wasijali kiwango kuwa hadi yafikie viwango vya Kimataifa waachane na hilo walete magari sokoni.Waangalie kama yana soko.Waanze kwa kuangalia soko la ndani kama yanahitajika basi.Nyumbu zingeweza kabisa kuanza kuuzwa.Ingekuwa ni India au China magari hayo yangeshauzwa karibu dunia nzima.Wachina na wahindi hawahangaiki hata siku moja kuangalia sana kama bidhaa zao zinafikia kiwango cha kimataifa au la.Kwao la msingi kitu kama soko linakihitaji inatosha kiwe original au feki cha muhimu ni kuuza.Anayetaka anunue asiyetaka aache.

    Kuna Chuo kidogo Cha binafsi cha Ufundi kinaitwa Bruno kama sikosei Pale Buguruni Dar es Salaam kimetengeneza gari ya mbao za hovyo hovyo na gari hilo linatumia mafuta ya taa.Gari lile liliweza safari hadi Bagamoyo toka Dar es salaam likaenda na kurudi bila ajali wala nini.Linaonekana kama feki lakini kama linaweza kwenda mbele atengeneze mengi auzie watu vijijini kama watu wa mjini hawataki. Ataendelea kuimarika kitekinlogia taratibu kadiri anavyoingiza pesa za mauzo.Ingekuwa India au China Gari lile ungelikuta sokoni watu wanaliuza.Sababu wao hawaogopi.


    Tanzania tunahitaji kuwa na Ma-copy cats kama walivyo wahindi na wachina.Bidhaa ikitoka leo Marekani kesho waweza kuikuta bidhaa ile ime-kopiwa na kufanyiwa marekebisho kidogo na kutengenezwa chap chap kwa jina lingine.

    .Mfano una-copy Coca Cola halafu unabadili formula kidogo ya kutengeneza hiyo soda halafu soda yako mpya unaiita Cocopola hakuna atakayethubutu kukushtaki popote. Unacopy gari ya mjapani ila unabadilisha mambo kidogo mfano badala ya usukani kuwa kulia au kushoto wewe unauweka katikati,Halafu hiyo gari badala ya kuita Toyota unaiita HOYOTA.

    Wahindi wana gari zao feki feki zinaitwa Mahindra,Tata,Ashok,na baskeli zao za Guta zisizokidhi viwango vya kimataifa n.k lakini maisha yanaenda na wanauza.

    Marekani na ulaya hawataki baiskeli feki ya Guta lakini watanzania wananunua.

    Mchina huiga vitu vingi tu mfano baiskeli.ila hubadilisha mambo madogo tu mfano unakuta ukifunga nut za Mchina zake unakuta zinafunga kuelekea kushoto badala ya kulia.Yote ukiwa ni ujanja wa kukwepa asionekane ka-copy ! Ujanja ambao watanzania pia tunaweza! Kinachotakiwa unaiga bidhaa,unaifanyia modification kidogo,unaipa bidhaa hiyo jina jipya unaipeleka sokoni ukishaiandika made in Tanzania au styled in India,China,Usa ETC

    Nashukuru nilipita safari moja pale Sinza,Dar Es salaam Kuna Eneo Linaitwa Sinza Kwa Wajanja nadhani kweli kule kuna wajanja wa kutengeneza bidhaa ila bahati mbaya wengi ni wachaga tu,Makabila mengine na watanzania wengi wakiwemo wasomi ni vizuri nao wakawa wajanja kama wahindi,wachina,wakorea,wataiwan,wasingapore na hawa wakazi wa Sinza kwa wajanja.

    Inatia Uchungu kuona baaada ya miaka 40 ya uhuru hatuna hata kiwanda cha kutengezeza vijiti feki vya kuchokonolea meno(toothpick) !yaani eti navyo vinatoka China!Vinaagizwa kwa hela za kigeni! Hivi nchi hii tuna wazimu! Mainjinia wote tuliosomesha toka tupate uhuru hakuna awezaye kuanzisha kakiwanda kakuchonga hutu tujiti twa kuchokonolea meno? Wakati tuna miti inatengeneza mifagio iitwayo chelewa ile ukichonga unapata hivyo vijiti.

    Michuzi kanunue wembe wa shilingi mia moja tuanze kuchonga vijiti vya kuchokonolea meno. .Tusisubiri Maprofesa watanzania wa Engineering wa vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi waanzishe hivi viwanda vya vijiti wako busy sana Darasani wakifundisha nadharia wanafunzi wao.

    Tokea uhuru wako busy sana kufundisha nadharia isiyozalisha hata kijiti cha kuchokonolea meno!

    Koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2007

    Saidi,
    Nafurahi kwamba kwa kukujua kwangu kwa miaka mingi umekuwa
    ukiwa-inspired
    and General Ulimwengu. If i may recall his days correctly;he was not
    keen on
    specific areas to educate and correct. His broad range of subject is
    what
    put him in a position to "inspire" many including your self.
    Why am i using this example?, because i am displeased with your efforts

    kulishikia Bango hili suala la WTM. Naona hukuchoka kuli-put "out in
    the
    open" but from your todays notes...it looks you are close to taking a
    step
    or initiate a move kuwa -sue hawa jamaa.Thats solely up to you.My
    question
    to you is.... Mbona kuna soo many "Skendoz" Nyumbani amabazo umezitoa
    only
    once or twice; if more than that,then it was just more in a informative
    way
    bila kutofautisha na magazeti mengine ya nyumbani ambayo huandika
    "udaku"
    just for the sake of selling headlines.
    Kama utasema umezisahau au zimekupita, then I AM WILLING TO REFRESH
    YOUR
    MIND!.
    1.Tanesco na Richmond. (imezimwa na inataka kusahauliwa-but hela ya
    wadanganyika haitasahaulika $ 175 )
    2.BAE Systems na Rada.($40
    3.Bank of Tanzania na Dalali-balali( no final figure $ 200), iko very
    current but you have disatance your self, mainly for fearing to kill
    "ASPIRATION" zako kuwa Rais wa Tanzania -2025-if i remember well.
    Base of my light knowledge of your self, the size of your wallet is soo
    huge
    in terms of business cards,therefore, it is my (our) assumption that
    getting
    inside information or "Memos" on those aforementioned "SKENDOZ" will
    not be
    an issue to you.
    Lastly, i wish you the best on your efforts to educate and kuwa-komboa
    Wantanzania.Lakini, usitumie vi-"skendo" mtoto kujenga jina na
    kuwapaka
    matope watu huku ukiacha yale Watanzania wanayohitaji kuyajua na
    kukombolewa
    nayo yakipita.
    (KAMA HII GLOBU-as Michizi Says,ni ya uwazi i wish this to be posted on
    the
    front Page.

    Mzanzibara

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2007

    We unayejiita mzanzibara(mzenji ni mzenji tu na wa bara ni bara) bora ungeandika maoni yako kwa lugha moja, aidha kiswahili au kingereza.
    Umechanganya lugha na hata ulotaka kusema umejichanganya pia na kutoeleweka ni kipi hasa ulichotaka kukieleza.
    Ni sawa na mtoto anayejifunza kusema lugha mbili kwa wakati mmoja. Akitaka kusema mojawapo, nyingine huvamia na kujikuta anatamka maloloso kama ulivyo wewe.

    ReplyDelete
  5. Yaani nasikitika kuwa nimeona maono ya Koloboi baadaye sana.Hata hivyo nina kubaliana nawe 100%!Yote uliyoandika ni ya kweli na yanahitaji katafakariwa haswa!Tunalalamika foleni za magari ni ndefu sana huku magari yanazidi kuingizwa mjini,barabara zenyewe ndogo na mbovu kila kukicha.
    Watu wanabanana kwenye madaladala kama mizigo.
    Ni kwa nini hao waunda mbinu wasomi hawafikirii kutumia maji ya bahari tulinayo kusafirishia watu na bidhaa kutoka upande mmoja wa Dar hadi mwingine ni swali la dola milioni!!
    Viongozi wakienda nje wanapofushwa na shamrashamra wanazokuta basi hata hawakumbiki kuwa tiketi zao zimelipwa na raia na kwamba wakiwa huko waangalie maarifa gani yakuigwa na kuletwa nyumbani kwa faida ya nchi.
    Inaudhi sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...