dege letu halina rangi siku hizi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2007

    sasa wadau hii ina maana hii ndege sio ya ATC au vipikwani hamna nemboya twiga tuliyo izowea

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2007

    Waipake rangi hizi hapa

    http://news.bbc.co.uk/media/images/38177000/jpg/_38177860_atc-300.jpg

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2007

    we michu vipi? mbona lina rangi nyeupe?! nadhani unamaanish rangi za taifa! haya. kama ni gharama kupaka tena rangi za taifa basi wafanya juhudi KUBWA kwa kumrejesha twiga pale mkiani juu maana alivyo pale mbele haikolei

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2007

    Ndege yetu hiyo inaweza kubakia na hiyo rangi nyeupe. Lakini kuna haja ya kuliipatia shirila la ATL umbo jipya. Wakati ndio huu.

    Shirika hili lilianzishwa kama la serikali. Ndio maana ya kuipamba ndege hiyo kwa rangi za alama ya taifa (bendera yetu).

    Kama shirika la taifa, ATL lilirithi nembo ya Twiga lakini kwa wakati tofauti.

    Alama ya Twiga ilikuwa ndio heraldry kikoloni kwa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa ni Mashua au Dau. Kwa Kenya ilikuwa ni Simba na kwa Uganda, Korongo (ndege). Nembo hizi zilirithiwa na nchi zetu huru za Afrika Mashariki.

    Kiutalii, kutokana na Kenya kutangaza Mlima Kilimanjaro (kana kwamba upo nchini Kenya): "Ukitaka kuona Mlima Kilimanjaro, njoo Kenya!" Tanzania ilijibu mapigo kwa kutumia slogan: "Tanzania: Nchi ya Mlima Kilimanjaro!"

    Kwa kutumia nembo ya Twiga, alama ya Tanganyika, ATL haikuleta umbo zuri kwa Tanzania; ilisahau Zanzibar! Ingawa Zanzibar ilijumuika kupitia alama za bendera yetu ya taifa.

    Lakini matumizi ya nembo ya Twiga na Mlima Kilimanjaro kuliifanya Zanzibar kusahaulika katika mikakati ya utalii, kana kwamba Zanzibar haikuwa sehemu ya Tanzania.

    Slogan ikabadilika ili kukidhi ya Zanzibar: "Tanzania: The Land of Kilimanjaro and Zanzibar!"

    Kwa kuwa sasa ndege yetu imevuliwa joho la kitaifa kirangi, kuna sababu tosheleza za kuwa na slogan inayoenda na wakati - slogan hai - ya mapito ambayo itaunganisha Tanzania kwa kutumia nembo za Twiga na Mashua au Dau.

    Nembo hizi mbili zina ujumbe wa aina moja, na zinaitangaza Tanzania yetu katika jitihada zake za maendeleo.

    Twiga ananyoosha shingo lake kufikia na kula majani ya miti mirefu; kajaliwa. Tanga la Mashua au Dau hujaa upepo na kuiwezesha mashua kupiga mwendo.

    Kama ulimwengu umeishajifunza kuwa "Tanzania: The Land of Kilimanjaro and Zanzibar", mathalani, kwa Kiingereza, slogan inayoenda na wakati inaweza kuwa "Tanzania: Soaring to New Heights!

    Endapo bado hatujafanikiwa kuufundisha ulimwengu, basi tunaweza kuendelea na slogan hiyo ya zamani na kuibadilisha kuwa new and improved:

    "Tanzania - The Land of Kilimanjaro and Zanzibar - Soaring to New Heights!"

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2007

    Ebwana weee! Kubwa na ninyeupeeeee kama yai la mnyama vile!

    Poa tu,inapendeza hata hivyo hivyo tu "No frills", kitu orgnic hicho mambo ya SAA yamefutwa na kifutio cha raba bendi kilichofungwa kwenye kalamu ya bick! he he

    SteveD.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2007

    Mambo ya ubinafsishaji hayo wakuache na rangi zako wanakuogopa?, sasa mkataba umekwisha wamekuacha hivyo hivyo bila ya kurudisha rangi ilituingie garama ya kupaka, Mmmmmmmm mambo hayo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2007

    Ukiona hivyo ujue ndege hiyo sio yetu wenyewe ila tumeikodi kwa muda toka nchi fulani, kwa hiyo wanaona ni gharama kubwa kwenda kuipaka rangi za Taifa na baada ya muda kidogo kuja kuzifuta tena kwa gharama kubwa.
    Umaskini bwana, kitu kibaya sana jamani!
    Mungu Ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 04, 2007

    Wadau hivi tuna ndege ngapi siku hizi? Maana hizi ndege ya mwaka 47' sio za kuamini kwa sana .

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2007

    Kwamba ule ushirikiano na SAA, moja ya makampuni makubwa ya ndege duniani, ulivunjika, ni kielelezo tosha ya kwamba Mtanzania ni mtu aliyelaaniwa na hatakaa aweze kujitoa kwenye lundo la umaskini.

    Kwamba tunataka sasa kurudisha ATC kuwa SU 100%, ni kithibitisho zaidi ya jinsi tusivyokuwa na business acumen.

    Biashara ya ndege ni ngumu na makampuni mengi yanajenga alliances ili ya survive. BA, KQ, KLM, Precisionair... wote wanatumia hii strategy. Kwa nini tulishindwa kukubali SAA wachukue controlling shares za ATC? Walipokuwa na 49% shares unafikiri wangefanya investment yoyote ya maana kwenye hilo shirika?

    Na sasa watu wanatuangalia na kutuona wa-TZ siyo watu wa kufanya nao biashara.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 04, 2007

    This is a rented plane. There are currently two planes operating for ATL and they are worked overtime!
    Mimi nimetoka kusafiri na Air Tanzania jana kutoka Dar mpaka KIA na kurudi. Service ndani ya ndege ime deteriorate sana. Yani, we acha tu. Lakini wana keep time ile mbaya, kitu ambacho lazima niwapongeze. Niliweza kwende Arusha asubuhi 6.30am and kurudi Dar by 5.15pm siku hiyo hiyo. And it's nice to note the pilots are still Tanzanian (alikuwa Capt. Lazaro). I think there are some changes planned for ATL (hence the new leadership) lakini kama watanzania lazima tuwape support naana badala ya kuwasema tu. Let us be constructive.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 04, 2007

    AWAL YA YOTE – AFADHALI UBIYA NA SAA UMEKUFA!
    PILI, HONGERA TC KUTOA NEMBO ON THE TAIL – AIBU GANI WALITUTIA KUMTOA TWIGA WETU NA HAPO WALIKUWA NA 49% SHARES TU. NA NYUMBA WAKAZIUZA NA KUTENGENEZA PESA WAO – HIVI TULIKUWA TUMELALA NINI? NI MATUMAINI YANGU WATAMRUDISHA TWIGA WETU. NA KAMA KUNA MTU TOKA TC ANASOMA HILI – TAFADHALI TAFUTENI KWA HUDI NA UVUMBA KUPATA NDEGE ZAIDI – TUMECHOKA KUPANDA KQ (KENYA AIRWAYS) – SERVICE YAO NI MBAYA AJABU – TUMEZOEA UKARIMU WETU BWANA AND THE PRIDE OF SEEING OUR AIRCRAFT IN A FOREIGN AIRPORT LANDED TO COME PICK US UP.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 04, 2007

    Ndege hiyo kwanza imekudishwa bila shaka toke middle east au sothafrica.kwanini hela zakina Balali na wengineo wanaokutwa wameiba wasinunua ndege moja tu kubwa 747 au zaidi itakayo kuwa inasafiri from tanzania to england or america im sure if it operates for one year properly they will be a ble to buy another one. otherwise walikifikirie hilko in future kwenye budget

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 04, 2007

    Nakubaliana kabisa na Anony wa 12.28 hapo juu. Namimi nimechoka kabisa kupanda KQ!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...