
mabosi wa kampuni ya mikopo ya easy finance wakitoa maelezo kwa wageni walotembelea banda lao uwanja wa mwalimu nyerere ama sabasaba leo. hawa jamaa hakika wanasidia watu wengi kwa mikopo ya chap chap tena kwa masharti nafuu mno

watu kibao wanatembelea easy finance kujua namna ya kupata mikopo kirahisi
we! nani kakwambia Easy Finace wanatoa mikopo ya masharti nafuu? hao ni kati ya taasisi zinazokiuka taratibu za kutoa mikopo duniani, katika umasikini huu uliokithiri ukiweka riba 30% kwa mwezi UNATEGEMEA NINI baada ya miezi mitatu KAMA SI KUDHULUMU DHAMANA ALIYOWEKA MKOPAJI?
ReplyDeleteNaomba nikuunge mkono uliyetoa maoni hayo juu. kwa jinsi wanavyochemka, siwezi kusema, ushasema yote.
ReplyDeleteKwa kweli Riba ya 30% wanacharge ukweli, lakini hawa Jamaa wanasaidia sana wajasiriamamli, mikopo yao ni short term na imelengwa kaw ajili hiyo, ukitaka mwaka wa kulipa si uende CRDB au NBC, tuache kuwa negative kwa kila kitu hao wanaokopa hapo hawajashikiwa bunduki, wameenda na wamesign agreement, tukubali kuwa market zinabadilika, na tuwaunge mkono wazawa wanapofanya jambo
ReplyDeleteKwa nini hamuwezi kuwasifia hata siku moja wazawa wanapofanya kitu cha maendeleo, mimi nimekopa Easy Finance na Riba yao ni negotiable, hii ni solution kwa serious business people with sort term / bridging finance issues, sio mikopo ya nyumba wala ya ndoa, mbona makampuni ya Wasauzi hamuyazungumzii na riba zao?
ReplyDeleteTunataka INTEREST RATE babu sio kusema mikopo ya chap chap. Ukipewa mkopo wa chapa chap wakati Interest Rate yake ni 35%- 45% kuna faida gani? ni kujikita kwenye umaskini bila kujua
ReplyDeleteanon hapo juu, Michuzi aliposema masharti nafuu hakumaanisha interest, nadhani alimaanisha muda mfupi kati ya application ya mkopo na kupewa mkopo..jamaa ukiapply leo mkopo unapata kesho, huko ktk mabenki ukiapply leo unapata baada ya miezi sita..Aminia Isaack
ReplyDeleteinterest 30%...huo ni udwanzi na kama ni msaada basi ni kuwaongezea watu umaskini tuu,na serikali lazima iweke CAP kwa hizi financial bodies interest wanayoweza charge la sivyo huu ujanja wa kutake advantage sababu watu wako desparate hatutafika popote
ReplyDeleteWATANZANIA SIKU ZOTE WAKIONA WAZAWA WANAFANYA KITU LAZIMA WATOE KASORO!!!SASA KAMA WEWE UMEONA INTEREST NI KUBWA SI UACHE HAO WATU WANAOENDA KUKOPA ZAIDI YA MARA KUMI HAWAJUI HILO TUACHE TABIA ZA KIZAMANI KUSEMA TU MANENO YASIOKUA NA MSINGI...HAWA JAMAA KAZI WANAYOFANYA MMEPATA KUJUA MATATIZO GANI WANAYOKUTANA NAYO?ATLEAST BASI MUACHE POROJO ZETU ZA KILA SIKU COZ HII MIKOPO TENA KWA MAANDISHI YA KARATASI IKO SEHEMU KIBAO TZ NA BORA HAWA WANOFANYA OFFICIAL TUACHE UZAMANI KAMA UNAONA KITU HAKIKUFAI UNAKAA KIMYA SIO KUKANDIA ETI KUONGEZA AU KUJIKITA KWENYE UMASKINI????NA HIZO SHIDA WATU WANAOTATULIWA NA KUENDELEA NA KAZI ZAO?TUACHE HIZI TABIA TUWE KIDOGO NA UZALENDO MAANA HATA MABENKI HAWAKUANZIA KWENYE INTEREST HIZI SO KWAKUA WAMEANZA IKO SIKU ZITAPUNGUA LAKINI SIO KUKANDIA TU NI..........NA NDIO MAANA TUNAENDELEA KUTAWALIWA NA WAHINDI HATA WANGEKUJA NA KUSEMA INTEREST 60%TUNGEONA SAWA NA KUENDELEA KUBAKI NYUMA TU SIKU ZOTE!!!!!
ReplyDeleteNyie watu, EasyFinance wana riba ya kuanzia 1% hadi 30% kutegemea na muda wa mkopo, amana uliyoweka na malengo ya mkopo.
ReplyDeleteSio kweli kwamba mikopo yote ina riba ya 30%.
Kwa maelezo zaidi cheki www.easyfinance.co.tz
E bwana michu huyo wa pili kushoto ni G' Mkili nini jamaa alikuwa na msimamo sana pale UDSM sijui huku Bank sasa hivi atakuwa kabadilika au vipi. Ila anapenda kutetea watu natumai mikopo ya wajasiliamali ataifagilia kama yupo kwenye authority.
ReplyDeleteNdugu yangu michuzi wakati mwengine jaribu kujua credability za watu unaowauza hapa. Yaani hata kujua siri ya mtaji wa biashara ya ndugu yetu huyu? Kaka chonde ndugu yangu....unakumbuka juzi tu ilibidi uchomoe issue ya Jack Pemba hapa...
ReplyDeleteanonymous hapo juu. Mkili hawzi kujihusisha na wajanja wa mjini. Mkili Kibosile katika GREEN ACRES ACADEMY hapa Dar. Amejaza wapiganaji wenzake huko. Natumai watoto watakuwa wakakamvu kama walivyo walimu wao na sio another ACADEMY generation kama iliyojaa hapa mlimani sasa.
ReplyDelete