Hivi karibuni mdau nilikua safarini mkoani tbr, shinyanga na mwanza. Nilitumia usafiri wa bus na train, hali niliyojionea ni kwamba wasafari wa train wanahitaji msaada wa haraka, kwani usafiri wake hivi sasa hauna 'appointment', kuharibika njiani na injini kushindwa kupanda viliama ni kiti cha kawaida. Serikali ifanye haraka mhindi akabidihiwe 'gogo' awaokoe walala hoi!
(mdau: abdallahmrisho.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2007

    Hongera sana mdau kwa ku risk camera yako kutuletea picha ya Gogo, Hii inanikumbusha zamani usafiri wa gogo unasimama toka mwanza mpaka Dar. Watu wengine wanapanda na kuku, nakumbuka kuna siku jogoo aliwika tukiwa ndani ya mchuma akatuamsha.

    Ukija upanda wa kigoma mabehewa yote yalikuwa "Mawese" or Palm oil, ila nafikiri siku hizi kuna Afadhali mdau Baada ya aliyekuwa waziri wa mawasiliano "Willium Kusira" kuweka sheria ya kutaka abiria wote wawe na seat miaka hiyo.

    Humo bwana kwa sasa ni panya mdau nakumbuka mwaka jana jamaa aliweka karanga kwenye begi lake Panya wakalitoboa bwana. kweli kuna haja ya kubinafsisha hii huduma ili kwenda na wakati.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2007

    Lakini kuna tetesi zimeshaanza kuenea miongoni mwa wafanyakazi wa shirika wa sasa kuwa muhindi atachemka na kuna njama za kuhakikisha anashindwa. serikali haina budi iliangalie hilo, kama kuna kitu watu watamkumbuka raisi Kikwete, basi ni kuwarudishia wakazi wa reli ya kati usafiri wa train wa uhakika!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2007

    HE !! "..KAJAMBA NANI.."

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...