Home
Unlabelled
jkt
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
namwona mzee kawawa na marehemu chief adam sapi,those were the times,jkt ilisaidia sana kuunganisha watoto wa maskini na wale wa vibosile.
ReplyDeleteaaaaah!! Yule pale Kawawa!!!! yupo Fit ila kitambi hicho vp?
ReplyDeleteNi macho yangu ama nimefananisha? Nimeona mtu kama Rashid (Kawawa a.k.a Mhogo Mchungu) na Marehemu Mwalimu Nyerere a.k.a Mchonga (RIP). Ni wao au nimekosea? Walikuwa kambi gani na hiyo ilikuwa ni operation gani? Ukiona Rais na Waziri Mkuu wanaenda kupiga kwata elewa hiyo ni shughuli pevu. Siyo viongozi wetu wa siku wanakemea RUSHWA wao wenyewe ndo wa kwanza kulamba rushwa!
ReplyDeleteKwa kweli jeshi lilikuwa zuri sana. Kwa maoni yangu ningependelea kama lingerudi. Angalia vijana wengi walivyo mayai mayai! Jeshi kama hilo la JKT lilisaidia kuwafanya vijana wengi kuwa jasiri na wakakamavu. Nasikia huyo mzee (kiongozi ) wa pili mbele kitambi chote kiliisha baada ya siku 3 tu! Inapendeza sana!
ReplyDeleteJKT ilikuwa ni nzuri sana, watu wanachanganyika bila kujali uwezo wa familia na baada ya wiki moja tu wote mnafanana wakati mwingine huwezi kutofautisha jinsia, ndio maana kuna tofauti kubwa kati ya vijana wa sasa na tuliopitia JKT, ila hawa viongozi katika picha nadhani kwata hawakupiga sawa sawa angalia mtu wa pili nadhani ni mzee RK bado tumbo limetokeza mbele. Kwa kweli aliyeua JKT alaaniwe, kwa sasa ni vigumu kuirudisha.
ReplyDeleteNi Mambo mazuri sana katika kuendeleza umoja wa kitaifa kwani mnakutana watu pande mbalimbali za nchi.
ReplyDeleteIla kwa sasa nschi yetu imeharibiwa na siasa, kila kitu kinaangaliwa katika mtazamo wa je kitaleta tija kwa chama tawala?, Maana wanajua wakiwaingiza watu kama "Ngangari" ndio watakuwa "ngangari kipeo cha kumi"
Ila kweli ni nzuri kuwajenga wasomi kuwa na feeling za hard time katika maisha na hivyo kuwafanya kuwa wazalendo zaidi wanaposhika nyadhifa za kuwatumikia walala hoi.
Michuzi haya mambo yanaumuhimu wake hata kwa sasa kwa sababu inasaidia kujuana kuongeza uzalendo na ukakamavu.
ReplyDeleteSio hilo tu kuna lile suala ambalo JK nyerere alilianzisha...unapojiunga na chama cha siasa lazima upate mafunzo kwanza ya kufahamu masuala ya kitaifa na hilani ya chama ukishafuvu ndio unakubaliwa kuwa mwanachama. Siku hizi hakuna hilo tena ..wanachama wanapatikana hata sokoni. Matokeo yake ndio hayo watu wanajikunga na chama kwa kufuata mtu. Na wanahama kutoka chama kimoja kwenda kingine kila siku bila kujua shughuli yao ni nni hasa kwenye chama.
Kujiunga na jeshi la kujenga taifa kutasaidia nini katika enzi hii ya sayansi na teknolojia? Kitu gani alifaidika nacho Nyerere au Kawawa walipoenda huko?
ReplyDeleteThis used to be GOOD. Tulijifunza ukakamavu, ujasiri, uzalendo, uadilifu, umoja na undugu. Viongozi wetu waliongoza kwa kunena na kutenda waliyonena. Leo mkuu anasema tusichangie harusi, lakini yeye anachangisha mamilioni anasherehesha watu! Haya, tutafika, hata kama ni kusiko. Makali ya bajeti ya Meghji yameanza kuonekana.
ReplyDeleteHellow Mr Michuzi nimeona suggestion mambo yarudi kama zamani, kumbuka pia kuna mabadiliko kibao sasa katika maisha kuanzia kwamfano serikali yetu tunasema inaendeshwa na katiba lakini Kama unafatilia bunge la tanzania, unaweza kuona kwamba hata bungeni kwenyewe kuna mabadiliko na matabaka pia. Maslahi ya wabongo yakitete wana mbunge aliyetoka kwenye chama cha upinzania anaonekana kama anazuia mikakati ya CCM nadhani wanahitaji kukaa na kuangalia katiba ya TZ inasema nini mbunge navyo fahamu mimi mbunge anachaguliwa na wananchi na anatetea masilahi ya wananchi sio ya chama kama waziri amechemsaha aambiwe sio akumbatiwe, kunamtu alisema " wazimbabwe ni wavumilivu sana" na mimi nakwambia mr michuzi sisi watanzania ni wavumilivu sana, Mambo haya tunao fanyiwa tumeuvumilia sana na tunaendelea kuuvumilia ila viongozi wetu wanatakiwa kujua kuwa tunaeleawa mchezo unaochezwa sasa huko bungeni.
ReplyDeleteTunacho takiwa kuwashauri hawa ndugu tulio wachagua watuwakilishe ni kitu kidogo sana kuchukua mifano mizuri kutoka katika nchi za wenzetu na kuacha mabaya " wachuje"
asante sana
Lowa
...usiwaamini hao wazee kazi yao ilikuwa tuu kwenda huko na kupiga picha za propaganda ili kuwaonyesha wananchi nao eti wanaishi kama wengine...kamba sana hao kumbe wakitoka hapo wanaenda kulala kwa mkuu wa jeshi na vimada na check up london
ReplyDeleteWasamaria wema wameendelea kujitokeza na kuwachangia wanafunzi 27 wa Kitanzania ambao wamekwama nchini Ukraine kufuatia serikali kukataa kuwalipia gharama za masomo nchini humo.
ReplyDeleteAkizungumza na Nipashe, Mkurugenzi wa Mipango wa Taasisi ya Elimu ya Sheria Nchini (TANLET), Bi. Nerakindo Kessy ambao ndio walioombwa na Umoja wa Vyama Vinne vya Upinzani nchini kufungua akaunti maalum kwa ajili ya wanafunzi hao, alisema kwa sasa akaunti hiyo ina zaidi ya Sh.milioni mbili na nusu.
``Tunashukuru Mungu kuwa watu mbalimbali wameendelea kutoa michango yao kupitia ile akaunti na mpaka tunavyoongea kuna fedha ambazo zinakaribia kuwa milioni tatu ,`` alisema Bi. Kessy.
Mwezi uliopita wenyeviti wa Umoja wa Vyama vya Siasa, Bw. Augustine Mrema (TLP), Bw. James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Freeman Mbowe (CHADEMA) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), walitoa ombi la kufunguliwa kwa akaunti hiyo na kuahidi kuchangia kiasi cha shilingi Milioni moja.
Fedha zinazotakiwa ni Sh. Milioni 13, sawa na dola 10,100 za Marekani. Pesa hizo zinatakiwa kwa ajili ya malipo ya malazi na chakula, aidha wanafunzi hao wanahitaji zaidi ya Sh. milioni 63 sawa na dola 39,000 kwa ajili ya ada.
Bi. Kessy aliwaomba wasamaria wema wengine kuendelea kujitokeza kuwasaidia wanafunzi hao ambao kimsingi hawana mtu wa kuwasaidi huko walipo zaidi ya Watanzania wenzao.
Aidha, alisema kesho (leo) anatarajia kuwatumia wanafunzi hao kiasi cha Dola 1000 ili ziweze kuwasaidia katika masomo yao huko Ukraine.
``Nilikuwa jana niwatumie fedha kutoka katika akaunti hiyo lakini kukawa na mambo fulani fulani yamenikwamisha lakini kesho (leo) nitawatumia,``alisema Bi. Kessy.
Alisema wameamua kuanzisha kadi maalum na kuzitembeza sehemu mbalimbali ili kufanikisha kazi hiyo.
Bi.Kessy aliitaja akaunti hiyo kuwa ni namba 201660043 ya Benki ya National Microfinance (NMB), tawi la Bank House, jijini Dar es Salaam.
SOURCE: Nipashe
huyo wa pili mwenye kitambi pia mwanajeshi?????
ReplyDeleteaisha habib
Yesu na Maria wewe Michuzi unauliza kama wananchi wanataka JKT (JANA KITUMBO TAYARI)iludi kama mambo yenyewe ni hivyo basi wananchi wanatakiwa wasiwe na vitambi.
ReplyDeleteNadhani yule wa pili ni Mzee wetu Mh. Rashid Kawawa. Ama kweli nguvu kitu cha kwisha nimemkumbuka bwana mmoja aliyekuwa na uwezo wa kurusha jiwe kutoka pale kituo cha basi Moroko hadi Kariakoo enzi za ujana wake lakini sasa hivi amezeeka kaishiwa nguvu hata akitema mate hayafiki chini!!!! Tuwaenzi wazee wetu na kufuata nyayo zao.
ReplyDeleteNamwona Mzee Kawawa na Adamu sapi (RIP) na wengineo!
ReplyDeleteWazee hao walijiunga ili kuunga nkono Jeshi hilo.
Siku hizi wazee wengi wa nmna hiyo wamepitia Jeshi hilo.
Michuzi bwana acha izo mambo ya gani hayo yarudi tena? Maendelea yanakuja kwa kuangalia historia na kusonga mbele sio kuangalia historia na kubaki huko huko. Sasa ivi historia inatakiwa itusaidie kushepu fyucha yetu na wala si vinginevyo!
ReplyDeleteNamwona Kawawa Hapo, duh si mchezo.
ReplyDeleteanon uchungu ndio nimeumalizia hapo kwani hapo mkurugenzi wa crdb anaona direct. Na pia ahsante kwa kuwa mfano mzuri wa waosha vinywa kwani umeshindwa kutoa maoni yako bila kutumia lugha stahiki.
ReplyDeleteSerikali ilikuwa na malengo mazuri ya kuwapitisha wahitimu kwenye haya mafunzo ila wakufunzi walikuwa na chuki binafsi kwa wanafunzi wao, kwa kweli mimi nilikuwa siifagilii hata kidogo.
ReplyDeleteWalioenda na vitambi JKT mbona walikoma. Baada ya wiki mbili kitambi kwisha! Afande anasema, "wewe unakuja hapa dume zima kama una mimba! Tutaondoa hiyo mimba sasa hivi! Haya! Kichwa chini, miguu juu!"
ReplyDeleteHapo Mtanzania anakula kiapo. akimaliza kula kiapo anaendelea kusilibwa na kauli mbiu "..Kipimo cha mtu ni kazi.." "..Mtu ni kazi.." "..Kilimo ni uhai.." "..Rasilimali ya mnyonge ni umoja.." "..Ubepari ni unyama.."
ReplyDeleteZikiisha kauli mbiu idhaa ya taifa tangu saa kumi na mbili asubuhi hadi saa sita usiku vipindi: Tunafungua siku na Swala na sala. Baada ya dua Matangazo ya Vifo. Yakiisha unasikia sauti ya Dozza, Mwana wa Manyema, Jabari la Muziki Hayati Marijani Rajabu "kumekucha jamaa, kumekuchaa, majogoo vijijini yanawikaaa, hata na jua mbinguni limetokaaa, wazalendo amkeni tukafanye kazi sasa..Oooh mama, tusonge mbele.." Huku Dozza anakuhamasisha na Abdalla Mlawa anakuwakia "..Wee amka, nakuona anavyovuta shuka amka.." Kumekucha inafuatiwa na Majira. Baada ya Majira, Taarifa ya Habari(iliyojaa siasa za chama), ikiisha mazungumzo baada ya habari/matangazo ya vifo. Asubuhi njema. Kwaya zetu. Ukumbi wa kina mama, wakati wa kazi, mchana mwema, Taarifa ya Habari. Matangazo ya Vifo. Mbiu ya Mikoa. Ngoma Zetu. Mwalimu wa walimu. Chuo cha Ushirika Moshi. Taarifa ya habari ya saa kumi. Matangazo ya Vifo. Ombi lako. Pole na kazi. Taarifa ya Habari ya Zenji. na vipindi vingine vya kizalendo mpaka saa ya kulala. Kesho tena hivyo hivyo, na keshotwa na mtondogoo vipindi vile vile kama jana. Hapo lazima uzalendo utakujaa na Nduli akijipendekeza kutafuta ugomvi atatimuliwa ajikute anajilipuliwa Home Office za mitaa ya Jeddah.
Itikadi sisizoeleweka, vipindi na habari duni toka radio za fm, tv,na magazeti ya udaku, na uduwanzi mwingine tangu asubuhi mpaka jioni ndiyo tunajikuta tunapokea hizo e-mail za wabadhilifu na bungeni kujadiliwa yanayojadiliwa.
Hatujachelewa hata kidogo kujiangalia upya ili kurekebisha pale tulipopaghafirisha na kupanga mambo ya kizalendo na kwa masilahi yetu sote.
Masalaam.
Naunga mkono JKT irudishwe.
ReplyDelete(Mimi binafsi nilienda JKT; OP Kambarage Masange/Luwa 1990/91) -M.E.R
wewe masaalam uliandika ratiba ya mavipindi ya radio Njaa ujamaa ni imani huna deal na mawazo yako ni ya kinyume nyume....na kwa taarifa yako siku hizi kuna sauti na mambo yanaongelewa waziwazi kuliko zamani ingawaje bado haitoshi,zamani hata kusikia husikii unachosikia tuu ni mtu kahamishwa na kiwanda au shirika limekufa,tunasonga mbele haturudi enzi za mikingamo na mawazo ya duka la kaya..dwanzi mkubwa wee!
ReplyDeleteKundi hilo la wahitimu lilikuwa la kwanza kufuatia Complusory National Service Act 1966 - baada ya wanafunzi wa vyuo vikuu kuipinga na kufukuzwa hapo Jumamosi ya Oktoba 22, 1966.
ReplyDeleteMzee kawawa na Adamu Sapi (mwenye ndevu kama Nyerere pichani) walijiunga na Kambi ya Ruvu kuunga mkono! Namwona pia kijana mmoja wa Chuo Kikuu ambaye alifukuzwa . Lakini wazazi wake walimlazimisha kwenda moja kwa moja kuomba msamaha na akaambiwa ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa!
Bwana Misupu, asante sana kwa hii picha ambayo kwetu wengine is very historic!
michu wavivi utawajuaa tu??! ona wanavuopinga vikali jeshi lisirudi hahahaahaaaaaa!
ReplyDeleteMheshimiwa ISSA HABARI ZA LEO..NAONA UNAWAGUSA WENGI PICHA NZURI HII NA TUMEIELEWA LUGHA YAKE..KIMO NA UMBILE LA MHESHIMIWA HAVIKUBALIANI NA "..TUKIO.." INAVUUTIA SANA..OBISITI ANACHEZANAYO TOKEA "..JKT..".KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..
ReplyDelete...Annoy wa 6:25 unmenikuna sana na maelezo yako...those were the days. naomba niongeze na 'Mikingamo','Karibu RTD','Hongera'.....
ReplyDeleteWewe chesi umekunwa wapi au wewe chakula nini Hahaha
ReplyDelete