wadau, niko katika harakati za kutoa kalenda la jiji la dar kwa mwaka 2008 ifikapo mwezi wa oktoba ambayo itakuwa na picha za mandhari kama hizi. atayependa kuagiza aniarifu mapema kupitia issamichuzi@gmail.com kwani zitakuwa idadi ndogo. mambo ya bei na namna ya kuipata nitawafahamisha baadaye. hii inalenga wabongo wote hasa walio nje na ambao wangependa kuwa na kumbukumbu ya bandari yao ya salama ilivyo kwa sasa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2007

    Safi sana Michuzi. Picha ni nzuri sana ama niseme bongo yetu ni nzuri, imependeza.
    Ombi moja bwana Michu, watumie na hao jamaa zetu mamtoni huko ambao wao eti kuonyesha Tanzania ama nchi za Afrika (isipokuwa Afrika ya kusini), Eti wao huonyesha vijijini tu kama huku kwetu kwenye nyumba za nyasi na maisha ya dhiki. Picha kama hizi hawaweki kabisa, na kama vile eti Tanzania yote ni Wamasai tu, manake wakiongelea Tanzania ama Kenya basi ni nyumba za nyasi, ng'ombe na Wamasai! Wananikera kishenzi.
    Hebu fanya namna uwachomekee kwenye miblog yao kinyemela waambie This is a real Tanzania, na sio zile wanazoonyesha wao kutudhalilisha, na bado kila siku wanakuja eti kutalii.
    Big up Michuzi, bahati mbaya mimi sitaagiza hiyo kalenda kwani nipo hapa hapa Bongo na isitoshe kipato changu kidogo, nitategea zile wanatoaga kwenye kalenda, taraatiibu nakata kwa umahiri, siku zinakwenda.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2007

    Annon hapo juu wewe ndo pumba tupu, hii sio real tanzania ni just part tu,real tanzania iko vijijini kwenye nyumba za nyasi na wananchi wasiojua watapata wapi mlo ujao.Dar es salaam sio tanzania ndugu yangu,wao wanaonyesha the reality.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2007

    Marekebisho kidogo kaka Michuzi. Ni kwamba sitaweza kuagiza hiyo kalenda kutokana na kipato changu hivyo nitasubiri zile zinazotolewa kwenye MAGAZETI, then taratiibu nachukua mkasi ama wembe, nakata kwa umahiri nabandika, siku zinakwenda.
    Lakini kweli,itakuwa Kalenda Baabu kubwa. Nakufagilia mama Michu.
    Natena ukitaka kumaliza, weka miezi kumi ta tatu badala ya kumi nambili kwa mwaka uwe totauti na wengine (Utani huu lol)

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2007

    marekebisho kidogo kwenye comment yangu ya mwanzo, juu kabisa. Ni kwamba nina hakika kalenda itakuwa nzuri sana kutokana na picha nzuri na Tanzania yetu, binafsi sitaweza kuinunua kwani kwanza nipo hapa hapa Bongo, kipato changu pia mh, kidogo saana, hivyo basi nitasubiri zile zinatokaga kwenye MAGAZETI, kisha nachukua mkasi ama wembe wangu taraatiibu na kwa umakini kabisa, nachana kisha nabandika ukutani siku zinaenda. Ila kama utatoa na za bure Michuzi, usinusahau bro!
    Ukitaka kufunika zaidi kaka Michuzi unajua ufanyeje, weka miezi KUMI NA TATU kwa mwaka (2008) babala ya ile kumi na mbili ya siku zote,yaani utakuwa umetoka kivyako vyako (utani lol)
    Otherwise, Big up kaka michuzi, Picha nzuri sana, na sio picha Bongo yetu nzuri sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2007

    Great idea, ila fanya isikugharimu mno mpaka sie wenye kipato kidogo ikatushinda kuinunua. Napenda kumrekebisha msemaji hapo juu kuwa watu wanaopenda maendeleo huwa wanasisitiza siku zote kupeperusha fikra chanya. Kuna nchi gani duniani ambako hamna sehemu zilizochoka? Ila, tuwe "Positive thinkers" na tupende kuwapa "Good Impression" watalii wetu, hii itasaidia kutufikisha japo hatua mbili mbele. Vitu kama hivi vizuri "first priority" ni sisi af baadae watu watengeze kalenda za picha za huko mugumu. Lete vituz michuzi!
    Babao

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2007

    UMASIKINI MTUPU UMETAWALA JIJI HILO NA NCHI NZIMA KWA UJUMLA,HUYO ANON ANAYESEMA WAZUNGU WANAONYESHA PICHA ZA NYUMBA ZENYE NYASI VIJIJINI HUO NDIO UKWELI.ASLIMIA 85 YA WATANZANIA WANAISHI MAISHA YA DHIKI.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2007

    Nomba utoe kalenda mbili moja ya Dar unayopanga kutoa (lakini picha ya juu ya pantoni usiiweke not that good) na ya pili ya the real Dar....tunafagilia kuona vitu ambavyo ni real. Weka hizo mbili uone zipi zitaisha mapema...the real Dar hazitachukua hata mda... I am teling you the truth.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2007

    usitengeneze kalenda ya bandarini tu bali tengeneza kalenda ya jiji la Dar. Weka picha moja au mbili za hapo nenda kariakoo weka moja, nenda makumbusho weka moja nenda kwenye hoteli za kule nje ya jiji za Dar zile za majani ya manyasi weka moja etc.Varieties naona itakua nzuri zaidi lakini kama unavyopenda kufanya. I wish you lucky but mind the cost cause usije ukatuuzia kalenda moja ikatu cost a fortune.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2007

    MICHUZI HIVI NANI AMEKUDANGANYA ETI UKITENGEZA KALENDA ZENYE PICHA YA JALALA LA DAR UTAUZA.
    SI BORA UNGETAFUTA PICHA ZA MAANA MIKOANI AU UKIKOSA KABISA TAFUTA PICHA ZA WAREMBO WA MISS TANZANIA NA WENGINEO UTAUZA. MFANO MZURI MUOMBE AZIZA UMPIGE PICHA UCHANGANYE NA WAREMBO WENGINE UTAUZA KALENDA YAKO KULIKO JIJI LILILOJAA WIZI NA WABADHIRIFU HUKU LIKINUKA KAMA MTU MWENYE KIBUDU.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2007

    point kabla hujatengeneza hizo kalenda jaribu kujua soko lako ni lipi
    1Kama unataka watu wa kiume nje na ndani ya nchi....hao mamiss waliopo Dar ukiwalipa watafanya photo shoot na utauza zote.
    2. Kam unataka kwa wataliii basi weka hilo jiji la dar na picha kama huzo unazotuonyesha sample
    3. kama unataka the real people wenye kupenda kujua nchi yao walio nje na ndani ya nchi do the right thing. Tafuta picha unique za nchi yetu. Kuna mambo mengi tu raia wa kawaida aliyeko bongo hajatembelea hizo sehemu believe me na hata walioko nje kuna sehemu nyongi wangewish kuziona. Hivyo watapenda kuziona hizo kalenda.


    my 6 cents

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 28, 2007

    sio vibaya kutoa maoni ni picha za aina gani mngependa, maana kuna option nyingi kama vile, wanyama , watu wakiwa ktk harakati za maisha , mazingira, etc
    Most of all nakubaliana na ukweli kuwa picha dhalili zinawakilisha nchi vibaya. ...ndo maana Paris inawakilishwa na minara mizuri sio nyumba mbovu wanazoishi wakimbizi .

    LAKINI TUKIONGEA SANA INAKUWA KAMA TUNAMFUNDISHA MICHUZI, NAAMINI TAYARI ANAJUA NINI CHA KUWEKA.

    WALE AMBAO TUNATAKA HIKI AMA KILE, TUJUMUISHE MAWAZO YETU KISHA TUTENGENEZE KALENDA ZETU WENYEWE.

    NASEMA HIVYO SI KWA SABABU YA UNOKO , HAPANA. WATU KUMI WANAPOSHIKA KAMERA, KILA MMOJA ANA JICHO LAKE. NA HILO NDILO LINALOTOFAUTISHA UMAHIRI WAO , NA MUHIMU NDICHO KINACHO JENGA PERSONALITY ZAO KAMA WAPIGA PICHA.

    MWACHENI MICHUZI APIGE PICHA ANAZOTAKA , THATS THE ONLY WAY MTAPATA PICHA ZENYE SIGNATURE NA TRADE MARK ALIYOZALIWA NAYO.

    MICHUZI NI MPIGA PICHA MWENYe KIPAJI CHA AJABU .

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 29, 2007

    Samahanini wadau, Namkumbusha tena Michuzi atupe picha ya mke wake na watoto, mbona umetuchunia?, kama hauna mke na watoto siuseme tu.

    ReplyDelete
  13. Hizo nchi zilizoendelea zenyewe huwa hazionyeshi mitaa yake ya hali duni au mbaya!Na si kwamba mitaa kama hiyo hakuna Ulaya..Iweje sisi tunaotaka kuvutia watalii ili kongeza kipato,kuondoa umaskini,kuweka hadhi nk tuonyeshe mitaa yetu duni?Ili nini?Ili tukimbize watalii na kuita wasamaria wema wa uwongo,wale wanaochangisha wazungu wenzao na kudai kawa pesa hizo ni kwa ajili ya maskini wa Afrika.Wao wanapopiga picha za kuonyesha hali zetu duni wanafanya kwa manufaa yao tu,si kwa ajili ya kuonyesha ukweli.Kama ni wa kweli basi wangepeleka picha za matatizo yao duniani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...