
sakata la wimbo ambao msanii tid anatuhumiwa kuugeza toka kwa mwanamuziki pasada umechukua sura mpya jioni hii pale msanii mwingine ismail kuja juu na kudai mirindimo ya muziki huo ni wake.
katika kukata mzizi wa fitina redio ya clouds 88.4 m iliwaalika ismail na tidi pamoja na prodyuza said comorien studio ili kuweka bayana songombingo hilo. pichani ni tid (shoto) ismail (kulia) na saidi comorien (mbele, kibandiko) wakiwa wanahojiwa kwenye kipindi cha 'mezani' haya ni baadhi ya yaliyojiri kama yalivyonaswa na globu yenu:
mtangazaji: tidi hebu tuambie vizuri kuhusiana na nyimbo ya 'nyota yako' inakuaje kuaje watu wanasema hovyo huko
tid: saidi na mimi tuliufanyaga kipindi sana. tulifanya demo, lakini hatukupata nafasi ya kuurekodi. yaani tulitengeneza demo huo wimbo toka mwaka 2002 ila siku urekodi wakati huo mpaka msimu wa 2006 na 2007.
nikaibuka ofishali 2006 nikamwambia saidi mi nataka unitoe bwana na zouk sababu najua hakuna sehemu inayopigwa mazouk makali afrika mashariki zaidi ya saidi mwenyewe, unaona bwana... akasema sawa. nakaenda pale nikamfanyia fanyia makorasi, akatengeneza biti, nikatoka mimi, nikarudi nikachukua biti, nikaja nikaingiza korasi ambapo nikaingiza verse zote hapo hapo, na pale tulikuwa mimi, daz, frenki, adamu na saidi mwenyewe tukashirikiana tukamaliza wimbo.
mtangazji: hapa kuna tatizo, inasemekana wewe uliisikia hiyo melodi sehemu na ukaiiga. umeisikia sijui toka kwa mtu anaitwa pasada...
tid: hapana. sababui hata nilipomfuata saidi namwambia nataka kufanya hiyo traki mi mwenyewe kichwani nilikuwa sina traki. nilikuwa na filingzi flani hivi. umenielewa? mi nimeimba yeye ndo katengeneza biti. sasa mimi ukiniambia pasada na hiyo nyimbo naona ni kama set-up, watu wamepanga kwa sababu wameona labda hii nyimbo iko juu sana. siku zote pasada na nani sijui wasingetokea akaitambulisha nyimbo yake isingehiti? lakini sababu sasa hivi nyota inang'aa kila mtu anataka kuitupia mawe idondoke. ukweli ni kwamba hamna cha pasada wala l'amour de pasada wala hivyo vitu haviekzisti na huyo msnaii wala haishi mozambiki. kuna posibiliti kubwa huyo msanii kaniibia mimi melodi, na ni kitu hata mimi nakigundua hivi sasa. wanaosema nimeiga wanakosea kwani mistari nimetunga mwenyewe na comorien akatia midundo yake. nadhani kwa kuona umeshika vyema kuna watu wanataka kunipakazia. hivi kwani huyo mnayesema nimeiga kwake hawezi kuwa ni yeye aliyeniiga?
mtangazaji: ismail, hebu na wewe tuambie kuhusu hiyo traki yako ulirekodi lini?
ismail: eeeehh...kwa kweli nyimbo yangu hii track hii nilirekodi mwaka 2003 pale metro studio (kwa saidi comorien) ambapo baada ya hapo nilisafiri na kurudi mwaka 2004, huku nikendelea kurekodi nyimbo zingine ili nitengeneze albamu. ikaja kutoka 'ninachotaka' nyimbo ya reggae. ila kuna siku nimekaa ndani mimi nikaona video ya tid inapigwa kwenye channel 5. nikampigia kumuuliza saidi comoreine hii nyimbo vipi, akasema imerekodiwa kwake, na akaniuliza kwani vipi? sikumjibu. nikampigiua simu mkurugenzi wangu ambaye aliahidi kufuatilia. baada ya muda nikasikia sijui jamaa wa msumbiji wanaitwa pasada.
mtangazaji: tidi anasema ametengeneza demo mwaka 2002 na wewe umerekodi mwaka 2003. ndo kusema inaonekana wewe ndo umemuibia tidi...
ismail: hamna, 2002 ilikuwa ni uwongo. hii melody nimetunga mimi mwenyewe. vinginvyo nisingekuja hadi hapa. ningezingua tu, unaona bwana. yaani nina uhakika hiyo melody ni yangu ndo mana nimefika hapa. ila sikupanga kuitoa hiyo nyimbo, ilikuwa ndani ya albamu.
mtangazaji: saidi comorien, hapa kuna anayesema alitengeneza demo ya ala tupu mwaka 2002, mwingine anasema kaja kurekodi nyimbo yake yenye melody ya kileo - hii imesimama vipi?
saidi comorien: hawa watu kila mtu kaja na melodi yake. kuna aliyetengeneza demo kipindi kirefu huko nyuma, demo yake ametengeneza myuzik tu, juzi kaja karekodi nyimbo yake,a na maledi ya kileo. na verse zake ameziandika wakati kuna mashahidi na watu hapa tukatengeneza nyimbo. nimetoa nyimbo ya tidi, imeingia redioni. ismail katuma meseji juzi kuuliza vipi mbona nyimbo fulani inafanana na nyimbo yangu? mimi nataka niweke wai tutoe utata kwamba mie nimechukua nyimbo nimemuuuzia tidi. kila mtu kwangu alikuja na melodi yake, nami nimemtengenezea myuzik. na naamini myuzik yangu haijafanana na ya pasada, sijui ya nani wala ya nani. myuzik nilomtengenezea tid ni tofauti na niliyomtengenezea ismail. sawa. mi naona kuna utata fulani kwa sababu kwanza walianza kupakazia kwamba tidi ameiba nyimbo ya mozambiki. mimi kama prodyuza, nilifuatilia hili jambo kwa undani sana na kutambua kwamba kuna kitu kinaendelea, kama si kuharibiana kuna ishu inaendelea. walitupa taito ya nyimbo eti inaitwa l'amour pasada, wakisema hiyo nyimbo maana yake ni 'nyota yangu'. ikanifanya mimi nikaenda ubalozi wa msumbiji kwa ajili ya kupata ukweli. jamaa ubalozini wakasema huyu mtu pasada hawamfahamu, na sio mtu wa mozambiki na kwamba kwao ni angola na albamu yake karekodia karibian, hakurekodia angola. tatizo hapa ni melodi. napenda kusisitizia hapa kwamba sisi ni watanzania. tusipende kujishushia hadhi kwamba tumeiba myuzik ya mtu. je kama ni wao wametuibia sisi? pengine wanataka kumshusha yeye ama mimi kwa kuwa ni BIG TIME na tidi ameshatoka. jamani, nyimbo sio 'nyota yangu' ile inaitwa l'amour pasada' MPENZI!! na huyo msanii kwao sio mozambiki, ni angola. yeyote ambaye anasema huyo msaanii kwao ni mozambiki naomba ajitokeze, amlete huyo msanii tumuone, sawa? kwa ukweli mie sintoweza kuleta konflikti kati ya tidi na ismail kwa sababu tidi tayari ni msanii ambaye keshatoka. ismail ni msanii chipukizi na tayari anajipanga kutoka, sawa? myuziki niliyotoa kwa tidi na ismail na huyo pasada ni vitu vitatu tofauti. biti za zouk zinafana; zouk za karibian zote zinafanana. biti ni hiyo hiyo. kinachobadilika hapa ni labda lugha na melody ndogo ndogo za vinanda. lakini biti ni hiyo hiyo!
tid: unapomwambia prodyuza unataka kufanya muziki ni lazima uimbe, si ndiyo? yeye anakutengenezea hata kama raf biti lazima itakuwa na elementi ambayo inakuongoza wewe kuimba. in aza sensi zat iz ze melodi. mimi nimetengeneza hiyo biti kuingiza sauti. nilipofikia tena, sikuimba tofauti. naye akanikuliza tidi iz zis ekzaktli wot yo wonti. nikamwambia yea! nikaimba na kutoa ile rizim ya 2006 endi 2007, yaani ile filingi yangu ya sasa hivi ya R&B. sidhani kama hizo melodi zinafana na meseji zinafanana. halafu ngoja nikupe kitu kimoja; afrika hapa nyimbo nyingi zetu za taifa zinafanana. sijui ni ninik. wi a konektedi thru wani kalcha. kama ni zouk, zouk lolote lina rizim ile ile... nyimbo ya taifa ya sauzi unafanana na ya bongo, kwa mfano.
mtangazaji: letz sei hii kitu ingetokea kwako, yaani ismail angeanza kutoa na wewe ukaja kusikia ametoa. ungechukua eksheni gani?
tid: i wud just let it ismaili ashaini. namwacha ashaini kabisa.
Ismail: mimi tid ni kama brazaangu. na saidi comorien ni kama brazaangu. mi nilichodauti sio kwamba kaniibia nyimbo yote. mi nilichodauti ni melodi kuendana, au si ndo hivyo saidi comorien?
wote wameiba mziki wa pasada, peleka court walipe copyright infringement, eti zouk zinafanana? hana point unaiga mpaka sauti
ReplyDeleteyani huwezi kuamini sijaona hata jibu lililoniridhisha hapo yote pumba tupu,wameshindwa hata kujitetea. huyo said ndo anatakiwa atoe maelezo ya kujitosheleza zaid, may be mtutafutie na hiyo ya huyo ismail na hiyo ya passada tutajua yupi ni mkweli hicho kireno wengine tumesoma,tunakijua vizuri.
ReplyDeleteHaya mahojiano/majibizano yangenoga kama yanngekuwa katika mfumo wa sauti na si text kama ulivyoyatoa. Muulize M. M. mwanakijiji au wataalam wengine wakupige tafu jinsi ya kupost sauti kama mp3, wav n.k.
ReplyDeleteWako wapi malawyer wao?
ReplyDeleteHizi shutuma hatakiwi kujibu mtu mwenye mda mchache anatakiwa kwenda hapo na kujibu ni lawyer wa mtu wasanii hawajui mambo ya sheria. Kwa hiyo sishangai majibu yao....you guys need to learn huwezi kuwa wewe meneja , lawyer, PR, stylist, advisor, dereva, stage planner, Choreography wewe wewe kama unataka ufanikiwe.
Ndio maana nchi nyingine kazi zipo sana kwa vile watu wanazitawanya...
Hire advisor, lawyer, stylist, personal assistant, speech writer etc sio mnihire wafanyakazi wa nyumbani tu tuuuuuu....ndio maana kuna vyuo tofauti bongo sas sijui mnataka hao wasomi wafanye kazi wapi?
Kama kaka yangu Michuzi nafikiri unahitaji kuhire blog asistant sasa hivi......he hehe hehhhh kweli unakua na haraka sana ukiweka vitu vyako huku. Assistant ndio kazi yake hiyo.....ajirini watu kucreate job mabakuli yapungue
Hawa jamaa ni wajinga sana kwa kweli. Hivi ndio wasanii huko tanzania wakiongea na media wanaongea pumba hizo kweli? huyo Said Cmorien anaujua ukweli na anaficha tu hapo. Kwanini maproducer huko hwataki kuumiza vichwa wanaiga iga tu kila mara? Ujinga sana huu
ReplyDeletewe anon unayetaka kusikiliza ya pasada bofya hapa utasikiliza zote mbili ya tid mwigaji na ya pasada original, compare halafu nambie nani kaiba
ReplyDeleteTID noma nilidhani ana kipaji kumbe tupandia kwenye migongo ya watu hata zeze anaweza kuwa kaiba sehemu ngoja tufatilie vizuri
1. huyo jamaa kwenye RADIO hajui kuuliza maswali. 2. kama kuna jamaa hapo juu kasema Said Mngazija ndio aliyetakiwa kusema ukweli ilikuwaje ukweli wa hao watu wawili yangeisha ausio. 3. wacheni malumbano jiungeni, kama Said Comorien unaujuwa ukweli watengenezee TID na ISMAIL kwa pamoja track, bila kulipwa umalize tatizo. 4. wa TANZANIA tusaidiane sio tuangushane, Mwisho TID inaonesha pengine umejuwa mwenzako katengeneza 2003 ndomana umesema 2002. Ismail namuona kama kasema ukweli ndomana hajajifanya 2001, kasema ukweli 2003 ila mungu ndio anajuwa imbeni kwa pamoja jamani wizi haufai TID na wengine siku nyengine muwe mna sign mnapoingia ku records file ziwekwe kwenye computer au bado mnatumia marimba?.
ReplyDeletewe kweli wakuja, we umeona mwanakijiji mtaalamu wa computer? lol nenda shule uondoe ujinga babu
ReplyDeletehii issue sasa ndio itawaaamsha watanzania .jamani tafuteni mziki wenu wa kitanzania mambo ya zouk siyo yenu na sasa yamemtokea puani huyoo tid .wabongo kwa kukopy tuu hatujambo na ndio maana ni vigumu sana kuendelea katika soko la mziki la kimataifa hatuna chetu asili yaani mziki wa kitanzania ambao yeyote atakayesikiliza atajua kwamba huo mziki si wa mahala popote bali ni tanzania kama vile wacongo ukisikia tuu unajua haoo ni wacongo
ReplyDeletesasa tid jifunze kaka chukua hili sokobongo lililokukuta kama changamoto ili ujaribu kucreate kitu halis cha mtanzania
mnaimba kiswahili mapigo ya kikongo.kiswahili - mapigo ya zouk,kiswahili mapigo kwaito,kiswahili mapigo ya american hip hop ,na mabaya zaidi nikiwasikiliza i can tell kwamba mnajaribu kuwa fikia wenyewe wenye identity ya hiyo miziki lakini hamuwafikii na hata mkiwafikia distributors au promota wa kimataifa kiasili hupendelea wale wasanii walio mahiri haswa ktk aina ya muziki inayohusika hata ukitumia hekima ya asili tuu soko la kimataifa lenye pesa na mafanikio makubwa kwa wanmuziki hawawezi kupromoti ZOUK ya TID na hali wapiga zouk mahiri wenyewe amabapo huo mtindo ulianzia wapo na wanafanya zouk original tamu na iliyojitosheleza siyo ya kuiga
jamani tupende sanaa ya kwetu ya tanzania hayo yoote mnafanya mansema inalipa lakni mwisho wake tutaishia kuwa wa kukopi tuu ,ni lini wacongo ,wasouth.wazungu ,wahindi au kenya na woote wale ambao wanmuziki wetu wa tanzania mnaiga mapigo yao,ni lini hao wote niliowataja watakuja kuhangaika kukopi mziki wetu wa tanzania kama vile sisi tunavyoona fahari kucopy mapigo na vionjo vya tamaduni za wengine na kujigamba kwamba ahhh! bongo bwana mziki wetu sasa umetulia , bab kubwa !
hongera che mundugwao,hongera saida karoli,hongera baba ya mziki (msondo),hongera mlimani kwa sana tuu
tid, pole kaka fanya mziki wa kitanzania achana na hayo ya wenyewe kwa kukopi utaishia kuwa third best na kamwe hautokuwa the best,
kama ni van gof basi kwa kukopi mapigo na vionjo vya tamaduni wa nchi nyingine basi utakuwa van gof wa plastiki
it seems like said kamuuzia tid melody ya ismail lkn anajibu pumba, mbona pfunk alikubali kwamba kamuuzia chameleon beat prof j na isu ikawa poa, na leo washkaji wamefanya colabo...mgodi wa kndoni upo juu lkn kwahili umechemsha we na prod wako...unatupotezea fans wko dude
ReplyDeleteYaani hapo mimi i still have doubts about the all issue sijui lakini ukweli wanaujua wao wenyewe kama waliiba au la... kazi kweli kweli huu kweli mwaka wa shetani kama temba alivyosema.
ReplyDeletewote wezi tu! Shame on them 'zouk zote zinafanana!!!! jibu ni kumgomea show zake ili ajifunze.
ReplyDeletesasa ungeweka nyimbo yenyewe hapa halafu tukajua ni kweli huyu bwana kaiba au kaibiwa cc tuliopo nje ubongo nyimbo hiyo hatuijui
ReplyDeleteMimi story ya wizi inaniboa, muziki umetoka bomba - Big up TID. Ulikuwa wapi hukutoka mapema wewe unae lalama? Ulikalia uchumi! Riziki mtu hupewa na Mungu sio wanadamu wacheni mtimanyongo vijana. Kama kuna wanaokudanganya uanze majungu na bado chipukizi hakutakii mema. Kaza buti nawe siku moja utoke. WACHENI HIZOOOOOOOO!!!!!!!!! UKO wapi Da Regina Mwalekwa uwape mipasho hawa
ReplyDeleteHAO WABONGO WOTE WAMEIBA HUO MZIKI KUANZIA BITI MPAKA MELODI,NA MSHIKAJI ANAWATOKEA KUTOKA BONDENI,NAJUA SAA HIZI MAVI YANAGONGA CHUPI!
ReplyDeleteT.I.D acha ushamba miwani ya jua kuivaa studio wapi na wapi????Tzan musicians have now to adhere with dressing code,outdoor classes should not b worn indoor
ReplyDeleteSasa tutaamini vipi kama kweli huyu producer huwa haibi hizo zingine zote alizowatengenezea wa2. Mfano hii Presha,, mimi naona kaiiba mahali,, tukichunguza vizuri tutaisikia mahali aidha Visiwani Haitiau Cape Verde wanakopiga mazouk ya uhakika
ReplyDeleteSasa tutaamini vipi kama kweli huyu producer huwa haibi hizo zingine zote alizowatengenezea wa2. Mfano hii Presha,, mimi naona kaiiba mahali,, tukichunguza vizuri tutaisikia mahali aidha Visiwani Haitiau Cape Verde wanakopiga mazouk ya uhakika
ReplyDeletewizi wa nyimbo hapo bongo haujaanza leo!na tangu nianze kusikia hii wiizz sijawahi kuona hata mara moja msanii kakubali kwamba kaiba hata kama alikuwa keshatoka!damm huyo cong'olie producer naona analeta stori zaq wapi pasada katoka!thatz out the point,yeye ndio muhusika mkubwa wa kuiba na kuwauzia wasanii wengine nyimbo....take care atakimbiwa kama prodyuza majani..
ReplyDeleteKwakweli hapa huyu Producer ndio atuambie
ReplyDeleteHao wote wezi hawafanyi kazi kabisa wanacheza huyo TID amesikia huyo nyimbo ya pasada bas angebadilisha hata mashairi??? wajinga They have to learn from Jide
ReplyDeleteNI VIZURI TUKAWA TUNACHUNGUZA KABLA YA KUTOA MAAMUZI.
ReplyDeleteMIMI NIMESIKILIZA NYIMBO ZOTE MBILI NA NIMEGUNDUA KUWA HAZIFANANI HATA KIDOGO.