WATANZANIA WAISHIO WASHINGTON DC WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAMA MWAJUMA BAKARI MWAYUNGU, MAMA MZAZI WA HASSAN MWAYUNGU WA NEWYORK, MAREKANI, KILICHOTOKEA JULAI 1,2007 SAA 9 ASUBUHI KWA UGONJWA WA KANSA.
MAMA MWAJUMA ALISHUSHWA AIRPORT YA DULLES WASHINGTON DC BAADA YA KUZIDIWA KWENYE NDEGE AKIWA SAFARINI KURUDI NYUMBANI BAADA YA MATIBABU KUSHINDIKANA. MAREHEMU ALIKUWA HOSPITALINI HADI MAUTI YALIPOMKUTA.
KAMA ILIVYODESTURI YETU , WATANZANIA WOTE TULIOKO NJE YA NCHI TUNAOMBA MCHANGO WA HALI NA MALI ILI TUWEZE KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI.
KUTAKUWA NA HARAMBEE SIKU YA JUMAPILI (LEO) KWA AJILI YA KUPATA PESAZA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU.KUANZIA SAA 7 MCHANA MARA TUBAADA YA IBADA KATIKA KANISA LA CATHEDRAL OF PRAISE 5311 43RD AVENUE HAYATTSVILLE, MD 20781.
KAMATI YA MAZISHI IMEUNDWA ILI KUFANIKISHA MSIBA HUU, KWA WALE WENYE MCHANGO AU SWALI LOLOTE WANAWEZA KUWASILIANA NA HAWAWAFUATAO:
YASSIN NJAYAGHA 301 379 0693TINO
MALINDA 240 338 4917
MAYOR MLIMA 301 806 8467
OMBYE NYONGOLE 240 462 9799
CECIE FRANCIS 240 682 4931
PEACE KACHUCHURU 301 367 6378
HELEWA 240 535 6883
MTOTO WA MAREHEMU HASSAN MWAYUNGA 718 810 3397
MUNGU AWABARIKI SANA
- TINO MALINDA
Hivi kwa nini hawa wasimzike tuu huyo marehemu hapo hapo USA? Mfano sisi waislam wa UK huwa hatupati taaabu ya kusafirishana kwani tuna makaburi yetu Pale Wansted na mengine yako kule Tottenham na naamini kuwa waislam wanayo makaburi hapo NEWYORK na DC na hii siyo big deal sasa hebu fanyeni mumzike huyo mama kama ni musilam na msicheleweshe mazishi
ReplyDeleteKama michango basi fanyeni michango ya Khitma au kumzika tuu hapo ambako naamini gharama hazitozidi dola 500
Huo ni ushauri tuuu toka kwa muislam mwenZENU-london ,uk
Hi Mtoa Maoni hapo juu, kwanza kabisa nashukuru kwa maoni yako. Mimi ni mtanzania hapa DC, kwa nini umeanza na sisi Waislamu? acha hivyo... desturi yetu sisi tunapenda watu wazikiwe kwao that's all. Asante
ReplyDeleteKwa kipi alichokifanya mpaka astahili nafasi hiyo!? Kashfa za Rada, ununuzi wa helicopter, ununuzi wa ndege ya Rais, ununuzi wa magari ya jeshi, Kashfa ya kufanya biashara akiwa Ikulu, Mikataba ya madini na usiri wake, Kasha ya kuwaingiza makaburu wa Net Group kwa mtutu wa bunduki pale TANESCO na hatimaye kuliacha shirika hilo hoi bin taaban. Haya ni mafanikio kweli yanayostahili apewe nafasi hiyo!? Ndiyo tunajua aliweza kukusanya mapato mengi ya kodi ukilinganisha na waliomtangulia je Watanzania waliona mafanikio yoyote na ongezeko hilo. Ni sawa na Baba ambaye mtaani anatamba yeye ndio mwenye mshahara mkubwa mtaana, lakini familia yake haifaidiki chochote na mshahara huo. HAFAI!!!
ReplyDeleteNENO SISI WAISLAM SI ZURI HATA KIDOGO SISI HAPA DC HATUNA USHENZI WA UDINI HATA KIDOGO, DINI ZOTE ZIMELETWA NA WAGENI KATIKA NCHI YETU WAKATI WA MABABU ZETU, HILO NENO SISI WAISLAMU AU WAKRISTO HALIKUWEPO. WAZO LA KUZIKA HAPA HALIHITAJI UISLAMU. WATANZANIA WOTE WALIO KUFA HAPA TUME WAPELEKA NYUMBANI NA HUYU TUTA MPELEKA NYUMBANI. KWA TAARIFA YAKO HARAMBEE YA KUMPELAKA NYUMBANI ILIFANYIKA LEO KATIKA UWANJA WA KANISA NA HAKUNA CHA UDINI HAPA PELEKA UDINI WAKO MAGOMENI HUKO HAPA DC HATUTAKI USHENZI HUO.
ReplyDeletePoleni wafiwa.
ReplyDeleteHata hivyo naomba kuungana na anon wa kwanza hapo juu. KWA NINI MSIZIKE HUKO HUKO? Mfano mzuri ni msiba wa SHEMSHA KENNEDY MAZARA (R.I.P) http://issamichuzi.blogspot.com/2007/06/tanzia_29.html ambaye tunaambiwa alizikwa Dallas.
Hata Wachagga Bongo siku hizi wamepunguza ishu za kusafirisha maiti kurudi Moshi.
Jamani mimi ni yule anon wa mwanzo kutoa maoni
ReplyDeleteKwanza naomba radhi kwani baada ya kusoma jina la marehemu ni MWAJUMA BAKARI MAYUNGU ambaye ni mzazi wa HASSAN MWANYUNGU nikajua kuwa moja kwa moja hawa ni waislam kama mimi
kutokana na maandishi ya dini yetu ni kuwa waislam wote ni ndugu. Sasa inawezekana ikawa mko sawa kuwa marehemu alikuwa SI MWUISLAM na kwa hio ninaomba RADHI kwani sikuwa na nia ya kuanzisha mjadala wa kidini bali nia na maudhui yangu yalikuwa ni kutoa ushauri tuu kwa hao wafiwa ambao nilifikiri ni waislam na kutokana na sheria za dini ya kiislam mtu akishafariki basi mindhali kama akishaoshwa na kusaliwa then azikwe mara moja.
Ila kama kutakuwa na michango yoyote basi ni ya kuwalipa jamaa ambao wanashughulika na masuala ya kule msikitini,kuosha maiti na mambo mengine madogo madogo bila kusahau pesa ya kulipia makaburi kwani katika nchi hizi za nje makaburu huwa yanalipiwa. Na baada ya hapo basi marehemu asomewe Khitma
Nadhani maelezo yangu hapo juu mmeyaridhia
wewe anon mtoa maoni. sisi tunapenda sana kuona watanzania wote wanapelekwa nyumbani bila kujari dini. mtu akizikwa hapa iwe tu imetokea kwa bahati mbaya au kwa matatizo ya pesa. mtu akizikwa hapa ni sawa na kumpoteza milele kwa nini nasema hivyo? ni kwa sababu itakuwa vigumu sana kwa vizazi vyake huko Tanzania kufunga safari za mara kwa mara kuja hapa kuona kaburi kama zilivyo desturi zetu watanzania. ndiyo hilo tu. Nani mkristo au mwislam si tatizo letu kabisa. wala majina yasikusumbue. Hayo majina ya kiarabu ni majina tu huko kwao huhitaji kuwa Mwislam kuitwa Aziz au bakari. Je una jua kwamba yule alikuwa makamu wa Sadam hussein bwana Tariq Aziz alikuwa ni Mkristu? ndiyo maana nasema dini hizi zimeletwa tu kwetu na hawa wazungu na waarabu na zisiwe ndiyo kipimo cha Ustaarabu wetu. Mimi nimekusamehe,
ReplyDeleteTINO MALINDA WATANZANIA WA DC METRO HATUNA IMANI NA WEWE KWENYE MASUALA YA FEDHA.
ReplyDeleteJUMUIYA YA DC MIGOGORO...KANISA UMOJA MIGOGORO....KANISA LENU NA KOMANYA MIGOGORO,WEWE NA JEERY(MZAIRE)MKAMPINDUA "MCHUNGAJI" KOMANYA ALIPOENDA BONGO KUOA.UKAANZISHA KANISA LAKO NA KULETA MCHUNGAJI MZURI SANAAA KWA INJILI ILA TUNAMWALIKA AONGOZE KWENYE IBADA ZA VIFO,UBATIZO LAKINI KANISA HALIONGEZEKI WATU MNAENDELEZA MASHINDANO NA KANISA LA KOMANYA.
TINO FUNGA NDOA,ACHANA NA UONGOZI KWANI HUAMINIKI.
basi naomba radhi nilifikiri Marehemu ni Muislam.
ReplyDeleteKwa hiyo naomba tusameheane