
napenda kutangaza wafuatao kuwa ndio washindi wa shindano lilopita la kuchagua tofauti katika picha hiyo juu (http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=shindano&x=62&y=13) na nashukuru washiriki wote kwa kuchakarika. ila jambo moja muhimu wengi walisahau; nalo ni kuweka jina ili iwe rahisi kutangaza matokeo. sikumbuki mtu akipewa pepa kisha akajibu maswali bila kuweka aidha jina ama namba ya mtihani kama hatakuwa amejifelisha mwenyewe. nadhani naeleweka. wengine wengi walipitia mlango wa nyuma (kwa kunitumia email) kwani hilo halipendezi ikizingatiwa kwamba lazima kila mtu aone juhudi zako hapa hapa.
washindi wetu ni
kichuguu
salim salim
dogo
mdau dar millionaire kashinda lakini kapita njia ambayo siyo. hivyo namdiskualifai. wadau mlioshinda hongera zenu sana na naomba mtaje picha muipendayo niwabandikie ama niwatumie. naomba mtaje humu humu na si kwa kupita mlango wa nyuma kama wengi walivyofanya.
washindi wa shindano kabla ya hili watapata zawadi zao kabla ya tarehe 20 mwezi huu kwani inabidi nizisake zote kwa mpigo na huwa sipendi kutoa zawadi mojamoja. matakwa yenu nayafanyia kazi
Michuzi mimi ni Dar Millionaire nakata rufaa kwa nini umenidisqualify bwana? Wakati mambo yote nimeweka hadharani kila mtu aone.
ReplyDeleteBravooo !!!!!!!!,
ReplyDeleteSafari hii nimeshinda mtihani, tena nimekuwa wa kwanza; makubwa hayo. Hii ni mara yangu ya kwanza kuwa wa kwanza kwenye mtihani wowote maishani mwangu. Hata watoto majirani zangu leo wataipata, kuwa kumbe Kichuguu naye ni mkali.
Hoyayaaaaaaa !!!!!!!!!.
Zawadi yangu nilikuwa nimeandika kwenye pepa ile kuwa nataka picha ya jamaa aliyepiga wimbo wa "Marashi ya Pemba." Nataka picha yake ya miaka ya 80 wakati akiwa OSS na kombora lake la nyuzi dazeni. Jina lake simkumbuki tena, ila nasikia keshafariki.
Sasa vipi Michuzi, nitapata na cheti cha ushindi wa "kwanza" kuambatanza na zawadi yangu hiyo?
Tarehe 20 ni kama wiki mbili na nusu kutoka leo, kwa hiyo nitasubiri. Hata hivyo napenda kutahadharisha kuwa nina uwezo mdogo sana wa kusubiri hasa baada ya msitali mfu kupita.
Michuzi tunaomba utuandikie basi jibu sahihi ni nini. Wengine bado tuko kwenye giza. PIcha zote kwetu zilikuwa sawa.
ReplyDeleteAnko michuzi asante sana ninashukuru kwa kuwa mushindi.....
ReplyDeleteLeo huku mashariki ya mbali lazima nisheherekee kwa ushindi huuu!
Anko michuzi mie nilishaweka bayana kuwa naomba picha moja mzuri ya jengo mapacha la BoT likionesha na kale kadogo ka kati kati... au ata zile mbili kwa pamoja....
Kama hiyo itakuwa ngumu sana... basi naomba snepu tamu ya ile askari monumenti yetu pale poster....
Asante sana anko michuzi.
Dogo... mdau wa mashariki ya mbali.
michuzi,
ReplyDeletenafurahi kushinda kwa mara nyingine tena,,winning is my destiny,,hhhhhhhhhhhhh
sawa, MI NAOMBA UNIWEKEE PICHA YA SOKONI KARIAKOO KULE SHIMONI,,NASISITIZA KULE SHIMONI, UKIWAONESHA WALUME WAKIBEBA MAGUNIA YENYE UZITO MARA TATU YA UZITO WAO,,MANA MTU ANA KILO 60 ANABEBA KILO 180 DUUUUUH..
NI HAYO TU..
SALIM SALIM.