
Wakati wa harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika kati ya mwaka 1954 mpaka 1961, jina moja lilitamba sana katika fani ya muziki. Jina hilo ni Frank Humplink. Humplink alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa maarufu sana wakati ule. Alikuwa akipiga muziki wake akishirikiana na dada zake wawili Maria Regina na Tecla Humplink.
Habari za kusikitisha ni kwamba Frank Humplink hatunaye tena. Mzee Humplink amefariki dunia juzi nyumbani kwake Lushoto,mkoani Tanga. Alizaliwa tarehe 3 Aprili mwaka 1927. Amefariki akiwa na umri wa miaka 80. Habari kwa kina nenda http://www.bongocelebrity.com/
Hivi kwa nini Mke akifa akiacha mume huwa hakuna mjadala au vikao vya wanandugu kujadili mambo ya mirathi ya mali lakini akifariki mume akaacha mke vikao vya mirathi huitishwa na ndugu na jamaa wakijadili mali.
ReplyDeleteWanasheria mko wapi! Hamlioni hili au kwa kuwa majaji wakuu wote toka uhuru ni wanaume hivyo mfumo dume unaonekana kuendelea tu?
Poleni sana familia, ndugu, jamaa, rafiki na watanzania wote kwa msiba wa mpendwa marehemu Frank Humplick. Mungu atusaidie tuwe na umoja amani na upendo katika wakati huu mgumu wa msiba. Amina
ReplyDeletepole sana injinia humplick kwa kufiwa na baba,tulisoma wote foe miaka hiyo.
ReplyDeletePoleni sana ndugu,jamaa na marafiki.Gwiji mwingine wa muziki katutoka hivyo.Huo wimbo wa Harusi unanikuna sana ukipigwa.RIP
ReplyDeleteNI HABARI ZA KUSKITISHA ILA NDIO MAPENZI YA MUNGU.MZALENDO ROHO INANIUMA SANA KUONA WATU KAMA HAWA WANAZIDI KUPUNGUA NA MAFISADI,MAJIZI BADO YANPETA NA KUTUINGIZA KWENYE MAMIKATABA YA KISHEZI.PUMZIKA KWA AMANI MZEE WETU.MWENYEZI MUNGU AKUPE RAHA YA MILELE NA MWANGA WA MILELE AKUANGAZIE.KAMA WALIOKUFA WANAKUTANA NA KUONGEA NAMSIHI MAREHEMU ASIMWAMBIE NYERERE MAMBO YA BUZWAGI NAJUA MWALIMU ATAUMIA SANA.MWL NYERERE NA WAZALENDO WOOTE WA BARA LA AFRICA.MPUMZIKE KWA AMANI.AMINA
ReplyDeleteKwa heri baba, RIP daddy Frank! Ni kweli kaka Michu Thecla yuko Kenya na Maria-Regina nadhani yuko Moshi. Hawa dada zake walikuwa na ni warembo sana mpaka leo. Niliwafahamu kwa kuimba na kucheza twist
ReplyDeleteYvonne na Winnie poleni kwa kumpoteza mjomba wenu Uncle Humplink
Cynthia, Fran and BJ poleni sana kwa msiba wa baba. RIP Mr Frank Humplick.
ReplyDelete