Home
Unlabelled
denmark
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
kila la kheri wanangu yaani, ndio wenyewe kabisa.
ReplyDeletemdau morogoro
jezi hizi mbaya tutafute design nyingine
ReplyDeletehicho kijamaa kifupi kinaonnekana hakiwezi kurudi bongo lazima kizamie.
ReplyDeleteTupe na matokeo basi !
ReplyDeleteVipi matokeo Braza Michu??wengine netiweki hazishiki sawasawa...hiyo timu inaitwaje??
ReplyDeletePigaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Njohole fanya fanya ujimix na masela tukawatoe manundu black mambaz.
ReplyDeleteBabao
Salaam waungwana....Bor Michuzi una skuli ya kufunza watu kupiga snepu ndugu yangu?? Manake huyo aliyepiga snepu alinichanganya kuona wadenishi wapo wa4 na vijana wa STAAZ wapo kama nyuki.... manake kama ndio timu hapo labda iwe magoli madogo au chandimu manake tukipiga fulu timu hapo lazima tuwapige mande...ha ha ha haaaa
ReplyDeleteall the best to STAAZ wajifunze tuanze dunculiza kwa ajili ya japo nauli Ghana 2008
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.....
Vipi mbona hujaweka matokeo ya mechi?
ReplyDeleteMICHUZI TUNAOMBA MATOKEO PLEASE...
ReplyDeleteKuna mdau ametabiri matokeo ya Taifa stars na Msumbiji.Lakini kuipa uzito hiyo hoja,Naomba nitangaze dau 20,000 za kibongo kwa mdau atakaetabiri matokeo hayo sawasawa hayo.na izi pesa naomba michuzi tuwasiliane uwe nazo.
ReplyDeleteNawasilisha.
nadhani ilikuwa mechi ya kushtukiza, yaani hakuna mtazamaji hata mmoja!
ReplyDeleteMbona utuwekei matokeo bwana michu sisi bado tunajifunza sasa usigope kutuwekea matokeo kila mbongo anajua kuwa timu yetu bado changa kwahiyo kufungwa kwetu sia ajabu ni moja ya kujifunza hata kama tutafungwa na timu ya daraja la5 hamna noma
ReplyDeleteSTARS YACHAPWA DENMARK
ReplyDeleteNa Elizabeth Mayemba, jijini
TIMU ya taifa, Taifa Stars, jana ilianza vibaya ziara yake ya kimichezo baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Boldklubben Skjold ya Denmark ya daraja la pili katika mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini humo.
Stars wapo nchini Denmark kwa ajili ya ziara yao mafunzo kabla ya kuvaana na Msumbiji katika mechi yao ya mwisho ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Matifa Afrika mwakani nchini Ghana.
Stars walicheza mechi hiyo jana usiku na bao la kufutia machozi lilifungwa na Amir Maftah.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, Stars wataendelea kucheza mechi za majaribio kabla ya kuondoa Jumatatu kwenda Uswisi ambako watacheza mechi tatu na kurejea nchini.
Katika hatua nyingine, wachezaji watano wa kikosi hicho cha Stars wanatarajiwa kuondoka leo baada ya jana kushindikana kutokana na matatizo ya usafiri.
Wachezaji hao ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Abdulrahim Amour, Shaaban Dihile, Meshack Abel na daktari wa timu, Sheiky Mngazija.
Kwa mujibu wa TFF, wachezaji hao wataondoka saa 10 jioni kwa ndege ya Ethiopia kwa ajili ya kujiunga na wenzao waliotangulia.
Timu hiyo iliondoka kwa mafungu na hilo litakuwa kundi la tatu baada ya mengine mawili kuondoka kwa nyakati tofauti.
huyo annon aliyesema jezi mbaya,hii design ni poa kabisa halafu jezi huwa zinachange kutokana na msimu hivyo zitajachange baadae b4 we go to ghana kwa hio hamna shida ziendelee hizi hizi tu.
ReplyDeleteMatokeo ni kwamba tumepigwa bao 2-1, timu ya taifa inafungwa na timu ya daraja la pili ya Denmark. Kweli wabongo tuna ndoto za mafanikio
ReplyDeleteStarz imelala 2-1.
ReplyDeleteEti Ally Mustapha ndo golie wa stars!! Huku kuna Kaseja mwenye uzoefu chungu nzima anakula jua bongo..
ReplyDelete..kweli wametudharau maana hata huo uwanja ni wa high school...maskini ni maskini tuu,tujitahidi kuondoa njaa zetu labda ndio tutapata heshima kidogo
ReplyDeletetuwatakie afya njema kwa maandalizi ili waje wote wakiwa wazima tayari kwa mechi ya mwisho
ReplyDeleteJamani hawa Taifa Stars wasisome kabisa hizi blog wanaweza wakashindwa hata kucheza mpira. Kha! wajameni Wadau wapeni moyo ndo wanatambaa
ReplyDeleteMichu, hivi Nico Njohole, Deo Njohole, Likembe Njohole wapo wapi??? Angalau huyo Renatus Njohole tunamsikia hao kakaze wamenda wapi?
Aminia Pius babaake, Kaseja amejaa tele watu wanaleta majungu tu. Haiwezekani kipa ambaye kwenye timu yake ni wa akiba akachukuliwa kwenye timu ya Taifa yule kipa wa kwanza akaachwa hasa kwa situation kama hii ya Tanzania ambayo wote ni watanzania. Wanaofahamu soka watakuwa wamenielewa, wasiofahamu lazima waibuke na mipumba yao!!!!!!
ReplyDeletesafi sana taifa stars wamepewa changamoto ya nguvu ,hongera barthez mwanzo mzuri kijana hofu ondoa si tuko nyuma yako.
ReplyDeleteHATUTAKI MAKIPA WAFUPI NA WASIO NA NIDHAMU KAMA KASEJA!bARTHEZ NI BETTER SANA.
ReplyDeletehili timu letu kweli limechoka yaani litimu inacheza na kitimu cha daraja la pili lakini bado linachapwa? hii kaazi kwelikweli. ama kweli ktk soka bado tupo karne ya 18.
ReplyDeleteKipa kama kaseja HAFAI kuichezea taifa star.Kwanza mfupi pili hana nidhamu nje na ndani ya uwanja.Mimi aliwahi kuninyang'anya demu wangu Mwile wa Morogoro.Atoe hapo ufupi wake!!!!fyuuu
ReplyDeleteThobias P. unajishughulisha na shughuli gani? Huo mpira baba, kama rahisi wewe unachezea timu gani? Hao wenzetu wameweka investment kwenye soka kwa muda mrefu sana, na hayo ndio matokeo yake. Kwa upande wetu sisi nia ipo, na njia ipo, muhimu ni kuwapa motisha hao vijana wetu (Taifa Stars) watuwakilishe vyema sio porojo porojo tu. Vijana wetu mie nimewapenda sana kifizikia wametulia muhimu sasa ni: nidhamu, bidii ya mazoezi, na kujiamini - Tutafika
ReplyDeleteBabao
Kama huna nidhamu, hakuna atakayejali "your looks", au umesuka msuko gani, au ulilala na nani kwenye michezo. Twende nao haohao stars wachache tu, ila waongeze kujituma! Tuko pamoja!
ReplyDeleteHATA MAXIMO ANAJUA KWA KUWA MECHI IMEBAKI MOJA HAKUNA HAJA YA KUONGEZA MCHEZAJI YEYOTE KWA SASA KWANI ANAWEZA KUWAVUNJA MOYO WACHEZAJI WALIOPO AMBAO WAMESHAFANYA KAZI NZURI SANA. ANAWAACHA WAMALIZIE NG'OMBE WAO .WANACHOHITAJI SASA NI SUPPORT YA NGUVU TOKA KWETU TOWAUE THE MAMBAZ. TAIFA STARS OYEE!!!
ReplyDelete