

msanii wa kimataifa toka bongo ambaye anaishi kwa watani wa jadi godfrey mwampembwa a.k.a gado anayechorea katuni gazeti la the nation amejiunga na wasanii frank odoi na madd kuunda kampuni ya sanaa, matangazo na promosheni katikati ya nairobi. leo alinikaribisha osifini kwake. huyu bwana ni tumbo moja na robert mwampempwa a.k.a bi mkora
BABA JIPOZE BABA. WABAYA WAKO WANIGERIA WAMEPIGA HODI MLANGONI KWAKO TENA KWA GIA KALI. WANAFUNGUA KIWANDA CHA SARUJI HUKO KUSINI...UPOOOOOOOOOO.
ReplyDeleteWALIVYOKULIZA KWENYE BLOG YAKO UMEPIGA KELELE WEEE NA HATA WADAU WENGINE KUDAI HAWA JAMAA NI WACHAWI.
RUDI UJIONEE MAMBO YA UBINAFSISHAJI HUKU KWENU NA GESI YA SONGOSONGO. MNIGERIA (SUMU YAKO) ANAJENGA KIWANDA CHA SARUJI. SIJUI UTAKIMBILIA WAPI MMAKONDEE WEEEEEEE. TOBAAAAA MIE.
Mwl Mwampendwa sons, Hawa jamaa wanatalent sana tokea tuko pale Mlimani primary tunafuta ujinga walikuwa wanachora sio mchezo. Nifuraha sana kuona watu uliokuwa nao wanafanya vitu vyao na wanaconquer Kenya,Africa. All the best with your new venture
ReplyDeleteGado namkubali hata jana nilitaka kununua kitabu chake cha end of ERROR lakini nimeshindwa kwa sababu naishi Bongo credit card sooo nilikuwa nasoma nation kwa sababu yake na Marehemu SON OF THE SOIL
ReplyDeleteChifu Fundikira afariki
ReplyDeleteHabari Zinazoshabihiana
• Chifu Kingalu alia na mvua ya kutengeneza 08.09.2006 [Soma]
• Naibu Mkurugenzi TBS afariki 28.11.2006 [Soma]
• Mwanafunzi Weruweru afariki ghafla 18.05.2007 [Soma]
Na Chuma Shomari, Tabora.
MTEMI wa mwisho wa Unyanyembe, Chifu Abdallah Fundikira (86), amefariki dunia.
Chifu Fundikira alifariki dunia jana mchana mjini hapa, kutokana na maradhi ya shinikizo la damu na kile kilichoelezwa kuwa ni umri mkubwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na wasemaji wa familia hiyo, Bw. Said Dachi na Bw. Said Fundikira, marehemu Chifu alifariki dunia saa sita mchana, akiwa nyumbani kwake katika mtaa wa Mwanza mjini hapa.
Wasemaji hao walisema Chifu Fundikira, alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu, maradhi ambayo walisema alikuwa akihangaika nayo kuyatibu bila mafanikio.
Taarifa hizo zilisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora ya Kitete, wakati mipango ya mazishi ikiendelea kufanywa, lakini yanatarajia kufanyika kesho, katika eneo la utemi wa utawala wake, la Itetemia mjini hapa.
Marehemu Fundikira, alizaliwa Machi 1921, Itetemia akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya marehemu Mzee Saidi Fundikira.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Tanga na baadaye elimu ya kati katika shule hiyo na kisha kujiunga na masomo ya sekondari katika shule ya Tabora, ambako alihitimu mwaka 1939.
Chifu Fundikira alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, mwaka 1940 hadi 1946 na kupata Shahada ya Kwanza ya Kilimo na mwaka 1957 alitawazwa rasmi kuwa Chifu wa Wanyamwezi akishika hatamu ya uongozi wa jadi katika himaya ya Unyanyembe.
Mwaka 1961 alichaguliwa katika Serikali ya Ndani iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Mkuu, marehemu Mwalimu Julius Nyerere na kuwa Waziri wa Maji, wadhifa aliotumikia kwa mwaka mmoja, kwani mwaka 1962 Tanganyika ilipopata hadhi ya Jamhuri, Chifu Fundikira, alikuwa Waziri wa Kwanza wa Sheria.
Mwaka 1964, alijiuzulu wadhifa huo, kutokana na kutokuelewana na Mwalimu katika utawala wake na kupumzika katika utumishi wa Serikali hadi mwaka 1967, alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti Bodi ya Shirika la Ndege la Afrika Mashariki hadi mwaka 1972 alipomaliza kipindi chake cha uongozi katika shirika hilo.
Chifu Fundikira, aliendelea kufanya kazi binafsi hadi mwaka 1990 alipoanza tena harakati za kisiasa za kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, akiwa na akina Prince Bagenda, Mabere Marando, Ndimara Tegambwage na wengineo na kuanzisha Kamati ya Kusimamia Mabadiliko ya Kisiasa nchini (NCCR).
Baada ya kuanzishwa rasmi mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992, Chifu Fundikira, alianzisha chama cha United Movement for Democracy (UMD) na kushiriki katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi nchini mwaka 1995.
Alikiongoza chama hicho hadi mwaka 1999 alipokiacha mara baada ya kufariki dunia kwa Mwalimu Nyerere na kuamua kurejea CCM miezi miwili baadaye na baada ya kumalizika uchaguzi mkuu mwaka 2000 aliteuliwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa, kuwa mbunge wa kuteuliwa hadi mwaka juzi.
Alimaliza utumishi wake wa ubunge na kupumzika akiwa mzee wa CCM hadi alipofariki dunia jana mchana.
Kwa mujibu wa mila na desturi za Wanyamwezi, chifu au mtemi anapofariki dunia, mazishi yake hufanywa usiku, lakini kutokana na mabadiliko, sasa Chifu Fundikira, atazikwa jioni wakati jua likikaribia kuzama au muda mfupi baada ya jua kuzama. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
hivi huyu bwana gado si ndiye yule ambaye nasikia alichora katuni ya raisi wetu akilambwa miguu na waandishi wa habari?
ReplyDeletemji kasoro bahari morogoro
HIVI MICHUZI WEWE NI MMAKONDE???
ReplyDelete