Msanii Juma Kassim, almaarufu kama Sir Nature, amechaguliwa kuwania tuzo za kituo cha Televisheni cha Channel O zijulikanazo kama Channel O Spirit of Africa Music Video Awards zitakazofanyika Oktoba 11 mwaka huu huko Johanesburg,Afrika Kusini.


Nature atakuwa akiwania tuzo ya video bora ya Afrika Mashariki na wimbo wake wa Mugambo, wengine waliopendekezwa kuwania tuzo hizo ni Kube wa Kenya, IDA wa Kenya akiwa na wimbo wake wa 'Make it Hot' Nameless wa Kenya akiwa na wimbo wake wa Sinzia, Peter Miles wa Uganda na wimbo wa L'ove' na Wyre wa Kenya akiwa na wimbo wa 'Make A Choice'.
shime wadau na tumpigie kura mwenzetu awe na nafasi ya kushinda. wenzetu kwa watani wa jadi na kwa mzee m7 wanachakarika ile mbaya kuwapa tafu wasanii wao. Utaratibu wa kumpigia kura Nature unaweza kuupata hapo chini
http://www.mnet.co.za/channelo/shows/nomination.asp?selnav=9

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AMINAYA BABAKE NECHA.Mwanangu ileile.Kamua baba kamua baba kamua tuzo hii ni yako.
    Wa Majita Bugunda

    ReplyDelete
  2. WANDUGU SAMAHANI NATAFUTA MAWASILIANO YA MR 2 AKA SUGU HUKO MARAEKANI KAMA BADO YUKO HUKO.NATAKATA UJE UTUFOKEE MAHALA FULANI UGHAIBUNI

    ReplyDelete
  3. nature unamuoa lini bi Pili?

    ReplyDelete
  4. hongera juma
    hivi,kuna kitu kimoja hapa sikielewi hivi na utitiri woote ule wa video za wanamuziki wa bongo ndio kusema video moja tuu ya juma nature ndio imeonekana kufaa?
    kwani za wenzetu wa kenya zina tofauti gani na zetu au hata za afrika ya kusini?
    Mhh tanzania iko kazoi kweli tena sio ndogo mbaya zaidi tunapenda kujisifia bila kusubirir kusifiwa
    nafikiri kuna kitu cha kujifunza hapa

    ReplyDelete
  5. acha bangi kijana

    ReplyDelete
  6. michuzi kaweka hiii taarifa ili tumpe taff mbongo mwenzetu sasa nyie mnaomjua sana huyu Jnature nakutaka kujua anmuoa lini pili, na aache kuvuta bangi? anzisheni blog yenu ya unyago ili mmfunze shwain nyie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...