Home
Unlabelled
mapambo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Sasa Bro Michu
ReplyDeleteWewe nakuamini kama mwandishi mahiri mwenye uzoefu, elimu na pia uwezo mkubwa katika uandishi.
Sio 'mkabara' ni mkabala ndugu na pia sio 'vayle' springs ni 'valley' Tafadhali ndugu usiwape makanjanja nafasi ya kukusogelea kwenye fani, uko juu baba! Pamoja na utani ktk lugha naomba hakikisha unatofautisha r/l, d/dh, l/r, s/th ili na watu wajifunze kiswahili chetu toka kwako mkubwa. Kama umekusudia kuvunja weka alama ya kuashiria kuvunja huko kwa kutumia italiki, herufi nzito, au alama za kufunga na kufungua semi.
Kiswahili sanifu 'mgane' sio jina rasmi la 'widower' ila ni 'mfaruku'. Na Mpakanjia hawezi kuwa mfaruku maana walishatalikiana anabaki kuwa 'mtalaka' kama mtoa maoni mmoja alivyokandamiza
Ila sikufundishi kazi
adagio
Mbona tunaabudu na kutukuza sana mambo ya UGHAIBUNI jamani?
ReplyDeleteHivi hakuna watu/wapambaji wakabuni upambaji wa KIAFRIKA?KITANZANIA jamani tukaona hapo niti vya mabua au mkao wa nyani/marimba jamani? Mwee!
Hii kasumba ya ughaibuni mpaka lini jamani? Vandumwe! Aka!
Anonymous hapo juu au adagio,
ReplyDeleteWewe unaishi Dar es Salaam au kijijini? Kama unaishi Dar umeshawahi kufika kwenye duka lao hao wapambaji? au unabwabwaja tu.
Kwa kifupi Kaka Michuzi AMEPATIA, duka linaitwa "VAYLE SPRINGS" na sio VALLEY. Wana duka karibu na Salamander na lingine Bilicanas na lingine liko huku London. La karibu na Salamander ni la Jason Gaikward, na la Bilicanas kama unaelekea keep-left cha tip top zamani ni la Brandon, lakini wote ni ndugu na (shamba la maua lao liko Mbagala). Na la huku London ni la Mama yake Jason. (Mrs Gaikward)
Usitake kumrekebisha Bro.Michuzi wakati wewe mwenyewe HUJUI.
Ndio maana Biblia inasema, "MUWE WEPESI KUSIKIA NA MSIWE WEPESI KUSEMA".
Jesse .J.
Haya yote ni manjonjo ya kimagharibi ambayo tumeyapokea bila kuchuja kama ilivyo kawaida yetu waswahili tulio na vichwa vya kunguru. Haiingii akilini watu tunakamuana pesa kwenye vikao visivyoisha, kisha tunagidia ulabu na kiasi kinachobaki tunadumbikiza kwenye mapambo na kulipia kumbi za gharama kubwa huku tukiwaacha bi. na bw. harusi wakipiga miayo.
ReplyDeleteNi bora hizi pesa zinazotapanywa naamna hii ziwe zinakabidhiwa kwa waoanaji waende kuanzia maisha. Tukifanya hivyo tutakuwa tumefanya la maana saana.Naomba kutoa hoja
Ndimi tpaul(agent)
Wewew adagio ebu ondoa ushamba wako utamfundisha michuzi wewe shule unajua wewe au unataka kujifanya babu kifimbo cheza
ReplyDeletehivi kwani kukoselewa kwenye lugha ni kosa? Mbona mwenyewe adagio amesema hafundishi mtu kazi? Ni maoni tu kama mtu unajivunia kiswahili angalao ukiongee vizuri. Sio swala la kutoka kijijini au mjini. Hilo la Vayle kweli kachemsha ila Jesse J. mbona umekuwa mkali? Kwa sababu amekosoa angazo la biashara au? lol
ReplyDeletetpaul kuwa makini Jesse.J atakumwagia mijineno ingawa umesema ukweli. Hatuthamini cha kwetu na cha kwao si cha kwetu tunaiga. Ndo hivyo mambo ya mabizinesi na uwekezaji wa ndani
ReplyDeleteNdugu Wapenzi wa Blog ya Michuzi, Nina ombi maalum kwa Bwana Michuzi na wapenzi wote kwa ujumla.
ReplyDeleteOmbi
Kuwe na Blog ya kukutanisha marafiki ili wawe familia baadaye. zamani kulikuwa na pen pal sasa kuwe na e-mail pal ila please watu wawe serious sio wafanye joke, itasaidia sana kukutanisha watu. Maoni yenu tafadhali
Nafagilia na nakubaliana na wazo la watu kukutanishwa kwa kupitia hii teknologia.....moja ya faida ni watu mtaweza kukutana, mkawa marafiki....vilevile jinsia tofauti zikikutanishwa mungu anaweza kubariki watu wakafunga ndoa na kuanzisha familia.......sitashituka kuona yale manegative ya kila kitu kuanza kukosoa hii hoja.
ReplyDeleteKaka Michuzi huyo Anony wa Aug. 27 time 9:30 AM EAT inaonekana anatafuta MCHUMBA huyo.
ReplyDeleteMwambie aende kwenye websaiti ya "www.WAYN.com" kuna wachumba kibao huko wanakutanishwa.
All the best!