Home
Unlabelled
maudhi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kipanya acha matani,umeniua mbavu maana kweli afanyi chochote amekaa tu kama zuzu.
ReplyDeleteMheshimiwa Rais amekuwa na kauli za ajabu kidogo, mara wafanya biashara wanaoonea wakulima watakiona, mara wafanya biashara wa korosho wanapangiwa bei, mara biashara ya mafuta inaingiliwa. Mimi sioni haja ya Rais kutoa kauli hasa ukizingatia matamshi yake yanailenga suko huria, ambayo serikali yake inadai kuwa inataka kueendeleza. Lakini tena serikali hiyo hiyo inatoa ruzuku kwa vyombo vya habari halafu inataka ishindane na vyombo binafsi.
ReplyDeleteKuna wakati mwanasiasa mmoja alitoa kauli kuwa CCM haina dira wala muelekeo, wanasema hivi na kufanya kile. Wakati mwingine hua namuona Rais Kikwete kama msoshialist fulani hivi kutokana na kauli zake za kuingilia soko huria. Mara utamsikia ana "waomba"wafanyabiashara wasipandishe bei, na wakati mwingine ana waonya.
Kama serikali ina nia nzuri ya kuinfluence market forces basi inabidi ijenge na kusimamia infrastructure ambayo itasaidia wakulima, waweze kupata, market access and information, mfano ni huu;
Ministry launches SMS for livestock dealers and farmers
Story by NATION Correspondent
Publication Date: 8/8/2007
A new information system will allow livestock traders and farmers to access to daily information on selected markets countrywide through a short messaging service (SMS) and the Internet. The National Livestock Marketing Information System is aimed at improving access to market chains and provision of national market information to producers and traders in addressing the market inefficiencies.
“Producers and traders want to know in particular the prevailing prices in various markets so that they are able to make decisions that will enable them get the best prices for their animals and animal products” said Livestock and Fisheries minister Joseph Munyao during the launch. The system is a joint initiative by the ministry and the Livestock Information Network and Knowledge System (LINKS), and will train data monitors from 25 key markets.
The move is expected to help farmers and dealers get better prices by keeping them in touch with the market.
Kauli za kisiasa hazisaidii kama ambavyo tumeona kwa suala la mafuta. Kwenye free market, soko ndilo linaloamua bei kwa hivyo kama serikali inataka kuinfluence bei ya soko basi aidha inunue mafuta na kuweka strategic reserve ama inunuena kuendesha vituo vya mafuta, ili iweze kuuza kwa bei inayotaka, lakini uzoefu unaonyesha kuwa njia hiyo ina mwisho mbaya.
Kazi ipo hapa.
ReplyDeleteSio ZUZU ni MSUKULE, maana msukule huwa inactive kabisa kutoa maamuzi yake, kila kitu unategemea kigagula wake
ReplyDeleteUsanii ukiupeleka hadi kwenye uraisi ndio matokeo yake hayo. Acha siasa kwenye uraisi, kuwa mtendaji. Juzi ndio kaniua kabsaa yaani anasema kuna mtu alimpelekea taarifa za uongo akamfukuza kazi mtu. Kwanini mtu akuletee taarifa za uongo? huna check and balance kuhakikisha? sasa ameapa kutomfukuza kazi mtu yeyote mpaka ulete ushahidi. kama umeshafanya uamuzi kwanini unajutia? Kwenye nafasi muhimu kama hiyo hutawafanya watu wote wakupende, chukua maamuzi kwa maslahi ya nchi. Mtu akiuudhika akasage chupa abwie.
ReplyDeleteMHESHIMIWA ISSA HABARI ZA LEO MAALIM..HUYU ."..MKWARE.." MWENZIE KAMUACHIA NCHI MAHALI PAZURI SASA UNALALAMA NINI..KAMA HUWEZI.."..LET THE KEP FIT WEAR IT.."..Kumradhi Jamani maneno"..MKWARE.."(Mpenda Ngono) NA "..MKWERE.." (Kabila) tofauti ya kimaandishi ni " A" na "E" kumradhi kama nimetumia visivyo.
ReplyDeleteha ha haaaa...hapo ni kaaazi kweli kweli!!! nadhani tukishaudhika tunalala na kesho ni siku nyingine!!! Mungu ibariki Tanzania na watu wake!!
ReplyDeleteJamani natisha!
ReplyDeleteMfano Waziri wa mipango na uchumi alisoma bajeti ambayo lengo ni kushusha inflation chini Waziri wa fedha akasoma bajeti ambayo inapandisha inflation!
Hakuna cordination kwenye budget process! Hivi kuna wataalamu huku Ikulu na wizarani kweli au kuna wababaishaji?
Suala lingine dogo kwenye bajeti waliondoa ongezeko la bei ya mafuta ya taa na kulibandika kwenye Dizeli eti ili wawapunguzie mzigo watu wa vijijini! Hivi ukipunguza bei kwenye mafuta ya taa ukabandika kwenye dizeli una akili kweli? Kwani hayo mafuta ya taa yanabebwa na nini si na magari ya dizeli! Sasa hizo gharama zilizoongezeka kwenye dizeli lazima mfanyabiashara azirudishe kwenye bei ya mafuta ya Taa! Yaleyale! Umedanganya wabunge kuwa umeondoa mzigo halafu unarudisha kupitia mlango mwingine!
Halafu ukipandisha dizeli hujui matrekta vijijini yanatumia dizeli si utasababisha gharama za mkulima kwenda juu na inflation kupanda juu huko vijijini?
Huu usanii kwenye bajeti ni wa kitoto kabisa na unaonyesha utaalamu ni sifuri kwa wapanga bajeti!
Mbona Raisi na mawaziri tumewapata safari hii! We acha tu.
Ni uswahili tu!
Maneno mengi utaalamu sifuri.
mimi nadhani mh.Rais anapaswa kujiandaa kabla ya kutoa kauli zake.Sasa leo anapotoa kauli hii halafu kesho akabadilika anaonekana kama hayuko makini vile.Ndipo watu wanapomuita msanii.Ila kuna issue nyingine ambayo naona ni serious pia.Wakati mh,Rais anapokwenda kuhudhulia vikao vya kimataifa,ningeshauri awe makini sana na wasaidizi wake wamuandae vya kutosha kukabiliana na maswali.Kuthibitisha hili naomba wadau m you tube;kikwete-world economic forum 2007.Yaani hapa kwa kweli mh,Rais sikuridhika kabisa na majibu yako.
ReplyDeleteone
Tanzania, Tanzania aaaa!!
ReplyDeleteNakupenda kwa moyo wotee!!
Nchi yangu Tanzaniaaaaaa
Jina lako ni tamu sanaaaaaaaaaaaa!!!
Nilalapo nakuota weweeeee!!
Niamkapo ni kheri mama weeee!!
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa Moyo wote.
Tanzania Tanzania,
Ninapokwenda safariniiiiiiiiii
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi!! Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu kabisaaaaaaa
Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote
WADAU NIMEKUMBUKA SANA WIMBO HUU HUWA UNANILIWAZA PAMOJA NA TABU ZOTE AMBAZO HAZINA SULUHISHO HATA TUKIPIGA KELELE MIAKA 100. NAOMBA NISAIDIENI KUMALIZIA BETI ZA MWISHO
Siasa na sanaa kaaaazi kweli kweli!
ReplyDeleteHili suala la Kikwete kumfukuza kazi mtu kwa majungu na kujifanya eti 'kusikitika' ni unafiki na ni usanii tu km ilivyo kwa usanii mwingine wowote. Kwa nini amfukuze mtu kazi km hana uhakika na tuhuma zake? Yaani jamaa bogus sana, hivi anapowalalamikia wauza mafuta hajui kuwa serikali yake ndio iliyopandisha kodi ya mafuta wkt ktk soko la dunia mafuta yameshuka bei kwa miezi hii miwili? Tumueleweje? Hata mawaziri wake nao ni bogus sana, hasa ukianziana yule waziri wa noti. Alipokuwa wizara ya magogo alichemsha, sasa tumempa wizara nyeti ya noti nako ni maumivu tu, sijui tufanyeje sasa! Ila ipo siku kitaeleweka.
Unajua wewe anonymous wa hapo juu umenikumbusha kitu kizuri sana. Waziri wa fedha alishindwa kuzuia magogo na kufanya biahsra za kuuza asali kule mali asili na sasa tunategemea ataweza kulinda mfumuko wa bei na kupanga bajeti. Kweli mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteMzee wa TBS
SERIKALI INAWASUKASUKA WALALAHOI
ReplyDeleteMwanzoni mwa mwezi wa saba Waziri wa Fedha Mheshimiwa Zakhia Meghji alisoma Bajeti ya Serikali Bungeni.Miongoni mwa mambo yaliyojiri katika Bajeti hiyo ni kupanda kwa kodi mbalimbali hasa ile kodi ya mafuta ya magari na mitambo (diseli na petroli) na mafuta ya taa. Kupanda kwa bei ya bidhaa hizo kulilalamikiwa sana sio na Wabunge tu bali hata Wananchi wa kawaida kwa sababu iliyo dhahiri kwamba bei ya diseli na petroli inapopanda kila bidhaa hupanda bei pia. Hilo linajulikana vema hata kwa mtoto wa chekechea.
Katika kuhitimisha hotuba yake kwa kujibu hoja za Wabunge, Waziri alilegeza kamba hasa kwenye kodi ya mafuta ya taa kwa kuwa ni bidhaa inayotegemewa na walalahoi walio wengi. Aidha ilizingatiwa kwamba kupanda kwa bei ya mafuta ya taa kungepelekea wananchi wengi kujikita katika matumizi ya mkaa,hivyo kuchochea uharibifu wa mazingira kwa kuwa miti mingi ingekatwa ili kutosheleza mahitaji ya mkaa kwa matumizi ya walalahoi.
Kushushwa kwa bei ya mafuta ya taa kulifanyika kwa makusudi ili kuwakoga walalahoi waamini kwamba serikali inawajali zaidi kwa sabababu “bidhaa yao” imelegezewa kodi na hivyo basi itakuwa ikiuzwa kwa bei chee. Hata hivyo, si kweli kwamba bei ya bidhaa hii sokoni ipo chini ukilinganisha na unafuu wa kodi uliotangazwa bungeni.
Kupunguza kodi ya mafuta ya taa pekee kulifanyika kwa kuzingatia uvivu wa kufikiri wa watumiaji wa nishati hii.kwa sababu sio rahisi mwananchi wa kawaida kuhusianisha kupanda kwa bei ya mkate, unga, sukari, mchele n.k, na kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli na diseli. Yeye atadhani kwamba petroli na diseli havimhusu kwa kuwa hanunui bidhaa hizo moja kwa moja kutoka sokoni. Atafikiri kwamba mafuta ya taa ndiyo yanamhusu zaidi kwa kuwa huyanunua moja kwa moja kutoka dukani akaenda kutumia nyumbani kwake. Kwa hivyo utaona kuwa swala la kupunguza bei ya mafuta ya taa ni swala la kisiasa zaidi kuliko kutoa unafuu kwa mwananchi mlalahoi.
Ipo hoja kwamba ukitaka kuwatawala watu milelele wanyime elimu na wadumaze kiuchumi.Baada ya kipindi cha miaka mitano tutakachoishi kwa kujifunga mikanda, waheshimiwa watakuja kusimama mbele zetu wakituomba kura. Kwa kuwa sisi tu wavivu wa kufikiri(kwa kukosa elimu) hatutakaa tuwahoji walitufanyia nini kwa kipindi chote hicho bali kwa sababu ya umaskini wetu tutakubali kupokea takrima ya pilau, kanga, fulana na kofia na tutawamwagia kura za kishindo. Tutakuwa tayari kutumiwa kama mabango kwa kuvishwa kanga,fulana na kofia zilizosheheni maandishi yenye kuwatangaza wao.
Kuna mbunge mmoja kutoka mkoa wa Kilimanjaro alisimama bungeni na kutetea kwamba bajeti ipite kama ilivyo bila kufanyiwa marekiebisho yoyote bila kuzingatia kwamba watakaoumia ni wananchi wa kawaida waliompigia kura za kumfikisha pale alipokuwa amesimama. Sijui alikuwa akijiamini nini.Labda naye ni mmojawapo wa mabingwa wa takrima. Hilo swala nitawaachia wapiga kura wake. Huenda ndivyo walivyomtuma.
Kwa mtaji huu basi tutaendelea kuwa watumwa ndani ya nchi yetu na kukabiliwa na ugumu wa maisha, bila kujua kwamba sisi wenyewe ndio chanzo, mpaka atakapojitokeza Musa wa kutuonea huruma na kututoa utumwani(umaskinini na ujingani)atuongeze hadi nchi ya ahadi( maendeleo endelevu na maisha bora). Hiyo siku haipo mbali inakuja. Tuvute subira ndugu wananchi.
thobiaschacha@yahoo.com
--------------------------------------------------------------------------------
Building a website is a piece of cake.
Yahoo! Small Business gives you all the tools to get online.