picha ya mwalimu bado iko kila sehemu sambamba na ya jk na kwa mujibu wa wauzaji wake zote zinauliziwa sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi Baba wa Taifa. Huyo alikuwa kiongozi wa kweli na hatatokea mwingine kama yeye.

    ReplyDelete
  2. MUUGUZI WAO NI MMOJA, KWAHIYO SISHANGAI.

    ReplyDelete
  3. Hapo zinaonekana sura mbili tofauti zenye mwelekeo na mtizamo tofauti kuhusu hatima ya Tanzania na watu wake. Kwani nini? Jadili.

    ReplyDelete
  4. Nyie mnategemea nini, Mtoto wa nyoka ni nyoka na kucheka na kulia zote ni kelele.
    Baba wa taifa hayupo nasi, lakini matawi yake mnayaona yanavyo fanya kazi, alipo tutoa huyu mzee tunajua wenyewe, Hatuna vita, hatuna makabila, kila unapopita nchi za nje unapata heshima kutokana na utulivu wa nchi yetu.
    Sasa kwa nini picha zisiuzwe.
    JK nae anaendeleza libeneke ya amani na maendeleo. Watanzania kaeni mkao wa kula.

    ReplyDelete
  5. JAMANI EH KIZURI HAKIDUMU DU!!!NYERERE FUFUKA UWAONE ULIOWAACHIA NCHI WANAVYOTUNYANYASA WANANCHI WA KIMA CHA CHINI!!!

    ReplyDelete
  6. Kuna mdau hapo juu kasema tujadili utofauti wa sura hizo mbili. Bila shaka anatka tujadili utofauti zao Urais wa Tanzania hadi Uenyekiti wa CCM.

    Kama picha zinavyoonyesha na matendo yao ni kweli JK Nyerere na JM Kikwete wana mitizamo tofauti. Wana itikadi tofauti. Hawaamini katika moja UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Ubepari umekita mizizi. JMK anafuata nyayo za mtangulizi wake BWM.

    Zidumu fikira sahihi za Mwenyekiti wa CCM Mwalimu JK Nyerere. Kwani nini naanza hivi? Kwa sababu fikira nzito za kimapinduzi zinazolenga kutetea haki, kuthaminiwa utu wa mtu na kumkomboa mnyonge kutokana na dhuluma na unyonyaji wa ndani (watawala dhalimu na mabepari) na nje (mabeberu, ukoloni mamboleo, utandawazi uliojaa wizi, soko huria linalowaacha wengi wakilia) siku zote hazifi.

    Mwalimu alisema fikra kama zake katu hazitakufa kwani zimekuwepo enzi na enzi na yeye ni muumini tu kama walivyo waumini wengine (Soma Africa Today and Tomorrow uk 23, Uhuru na Maendeleo, Azimio la Arusha nk). Aliamini katika usawa wa binadamu na haki kwa wote. Kwa imani na vitendo aliyatekeleza yale aliyoyaamini na hii leo Tanzania mnayoiona inang'ara katika uwanja wa kimataifa na matokeo ya kazi yake na SI MWINGINE. ASIJIGAMBE MTU.

    Ukisoma vitabu vyake, ukasikiliza hotuba zake na kufuatilia mwenendo wa maisha yake utakubaliana nami kuwa Mwalimu hakuwa MPENDA VITU. Aliweka mbele UTU ndio maana falsafa yake ya Ujamaa na Kujitegemea ililenga kuwaendelendeleza WATU na SI VITU kama ilivyo sasa, VITU NA UTAJIRI WA WATAWALA KWANZA. Ujamaa umezikwa. Na nikutokana na FIKIRA SAHIHI za Mwalimu na misingi endelevu ya kimaendeleo aliyoibainisha katika Azimo la Arusha, watoto wa masikini, yatima, wenye ulemavu, na wasichana walipewa fursa ya kusoma hadi vyuo vikuu vya nje tena BURE. Alijua fika kuwa Elimu ni Nuru, Mwanga na Mkombozi wa mnyonge. Leo hii wale waliokula kiapo kuwa ELIMU NI DHAMANA na KUWA WATAJIELIMISHA KWA KADRI YA UWEZO WAO (KIAKILI) KWA FAIDA YA WOTE wageuka nyamaume. SASA NI KWA FAIDA YAO. Mtoto wa masikini hasomi, yatima ndio basi tena. Na huo ndio ukweli. Hakuna kufikiria vizazi vijavyo. Hilo walimefuta waliokula kiapo. WATOTO WAO WANASOMA ULAYA NA MAREKANI, WATOTO WA KABWELA WANAFUKUZA MLIMANI. Hivi tunaandaa mazingira gani kwa nchi yetu? Kwamba watoto wa hao watawala watutawale milele? Huu USULTANI utalipeka wapi taifa letu?

    Mwalimu aliujua fika utajiri wa nchi yetu na mali asili zake. Hivi hatujiulizi kwa nini hakuingia Mikataba Mfu kama hii iliyopo sasa? Au alikuwa punguani asiyejua thamani ya almasi na dhahabu? Jibu ni wazi. Hakuwa na UCHU WA MALI. Hakuvaa hata pete ya dhahabu achilia mbali mikufu kama ile ya BWM. Hakutembelea Limozini. Hakuvaa mavazi ya bei ghali na makoti makubwa. Hakuwa na ziara za kiholela. Aliujua umasiki wa nchi yake na watu wake. Alibana MATUMIZI YA SERIKALI akajenga nchi. Mashirika, mabenki na viwanda mnayouza kavianzisha nani? Leo hii ukiuliza jamani kunani pale? Utajibiwa majibu alfu kidogo kwa kasi tena yenye hoja ya nguvu. Kasi isiyo na mwelekeo matokeo yake nini? Ajali na vilio. Mwendo Kasi Unauwa wanasema wanausalama barabarani. Na kweli uchumi unakufa.

    Waswahili husema matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno. Semeni na tendeni kwa vitendo kama alivyofanya JK. Komesheni rushwa na uuzwaji wa nchi kiholela. Watawala badilikeni na kuwa VIONGOZI KAMA MWALIMU. Ikumbukeni WASU - WATU ARDHI SIASA SAFI N A UONGOZI BORA kuwa ndio msingi wa maendeleo popote pale duniani.
    Mdau hapo juu katumia neno 'Matawi yake (Mwalimu) yanavyofanya kazi'. Ni kichekesho. Angalia Mkapa. Kafanya nini? Aliibaidirisha IKULU kuwa mahali PATAKAVITU badala ya PATAKATIFU. Ikulu si ‘matatizo matupu’ tena kama alivyosema Mwalimu. Ikulu ni raha tu na kuponda mali. Muulizeni Mkapa. Mkapa aliigeuza IKULU kuwa KIOSK.

    Mwalimu hakutaka UTUKUFU wala UHESHIMIWA. Alitaka UNDUGU, HAKI na USAWA. Na kweli alifanikiwa. Hakutaka matabaka ambayo mmeyajenga sasa. CCM MTANDAO na CCM BAKI ambao si WANAMTANDAO. "DHAMBI YA KUBAGUA NI SAWA KULA NYAMA YA MTU. ITAZIDI KUWATAFUNA KAMA UKOMA," hata muikemee vipi, ninyi ndio mumeianzisha. Kama matabaka na kubaguana kuko ndani CCM yenyewe, je mtu baki au mwanachama wa chama cha upinzani atabaguliwa na kukandamizwa kiasi gani? Huu ni Ukaburu ndani ya CCM. Mkitoka katika MTANDAO Mtabaguana hata kwa MITANDIO. Hapo ni pabaya kabisa. Mbele ni giza. Kwa mtandao huu hatima si nzuri kwa taifa.

    JM Kikwete alikuwa na ari kweli kweli lakini kakutana na vigogo. Wamemuwekea magogo na vigongo. Hawezi kushika kasi. Mgongano wa maslahi ni mkubwa. Hawampi na nafasi. Asipobadilika watu watamuhukumu wakisema ni walewale. Na huo ndio ukweli. 'THE BEAUTFUL ONES ARE NOT YET BORN.' Kituo Kikubwa.

    ReplyDelete
  7. Jamani someni kitabu cha Mohamedi Saidi(The life and the time of adulwahidi Sykes baada ya hapo msikilize mahojiano kwenye radio Butiama,Kikwete ansema ameweka ili awaokoe waislam kutokana na unyonyaji,unyanyasaji wa wakristu haya mambo hayajaweka wekwa directly lakini kwa critical thinking ndo hivyo especialy ukiangalia uteuzi woote wa Mrisho JK.

    Yetu macho.

    ReplyDelete
  8. NASHUKURU MTOA MAONI ANAYEITWA "Kituo kikubwa" KWA KUTOFAUTISHA KATI YA JK NYERERE na JM KIKWETE KUNA TOFAUTI KUBWA SANA KWENYE MAJINA ANGALAU KUNA WABUNIFU WAZURI SANA KWA UPOTOSHAJI KWA KUMPANDIKIZA JAMAA KUITWA JK NA MITAZAMO YAO NI TOFAUTI SANA KAMA ILIVYOELEZWA !

    "Zidumu fikra sahihi za Baba wa taifa"
    Mzushi

    ReplyDelete
  9. Kamaradi Mzushi, nafarijika na uungaji mkono wako wa hoja zangu hapo juu. Wamezidi kwa upotoshaji. Kituo Kikubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...