katika kuitikia wito wa wadau wengi sana walioutoa wa kuanzisha huduma ujumbe wa ndugu jamaa na marafiki kujiliana hali, kutafutana na hata kutakana urafiki wa kalamu, nazindua huduma hiyo leo hapa hapa ukurasani huku nikiwahakikishia wadau wote kwamba katika hili waosha vinywa hawatoona ndani kwani maoni yasiyohusu na ya kuponda nitayapiga chini. hivyo kuweni huru kutuma picha na salamu za popote ulipo kama alivyofanya mdau huyu na familia yake.


Mie ni mdau wa globu hii ambaye ni mwandishi wa vitabu vya watoto hapa USA, na moja ya kitabu changu kilichotoka mwezi july mwaka huu ni " Don't touch the calabash" Nimetuma picha ya mai waifu wangu pamoja na mai watoto wangu tukiwa Washington DC ambaso sasa ni wakati wa spring maana maua huchanua kwa pamoja. Natumai kupata ujumbe kupitia hapa toka kwa ndugu na jamaa na marafiki tuliopoteana siku nyingi na hata walio karibu nasi kwa sasa...


Asanteni

Projestus Rwegarulila

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. KAKA MICHU NAKUPONGEZA KWA ILO WAZO.

    LAKINI NAKUSHAURI HIYO TAHADHARI YAKO INANITISHA NAONA SIO WONINGI TU BALI NA KAUBABE KWA MBALI.

    SASA MFANO HUYO BRO PROJESTUS RWEGARULILA HAPO AMEANDIKA.NAOMBA KUMNUKUU "Tukiwa Washington DC**AMBASO** sasa ni wakati wa ...."mwisho wa kumnukuu.

    SASA TUSIMWULIZE NENO **AMBASO** MAANA YAKE NI NINI?WADAU TUNA HAKI YA KUHOJI KAMA NI KIHAYA AU KIDHUNGU AU KISWAHILI?

    HAYA BRAZA RWEGA BIG INFWAKTI MIMI SIKUFAHAMU ILA NAKUPA PONGEZI KWA KAZI UNAYO IFANYA.

    ILA MBONA UMEJIPENDELEA WEWE TU KUTAJA MY NAME YAKO TU BILA KUTANA MY NAME YA MY WIFE WAKO NA WATOTO?

    INGEKUWA VEMA KAMA UKITUSHIRIKISHA TUJUE MY CHILDREN WAKO NI WAKINA NANI KAMA NI KOKU AU NANI.

    BRAZA MICHU TAFADHALI SANA NAOMBA MTUNDIKO WANGU USIUMINYE BORA UNAIAMBIE NIU EDIT.
    ENE WEI TUTAFIKA TU.

    ReplyDelete
  2. ILA HATA MIMI NIMEPOTEZANA NA WATU KIBAO ITABIDI NITUMIE HII CHANSI KUWATAFUTA.

    ILA NGOJA NIVUTE PUMZI KWANZA NIONE MAONI YA WADAU KUHUSU HUYO BRAZA NA HILI ZOEZI.

    NA PIA NIONE UWEZO WA MITHUPU KUZUIA NGUVU ZA WADAU AMBAZO POLITISHANI WANAZIITA NGUVU YA UMMA.

    ReplyDelete
  3. Nshomire!

    ReplyDelete
  4. D.C Sasa hivi ni Spring??

    ReplyDelete
  5. D.C Sasa hivi Spring? It can't be

    ReplyDelete
  6. Kaka michuzi, Nafikiri ni jambo zuri akiweza kuweka anwani yake pia ili wahandishi wa hapa nyumbani wa vitabu vya watoto waweze kubalishana naye mawazo.

    Jambi jingine kaka Michuzi, niliona mwandiki machachari wa makala wa gazeti la The Citizen, Erick Kabendera, alikuwa kwenu uko. Eti hamtaki kusoma mnakwenda kwenye mdundiko? Makala ilikuwa nzuri maana jamaa kafanya utafiti na nilifurahi walivyoitafsiri kwenye gazeti Dada la Mwananchi. Naomba tu wadau na wenyewe watoe maoni yao maana watu wengi wanasema wazaramo hawataki shule ila sijawahi kuona Mwandisho yoyote anakwenda uko.
    Link yake hii hapa.
    http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=1081

    ReplyDelete
  7. Iwe Projestus Rwegarulila, waitu bwana, hongera kwa hiyo projekti!

    Lakini unatwambia"...sasa ni wakati wa spring maana maua huchanua kwa pamoja."

    Jaribu kuwa update!!!

    Sasa si wakti wa "spring"!!!!!!!! Ni wakati wa "summer" ambayo, oficially, yaisha juma lijalo hapa Amerika!!!!

    ReplyDelete
  8. NDAKI
    Hapo ni mkono tu umeteleza kaka alikuwa na maana "ambako" au vipi mbona na wewe pia umekwaruza hapo badala ya (kutaja) umeandika "kutana"?hicho ni kidhungu,kinyantuzu,kisukuma au kiswahili???check kwanza kibanzi kwenye jicho lako kabla haujaanza kucheck vya wenzako.
    nawakilisha.
    CHA CHANDU

    ReplyDelete
  9. Asante sana umesaidia sana mtu akituma comment yoyote ya kuponda usiweke tutakuwa tunakuletea picha nyingi sana zetu pia asante kwa kumsaidia mdogo wangu kuwa pata rafiki zake wote wamemjibu hata wengine alikuwa hawakumbuki ulipost tangazo lake wakati fulani hapa

    ReplyDelete
  10. CHA CHANDU nimekusoma Wabheja sana mwanawane.

    Niliandika makusudi kuona kama wadau wako makini.

    Ila ka ukweli mkono hakuteleza ila keybord yangu ni MANYO sio AUTO.

    Asante mdau

    ReplyDelete
  11. Ndio maaana nasema michuzi una akili sana manake kwa kuzuia mambo ya kashfa kwenye hii globu yetu ni muhimu sana mimi nilijuta kuweka picha yangu humo manake wenye chuki binafsi walinitukana sana,hivyo zuia mambo yote ya kashfa humu.KIDUMU NGULOBU YETU.

    ReplyDelete
  12. Miguu ya mke wake Porojetus nimeifagilia sana.

    ReplyDelete
  13. Hi Projestus,
    Please, naomba msaada wako mimi namtafuta Inocent Regalulira, mara ya mwisho niliambiwa yuko USA naomba mawasiliano naye.

    ReplyDelete
  14. Hongera sana bwana Projestus,mambo safi lakini mimi nilianza kumuangalia kwanza my wife wako katika picha mzuri sana,halafu na yeye katokea kule kule kwenye migomba na senene Bukoba.
    Asante sana kwa picha siku nyingine weka za wife peke yake basi.

    ReplyDelete
  15. Namtafuta brother wangu Jazzy B mara ya mwisho alikuwa Wichita
    Najua nitapata mtu anamjua tafadhali
    John K (London)

    ReplyDelete
  16. Looks like a happy fwamily. Hongereni sana.

    Kuhusu Spring, mi nina uhakika aliituma hii picha na ujume wakati wa Spring ila Bro Michu ndo kachelewa kuiweka. Maana nobody hawezi kuchanganya spring na Summer, labda kama ana siku 2 tu tangu aingie huko ktk hiyo nchi alipo. so wadau mjue aliyechemsha si Bro Rwenanihii, ila ni huyu huyu Bro Misoup wetu.
    Misoup usiibanie hii, maana sijatukana wala nini, nimeielewesha globu, au vepe? Teh Teh

    ReplyDelete
  17. kuchagua unajua mjomba manake uwo mguu wa mamaaa,duuu!nadhani nae atakuwa ishomirE,na nyinyi kwa nyinyi tu ndo huwa mnawezana.
    hongera mdau!
    ZIONIST

    ReplyDelete
  18. jamani jamani Spring in August?? Nshomire bwana!

    ReplyDelete
  19. Ndugu yangu Nshomire samahani sikujui wewe wala familia yako ila huyo mai waifu wako downtown chini ya sketi ametulia, sema ndio hivyo ni mali yako. Nasubiria huyo mchumba laiyechukua sura ya baba (huyo aliyepakatwa huyo). Kwa misosi ya kimerekani najua atakuwa reachable muda si mrefu.

    Mwisho kabisa nakutakia kila la heri katika jitihada zako za kuwatafuta mliopoteana.

    PS: Michu usibane comments hii ndio raha yenyewe ya blog inapokuwa for social affairs

    ReplyDelete
  20. Bro Michu jamani mbona umepiga mkwara hivyo? Unajua waosha vinywa a.k.a wamwaga sumu wapo na watakuwepo. Ndo maana ya duniani kuna watu na viatu.

    Legeza masharti angalao watu watoe maoni, sifa na hata changamoto ila wasitukane tu.

    Ila Ashomire maiwaifu wake yuko bomba sana na vile amemkalisha front seat, si muchezo anawashinda baadhi ya Vi-Vodakom. Wamependeza na watoto wana afya

    Kwa heshima ya Bro Michu na taadhima ya wadau wenzangu naomba kuwasilisha

    mwendapole

    ReplyDelete
  21. Duh! Tayari wameshaandika upuuzi na wewe bila kujali ukaupost hapa! Halafu unataka watu waweke picha zao hapa!

    ReplyDelete
  22. Naomba Mungu asinitie MAJARIBUNI nikatuma picha naweza kufa kabisa kwa hayo maneno ya waswahili wenzangu, duuuuuh!!! Yaani Michu hapo ndo ume edit zile mbaya saaana??? Kaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  23. Jamani mi,ninamtafuta Rafiki yangu mmoja anaitwa EDWIN CLAVERY RULAGILWA ni muhaya huyu jamaa mara ya mwisho tulikuwa wote pale Kilombero Sugar primary school,Babake alikuwa askari polisi 1976-80,Lakini waliamia Bukoba,Michuzi naomba niulizie wadau huko mi niko USA,KAMA NI MZIMA AU..........

    ReplyDelete
  24. ukitaka kutukana wewe andika kidhungu michuzi mpaka apeleke kwa mtu wa kutafasiri too late...lol

    ReplyDelete
  25. Na mimi namtafuta huyo Innocent Rwegarulila (Bube). Anyefahamu anapatikana wapi atujulishe.

    ReplyDelete
  26. Shumwaramu Weitu Mr.Projestus Rwegarulila,safi sana nafurahi kusikia kuwa unandika vitabu vya watoto - itakuwa vizuri kama vinaendana na ka-utamaduni ka kiafrica basi ningependa kuwanunulia wanangu ili wasome umeisha weka AMAZONI? Obakeise Weitu++++

    +++‘People cannot be developed, they can only develop themselves. A man develops himself by making his own knowledge and ability and by his participation as an equal in the life of the community he lives in’++++

    ReplyDelete
  27. Hi Projestus,
    Nakusifu kwa kuandika vitabu vya watoto.wewe ni Mtanznaia wa pili ninaemfahamu anaandika vitabu vya watoto akiwa ughaibuni.Yupo Tolo Mollel ambae ameshinda several prestigious awards nchini Canada.Alikuwa anafundisha Theatre Arts University of Dsm.Naomba kujua nitapataje kitabu chako for my collection.
    Kaka Mich good work!Especially kama utakuwa unkarantini kupondana wabongo.

    All the best,
    mtamaduni.

    ReplyDelete
  28. (samahani kama huu ujumbe utatokea mara ya pili, hii skripti ya blogu hainiambii kama imeweza kutuma au la)

    Bw Michuzi, tafadhali bakiza hili blogu kufanya kile lilikuwa linafanya: serve out classic professional photos by the leader in the industry. Limetokea kuwa possibly the most popular blog by a Tanzanian. Hii ya kukaribisha watu kujionyesha wanachofanya na wake zao huko DC au kukosoana kiswahili siyo kitu watu tuliosubscribe kwa feed za Michuzi blog tunategemea.
    Please let someone else afanye hayo, usiharibu hii kitu nzuri.

    ReplyDelete
  29. Nakushukuru Bro. Michuzi/Misupu kwa kuweka hili wazo ktk BLOG yako. Mimi ninaomba kama kuna mtu anajua Bw. Karungula yuko wapi kwa sasa kwani mara ya mwisho tuliacha naye jeshini pale RUVU mwaka 1985 kabla ya mimi kuja huku CANADA mwaka 1988. Kama kuna yeyote anafahamu alipo au ana anuani yake basi anitumei kupitia kwenye hii BLOG maanake huyu Bwana alikuwa rafiki yangu sana hivyo ningpenda kuendelea kuwasiliana naye !!!!

    ReplyDelete
  30. Ahh, what a nice looking family - your children look soo cute - baby girl looks as kind as her mother - baby boy too. I wish you well. And kudos for writing childrens books - I hope they have lots of African illustrations. Are your books available in TZ? Where, pray tell?
    From just another Mdau.

    ReplyDelete
  31. Wewe Bw. Celestine Kayenze, hapo juu ni Mr. Karungula yupi unayemzungumzia au kumuulizia ????? Tafadhali fafanua zaidi ndipo utakapoweza kusaidiwa !!!!!

    ReplyDelete
  32. mimi namsapoti kwa nguvu zote huyo mdau Dan wa hapo juu kwa kusema kuwa hii idea siyo yenyewe Michuzi kwa kuileta hapa. kwa jinsi nionavyo huu ukurasa utakuwa unajaa picha za kila anayejisikia kuuza sura na kujisifia tu na kutukosesha kupata habari na picha muhimu. watanzania kwa sifa wameshindikana. napendekeza ungekuwa na segment tofauti katika hii2 blog yako kwa ajili ya wale wanaotafutana i.e kama vile tu kwenye kipengele cha kumbukumbu, etc

    ReplyDelete
  33. mzee nimekukubali

    ReplyDelete
  34. Namtafuta msichana anaitwa Neema Usiku,maana nimemwandikia bwana Michuzi email aweze kunisaidia kuweka ad yangu kwenye blog yake naona ameniwekea kiwingu kabisa...I don't know kama Michuzi anajua Umuhimu wa kumtafuta mtu.

    Anyways,anybody with information za Neema Usiku please!~....

    ReplyDelete
  35. aganndi!...kuna mdau kanirusha stimu...wazaramu temeenda shule bwana ( au bibi? )...it looks like that but its not the case...hatuchezi mdundiko tuu tupo tuliofutafuta ujinga kidogo look around you...mbona kuna sindimba, kitoto, kihoda na nyingine nyingi kwani zachezwa na nani ndugu yangu...pia naona humu ndani muko na sly foxes wa maiwafu za watu...angalia alafu meza mate tuu...au subiri mkono udondoke uudake kudadadeki

    ReplyDelete
  36. wewe poloje nataka uniambie wewe ni mtu wa kijiji cha wapi,pengine unaweza kuwa ndugu yangu bwana! onshulile efamili yawe

    ReplyDelete
  37. BREKING NYUUUUUUUZZZZ MISS TZ 2007 SASA NI LILIAN ABEL KUTOKANA NA UKWELI KUWA RICHA ALIKOSEA ILIBIDI AKASHINDANE NA WAHINDI WENZAKE UDOSINI. HIVYO WATZ KUWENI NA AMANI KWA HILO! RICHA NI MISS INDIA-TAWI LA TANZANIA!

    ReplyDelete
  38. wewe real fighter umeanza tabia mbovu za akina mtikira. huo ni ujinga hasa ktika karne hii. na kukumbusha hii hii sio blog ya wajinga kama wewe. anzisha yako. uzawa umepitwa na wakati.

    ReplyDelete
  39. Wewe ni Projestus wa Gera Mtuza kwa ta Rwegarulila? Hata mimi nakujua. Natoka hapo hapo kwenye kijiji chako. Nimekuona umekuwa mpaka una my wife wako na watoto. Keep it up bro. Nitafute nikupe michapo.

    ReplyDelete
  40. Nawashukuru wadau wote mlio changia ila wengine tuna hamu ya kuwajua ingawa ni wachache mlio weka majina yenu.Kwa wale wapenda maendeleo vilevile tunawaona na wale wenye kupenda kufrahisha nao pia tumewaona.Sisi tulioko ughaibuni tuna hamu sana na nyumbani na ndiyomaana tunaingia kwenye blog ya michuzi.Kwa walio ulizia vitabu vyangu vinapatikana hapa USA kwa $10 kila kitabu. Kama kuna mdau aishie Tanzania angependa kupata kitabu kimojawapo aniandikie na nafanya mpango wa kuviprint huko nyumbani hivyo bei itakuwa poa.e-mail yangu ni rwegap@yahoo.com projestus

    ReplyDelete
  41. Wadau mbona wengi mnaficha majina
    yenu? nafikiri hii ndiyo inachangia wengine kutumia lugha au utamaduni usiokubalika.Projestus

    ReplyDelete
  42. Wewe CELESTINE KAYENZE hapo juu ni Mr. Karungula gani unayemuulizia kwani mimi nawafahamu akina KARUNGULA wengi waliopitia RUVU JKT ??? Weka wazi sera zako ili ufahamishwe kama unavyotaka !!!! Wasalimie huko CANADA na karibu nyumbani hata kuja kusalimia tu inatosha !!! Wacha kujichimbia huko UGHAIBUNI tokea miaka hiyoooooooooooo !!!!

    ReplyDelete
  43. Wadau wenzangu rafiki yangu ninayemuulizia ni Mr. Deo Karungula. SAmahanini sana kwani nilikuwa sijaweka wazi sera zangu. Naomba basi mnieleze huyu bwana yuko wapi kwa sasa na ninaweza kumpata vipi (anuani) !!!!!

    ReplyDelete
  44. haijambo familia? watoto wamekuwa wakubwa? tunaomba/tuwekee picha zao tumewakumbuka.mdau dsm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...