Semina na mtumishi/mwalimu Christopher Mwakasege.

Tar 03/08/2007 special for couples,
fee is only £10 per couple.
saa 9:30 mchana

Tar 04/08/2007 semina ya watu wote kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka jioni hakuna kiingilio.

Tar 05/08/2007 - kuanzia saa 08:00 mchana watu wote,
hakuna kiingilio

Mahali: Vision college,
68 WALLIS ROAD,
HACKNEY WICK,
LONDON, E9 5LH

Watu wote mnakaribishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. jamani watu wa London kama mnanafasi nawashauri mwende kumsikiliza huyo jamaa anamaneno mazuri sana. yaani kwa kila mtu mwenye kuhitaji upeo wa kuelewa mambo zaidi Go for it. Jamaa hakuboi kwa seminar yake unatamani kuwa unamsikiliza hata akimaliza kuongea. Mimi si mshabiki wa dini ila huyu mtu ana exposure ya kutosha sana.

    ReplyDelete
  2. Nawaonea wivu watu wa London. What a BLESSING!!!! Na sisi wa nchi zingine tukumbukwe jamani na wanaopanga hizi ziara.
    Kila la kheri watumishi wa Mungu.
    Anon hapo juu nakubaliana na wewe. Hii ni zaidi ya mikutano ya kiinjilisti. Mtu ukihudhuria unapata full package.

    ReplyDelete
  3. ANON August 3, 2007 9:21:00 wache upapembe wako du

    ReplyDelete
  4. hawa wachungaji wa siku hizi wanannishangaza sana walipewa na mungu hizo karama /vipaji vya kuchapa neneo na kuwaongoza watu katika muenendo wa kimaadili walipewa buree na almighty
    lakani anagalia siku hizi walivyomstatri wa mbele ktk kuuza uwezo wao amabao mungu amewapa bure
    anagalia mungu amesema nini juu ya hii issue
    hakika utawajua kwamaba siku hizi ni biashara na watumishi wengi tuu wanajifanya wakristo lakini sio kweli kama yeyey ni mkristo basi je isisngekuwa vema kufanya kazi zake kwa kufuata muongozo aliowapa kristo mwenyewe ktk biblia? hebu fikiria jinsi wanavyotumia jina la yesu eti wanaponya ... na japao ukweli unafahamika kwamba wanaongeea na wale watu kabla hakuna tofauti na wafanyabiashara wengine ninaowafahamu kama popof.ben hein,mtikila,kaswege,matelevangelist wooote,kakobe na wale woote wanaoclaim eti wanaponya watu na kuperform miracles
    tafadhali msikubali kutoa fedha kwa ajili ya semina hiyo kama yeye anafanya kazi ya mungu na aalike watu bure kwa sababu kipawa hicho alipewa na mungu bure na biblia inaseama hivyo

    ReplyDelete
  5. weeeee jamaa wa August 3, 2007 1:54:00 PM EAT,hayo ni mawazo yako potofu waache wahubiri waendelee kutangaza neno la mungu, kama wewe hauko tayari si tuko tayari kutoa hela kiasi chochote kile wanachotangaza.
    ushindwe kwa jina la yesu na ulegeeeee kabisaaa!

    ReplyDelete
  6. anonymous wa August 3, 2007 1:54:00 pole mwee! unatia huruma sana.huo mgomo fanya peke yako, wenzako tutalipa tuu.

    ReplyDelete
  7. nimekubali maoni yenu ninyi anany wawili hapoa juu .
    hivi mlishawahi hata siku moja kufikiri na kujiuliza ni kwa nini huyo jamaa na wachungaji wengine woote wanaoclaim kuokoka WANACHARGE PESA ktk huduma za kiroho ?
    ebu jiulize hao akina kaswege wanafuata mfano wa nani kwa mujibu wa maandiko? kama wanafuata mfano wa mwanzilishi wa ukristo basi hamwoni kwamba Yesu mwenyewe angakuwa tajiri sana kwa kuuza huduma za kiroho? na what happens kwa masikini wasio na mipesa (ponds) ndio kusema hawatoweza kupata huduma za kiroho?
    wacheni kuwa naive someni biblia kwanza halafu muwaangalie hawa akina kaswege kama kweli ni watumishi wa mungu hebu nikuulize ni mtumishi gani wa mungu anyemwabudu yesu? badala ya kumwabudu Mungu(yehovah,Yahwekila kitu kwao wao jibu ni yesu je ni kweli jibu la kila kitu ni yesu ..... je ndivyo yesu mwenyewe alivyosema hivyo? someni biblia jamani ili hawa watumishi wa shetani waangushwe na nguvu za mungu (yahwe/yehovah)
    hivi mmeshwahi kujiuliza kwa nini mtumishi huyo mwokovu hana kazi anasema kazi yake ni kuchapa neno tuu? je hii ni kweli ? inawezakana vipi kusustain familia yake na maisha yake kama hatouza huduma ya kiroho kwa kuwadanganya watoto wa mungu kwamba ni donation,mara fungu la kumi ... alimradi tuu
    Hivi manajua kwamba hakuna mchungaji wa kitanzania mwokovu ambaye ni masikini au (anayeishi maisha modest) mnafahamu hilo? ask yourself why? najua wengi wenu mnaoclaim kwamba mmeokoka mtanipinga .... yes man kila haki ninachowataadharisha ni kwamba msichukue kila kitu au kumwamini kila mtu anayedai ni mchungaji na kuperform miujiza na kutaja jina la yesu so many times and loud kwamba huyo ni mtumishi wa mungu
    BIBLIA imesema wazi jinsi ya kumtambua mtumishi wa mungu na juu ya utoji wa huduma ya kiroho
    pia imesema wazi kwamba yesu sio mungu na kwamba imeandikwa kwamba ni Mungu pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa ,siyo yesu,bikira maria wala yeyote yule ,huduma zoote za kiroho ni kipawa kutoka kwake (Mungu) na siyo Yesu na mungu amempa mwandamu bure wala si kwa fedha ili woote tuweze kuiskia mafundisho yake Yehovah /Yahwe na tupractice na kyaeneeza kwa wengine huku tukiendelea kumwabudu na kumtukuza Mungu tuu na si yeyote yule
    huyo jamaa ni mtumishi wa shetani muwe waangalifu saana naye na hayuko peke yake wako wengi tuu wengine akina askofu kakabe ,televangelist Popof na wengine wengi tuu

    ReplyDelete
  8. hapa mnakosea mnapolaumu wachungaji au watumishi wa mungu kuwa wanataka pesa,wakulaumiwa ni waandaji wa hayo mahubiri ndio wanaopanga kila kitu,yeye amekaribishwa tuu.
    Wanaojua umuhimu wa mahubiri haya ndio hata kwa pesa yoyote ile wataingia.

    ReplyDelete
  9. inawezekana unachosema ni kweli kabisa hasa kwa wale atumishi wa kweli labda hawajuai kinachoendelea kwamba ni pesa tuu ndio inayotakiwa ili mtu mwenye kihu ya neno la mungu aweze kuhudhuria huo msenina ya kiroho.MMMH! ingawa bado naona hii ni kichekesho under normal circumstances ni vigumu sana kwa mtu awaye yoyote yule hata kama si mchungaji kuburuzwa kutoa huduma ya kiroho na ya kimungu bila kujua taratibu za kuliandaa tukio hilo.

    mimi bado nawashauri ninyi jamani anagalieni kananuni za biblia kuhusu mtumishi wa kweli wa mungu na kanauni za utendaji kazi za kitumishi halafu anagalieni yesu amesema nini juu ya Pesa na watumishi wanaomwakilisha hapa duniani.

    msiwe naive hivi sasa ulimwengu umejaa watumishi wengi sana wa shetani.mmojawapo ni huyu Mwakasege, wanaotumia jina la Yesu na kutenda dramatic miujiza kwa jina la yesu tena hupendelea kuitwa vyeo kama baba mchungaji,askofu nk wanatoa pepo hadharani na kusali hadharani kwa sauti kubwa kwa jina la yesu.Tena wengi wao hata wanabebewa biblia na wanacongreagation sababu yeye ni mtumishi wa mungu na hawaishi kuwaabia watu wamwabudu yesu badala ya mungu na kudai kwamba shida zako zoote ulizonazo basi zitatatuliwa na yesu .mhh hii ni kali kwelikweli.Ni kweli shida zetu zinatatauliwa na bwana yesu?hivi ndivyo biblia inavyosema?

    mbaya zaidi kazi hawana ili waweze kijikimu wao na familia zao matokeo yake ni kusisitiza fungu la kumi na donations kutoka kwa wafuasi wao masikini kwa kudai eti ukitoa bwana atakuzidishia .ni kweli ? ni bwana gani anayewazidishia wachungaji tuu na waumini kila kukicha maisha yao yapo vile vile na if anything yanazidi kudididimia ?
    uliza fadha hizo wanapeleka wapi ?zinafanya kazi gani?

    BENN HINN
    Mwaka 2005 mchungaji mmoja mokovu wa kimataifa BENN HINN huko nigeria aliandaa mkutano mkubwa wa uponyaji mjini lagos .aliingia airport na jet maalum expensive ambayo hata viongozi wengi tuu hapa africa hawana uwezo wa kununua
    alishuka na trupu lake na woote kuelekea kwenye mahoteli ya 5 star
    kesho yake wakaenda kwenye crusade hilo ambapo walikusanyika watu 300,000,
    benn hinn alihubiri lakini hakuwa na ule moto wa siku zoote mwisho wa mahubiri akiwa amekasirika akasema kwenye kipasa sauti "DOWN THE DRAIN 6 MILLION DOLLARS IS GONE " alishindwa kujizuia. aparently yeye na organisers wake walitegemea kupata watu milioni sita lakini haikuwa hivyo
    mpaka leo benn hinn haendi huko tena sababu iligundulika ni jinsi ganai wanvyofanya biashara na ilizua mtafaruku mkubwa kwenye vyombo vya uchungaji vya kipetecostal hasa wale waliokuwa waaminifu wakifikiri kwamba wanafanya kazi ya mtumishi wa mungu kumbe.... pia wachungaji local wa pale walikula milioni moja na zingine wakidai ni maandalizi .

    jamani mswaamini hawa wachungaji mkitaka kuwajua na kuwa pima someni ndani ya maandiko kisha mtaona wenyewe hili ni wimbi la watumishi wa shetani na walishatabiriwa siku nyingi na mwamnzilishi wa kazi za kitume yaani Yesu kristo
    swali la msingi ni vema kijiuliza kuna mchungaji gani masikini au mwenye maisha ya kawaida tuu kama mimi na wewe? na hasa huyo mwakasege ni mtu tajiri sana ukilinganisha na maisha ya modest ya wengi wetu hana shida mwakasege ,mali yoote hiyo aliyonayo ananpataje kama yeye anafanya kazi ya kiroho .acheni kuwatajirisha hawa watu toeni sadaka zenu kwa usiri tena kwa kiwango kile utakachojiweza na si kwa sababu mwakasege anasema pounds kumi huduma ya kiroho ni huduma ya bure imetoka kwa mungu bure
    pesa na kazi za kitume au huduma za kiroho ! wapi na wapi
    ama kweli yasu mwenyewe alitabiri haya na alisema kweli kabisa kwamaba siku za mwisho watu watafunikwa na lawlessness watacool off spiritually na hawatawoza kuona na kutambua .vingozi wa kishetani wanotumia jina la yesu watawaburuza wengi tuu ili wawaamni washindwe kufuata biblia wao wenyewe mpaka hawqa ataumishi feki wawatafsirie.mbaya zaidi wanhalalisha doctrine za kidunia na kuwafumba mamailiaoni ya watu masikini wenye kihu ya wokovu wa kweli na kihu ya neno la mungu
    pese pesa pesa ! hakaika yesu angelikuwa tajiri sana kama angeliuza huduma za kiroho na kulazimisha watu watoe mapesa matajiri sana tuu kama wangekuwa kama mwakasege

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli Mwakasege ni mzuri sana katika kutoa neno la Mungu na Maombi, nimeshahudhuria mafundisho yake kadhaa nikiwa Bongo, ila hili suala la pesa hata mimi limenipa utata.

    ReplyDelete
  11. JINA LA YESU KRISTO LIBARIKIWE

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2008

    Kila mtu anaweza kuwa na mtizamo wake/maoni yake juu ya jambo lolote katika jamii.Kitu cha msingi kutambua ni kwamba imani ni dhahiri ya mambo yasioonekana!Ninapoamini imani yangu itaniponya niweze kuuona ufalme wa mbingu hakuna atakayebadili imani yangu wala haipo sababu.Kwa hiyo ndugu waache wahubiri waenedelee na kazi ya Bwana.iwapo kati yao kuna farisayo atadhihirika parapanda litakapolia.
    Pia ni bora yule anayeiba na kuhubiri upendo,amani,mshikamano kuliko fisadi au magaidi wanaoua miili na roho na wale wanaochocheana kutekeleza mabaya yote.
    BWANA AWE NAWE,AMEEN

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2008

    Kila mtu anaweza kuwa na mtizamo wake/maoni yake juu ya jambo lolote katika jamii.Kitu cha msingi kutambua ni kwamba imani ni dhahiri ya mambo yasioonekana!Ninapoamini imani yangu itaniponya niweze kuuona ufalme wa mbingu hakuna atakayebadili imani yangu wala haipo sababu.Kwa hiyo ndugu waache wahubiri waenedelee na kazi ya Bwana.iwapo kati yao kuna farisayo atadhihirika parapanda litakapolia.
    Pia ni bora yule anayeiba na kuhubiri upendo,amani,mshikamano kuliko fisadi au magaidi wanaoua miili na roho na wale wanaochocheana kutekeleza mabaya yote.
    BWANA AWE NAWE,AMEEN

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 20, 2008

    hiyo amount ni gharama ya kulipia ukumbi na viti,hata kanisani tunatoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa n.k.Kwa hakika hakuna kinachoweza kufanyika bila pesa.Nampa pole sana tena sana huyo anayeshangaa kuhusu kuambiwa kiingilio.Je watahubirije wasipopelekwa?Ulifikiri Mungu alisema tutoe kwa ajili ya nini kama mambo yote yangekuwa free?.Na kwa taarifa tu
    YESU NI MUNGU.Soma biblia yako vizuri

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 20, 2008

    Ya Kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu.Kupata huo ukumbi wa mkutano ni pesa hivyo ni lazima aliyeandaa achangishe wenye kuelewa juu ya umuhimu wa hiyo semina.Sio lazima mhudhrue wote wachache watakaohudhuria ndio watakaopeleka neno hilo kwa wengine.Kama ilivyo kwenye elimu kuwa sio wote wanaokwenda shule ila wanaofaidi ni wengi zaidi ya waliolipa ada ya kwenda shule

    ReplyDelete
  16. hivi ninyi mnaolalamika kuwa watumishi wa Mungu wanataka pesa mna matatiza gani?
    Mbona kwenye kumbi za starehe zinatolewa lakini hamlalamiki?
    Nawaomba kama mnataka kuishi kwa amani acheni mambo ya Mungu yakae yalivyo kwani hata wewe usipotoa Mungu si maskini atainua watu wa kutoa hivyo naomba mfunge vinywa vyenu Mungu asije akawaadhibu.

    ReplyDelete
  17. Bwana asifiwe ndugu zanguni. kwakweli nimeshindwa kuwaelewa wapendwa kwani kinachowafanya muwe na maswali mengi juu ya hayo msemayo ninini??? Hivi wategemea Mchungaji aende huko alipe ukumbi, viti na huduma nyingine wewe kazi yako kwenda kusikiliza tu?? Jamani utoaji pia ni moja ya matendo mkuu ambayo tunafundishwa, jamani mtafuteni Mungu kwa gharama yoyote ile sio ukiwa unashida ndio umtafute, acheni kuwachambua watu huo sio ukristo jamani kama unaona mtu hakufai basi kaa kimya. Hasira ya Mungu isije ikakufika ukaanza kumtafuta Mungu kwa gharama ya pesa unazozipondea siku ya leo. Mungu anatupenda sana ndio maana anawatoa watumishi wake ili waweze kutulisha neno nasi tuliishi. Nawatakia tafakari njema wale wote waliokwanzwa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 29, 2009

    jamani ndugu zangu wakristu msiwe kama watu ambao hawakwenda shule kumbukeni mwenyezi mungu mwenyewe aliweka fungu la 10 kwa ajili ya ukoo wa lawi kwa ajili ya wao kutumikia nyumba ya bwana ndiyo maadna ya asilimia 10 ifanye kazi ya huduma ya mungu kama sasa hivi kama mjuvyo kila kitu kinahitaji pesa uchapisahaji wa habari, kukodi makumbi ya mikutano kama wanasafiri ni fedha inagharimu kuwasafilisha hawawezi kwenda kwenye shilika la ndege kuomba tiketi za bure, pia maandalizi mengi yanahitaji pesa sasa wasipotumia hivyo kukumbusha fungu la 10 itakuwaje na niwakati gani atapata nafasi ya kusoma biblia na kuzingatia na huku aje atoe ufafanuzi kwa watoto wa mungu kama unakumbuka vizuri hata yesu aliwaambia wanafunzi wake nendeni mkikaribishwa kaeni na kuwaubiria juu ya ufalme na mkikataliwa basi ondokeni wali msiangalie nyuma sasa ninyi mnaopinga tafadhalini kaeni kimya kama hamtoweza kuchangia kumbuka hata kupiga simu pia ni gharama na hao wanaowasikiliza na kukesha kuwaombea kama watakosa chochote unategemea wataishi vipi?
    Angalia mfano mzuri wa kanisa katolika na fedha za sadaka ndizo zinazoendesha maisha ya mapadre na misaada mingine kutoka roma na huko roma pia kuna michango wanachangiwa kama kanisa na hata vyombo vya kimataifa kwa ajili ya uduma hizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...