Mganga na Nyaoga Mahombolage, Wanasikitika kutangaza kifo cha BABA yao (pichani) kilichotokea leo Howard University Hospital, Washington D.C.

Msiba upo 1801 Mount Pisgah Ln #31,

Silver Spring MD 20903.


Tunaomba michango yenu ili tuweze kuusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania.Tuna weza kuwasilisha michango yetu kwa ndugu zetu Mganga na Nyaoga Mahombolage, nyumbani kwao address hapo juu


Vilevile unaweza kuwasilisha michango kupitia :

BANK OF AMERICA

ACCT# 446005082674

ROUTE# 052001633

Kwa jina la Mganga Muhombolage


jitihada zinafanywa ili tuweze kusafirisha mwili wa mareheu kati ya j/mosi 11 agosti, 2007 ama j/pili 12 agosti, 2007.


Vile vile unaweza kuwasiliana na wafiwa kwa namba zifuatazo;

202 374 0988,

202-243-9740,

301-559-3761

301-379-0693


Asanteni Sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mganga Muhombolage, Pole saana kwa msiba wa marehemu baba yetu mzee MUHOMBOLAGE, kwa niaba ya crue ya Hiza Abdalah Senkubo, Hamis Mwisongo na Elias Kayandabila Ex-mzumbe boys tunakupa pole sana kaka yetu Mganga.
    Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu baba yetu, amina!

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wafiwa

    ReplyDelete
  3. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.Amin

    ReplyDelete
  4. Mungu amlaze mahali pema peponi baba yetu poleni wafiwa
    Lizzie

    ReplyDelete
  5. Natoa pole nyingi sana kwa wafiwa(Muhombolage Family)Kwakweli Mganga na Nyaogo huko aliko mzee wetu anawashukuru sana kwa jitihada ambazo mlizozifanya kwa kusaidia mzee apate matibabu.
    Nyaoga you stop your life to take care of your father with this busy life in America.Mwenyezi mungu awe nawe katika kichwa chako na kufiriki kwako,macho yako na kuona kwako,masikio yako na kusikia kwako,mdomo wako nakila utakalo ongea,kwenye mikono yako na utendaji wako na akili yako na kufikiri kwako.God bless our father's soul Amen.

    ReplyDelete
  6. NAPENDA KUTOA POLE NYINGI KWA WAFIWA NA MUNGU AULAZE MWILI WAKE MAHALI PEMA PEPONI.
    MIMI NAFURAHI SANA KUONA WADAU WANAWEKA MATANGAZO YAO KWENYE BLOG HII YA MICHUZI KAMA YA VIFO, DANSI, BONGO FLEVA, NIGHT OUT NA MAMBO KIBAO.
    NASHANGAZWA NA KITU KIMOJA, HIVI MTU UKITOA TANGAZO LAZIMA UTAKE WATU WATOE MICHANGO?
    KAMA TUNAJUA KUSAFIRISHA MAITI NI GHALI KUTOKA HUKO MAJUU KUJA HUKU BONGO, KWA NINI TUSIMUWAHISHE MGONJWA ILI AFIE NYUMBANI AMBAKO PIA TUNAWAFAHAMU TUTANAONA NA KUWAAGA KWA MARA YA MWISHO.
    MARADHI MENGINE NADHANI HUWA TUNAAMBIWA KABISA NA MADAKTARI KUWA MGONJWA WETU JAMANI KUPONA NI MAJALIWA! TUWE TUNAENDA NA WAKATI KIDOGO.
    HALAFU NASIKIA HUKO ULAYA NA MAJUU KUNA MAKAMPUNI UNACHANGIA KILA MWEZI KWA AJILI YA KUKUZIKA KAMA UKIFA. KWANI NYIE NDUGU ZETU WA HUKO HAMJAJIUNGA NA MAKAMPUNI HAYO ILI KUONDOKANA NA ADHA KUBWA MNAYOPATA YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU?
    KAMA NIMEKOSEA NISAMEHENI LAKINI KWANGU NI USHAURI. USHAURI UNAWEZA KUWA MZURI AU MBAYA. AHSANTENI.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wafiwa. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  8. Anonymous wahapo huu , majuuu hakuna mambo kama hayo yakulipia kidogo kidogo ili, usafirishiwe muuli wa marehemu wako.. kwanza lengo lako linakuwa nikumponyesha mzazi wako sidhali kama utataka kumrudisha nyumbani eti hali yake ni mbaya ..pili ndege hazisafirishi watu waliozidiwa sana. Naona kama ulivyosema utakuw aumekosea sana kwa mawazo yako.. yah YOU ARE VERY WRONG. Poleni Familiya ya Dr Muhombolage.. tuko pamoja nanyi..

    ReplyDelete
  9. Poleni wafiwa,mungu awape faraja...we anon wa 8:16,wacha maneno ya namna hiyo,wakati wenzio wanaombeleza. Umeshawahi kufiwa wewe? Kuona mtu anaamua kutoa pesa kumleta mzazi wake mbali kote huku, ni katika kujaribu kuyaokoa maisha yake..huu ndio upendo na hizo baraka walizozipata watoto wa marehemu ni kubwa kuzidi we unavyofikiria. Wacha maneno ya kashfa, unasema wangemrudisha kabla hajafa kupunguza gharama, we ukiwa unauguliwa unadhani unaamini/kukubali kuwa mgonjwa wako atakufa? si unasali mungu na kujipa moyo kila dakika. Wacha bwana, mambo ya kitoto wakati kama huu.

    ReplyDelete
  10. Acheni kuvunga watu hapa....eti ndege haisafirishi mtu mahututi....kaaa kimya kuliko kutoa comment iliyopinda.....kinachoeleweka ni kwamba mzee alikuwa mgonjwa na isingekuwa busara kumrudisha akiwa hoi kwani ya mungu mengi na siyo vibaya kupambana mpaka dakika ya mwisho....pole sana ila sio vema kuropoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...