
wizara ya habari, utamaduni na michezo imekamilisha utekelezaji wa agizo la jk la kutaka ianzishe tovuti itayowezesha wananchi kuwasiliana na serikali yao kutolea maoni, ushauri au kero zao alilotoa wakati wa semina elekezi ya viongozi wakuu wa serikalini huko ngurdoto, arusha.
akitoa tarifa hii leo katika ukumbi wa maelezo,mkurugenzi wa idara ya habari kassim mpenda (pichani) amesema tovuti hiyo http://www.wananchi.go.tz/ tayari iko hewani itaimarisha dhana ya uwazi na uwajibikaji serikalini ambayo ni nguzo muhimu ya utawala bora. hata hivyo uzinduzi rasmi wa tovuti hiyo ambayo tayari inafanya kazi unatarajiwa kufanyika mwezi ujao.
mzee mpenda amesema kila atayewasilisha maswali au kero serikalini atakuwa anapatiwa majibu kutoka wizara husika katika kipindi kifupi iwezekanavyo na itaendeshwa na idara ya habari ama maelezo.
amesema kazi kubwa zilikuwa kunganisha mitambo ya ujumbe mfupi wa simu kupitia kampuni za voidacom, celtel na tigo na kwamba maofisa habari katika wizara zote wameshapatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mtandao huo kwa kujibu hoja mbalimbali za wananchi.
http://www.kero.go.tz/
ReplyDeleteLink ya kutoa kero ni hiyo hapo michuzi.
Haya tena Bwa mchuzi mambo yale yale ya kukurupuka kutoa saiti wakati haijakammilika. Nimejaribu kwenda kwene ukurasa wa kizungu naona wanasema " UNDER CONSTRUCTION" Sasa kama wanajua haijakamilka kwanini waiweke online?
ReplyDeletehalafu naona eti wanasema uchambuzi kwa kiingilishi ni survey. Hivi uchambuzi jamani sio analysis? au mie ndio sijui kinngreza na kiswahili halikadhalika?
MARICHA U'RE RIGHT!
ReplyDeleteYAANI HI SERIKALI YETU MBONA INAPENDA MAMBO YA ZIMA MOTO.
MI NAJUA HII WEB MUDA MREFU ILIKUWA INATAYARISHWA SASA LEO HII NIME BOFYA KWENYE SEHEMU YA HABARI MAJIBU YANAKUJA UKURASA HUU UNATENGENEZWA.
HIVI KWELI BONGO WATU ZAIDI MILIONI 36.WATAALAM KIBAO WA WEBSITE.HADI WATU BINAFSI, WASANII WANAWEBSITE ZAO NA ZIPO FULL ACTIVE.
SERIKALI KABISA MNATUWEKEA HEWANI VITU NUSU NUSU ETI MNAJINADI IPO TAYARI INASUBIRIA UZINDUZI.
CHONDE CHONDE TULIENI FANYENI MAMBO YA UHAKIKA.HIZO HARAKA HARAKA NDIZO ZINAZOSABABISHA HADI MNAKIMBILIA KUSIGN MAMIKATABA BILA KUJALI WADAU.
ENE WEI TUTAFIKA TU
miyeyusho hiyo..kero mtazisoma? sijui hebu tujaribu
ReplyDeleteSurvey - inaweza kuwa kama kukagua lakini sio uchambuzi. Analysis ndio uchambuzi lakini kiswahili chetu mwee.
ReplyDeleteMimi swali langu nilifikiri majibu yatakuwa yanachapishwa hadharani? Hiyo TRL ni ya nini?
Honesty kama wanataka kuwa una usawa hamna kufichakitu akiuliza mtu swali lijibiwe hadharani.
na wewe Lema upo bro? lakini na ile IPPMEDIA mbona update inachukua 24 hrs,hebu rekebisheni sio kusubiri bandika bandua after 24hrs news za maana zinabidi ziwe updated all the time kama hapa kwa brother michuzi
ReplyDeleteHiki ni KIINI MACHO tu hiki.
ReplyDeleteHoja nzito na za ukweli zinazoihusu serikali kuu wala hazitamfikia JK, na kama zikimfikia basi zitakuwa zimeshakuwa HEAVILY EDITED.
Nyie subirini tu.
Ndugu wanawanchi na Watanzania wenzangu, ni wajibu wetu kupongeza pale yapokuwepo mafanikio. Na pia haki yetu kukosoa pale tunapoona ipo kila sababu ya kufanya hivyo. Na huo ndio UHURU WA WATU. Naipongeza serikali kwa hatua hii ya kuanzisha tovuti. Lakini usiri na uficho unaowekwa unakatisha tamaa na kuonekana tuvuti hii ni kiini macho tu. Napendekeza usiri huo uondelewe. Tuwe wawazi. Tuanike hadhari kero na tujibiwe hadharani na si kwa kificho. Kwa tuwe na siri kwa matatizo ya umma huku umma ukiumia?
ReplyDeleteNashauri pia picha ya Rais imuonyeshe akiongea na wananchi USO KWA USO na kuwasikiliza kwa makini ni si kuwapa kisogo na kuwatega mgongo kama ilivyo katika picha hii. Kimantiki na katika tafsiri za picha hii inamaanisha kuwa hata mseme vipi yeye ana yake na hayuko tayari kuwasikiliza. Na asemacho yeye ndo hicho kifuatwe bila kuhoji. Picha hii inakwenda kinyume kabisa na malengo ya tovuti hii.
Ukipeleka kero yako kupitia http://www.kero.go.tz/, itabidi uchague ni wizara gani ya serikali inahusika, ikiwa ni pamoja na Ikulu.
ReplyDeleteKama hujui ni wizara gani husika, unataja pia. Unaweza kuandika jina lako au hapana!
Halafu unapewa nambari (au PIN #) ya kufuatilia jibu baada ya kama siku nne hivi za kufanya kazi.
Hakuna mwingine atakayeweza kusoma kero yako na majibu yaliyotolewa!
Watu wengine huogopa kuwa pengine huo ni mtego wa serikali kwa ajili ya mambo ya upelelezi na usalama wa nchi! Sijui.
Jamani kuna habari kutoka benton harbor michigan(USA) eti dad mmoja aitwaye mariam obrieno ameteuliwa na rais kuwa mbunge.Wadau tunataka tujuwe inakuwaje,huyo dada anafanya kazi ya kufuta mavi huko marekani hata shule haipandi atakuwa mbunge wa nani?jamani tufikirie hizi habari za kuteua mazezeta inakuwaje?
ReplyDelete