katibu mkuu wa umoja wa wanawake tanzania (uwt) mh. halima mamuya amejiuzuru wadhifa wake kwa kile kilichotajwa kutowajibika ipaswavyo. hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa zaidi ya kwamba uwt imeridhia uamuzi huo na imeshamchagua mtu wa kukaimu nafasi hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Michu na wadau wenzangu. Kweli nimeamini yale yaliyotabiriwa! wachana na Jembe na Nyundo watu wangu na bado yatakurupuka mengine. Ila afadhali, pole na hongera!!

    adagio

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi maneno hayoooooooooooooooooo!!!!!!.Kazi kweliiiiiiiii!!!!!!!.Kikulacho ki nguoni kwako.

    ReplyDelete
  3. ni makosa kuuita UWT, Umoja wa Wanawake Tanzania. UWT ni umoja wa wanawake wa CCM Tanzania. Badala ya UWT nafikiri ingekuwa UWCT.

    ReplyDelete
  4. makubwa!kwanza wazazi maregesi chini pwaa,sasa mamuya uwt,haya ngoja tusubiri linalokuja.

    ReplyDelete
  5. Hapa hakuna kitu huyu atakuwa ameshinikizwa tu na vigogo wenzake.

    ReplyDelete
  6. Bro michuzi uwage specifik, nakuaminia kama muandishi wa habari wa siku nyingi, sasa kutokuwajibika kwa nani?, chama, huyu mama ama?

    ReplyDelete
  7. amejiuzuru au amejiuzulu?

    ReplyDelete
  8. Anony wa august 18, 1: 14 umeuliza suala la maana sana, kweli Michu mwandishi wa habari wa siku nyingi unashindwa kutofautisha 'l' na 'r', unafikiri umekuja Dar es salaam leo.

    ReplyDelete
  9. Mi naona bado sana, Maregesi na huyu mama Mamuya sio uoza pekee ndani ya jembe na nyundo. Bado kuna uvundo wa kutosha sana, ukianziia na katibu wao mkuu, ni mropokaji sana na hana simile. Ila nina matumaini watazidi kusafisha jembe na nyundo, ili kiwe chama bora cha kuwakilisha hasa jembe na nyundo.

    ReplyDelete
  10. Jamani Jembe na Nyundo kuna wanafiki wa kuua. Kama ni kukosea kwenye utendaji hasa kwenye sakata la kuuza sijui kukodisha sijui ndo kuwekeza jengo la Ambassador Plaza/Gogo Hotel, mwanasheria wa Umoja huu wa wanawake wa CCM ni Mh. Jaji Sinde Warioba kama sijakosea, yeye alitoa ushauri upi wa kisheria? Maana yeye ndie aliyekuwa wa kwanza kuona mapungufu ya mkataba wa waliokuwa wapangaji wao The Kilimanjaro Band/Njenje na kuushauri umoja huo kuwatimua hawa wanamuziki waliokuwa wameanza kuwekeza kwa mkataba wamiaka 5 ili huyo bepari mwenye pesa nyingi apewe.

    Wakati hoja ya kuipiga nyundo Ambassor Plaza inawekwa hapa mwezekaji hatajwi wakati anajulikana. Michu usijidai humjui. Mimi nilikuwa nasubiria tu nani atatolewa kafara kwa hili.

    Halima sawa, ila watanzania tunahitaji maombi ya ziada maana CCM na wanafiki wake wanakoipeleka hii nchi siko!! Mambo ni mengi sana na laiti watanzania wangepata nafasi ya kuyajua kiundani, wengi wangeweza kutaka kuipindua hii takataka Jembe na Nyundo!

    Michu naomba usiibanie hii maana kuna moja ya Eddo mzee wa Richimonduli umeiweka kwapani

    adagio

    ReplyDelete
  11. anon wa 5:31:00 si useme tu,unaogopa nini? dili la ambassador/gogo hotel ni la manji aka mfadhili mkuu,kwani siri?

    ReplyDelete
  12. Anon. was August 18, 2007 5:31:00 PM EAT. Nena mwanangu nena usiogope.

    ReplyDelete
  13. POLE DADA KWA YALIYOKUKUTA, LAKINI KAMA HUO UBADHILIFU UMEFANYIKA NATUMAINI HUKUWA MWENYEWE MAANA VYAMA HUWA NA SIGNATORIES ZAIDI YA MMOJA. TAJA WENZAKO NAO WAUMBUKE PIA.

    JAMANI MADARAKA YANAHITAJI SALA LA UTAFUNGWA KAMA SIO KUUMBUKA HIVI. MSICHEKE

    ReplyDelete
  14. Lakini ni Mzuri! Utadhani binti wa miaka 27!

    ReplyDelete
  15. Mheshimiwa ISSA TUNASHUKURU KWA UJUMBE KAMA HUU “..MAMA SHIKAMOO..” HONGERA KWA KUONGOZA NA KUN’GATUKA UWT…MAMA U LOOK INTELIGENT, NA AISHII HAPO TU “..U LOOK KUTE..” HONGERA SANA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...