
HABARI ZILIZOTHIBITISHWA NI KWAMBA HADI JIONI HII JUMLA YA WATU 28 WAMEPOTEZA MAISHA YAO NA ZAIDI YA 30 NI MAHUTUTI KUFUATIA AJALI YA BASI LA ABIRIA LA SABCO LILILOKUWA LINATOKEA TUNDUMA KUELEKEA DAR KUVAANA USO-KWA-USO NA ROLI LA MCHANGA SEHEMU ZA IGURUSI, WILAYA YA MBARALI. PICHA ZINGINE BOFYA HAPA KWA MJENGWA NA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
TUOMBEE MAJERUHI WAPATE AHUENI NA MUNGU ALAZE ROHO ZA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI - AMINA


Roho za Marehemu zipumzike kwa amani.
ReplyDeleteIla nahisi tunaitaji kuweka matuta mengi iwezekanavyo kufanya hayo mabasi ya abiria(magari mengine) yaende mwendo salama kwenye ya hatari
JAMANI HII IMEZIDI YAANI HAO MADEREVA WA MABASI BONGO WAMEKUWA WABAYA ZAIDI HATA YA MAGAIDI WA KULE NAJAF AU BAGHDAD YAANI WANAKATA ROHO ZA ABIRIA KAMA VILE WANATUMIA RPG AU IED. MARA MTU KUMI, MIA KWA MWENDO HUO SI ABIRIA WA MKOANI WATAKWISHA?.............
ReplyDeletemfkasera
kc,ks
Ingekua kuna sheria ya kuwalipa fidia wote waliokua kwenye ajali hiyo, hawa watu wenye magari wangeajiri madereva wazuri.
ReplyDeleteKesho mwenye gari atarudi barabarani siku si nyingi bila kuwaza ni watu wangapi wamefariki na hao watu ni wangapi walikua wanawategemewa na familia zao. Ameshaharibu maisha ya watu kabisa. It is a shame.
Wangekua wanafilisiwa mpaka penny yao ya mwisho
Wakati mwingine wala sio madereva wanasababisha hizi ajali. Mimi ninaona ni pressure kutoka kwa maboss wao. Driver anatakiwa afike Dar kwa masaa fulani halafu labda anatakiwa afanye trip nyingine the same day. Asipofanya hivyo siku si nyingi kaji itaisha. Labda driver hajalala siku mbili.
Serikali ingetakiwa inawashika hawa wenye kumiliki haya magari ya long safari. Mmoja akifilisiwa ili hela awalipe majeruhi na waliofiwa, akitiwa jela mmoja wa hawa wenye magari au kitanzi labla watajifunza. Kwa vile hiyo haina tofauti na yule aliyechukua bunduki na kuua. Wote ni wauwaji tu.
Bro Michuzi kama nilivyosema jana, huu ni uzembe wa madereva, hawazijui saini za barabarani na serikali lazima iwajibike kuwalazimisha madereva wazijue saini za barabarani, kugongana uso kwa uso chanzo chake nikwamba hapo palikua na kona ndogo au kamlima ambako huoni anayekuja, na kwakawaida watengenezaji wa barabara hapo wamechora ule mstari ambao unakataza ku-overtake, ule mstari ambao haujakatikakatika, kiswahili sijui ni mchirizi au nini.
ReplyDeleteSi unajua kuna ile mistari inayogawanya barabara, na hio iko aina mbili, wakukatikakatika unaruhusiwa ku-overtake na ule mstari usiokatika huruhusiwi ku-overtake kutokana na situation, kona kali au sehemu yenyewe ni vigumu kuona gari linalokuja kwa mbele yako kutokana na kamlima.
Huwezi ukagongana hivi uso kwa uso na dereva anayekuja bila kuzikiuka hizo sheria.
Serikali isisitize haya masomo ya nadharia, kwani madereva wengine wakijua kuendesha tu basi wanaona kila kitu kwao ni swari.
Umewahi kumuona dereva wakibongo akasimama kwenye kivuko cha wapitanjia? [zebra]
Ni wawili kati ya maelfu wanaofanya hivyo.
Tutamalizana kwa mtindo huu tena kwa uzembe wa wachache
Tunawapa pole familia za marehemu na majeruhi katika ajali ya SABCO! Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi na kuwafariji wafiwa! Mimi bwana nilikuwa kati ya abiria ndani ya bus la SABCO nikitokea Tunduma lakini mwisho wangu ilikuwa ni mbeya!
ReplyDeleteKwa kweli mwendo ulikuwa mbaya sana maana wafanyabiashara wengi walikuwa wakihitaji wafike mapema Dar ili waiwahi mechi ya Stars v Msumbiji! Moyo ulinidunda sana hasa jinsi gari lilivyokuwa likienda lakini nilimshukuru Mungu nilishukia Mbeya salama.
Poleni sana familia ya mnenguaji wa taarab na mfundaji wali ndani ya kitchen part Shenazi na mdogo wake ambao nao walitokea Tunduma ambapo walienda kustarehe kwa raha zao, baada ya kupata offer ya ATM yao ambaye bahati yake nzuri yeye alielekea Congo hivyo marehemu hao kurudi Dar baada ya kumaliza kujivinjari! Nakumbuka vicheko vyao ndani ya White house hotel usiku kabla ya kuanza safari asubuhi yake kurudi Dar!
Tunalaani vikali uzembe wa madereva ambao hawajali sheria za barabarani na kutokuwa makini na kujisahau kuwa wamebeba binadamu ambao kuzimika ni kama mshumaa!
Inasikitisha sana kuaona maisha ya watu yanareketezwa, kwa mfano dereva amekufa sasa kesi isiishie hapo kwani kama basi alikuwa kwenye kasi sana sasa gavana ilikuwa inafanya kazi ?
ReplyDeleteKama haifanyi kazi inabidi Mwenye mali awe muhusika
Nawapa pole wote waliopatwa na mkasa huo,tunawaombea-mimi niliacha tangu mwaka jana baada ya moyo kudunda kwa msaa 8 yote nilipokuwa kwenye gari la hiyo kampuni jinsi wanavyokimbiza.
ReplyDeleteJAMANI WASOMI WA BIASHARA- KAMA SME's NI KAMPUNI ZENYE WAFANYAKAZI CHINI YA MIA INAKUWAJE HAPA DAILY NEWS LEO INATOA TANGAZO KUWA KUNA CONFERENCE KIINGILIO USD 300 NA KULA NA KULALA USD 270?HII CONFER. NI YA WATANZANIA KWELI?AU NI YA WAHINDI NA WAZUNGU?
Hayo malori kuyaweka bodi ya basi ni hatari.Wayazuie yote na anaytaka anunue basi
ReplyDeleteWahusika wa mambo yanayohusiana na ajali wamefanya nini? Namaanisha wanasiasa wanaotunga sheria, wanaosimamia utekelezaji washeria hizo na waotoa hukumu. Pengine wamejisahau, hawajui tunachotaka sisi wananchi, ni vizuri tukatafuta njia nzuri yakuwajulisha tunachokitaka. Cha kujiuliza sasa baada ya miaka mingi ya kufa, kulemazwa, na kupoteza mali, tuipeleke vipi HOJA yetu? Kwa maana namna tunapeleka hoja zetu kwa sasa haifai.
ReplyDeleteAmani