mwakilishi wa umoja wa afrika katika umoja wa mataifa mh. amina salim ali. huyu ni mwanamke mwingine wa shoka anayeiweka bongo katika ramani ya kimataifa pamoja na kina dk.rose-asha rose migiro ambaye ni naibu katibu mkuu umoja wa mataifa pia profesa anna tibaijuka bosi wa shirika la kimataifa la makazi (unhabitat) na kadhalika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. kaka Michuzi hawa akina Mama unawafagilia sana,WAMETUSAIDIA nini watz kwa nafasi zao hizo?
    Huyu mama Tibaijuka yupo hapo muda mrefu sana,lkn hajasaidia hata mtz mmoja kupata makazi bora,sana sana makamu wake mama Mugaile wa Kenya"anampiga"bao kila mwaka kwa kupeleka bajeti kubwa ya UN ya makazi barani Afrika kwao Kenya,,huyu mama Profesahana lolote kwa watz
    Mama Migiro nae hana jipya,,alikuwa waziri tz kwa miaka mingi kabla hajaondoka,,alifanya nini kwa akina mama wenzake na kama sio kw ataifa kwa ujumla?
    Mama Amina nae hana jema kwa watz,sifa yake kubwa labda alipokuwa nchini TZ hasa waziri ZNZ ni utawala wake wa mabavu na ulio na sifa ndogo ya demorasia,,alisika sana kwa uvunjaji wa haki za binadamu hasa alipolazimisha na kusimamia mwenyewe zoezi la kuwahamisha wenye maduka wote walio na ushabiki wa chama cha CUF pale darajani wavunjiwe maduka yao chini ya utawala dhalimu na wenye ukiritimba wa mzee Salmin
    Kaka Michuzi,tz ni tofuti na nchi zingine"kila mtu abebe mzigo wake"hawa watu wa JK kama waliopita hawana lolote la maana

    ReplyDelete
  2. you have Interlectual personality..your great mama amina

    ReplyDelete
  3. naona umeegemea zaidi kwa kina mama. Au wewe ni M-Beigin?
    Kuna Prof. Ibrahim Lipumba ambaye naye anapeperusha bendera ya Tz huko majuu kama mshauri wa kiuchumi kama sikosei. Nikikosea munisahihishe wadau....
    Dr. Migiro si wa kumlaumu sana. Labda Prof. Tibaijuka. Huyu ana kila sababu ya kulaumiwa kwa sababu fungu lote la mazingira liko kwake na kashindwa kujenga hoja kurekebisha makazi ya nchini kwake. Mama Amina naye angeonyesha basi huo ubaguzi wake aliokuwa nao hapa kwetu wa kiitikadi za chama akauvalisha sura ya ki nchi akaipendelea Tz.

    ReplyDelete
  4. Kwako anonymous wa September 30, 2007 10:11:00 AM EAT

    Ukweli wa comments zako ni kuuweka katika positive ndiyo maana halisi ya hawa akina mama kuitwa wanawake wa shoka unapokuja.
    Dhahiri inaonesha hawa watu wanafanyakazi bila ya kufuata upendeleo, wanafuata maadili ya kazi zao. Kama kuna mtu anataka hawa wa akina mama wafanye kazi kwa kuipendelea Tanzania tu basi wamechelewa, wamepewa dhamana ya kuitumikia jamii ya watu wote na waso watanzania.
    Sina ushahidi na huyo mama wa Kenya, lakini kama unao ushahidi dhidi ya hayo anayofanya, ninakuuliza umeshachukua hatua gani?

    (Kama hujui pa kuanzia nenda katika ofisi za habari za UN - wana ofisi hapo Dar au ingia katika tovuti ya UN)

    ReplyDelete
  5. Hivi kwa nini hao kina mama wanashindwa kuleta chapaa hapa Bongo??? Huyo Tibaijuka sijui walimdanganya nini akaenda kuwajengea watu nyumba dodoma kuondoka watu wakazibomoa na mradi nasikia umekufa.

    Halafu nasikia kuna deal aliingia na Mama Mkapa wakajenga vijumba kadhaa pale Sinza jirani na njia panda ya kuingilia Chuo Kikuu UDSM eti ndio mradi wa makazi wa Habitat??

    Jamani, kwa nini wanashindwa kuweka sera nzuri ya kuleta chapaa na kuacha maskini wakamate hizo pesa wajenge?? Au kaka vipi zijengwe nyumba kwa utaratibu unaoeleweka sio huu utaratibu wa kibongo bongo utafikiri kibopa kadondosha msaada kwa omba omba maskini

    ReplyDelete
  6. Mama Amina sio mwakilishi wa AU katika Umoja wa mataifa. Ni mwakilishi wa AU nchini Marekani makazi yake yakiwa Washington DC. Kaka Michu fanya masahihisho!!

    ReplyDelete
  7. watanzania tuache kuendekeza wanasiasa. siasa hazitaifikisha nchi hii popote pale.

    mimi kwa upande wangu nadhani wanawake wa kupigiwa nawapeni kwa uchache ni:
    Prof.Verediana MasanjaHisabati]. Prof.Mwaikambo[utabibu].
    Prof.Penina Mlama[sanaa].
    Jaji.Augusta Bubeshi[mahakama rufa]
    Dr.Chijoriga[finance]

    ReplyDelete
  8. mimi niko marekani na ni mbunge wa kuteuliwa na raisi bwana na uchaguzi ujao mtaniona.Chati hizo nitafika tu,hapa nikimaliza cheti changu cha CNA(certified nursing ass.)Nitaanza kampeni.Mnipigie kura.Nipo michigan benton harbor.269-861-6293

    ReplyDelete
  9. UISLAMU KAZI ALIPOKUWA HAPA NYUMBANI SHUNGI LILIKUWA ALIMTOKI ! SASA YUPO MAREKANI AOGOPA KUONEKANA SIASA KALI !(tafadhali michuzi usiibainie hii kwa heshima yako naomba wakilisha)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...