KUNA HABARI KWAMBA KIMBUNGA CHA TSUNAMI HUENDA KIKAIKUMBA PWANI YETU NA KUNA MAGARI YANAPITA KUTANGAZA KUWATAKA WATU WAWAHI KURUDI NYUMBANI NA KUFUNGA MILANGO NA MADIRISHA. KWA MUJIBU WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TSUNAMI HIYO HUENDA IKASABABISHWA NA MTIKISIKO MKUBWA SANA WA ARDHI ULIOTOKEA SEHEMU ZA MAGHARIBI YA KISIWA CHA SUMATRA HUKO INDONESIA NA WAMETOA TAHADHARI KWA WAKAAZI WA PWANI YA BAHARI YA HINDI KWAMBA HUENDA IKAGUSA HUKU WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA. HADI HIVI NINAVYOANDIKA HALI NI SHWARI NA WATU WANAWAHI MAJUMBANI...
habari kamili ya tetemeko huko indonesia bofya hapa BBC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu Atawanusuru WaTanzania woote na kuwaeka salama salmini katika tetemeko la ardhi. Inshallah Atawaepusha na hili Tsunami na menginewe yoote. Nawatakia kila la kheri katika ramadhani tukufu na mwenyezi mungu awaeke safe maishani. Ameen.

    ReplyDelete
  2. Mungu wangu, Tz inaviraza kweli kweli, hesabu gani wamepiga hao mpaka kufikia conclusion hii.

    ReplyDelete
  3. Wafunge milango na madirisha? Si upepo na maji yatapita katikati ya nondo (ukizingatia nyumba zetu zilivyo)!!

    ReplyDelete
  4. KWANZA NAKUSHUKURU SANA KAKA MICHUZI KWA KUTUPATIA BREAKING NEWS KWA WAKATI MWAFAKA.

    MAANA NIMETEMBELEA WEBSITE KAMA NNE ZA VYOMBO VYA HABARI VYA HAPO BONGO HAKUNA HATA MMOJA ALIYETUPA BREAKINGS NEW.

    KUBWA WADAU KILA MMOJA KWA IMANI YAKE BASI TUMWOMBE MWENYEZI MUNGU ATUEPUESHE NA KIMBUNGA HICHO KWA MAPENZI YAKE.AMINA

    PIA TUWAKUMBUKE KWENYE SALA ZETU NDUGU ZETU WA KISIWA CHA SUMATRA,INDONESIA KWA MAAFA YALIYOWAKUTA.

    WADU WASAMBAZE TAARIZA ZAIDI ZIWAFIKIE WATU MBALIMBALI.

    KWA TAADHARI PIA,WALE WANAOTUMIA USAFIRI WA KWENYE MAJI KAMA KIGAMBONI ITAKUWA VEMA WAKICHUKUA HATUA TAHADHARI NA USALAMA ZAIDI ZIZINGATIWE UKICHUKULIA VILE VIVUKO VY MV ALINA NA KIGAMBONI NI VICHAKAFU NA VIBOFU.

    ASANTENI

    MUNGU IBARIKI AFRICA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  5. Hamna lolote, Dr Mhita huwa ni mzushi huwa haqtoi taarifa za kweli.

    ReplyDelete
  6. vyombo vya hali ya hewa wala si vya kuviamini. Wameona huko indonesia wanakisia itapiga bongo. Mbona hii habari sio ya kitaalamu? Weka details tuone."TSUNAMI HIYO HUENDA IKASABABISHWA NA MTIKISIKO MKUBWA SANA WA ARDHI ULIOTOKEA SEHEMU ZA MAGHARIBI YA KISIWA CHA SUMATRA HUKO INDONESIA" Kwa hiyo wanahisi tu? Hii kitu itapiga siku ingine wala hatutakuwa tumejiandaa

    ReplyDelete
  7. TANZANIA NIWAAMBIE KITU!KWA KWELI TUNAHITAJI KUOMBA SANA YESU YU KARIBU KUCHUKUA WALIO WAKE SIKU MOJA MTANIELEWA HERI TUTUBU NA KUTENDA MEMA,HIZI NI DALILI ZA MWISHO WA DUNIA ZILIZONENWA KWENYE BIBLIA,TAFADHALI TAFADHALI NDUGUZANGUNI TUTUBU NA TUACHE DHAMBI.AMEN

    ReplyDelete
  8. Kudadadek!
    Hakukuwa na lolote. Watu tumeacha nyumba zetu Ostabei na kwenda kulala hotelini Tabata, kumbe BOSHENI.
    Kwa wale waliosoma zamani kama mimi mnakumbuka ile hadithi ya Kijana aliekuwa amezoea kupiga kelele kuwa amevamiwa na mbwa mwitu wakati akienda kutafuta kuni?
    Watu wakija kumsaidia anasema nilikuwa natania tu.
    Siku alipovamiwa kweli na kupiga kelele watu wakamu-ignoo wakisema anatania huyo tumeshamzoea. Kumbe kavamiwa kweli.
    Sasa Mamlaka ya Hali ya Hewa ndiko huko wanakotupeleka.
    Siku watakuja kutangaza kitu cha ukweli tutasema tumeshawazoea hao hamna lolote. Kumbe linapiga kweli.
    Haya!

    ReplyDelete
  9. Haya ndio matatizo ya shahada za kwenye mitandao. Kweli mtu na akili zake timamu utakimbilia nyumbani na kufunga milango na madirisha? kwikwikwikwikwi
    ukijifungia humo ndio kwamba maji hayataingia kwenye nyumba au? huu ni mtindio wa ubongo, Michuzi huyo mtu/watu wanaotangaza hii habari inabidi waelimishwe kuhusu Tsunami. Tatizo la nyumbani ni kwamba hao wanaonekana ni wataalamu hawana lolote kichwani. wanataka waitwe Dr. Prof. nk. wakati upumbavu mtupu upo kichwani.

    ReplyDelete
  10. "......The Pacific Tsunami Warning Centre originally issued a tsunami warning for wide areas of the region, saying "earthquakes of this size have the potential to generate a widespread destructive tsunami that can affect coastlines across the entire Indian Ocean basin"." Thousands of tourists and local people inhabitants were urged to evacuate coastal areas of east Africa and beaches. However, Kenya, which had warned that a "massive tsunami" was approaching, later downgraded the alert, saying that the tremor would only cause high tides along the coast.

    Before the alert was downgraded, police were sent to clear the beaches around the port city of Mombasa, while residents crowded on to buses heading away from the shore....." source: www.guardian.co.uk/kenya

    Sasa kuna tatizo gani kama na sisi Tanzania tumekuwa alerted na Dr. Mahita?????? Better safe than sorry!

    ReplyDelete
  11. Mie si niliwaambia hapo juu Tarehe September 12, 2007 11:54:00 PM EAT. Mmeamini maneno yangu sasa? Idara yetu ya hali ya hewa haina vifaa vyovyote vya kuhakikisha. Wenyewe wamesikia tu zali huko Indonesia, basi mtu akakurupuka na kusema hii itapiga hadi kwetu. Hakuna procedures zozote za kuhakikisha. Dr Mhita vipi babu?

    ReplyDelete
  12. Waosha vinywa ...haooo. msipoambiwa mnalalamika mkiambiwa mnalalamika...hata kama ingekua ni drill fanyeni siku ikija kweli weew lala nyumbani kwako ...ulifa tutakuzika...mbona drill ziko kila mahali na hamna anayelalamika? Kutoendelea tu na ufunyu wa mawazo...watu tunafanyiwa fire drill, disaster drill, huricane, tornado you name it...tunakimbia ...na tunarudi ndani bila kulalamika....hii kidogo...oh yule kijana na fisi...well...be him...utaachwa nyuma...

    Acheni kulalamika sana na uvivu...

    ReplyDelete
  13. wabongo kweli tuko nyuma kimaendeleo...mkipewa tahadhari mnasema miyeyusho...je msingepewa mngesemaje? thats the all point of what we call alerting....nendeni na wakati...tuna jihadhari na majanga...kama yanaweza kupiga nchi nyingine yatashindwa vipi tanzania? get ur facts straight...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...