haji sunday manara (shoto) akipongezwa na mhariri wa habari wa gazeti la habarileo mgaya kingoba baada ya kuchaguliwa kuwa katibu mwenezi mkoa wa dar kwenye uchaguzi mkuu wa ccm wa mkoa huo. haji ni mwanae sunday manara kompyuta na pia ni mwandishi wa habari wa siku nyingi na mchambuzi mahiri wa michezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. ....hONGERA SAANA KAKA, HUO NDIO MWANZO WA MAFANIKIO, NA JUHUDI ZAKO NDIZO ZIMEKUFIKISHA HAPO.HONGERA! ASKOFU.

    ReplyDelete
  2. Ina maana wewe Michuzi hukuwepo uwanjani siku ya Jumamosi Usiku? Mbona hatuoni picha za mchezo huo au ni kwa sababu tumeshindwa? Ndio zenu hizo waandishi kutuziba masikio kwa vifanikio vidogo lakini mkishavurunda kimya. Maana hata sasa ukisoma magazeti yote ya bongo timu sasa inaitwa Taifa Stars na siyo tena JK Boys.

    ReplyDelete
  3. Hongera Haji, toka Bunge Primary ulikuwa na juhudi kubwa. Yule mdogo wako Sakina yupo wapi?

    ReplyDelete
  4. hongera sana somjoo!!! duuu juzi juzi tuu ulikua unagombea udiwani na chama pinzani leo tena uko ccm duu kweli nimekuamia, mjuba mshikaji wako je na yeye anagombea nini au ndio bado cc? kama umenisoma hapa basi niandikie kwenyewe em2da@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. sakina ameolewa

    ReplyDelete
  6. Hongera saa Hajji,halafu wewe anoy wa 11:01 mbona upo hivyo,hii ni picha ya Haji na tunapaswa kumpongeza Hajji,habari za Sakina subiri picha ya Sakina ndio umuulize kama kaolewa acha uharibifu ebooo!

    ReplyDelete
  7. We anony unayemuulizia Sakina ingekuwa haki kama ungemuuliza na Haji kama kaoa,aukama wazazi wake wazima we unamkumbuka Sakina tu?angalia sana siku utakuja kufungishwa ndo ya mkeka.

    ReplyDelete
  8. Waosha vinywa kama kawaida yenu. Sasa mie nimemuulizia Sakina nyie mnaanza kurukia. Hamjui tumetoka wapi. ACheni mambo.

    ReplyDelete
  9. Sitakuwa kibaraka, asema Manara
    Na Ester Bulaya
    KATIBU wa Siasa, Itikati na Uenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam , Haji Manara, amesema kuwa hatakubali kuwa kibaraka wa viongozi kwa maslahi binafsi, kwa kisingizio cha kumsaidia katika kampeni za kugombea nafasi hiyo.
    Haji aliyasema hayo juzi katika ofisi za tawi la Kariakoo Kaskazini zilizopo mtaa wa Likoma, katika tafrija fupi ya kumpongeza kushinda kiti hicho.
    Alisema kuwa hatamuonea haya kiongozi yeyote wa mkoa kumueleza ukweli akienda kinyume na ilani ya Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu ya kumuunga mkono na kumpigia kampeni ili ashinde.
    Katibu Mwenezi huyo wa Mkoa, alisema kuwa anaamini kuwa viongozi hao wa mkoa wa Dar es Salaam walijitolea kumfanyia kampeni, kwa sababu wanajua uwezo wake na wana imani kuwa anaweza kushika nafasi hiyo.
    "Wakati wananifanyia kampeni, baadhi ya viongozi wa Dar es Salaam, niliwaambia kwamba mnifanyie kampeni kwa kuwa mnajua uwezo wangu, lakini si kwa sababu mnataka nipate nafasi hii ili niwe kibaraka wenu, hilo sitakubaliana nalo, bali nitafanya kazi kwa maslahi ya Chama", Alisisitza.
    Alisema kuwa atahakikisha kila mwanachama wa CCM anapata haki yake bila ubaguzi na bila kujali ngazi yake ya uongozi.
    Aliwashukuru wanachama wa tawi la Kariakoo kwa kutambua mchango wake akiwa mjumbe wa halmashauri ya tawi hilo.
    Alisema kuwa yeye ni mtumishi kwao na wao ni mabosi, hivyo wana kila sababu ya kumuagiza kufanya shughuli za Chama.
    Nao wanachama wa tawi hilo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kata Selemani Katto, wamemtaka Haji kutosahau alikotoka, na kusimamia kwa kina utaratibu wa kuchagua mgombea bora na si mwenye uwezo wa kifedha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...