
wanakijiji tuliwakilishwa vyema na kaka maggid mjengwa na mshairi mrisho mpoto ambaye wakati wa kufungua champeni ya dafu alighani shairi kusifia mnazi na pia utamu wa boga ambalo da'mija na mai hazbendi wake walikata kama keki ama ndafu, mwafrika merinyo (shoto) ndiye aliytekuwa mpambe wa bwana harusi wakati mai waifu wake ailinda sawe 'mama afrika sana' alikuwa wa da'mija
.jpg)
mdau na mwanamke wa shoka mija shiya sayi majuzi alifunga pingu za maisha na wa ubani wake wa muda mrefu david manju ambaye ni mmoja wa wabunifu mitindo ya mavazi ya kiafrika mashuhuri nchini naambaye aliwahi kuwa na roots and kulture ya jah kimbute miaka hiyooo. harusi hiyo iliyofana sana ilikuwa ni ya kipekee kwani ililenga mila za kiafrika kwa maharusi na wahudhuriaji kufanya mambo ya kuutukuza uafrika wetu kwa nguvu zote. picha zifuatazo zitamalizia maelezo. ikumbukwe da'mija ni mmoja wa wanawake wa shoka wanaoendeleza libeneke la kublogu na pia ni kiongozi wa jumuiya ya wanabloga
.jpg)
siku ya sendiofu da'mija na matroni wake ailinda sawe wa afrika sana walitoka namna hii

maharusi wakiingia ukumbi wa stesheni ya tazara katika mavazi yaliyobuniwa na kutengenezwa na wao wenyewe
.jpg)
limo la maharusi lilipambwa na kupambika
sasa mbona wametumia macho panzi? Si wangetumia Punda? Huo ndio ulikuwa usafiri halisi wa mwafrika. Wameharibu hapo
ReplyDeleteHata mimi ndio nashangaa ilitakiwa watumie Punda au Mkokoteni kuendeleza theme ya harusi ambayo ilikuwa ni Utamaduni wa Kiafrika. Huu Mcede umeharibu kabisa theme ya harusi.
ReplyDeleteMimi pia nashangaa.
ReplyDeleteKama walishindwa kabisa kupata GARI lililotengenezwa kwa MABUA, basi walau hata wangepanda gari aina ya NYUMBU ambalo linatengenezwa hapahapa nchini, kule Kibaha.
Wamependaza sana na wazo lao la kuonesha uafrika nimefurahia ila kwa suala la usafari mimi nashauri Bwana Michuzi hebu waulize walinyimwa na watu wa usalama barabarani kutumia punda au farasi? Tusiwalaumu kwanza safi sana kwa ubunifu nimewakubali
ReplyDeletenaomba niulize walifungia kanisa gani?km kanisani Merinyo uliingia na rasta???kama wapapenda dumisha asili si wangeenda makumbusho kufanya sherehe yao...kenge mtu wakubwa..na hooney moon mkalishane maboga yenu na tana mtandike shuka jeupe ole wenu muweke nyanya au randi
ReplyDeleteMi kwa kweli nashindwa kuwaelewa wabongo kwa ulimbukeni hatujambo. hebu tuelezane uafrica maana yake ni kuonyesha mazingira ya dhiki? Usafiri uwe punda, mkokoteni au gari la mabua? Kwanza muelewe hayo mambo ya punda na mikokoteni hata wazungu walikuwanayo hatukuanza sisi. Mi hii concept ya vitu duni vya asili kwamba ndio u-Africa naikataa kabisa. Hii itakuwa ni inferioriy complex. Kuelezea uAfrica katika karne ya 21 kwa kutumia vitu vya karne mi siikubali hata kidogo. Kwani Africa haina haki ya kuonyesha vitu vya kisasa? hii concept kwamba kila kitu kizuri cha kisasa ni kinyume na U-Africa kinadumaza mawazo yetu kwamba sisi sio wa kuendelea. Hatupotezi uafrika kwa kuwa na mambo ya kisasa, hata wazungu walitoka huko mnakosema ni u-Afrika. Nani kawaambi maboga asili yake ni Africa au yanapatikana Africa tu?
ReplyDeleteKunywa dafu badala ya champagne ni U-Africa? Mbona hata hiyo concept ya kuwa na champagne wakati Harusi siyo ya kwetu?