
picha hii ilipigwa julai 5, 2006 kwenye maonesho ya sabasaba ambapo afande mwamunyange alikuwa akisalimiana na mh. dk asha-rose migiro wakati huo akiwa waziri wa mambo ya nje na afande mwamnyange ndio kwanza kachaguliwa kuu mnadhimu mkuu jeshini
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth

picha hii ilipigwa julai 5, 2006 kwenye maonesho ya sabasaba ambapo afande mwamunyange alikuwa akisalimiana na mh. dk asha-rose migiro wakati huo akiwa waziri wa mambo ya nje na afande mwamnyange ndio kwanza kachaguliwa kuu mnadhimu mkuu jeshini
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ule utamaduni uliozoeleka/uliojengeka wa Wakuu wa Majeshi kutoka Mkoa wa Mara naona JK sasa ameuvunja.
ReplyDeleteSijui itakuwaje! Tusubirini.
Kwani Twalipo alitokea Mara????Sarakikya alitokea Mara???
ReplyDeleteWewe anonymous wa hapo inaonyesha huna kumbukumbu nzuri kwani wametoka sehemu mbali mbali za Tanzania ILA mkoa wa MARA ndio wametoka wengi. Sasa nakupangia kama walivyokuwa hapo kabla ila kunradhi wadau kama nitakosea: 1. General Sarakikya (Arusha), 2. General Twalipo (Mtwara/Lindi), 3. General Musuguri (Mara), 4. General kialo (Mara), 5. General Mboma (Mbeya), 6. General Waitara (Mara), na 7. General Mwamunyange (Mbeya). Hivyo 3 toka Mara, 2 toka Mbeya na 1 toka Arusha na Mtwara/Lindi. Nadhani umenipata hivyo sio kweli kuwa WOTE walitokea MARA kama UNAVYODAI !!!!!!!!!
ReplyDeleteKumbukumbu zangu zinaonyesha july 2006 mheshimiwa alikuwa hajateuliwa kushika wadhifa huo wa UN.UMEGONGA HAPO REKEBISHA MZEE
ReplyDeleteMichuzi sahihisha- Migiro aliteuliwa UN january, 2007.hiyo picha ni ya july, 2006 akiwa bado waziri.
ReplyDeleteJenerali aliyestaafu Waitara kama taarifa za Gazeti la Tanzania Leo ni kweli basi huyo Generali ni anashangaza.
ReplyDeleteHotuba yake imenukuliwa hapa:
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/9/14/habari1.php
Na pia habari hiyo iko katika Gazeti la Tanzania Daima leo Tarehe 14 sep 2007 TOLEO NA.1015
Habari hiyo inasema Hivi:
"Naye Safina Tibanyendera, anaripoti kuwa aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama anayemaliza muda wake, Jenerali George Waitara, amepiga marufuku imani ya dini ya kilokole ndani ya jeshi hilo, kwa madai kuwa ulokole unaweza kumtoa mtu katika taratibu za kijeshi.
Waitara alisema hayo jana wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam na kuwataka maofisa wa jeshi hilo wanaojiona wameokoka kwenda makanisani kuliko kuendelea kuwa wanajeshi.
“Tusiingize ulokole kwenye jeshi…imani ni imani, kiongozi akiwa mlokole na wafuasi walokole itakuwaje? Tukianza kusema huyu hastahili kufanya kazi hii kwa sababu ni mlokole, hapo tutakuwa tunaleta migawanyiko, na mtu wa namna hiyo anayeleta ulokole kwenye jeshi, kazi itamshinda,” alisisitiza Waitara.
Hivi hao walokole jeshini walimfanya nini Waitara hadi awapige marufuku? Ni kitu gani kilichoko katika kazi za kawaida za jeshi walimkatalia kufanya hadi atoe kauli nzito kama hizo?
Ieleweke kuwa walokole wapo dunia nzima majeshini. JWTZ si la kwanza kuwa nao na tena wana vyeo Vikubwa kuliko Waitara na watu wanawaamini kivita.
Hivi huyo Generali hajawahi hata kupelekwa kozi ya haki za Binadamu ya siku moja?
Na kama Generali, hivi utawala hajasomea hata kozi ya wiki moja kujua statement ipi aisemee wapi?Hivi na ujenerali wote hajui wapi hatakiwi aseme nini.
Kama ni kweli habari hizo Kaliaibisha jeshi na majenerali wa Tanzania mbele ya umma.
Kama habari hizo ni kweli Ni vizuri anapoondoka asilipake matope jeshi lionekane jeshi lisiloheshimu haki za binadamu.Ni vizuri akaondoka salama kimya kimya.
Kama ana matatizo na walokole angemalizana nao huko huko kijeshi.Ziko mahakama za kijeshi n.k
Pia kama anaona hawafai jeshini na wamevunja taratibu za kazi ziko kanuni na taratibu za ajira angetumia hizo badala ya kukurupuka na kuropoka mbele za waandishi wa habari.
Ukianza mambo ya kuongelea ukabila ni sawa na kula nyama ya binadamu ......... mbona Gen. Robert Mboma aliyekuwa Mkuu wa Majeshi (1994 - 2001) alikuwa anatokea mkoa wa Mbeya? Gen. Abdallar Twalipo je naye ni mnyakyusa?
ReplyDeleteMura!
ReplyDeleteSasa jesi rimeansa tena kutangatanga rinasahau nyumbani! Rimeondoka tena poti (Mara) na kwenda mbeya? Huyu jemedari anasahau kuwa JWTZ maana yake ni Jesi ra Wakurya Tangu S(z)amani?
Mkuu wa Majeshi mstaafu kama kasema dini ya walokole haitakiwi jeshini kakosea.Katika Military Science dini ni zote ni muhimu sana labda kasahau alisoma zamani.
ReplyDeleteKuwa na watu wa dini tofauti ni muhimu kwenye military intelligence, katika mbinu za kivita na vita zenyewe.Ndio maana Jeshi la marekani lina dini karibu zote .Nchi nyingi ambazo majeshi yao hayana watu wengi wa dini tofauti nyingi huwa rahisi sana kupigwa.
Hata intelligence haiwezi fanya vizuri kama una watu wa dini moja,wenye mtizamo mmoja na wanaoongozwa na fikra za aina moja.Sababu dini hujenga kuaminiana.Mfano ukiwa na waislamu wanaosali msikiti mmoja ukawapa assignment ukataka mmoja asimamie mwingine, yule BOSS uwezekano wa kupata taarifa sahihi ni mdogo sababu huyo mwingine hata akileta taarifa ya uongo anayesimamia aweza mwamini kisa ni Islamu mwenzie wanayesali msikiti mmoja hawezi kudanganya! Dini inakuwa kigezo cha kuamini mtu badala ya utendaji kitu ambacho ni hatari kijeshi! Sasa ili upate taarifa za intelligence sahihi unachanganya watu wa dini tofauti kwenye assignment na nafasi nyeti.
Hata mapinduzi na hujuma za kijeshi ndani ya jeshi au nje huwa ngumu ukiweka watu tofauti kidini kwenye nafasi za juu au nyeti kuliko ukiweka wa aina moja.Ukiweka watu wa aina moja feedback ya intelligence toka chini toka maeneo mengine inakufa.Matokeo yake juu hakupati taarifa sahihi zilizohakikiwa na watu wengine wa tofauti hivyo hupati refined information.
Anyway labda Waitara yeye anajua vita unatumia silaha tu hajui kutumia dini kama war tool.Vita za kisasa siyo tu mtutu wa bunduki peke yake ni combination ya vitu vingi.Dini nazo zimo na zinatumiwa tena sana negatively au positively katika vita.Na kuzitumia kwa ufanisi unahitaji nyingi na usirundike watu wa dini moja kwenye nafasi nyeti au za juu wengi unahitaji mchanganyiko for check and balances na kuhakikisha utendaji kijeshi ni wa ufanisi mkubwa.
Kwa ushauri wangu Nadhani hatakiwi kufuta dini ya ulokole bali kama anaona kuna walokole hawafuati taratibu za jeshi awashughulike kama wahalifu wa kawaida wa jeshi asiuadhibu ulokole au dini ya kilokole.Taratibu za jeshi zinaeleweka.Mfano jeshi halina ijumaa,jumamosi wala jumapili sababu kijeshi vita inaweza shuka siku yoyote kwa hiyo mtu kwenda kazini ijumaa kama ni muisllamu,jumamosi kama ni msabato,na jumapili kama ni mkristo ni kitu cha kawaida jeshini