Penati yavunja mechi ya Simba, Yanga Marekani

Na Mobhare Matinyi, Washington DC

Penati iliyotolewa kwa ‘Yanga’ na mwamuzi Lucas Mkami ‘DJ Luke’ kunako dakika ya 89 ya mchezo, ilisababisha kuvunjika kwa pambano kali jana Jumapili baada ya wachezaji wa ‘Simba’ kuigomea na kutoka uwanjani huku matokeo yakiwa 3-3.

Mwamuzi Lucas ambaye kwa kawaida ndiye kocha wa timu wa mashabiki wa Yanga mjini hapa, alilazimika kutoa penalti hiyo baada ya mshambuliaji hatari wa Yanga, Abdallah Maqubel, kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki wa Simba mwenye misuli, Ray Abraham. Hiyo ilikuwa penalti ya pili kugomewa na Simba baada ya ile ya kipindi cha kwanza.

Wachezaji wa Simba wakiongozwa na kipa wao, Saleh Londa ‘Mstahiki Meya’, walilalamikia kwa madai kuwa mshambualiaji wa Yanga alipiga chini na kuumia baada ya kubanwa na beki wao. Wachezaji wa Yanga wakati huo walimbeba mwenzao kumtoa nje na wote kuwahi maji kabla ya kurejea kumpongeza mwamuzi.

Zogo hilo lilidumu kwa dakika takriban kumi na ndipo kocha wa Simba, Santa Chacha ‘Popadic’ alipoamua kuitoa timu uwanjani huku baadhi ya wachezaji wake wakiongozwa na Vincent Ndusilo, wakiwa tayari wameshavua jezi na kuvamia nyama zilizokuwa zikichomwa uwanjani hapo.

“Huwezi kutoa penalti kwenye mechi ya Simba na Yanga dakika ya 90 ya mchezo,” alidai kipa wa Simba, Londa ambaye dakika kumi kabla ya penalti hiyo alionesha umahiri wa ajabu alipookoa mkwaju wa kichwa uliopigwa na Hussein kufuatia kona. Awali Londa aliyekuwa kikwazo kwa Yanga, aliokoa shuti baada ya Maqubel kubaki naye uso kwa uso kwenye dakika ya 18.

Simba ilianza kwa kufunga bao la kustua kwenye dakika ya kwanza kupitia kwa Shabaan Ramadhani ambaye pia aliisawazishia Simba bao la tatu kwenye dakika ya 84. Bao la pili lilifungwa na kiungo machahari Liberatus Mwang’ombe kwenye dakika ya 34.

Yanga walisawazisha bao la kwanza kwenye dakika ya 15 lililofungwa na Hussein Ibrahim. Dakika ya 38 Maqubel aliyeinyanyasa ngome ya Simba alipachika bao la pili na kuongeza la tatu kwenye dakika ya 58.

Ukiondoa dosari hiyo ya penalti kulalamikiwa, mchezo huo ulikuwa mkali hasa kufuatia kila timu kuwa na mchezaji wa kiwango cha kimataifa na uwanja kufurika mashabiki waliokuwa katika sherehe za kumaliza majira ya joto, huku karibu nusu yao wakiwa akina dada warembo.

Ili kuidhibiti Simba, Yanga ilimuagiza kocha wake Lucas, kumuita mshambuliaji Maqubel kutoka Reading, Uingereza. Habari ambazo hazijathibitishwa zinadai mshambuliaji huyo Mtanzania anatarajiwa kwenda Sweden kucheza soka la kulipwa hivi karibuni.

Simba ilimtumia kiungo hatari Elvis Mnyamuru ‘Doto’ ambaye itakumbukwa kwamba alikuwa mmoja wa wachezaji walioitwa na kocha Maxime kuunda kikosi cha Taifa Stars kabla ya kwenda safai ya Brazil. Hata hiivyo, Doto ambaye amewahi kuichezea Twiga ya Dare s Salaam na timu ya daraja la kwanza Botswana, alirejea Marekani kwa sababu za kikazi kabla ya mchujo wa kwenda Brazil.

Timu katika mchezo huo uliohudhuriwa na Mtanzania mcheza basketi nyota hapa Marekani, Hashim “Tall”, zilikuwa:
SIMBA: Saleh Londa, Raymond Abraham, Naumu Chahe, Evans Shangarai, Adam, Elvis Mnyamuru, Rashid Beach-Boy, Liberatus Mwang’ombe, Shabaan Ramadhani, Kendo, Vincent Ndusilo.
YANGA: Dadi Rouba, Tiffa, Victor, David, Yahaya, Abdallah, Richard, Hussein, Dickson, Maqubel na Danny Kiondo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. saleh londa nae kipa ? siasa vipi hawezi ? au ndio hafuati nyayo za baba yake ?

    ReplyDelete
  2. OMBI

    Tuwekee picha za harusi ya DAMIJA iliyofanyika jumamosi tarehe 01 Septemba 2007.

    Mdau

    ReplyDelete
  3. Wenye ngoma wako wengi. ndio huyu ben anayo pia. na pesa zake ni za msimu. mara anachacha, mara anainuka ndio ivyo.

    ReplyDelete
  4. Tunaomba picha za harusi ya da mija.

    ReplyDelete
  5. Breaking newsssssssssss!

    Miss India 2007, Oooops, Miss Tanzania 2007, ameamua kulivua taji hilo na kukabidhi gari na pesa kwa kamati ya Miss Tanzania, kutokana na kile lichodai "Nafsi yeke binafsi kumsuta"! Hakuweza kufafanua zaidi alimaanisha nini kwa kauli hiyo!

    Hii ni habari mpya kabisa, hata bro Misoup hana!

    Maelezo mengine yatafuata baadae!

    Stay tuned!

    Choko choko!

    ReplyDelete
  6. YANGA SASA MMEZIDI!!! Yaani mechi kati ya mashabiki huku ughaibuni mnataka kubebwe!

    YANGA na mashabiki wake ni aibu tu!!

    ReplyDelete
  7. kuna kijana wangu hapo BEACH-BOY kama kawa aliweza kudhihirisha kwamba SIMBA ni balaa ingawa yanga kama kawaida yao wanataka kubebwa tu kila siku...
    BEACH BOY ebu nichecki kuhusu ile ishu ya AZIZI ili nijue imefikia wapa na tufanye nini
    kasera, hapa
    KC,KS

    ReplyDelete
  8. Hizi nyuzi mbona hazisemi Simba walimchezesha yule mwanamama kutoka Philly? au Yanga wanaona aibu wameshindwa kufunga midume mitupu.......

    ReplyDelete
  9. dANNY kIONDO YUPI HUYO? MPIRA KACHEZA WAPI MTOTO WA GOROFANI?

    ReplyDelete
  10. Wadau wa washington DC naomba msaada wenu kunifikishia ujumbe huu kwa ndugu yangu Ndusilo tuliyepoteana tangu akiwa high school. Anaweza kunipata kwenye 978 223 0074. Nitashukuru sana kwa msaada huo. Natanguliza shukurani nyingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...