
Kutoka kulia wa kwanza ni Rivaldo umri miaka 17 wa timu ya Benfica ya ureno ambae ni mwenye asili ya Kitanzania,akiwa katika mazoezi ya timu ya Msumbiji juzi akijitayarisha kuja Dar Tayari kukabiliana na Taifa lake la asili Tanzania.
hii ni mara ya kwanza kwa Rivaldo kutua Dar,alizaliwa mji wa Nampula na kukulia huko akiwa na wazazi wake ambao wote ni kutoka Tanzania. Rivaldo ni mchezaji pekee wa timu ya Mambas ambae anaweza kuongea Kiswahili (sio safi sana) pamoja na lugha yake ya kireno.
kabla ya kutua ktk klabu ya Benfica Rivaldo alikuwa ktk majaribio ya miezi kadhaa ktk klabu ya Manchester United ya England, ambao alifuzu vizuri ktk majaribio yake lakini hakuweza kupata Kibali cha kumfayia kazi hapo England, kwa hiyo ndipo alipohamia ktk timu ya Benfica mwaka jana.
Tunaomba TFF kuanzia sasa iamke na kujenga Stars yenye sura mpya,TFF kwa kushirikiana na wadau popole walipo duniani tushirikiane ili vifaa vyetu kama akina Rivaldo vije kuimarisha Soka yetu ya Tanzania kama nchi nyingi zinavyofanya duniani.
Hii ni kweli! Tanzania huwa hatuthamini wachezaji wetu mpaka tusikie wanachezea timu kubwa. Kusema kweli kuna vijana wengi wa kitanzania ambao nina uhakika wanacheza mpira nje lakini wanakatishwa sana tamaa na utaratibu unaowekwa na TFF. Nakumbuka siku kadhaa nyuma Tenga alishawahi kutamka kuwa Watanzania wote wanaocheza nje ni "wababaishaji" kasoro Matola tu. Yes ofcourse unawaita wababaishaji kwa kuwa hawajapata deal kubwa kama Matola?? Tukumbuke nchi za wenzetu zinaokoteza wachezaji wao hao hao wabaingaizaji huko Ulaya na USA na kuwaweka katika systeam kabla hata hawajafika timu kubwa na kuwapa muongozo ulio bora. Na ni hao hao ndio wanakuja wakiwa na nchi zao na kutufunga kila siku. Ushauri wa bure kwa TFF ni kwamba kuanzia leo waanzishe database ambayo itakuwa inafuatilia maendeleo ya vipaji vya kitanzania abroad. Hii itatufanya tuwe na azina kubwa ya wachezaji hapo baadae. Pili watanzania wenyewe tubadilike na tuache majungu. Kuna tukio liliwahi kutokea siku si nyingi pale Mchezaji wa kitanzania anayeishi DC Washington alipoitwa katika kikosi cha Maximo. Magazeti, Redio na Wananchi walichachamaa kumtolea mimacho kijana wa watu utadhani mwizi. Ukweli ni kwamba mchezaji anayecheza daraja la pili au la tatu au hata PDL au labda tuseme Amature league nje nadhani anaubora zaidi ya mchezaji wa Kagera Sugar au Lipuli ukitazama kiundani zaidi kwani wenzetu huku wana facilities zote zinazotakiwa, lishe bora nk. Leo umtoe Mwaikimba vumbini ukamchezeshe Taifa Stars na ndo yale tunayoyaona kila siku mtu anakimbia hadi analipita goli!!
ReplyDeleteWakina Rivaldo tuko wengi na ukweli ni kwamba deal zikitokea watu wanakula urahia hata wa Malawi kwani nini. Ni bora uitwe shujaa ugenini kuliko kuitwa mbabaishaji nyumbani.!! Najua midomo mirefu mtachonga lakini ukweli mnauona. Tuombe huyo Rivaldo aisitufunge maana uchungu wake utakuwa ni sawa na wa mama tena wa kiafrika kutukanwa na mtotoe!!
Angalieni Rivaldo mwingine huyu tunampoteza!!
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=mQCzGYBfpow
Huyo dogo jina lake kamili ni Daúde Massude. Nimekuwa nikimfuatilia muda kidogo ila sikujua kama ni m-bongo. Aliibuliwa na Carlos Quiroz, kocha msaidizi wa Manchester United, wakati wa mechi za vijana huko Musa-Mbiki mwaka 2005.
ReplyDeleteLakini sikuwahi kujua kama ni mtanzania.Manchester 'wamemuweka' Benfica ili 'akishaiva' wamchukue kamili.Lakini mbona sisi watanzania tunaacha 'mali' zetu hizo zipotee hivyo? Tumekazana kuwafutia watu uraia (Said Maulid, Jenerali Ulimwengu, n.k) wakati wenzetu wanabeba tu wachezaji wetu.
Kuna mtanzania mwingine alikuwa ancheza huku UK miaka ya 90 mwishoni/katikati ila aliandikwa kama South African na akawa naomba asaidiwe aupate utanzania 'wake' ila sijui hiyo habari ikaenda vipi. Pia kuna dogo, akiitwa Pallangyo nadhani,(alikuwa na miaka 17)alikuja UK miaka kama 4 hivi iliyopita akafanya majaribio na klabu za UK ila 'wakasema' abadili uraia ndio apewe kibali cha kazi.Sijui nini kimeendelea.
Pia Kally Ongala nae tumemkosa tayari.Siwezi kusahau jinsi alivyokuwa ameisaidia Yanga ktk Kagame Cup ya mwaka 1999.Nasikia kuna dogo mwingine wa kizenji 'anasoma' ktk academy ya Arsenal.Ni kweli?
Nilikuwa mpinzani sana wa sheria ya dual citizenship ila sasa nasikia roho inaniuma kumuona Daude Massude (Rivaldo) akiwa anachezea Musa-Mbiki. Tubadilike wajameni!
tanzanianboy@gmail.com
Tanzanians are so full of claiming one famous person as theirs, yet are so futile in applauding the whole issue of nationalism and patriotism. The laws states that ones place of birth determines his/her nationality. For that reason, this young kid is legally a Mozambican despite having Tanzanian parents. I don't see any point of priding here!
ReplyDeleteHata kama kutakuwa na wachezaji wenye vipaji waliozaliwa nje ya nchi au waliohamia nchi za nje, itakuwa ni vigumu kuweza kuchezea Taifa Stars kwa kuwa dual Citizenship hairuhusiwi Tanzania.
ReplyDeleteWapo wengi wa namna hiyo huku !wengine ma DR, wengine ma Engineers ,wengine wanasiasa (Obama wa Kenya ) tunawazaa katika mihangaiko yetu ya maisha.
ReplyDeleteDual citizenship itawasaidiea kuwajenga uzalendo na in return watasaidia nchi zao za asili
Mr Dar
Anon. Sep 6, 5:38, and u r? Ungependa tujivunie nini? Hizo sheria ulizozigusia za wapi? Kama mie nimezaliwa Uingereza mie, Mwingereza pia?
ReplyDeleteMie Mtanzania, Babao
We anony wa 5:38am, we are not discussing the issue of miss Patel here. Hapa tunaongelea maswala ya soka la Bongo. Usitake kutuchanganya na kiingereza chako hiki uonekane unajua sana mambo. Issue ya uraia na maswala ya miss Patel yameisha, hamna nyimbo. Waswahili wanasema 'Funika kombe mwanaharamu apite', we can not cry over spilt milk. Tanzania go, go go go go!! Tanzania gooo.....
ReplyDeleteAnon wa 5:38:00,
ReplyDeleteSheria gani hiyo inayosema place of birth ndiyo inadetermine nationality ya mtu? Kwa Tanzania mtu anaweza kuwa raia either kwa:kuzaliwa na wazazi/mzazi mtanzania au kuomba+kuandikishwa.
Kwa msingi huo 'Rivaldo' alikuwa mtanzania hadi alivyoamua kuukana uraia wetu.Kama haujui sheria za uhamiaji za TZ zikoje bora unyamaze tu.
Huyu dogo mpaka alipofikia sasa anaweza kabisa kuichezea Tanzania na kama kweli TFF wako tayari kumfatilia na kama tukipita kwenda kukipiga Ghana basi huo utakuwa mwanya wa wazi kabisa kuweza kumshawishi ili abadili uraia na kuweza kukipigia JK11, sijaona ugumu wowote wa yeye kubadili uraia na kuwa mtanzania kama bado atakuwa anatumia passport ya Mch(s)umbiji,sababu ameshajenga jina lake tayari kule benfica sababu tumeona wachezaji wengi tu wametuma maombi yao FIFA na kukubaliwa bila kipingamizi sababu huyu dogo wazazi wake wote ni watanzania NO! PROBLEM kazi kwenu TFF kumlaghai huyu dogo abadili mawazo.
ReplyDeleteKwani Shaban Nonda alichezea burundi na sasa anachezea RDC kwajili ya mama yake, EASY!
TFF kaza buti mtuletee mtoto huyo
nadhani kubwa kwa sasa na kwa vile viongozi wa sasa wanapenda michezo ni kushawishi sheria ya double natioanality ifanye kazi. ni kweli kwamba inakuwa shida sana kupata kazi au hata timu ukiwa siyo raia wa hiyo nchi. mpaka uwe mchezaji mkubwa sana ndo inakuwa rahisi. kweli hatupati wachezaji wa nje kwa vile tayari wana uraia wa nje na kwa hiyo tayari walishaukana uraia wa tanzania. nadhani tuanze na hilo
ReplyDeleteIt's me again anonymous of Sep.6-5:38. The issue of nationality and patriotism has always been touching to me, especially when it's Africans are concerned. Let me ask everyone of you just simple question: "I'm a Tanzanian. My wife in White American. My son was born in USA. Is he American or Tanzanian? And why? explain.
ReplyDeleteOn the issue of this young kid Rivaldo. I think he is a Mozambican, legally speaking by laws of birth--Jus soli. Kama ni law naijui vizuri sana ndugu, nimekwenda shule kwenye mambo ya laws. There is always a feeling of happiness when we say someone is Tanzanian because his/her parents or one of them is Tanzanian. Just like it's to the beautiful lady Miriam Chemoss. There is a tag of war between Kenyans and Tanzanians, each claiming to own Miriam. In reality, she considers herself Kenyan, and i support her if she was born there. Thanks.
Kwa uelewa wangu, mtu akiwa na umri chini ya miaka 21 kwa mujibu wa FIFA anaweza kuchezea timu yoyote aipendayo haijarishi mzaliwa wa wapi na nchi gani anataka kuchezea. Kwa upande wa Tanzania mtu chini ya miaka 18 anaweza kuwa na uraia wa nchi hata 3 i.e kuzaliwa TZ, uraia wa baba pamoja na uraia wa mama. Hvy hy dogo bado anaweza kucheza TZ akiamua kwa kuzingatia sheria za FIFA, kwa upande wa TZ bado anasifa za kuitwa raia.
ReplyDeletehuyo anon sept 6,5;38 ni yule fala wa kihindi RajPatel wa tanzatl.org analeta upuuzi wake wa kibaguzi.Mnaona mliokuwa mnamfagilia yule kidampa aliyekuwa miss Tanzania wa kuchovya?Deep inside hawatuoni kama sisi ni watu kama wao.
ReplyDeleteAnon sep 6. 5:38. Napenda kukujibu swali lako. Kwanza kuhusu swala la mtoto wako ni kwamba akifikisha miaka 18 anauwezo wa kuchagua urahia autakao which I believe atachagua wa USA. Kama tungekuwa na dual citizenship then angekuwa na uwezo wa kuwa rahia wa nchi zote mbili. Kwa kuzingatia Rivaldo ndio kwanza ana miaka 17 basi hata ajafikia umri wa kuamua nchi gani achezee. Sasa ana uwezo wa kuchezea nchi yeyote ( TZ or MOZ)mpaka hapo atakapo fika miaka 18. Kwa hiyo TFF bado wana nafasi ya kumshawishi aweze kuuukana urahia wa MOzambique pindi afiakiapo 18 hapo mwakani. Napenda kukupa mfano halisi: kuna mchezaji wa Ivory Coast ambaye alikuwa katika kikosi cha World Cup na sasa anachezea nchi ya Wazazi wake Ghana baada ya wa Ivory kutomwita katika Qualify.
ReplyDeleteWEWE RAJPATEL TUNAFAHAMU MAWAZO YAKO, NA TUNASHUKURU KWA KUZIDI KUCHANGIA KAMA UNAVYOIFANYIA NCHI YETU.
ReplyDelete