
wadau mlikuwa bize sana na taifa staaz kiasi cha kusahau kwamba jana ilikuwa ni siku ya elimu ya kimataifa ambayo maadhimisho yake yalienda sambamba na kuhitimisha wiki ya tamasha la vitabu pale karimjee ambapo watoto wa shule mbalimbali walikusanyika kwa shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na kujisomea, kupigiana hadithi na kadhalika

Bw. michuzi naomba nikusahihishe. Hii siyo siku ya elimu(education) bali ni siku ya ujuzi wa kusoma na kuandika(literacy) ambayo ni sehemu ya elimu lakini sio elimu per se kama inavyojidhihirisha kwenye bango hapo juu.
ReplyDeleteWadau wengine mnasemaje?
TPC, labda tuongezee kuhesabu pia ISOMEKE Siku ya Ujuzi wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
ReplyDeleteKwa muda mrefu tafsiri yake sahihi imetumika kama Siku ya Kisomo Duniani.
Kisomo kina maana ya kusoma, kuandika na kuhesabu.
nyongeza za maoni ya chacha...hii ni siku ya kufuta ujingwa kwa kuhamasisha kampeni za kujua kusoma na kuandika.
ReplyDeletewewe anon, hapo juu kwani kusoma na kuandika vinatofautianaje na elimu, au elimu hasa ni nini au kitu gani,Je wenye elimu hawahitaji kusoma na kuandika.
ReplyDelete