champeni ya dafu inanywewa na maharusi

wanameremetaaa...wanameremetaaaaa manju na da'mija jama, wanameremeeeetaaaaaa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Brother Michuzi hili tukio limenivutia sana. kwa kiasi kikubwa limebeba asili yetu Afrika. Haya mambo kumbe yana namna ya kuyaweka sawa kwa asili yetu tu. Ukoloni umetujaa vichwani mpaka tunaamini kuwa wanayoyafanya akina Bush, Brown n.k. ndiyo ya kistaarabu.

    Aaah, hii imetulia bwana. Boga, Dafu!!.

    Umaskini na uvivu wa kufikiri tu ndo umetufanya tuvitose hivi vitu. Hongereni sana Maharusi. Kwa mtazamo wangu, imebamba ile mbaya. Mpaka kipande hiki cha mwaka, ya kwenu ndo kali jamani.

    From: The Serengeti Of Flowers (SOF)

    ReplyDelete
  2. Aisee hii harusi mimi naifagilia WA WA! sio mchezo hawa jamaa wapiga bao kwani harusi yao babu kubwa wamewashinda wanaotumia mamilioni ktk harusi zao nawatakia kila la kheri muishi maisha mema mzae. mjukuu na vitukuu vyenu mje mvione inshallah,

    ReplyDelete
  3. Absolutely A++ Beautiful wedding - Hope to see more creative people mixing both African Culture with some modern touch here and there. Well done!!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Da minja kwa kufanya harusi nzuri. Ila kuna jambo hapa moja ambalo kwa kweli mimi nimeona ni bora nitoe maoni yangu. Alichofanya Da Minja hapa ni moja kwa moja 'translation' ya Western wedding style katika kile ambacho yeye anasema ni Kiafriaka,hii ni sawa na kusema katumia product nyingine kwa kuendeleza desturi za kizungu. Je wapi katika makabila yetu huwa wanakata boga kama keki ya Harusi? hii ni kuchanganya mambo kabisa wala si u-afrika au u-Tanzania. Katika mila za kiafrika kila jambo huwa lina maana yake, inawezekana kabisa kuna makabila ya kitanzania ambayo hukata boga au titi maji kama ishara furani ya yenye maana kwao. makabila mengine huvunja chungu kuonyesha kwamba ndoa hii haitavunjika mpaka hiki chungu kiunganishwe.wengine huruka fagio na mengine mengi ya kiasili yenye utamaduni wa kiafrika na siyo Da-minja alichofanya,yeye kafaya 'pure copyright' ya western style kwa kutumia product nyingine, Madafu kama champane na keki kama boga. Huku ni kuchanganyikiwa. Halafu katika mila hasa za kiafrika ulisha ona wapi bibi harusi ana cheza siku ya harusi yake? semeni ukweli ! Mwanamke wa kiafrika huwa mwenye aibu na heshima sana na siku ya harusi yake huwa macho yake yako chini kuonyesha heshima ya kiafrika na "reservation" ya u-anamke wa kiafrika-Mwanamke wa kiafrika hawezi kuchekelea anapoolewa hata kama kitendo hicho kitakuwa kimemfurahisha kiasi gani bado ataonekana mwenye aibu na ataficha uso wake. sasa swali ni kwamba hiyo harusi ya Da-Minja ilifuata mila zipi za kiafrika au kabila gani la kitanzania? je kukata boga au titi maji kuna maana gani ya kiafrika au katika kabila gani hapa nyumbani hufanya hivyo? Mimi naona Da minja just an 'Intertainer' na kaleta kitu cha kushangaza na kuburudisha tu wala si uafrika au utanzania. Namtakia maisha ya furaha katika ndoa yake na mume wake na wapate watoto kama mchanga wa bahari na miungu yote wa mababu wa kale waje wamsimamie.
    Ndaga fijo
    Joune Nyakyusa.

    ReplyDelete
  5. This is the best wedding ever. I love this. Watu wabunifu kama hawa ndo wanatakikana katika jamii zetu. nawapongeze mno maharusi hawa. wametia fora, hasa unapounyambulisha utamaduni unaopatikana ndani ya watanzania hadi hatua nyingine ya modernity.
    Well done

    ReplyDelete
  6. Waw! hongereni saana maarusi, kwakweli nimefurahishwa na maandalizi yenu! By the way David, you have proved to be the true African, tangu Mwenge, Roots & Culture and Now! Ningependa sana nipate makala ya kitabu chenu cha mitindo, kama kipo tutumieni mahali kinapopatikana.
    CONGRATULATIONS!!

    ReplyDelete
  7. HII NDIYO SAAAAAFIIIIIIIII! HONGERA SAAAAANA DA MINJA, MAMBO YA SHUGA HAKUNA HAPA WADAU SI MNAONA VITU HIVYOOO!

    ReplyDelete
  8. Wewe Anon: September 11, 2007 8:16:00 PM EAT


    Lengo la maharusi hawa sio kufanya harusi ya kiafrika ila ni kutumia vitu vya kiafrika kufanya harusi inayokwenda na wakati wa sasa naomba hilo uliewe. Wao lengo lao ni kuonesha kuwa tuna vitu vya kiafrika vinavyoweza kutumika na kufanikisha harusi au sherehe zetu kama mtu utapenda sio lazima. Unaweza kuendelea na mavazi ya kigeni na champgne, keki n.k.

    Kama ulishaoa pole mie nimeshapata wazo la wed langu hapo

    ReplyDelete
  9. Naam tukiendelea kwa mtindo huu nadhani waTanzania tutakuwa watu wa kuigwa (trend-setters) na sio wa kuiga vya wenzetu (trend followers). Hongera maharusi for this historic event.

    ReplyDelete
  10. Hongera Da Mija na David Manju,
    Mmependeza sana, tena sana tu.

    Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu hiyo harusi siyo ya Kiafrika au Kitanzania per se, bali ni tasfiri ya harusi za kimagharibi ambapo mmefanikiwa vizuri kujumuisha vitu mbadala.

    Halafu hiyo ya kwenda kanisani vipi tena, hakuna mmbadala unaozingatia uafrika/utanzania?

    Uzuri pia ni kwamba gharama inakuwa nafuu sana huna haja ya kuchangisha dunia nzima... kweli nyie wajasiliamali, nimewakubali!

    Sijui kama wengine mmeona jinsi wageni waalikwa walivyoduwaa, wanaochekelea na kufurahia naona ni maharusi na wapambe wao.

    ReplyDelete
  11. wow!!!!!!...jamani this is lovily...hongera saana da DAMIJA....KWANZA KWA KUDUMISHA MILA ILE NYENGINE ILISHINDWA!!!...MMEPENDEZA WENYEWE NA NAWATAKIWA HERI NA FANAKA KATIKA MAISHA YA NDOA......IYO ILIKUWA LAZIMA INOGE VICHWA VYA MADESGNER....ATLIST NIMEPATA IDEA YA AFRICAN WEDDING FASHION....

    ReplyDelete
  12. Nyakyusa uko right kuwa ni copyright ya western weddings!! Lakini kumbuka haya... uigaji umeanza long time ago yaani since ukoloni ..ila kilichowashinda wengi ni kuiga kwa kutumia african products.. kitu ambacho maharusi hawa wamepiga bao!! Haya ndio mambo yanayotakiwa wanaruhusiwa kuweka vionjo vyote vya kiwestern lakini kwa kutumia malighafi za kiafrika. Kwa mtazamo wangu wamekosea kidogo tuu katika usafiri wa maharusi.. wangeweza kutumia farasi au something like that..na labda sio limo... keep up guyz.

    Issue ingine ni gharama nina uhakika watu wangeiga mwelekeo huu wangeweza kuokoa hela nyingi na kufanyia mambo mengine muhimu zaidi katika kuendeleza maisha yao.

    ReplyDelete
  13. Hongera sana sana tena sana David!Wewe toka zamani unafanya vitu vya uhakika!!Keep it up!
    Wewe, mkeo pamoja na wasimamizi wote mmependeza.
    Hongera pia kwa kufanya harusi ya kiTanzania ya kisasa.
    Sioni kwa nini tuige harusi za ughaibuni, za matajiri wa ughaibuni,kwa kuchangisha watu wengi baadaye tunajisifia kuwa ilikuwa bonge la harusi!!!Bonge la harusi kwa gharama za wengine?Wenzetu wanafanya harusi kufuatana na uwezo wao.
    Vinginevyo tufanye 'Bottle Wedding Party' kila mtu aje na maakuli yake....
    Hongera sana Manju and by the way jaribu kuonekana zaidi ktk maonyesho,wewe unatakiwa uwakilishe zaidi Bongo ktk Fashion shows.Style zako ni unique.Uko wapi kaka yetu?All the best.

    ReplyDelete
  14. Ok!mimi nimekubali kwamba da minja amefanikiwa kutumia vitu vyetu vya asili badala ya kutumia vitu vya kizungu. Lakini wadau katika mila za kiafrika kila kitu kina maana yake,sasa swali kukata boga badala ya keki maana yake ni nini? je Madafu maana yake ni nini- sababu katika uzungu champagne hutumika kama kupongezana, keki ni Ishara ya upendo( unajua tena utamu wa keki 'wilkinson'-hapa michuzi atasema nimetukana hahaha!).Sasa da minja naomba unisaidie hili swali,kukata boga ni ishara ya nini na katika mila za kabila gani Tanzania? na kunywa madafu ni ishara ya nini na inatoka katika kabila gani hapa au nchi gani ya kiafrika? sisi huku ughaibuni tuna penda sana kueleza mambo yetu na wazungu wanapenda sana kujua mila zetu natumaini kama nitatoa maelezo mazuri yata nisaidia na watu wengine wata penda sana kufuata. Bado nina kueshimu kwa kuwa mwanzilishi wa hii "kitu imeshinda watu wengi kufuata" na nitakutumia ku panga harusi yangu iwe ya kiafrika 100% wala si 'blending' ya kizungu na kiafrika.
    Nakutakia furaha tele na Mizimu ya mababu ije ikutemee mate ya baraka na upate watoto kama mchanga wa pwani( ada ya shule usiulize mizimu hahaha! ).
    Ndaga fijo,
    Nyakyusa washington
    (michuzi nitakuwa Canada kwa wiki mbili nasikia unakuja canada mjomba?)

    ReplyDelete
  15. Huyu bwana mwenye ndevu zenye mvi alikua anasubiri nini mpaka sasa anaamua kuoa? au ndio baba mtu?
    Kama sie baba mtu, nitajiuliza maswali na makwesheni!
    Hata hivyo hatusi imependeza kushinda zote tulizoona hapa. Big Up Hata mimi nitafanya hivyo, nimeshaiga.

    ReplyDelete
  16. DAVID NA DA MIJA NI BINADAMU KAMA BINADAMU WENGINE. KWA MTAZAMO WANGU, WAO WAMEJARIBU KUIELEZA JAMII KUWA KUNA NJIA MBADALA YA KUWEZA KUFANYA HAYA MASUALA YANAYOHUSIANA NA SHEREHE 'ZETU'.
    SIDHANI KAMA KULIKUWA NA 'SCRIPT' ILIYOTOKA KABLA YA SHEREHE YAO TUNAYOWEZA KIJADILI KUWA WAMEKOSEA HAPA AU PALE.
    KILICHOPO NI KUWA NJIA TUMEIONA KWA HIYO WENGINE WANAWEZA KUFANYA ZAIDI YA WAO NA HATIMAYE KUFIKIA KULE WADAU AMBAKO WADAU WENGI MAWAZO YAO YANAKOLENGA.
    HII NI SAFARI NDEFU SIYO YA WAO TU, BALI NI WATU WOTE.
    MAARASI NAWAPONGEZA KWA UBUNIFU WENU NA NJIA MLIYOIFUNGUA.

    KUHUSU KUFANYA HARUSI KWA KUZINGATIA MILA HASA, NADHANI HAPA TUTAKWAMA MAHALI FULANI KWANI MIINGILIANO YA WATU KUTOKA KABILA MOJA HADI JINGI LITAFANYA HILO KUWA KIKWAZO, KWA MFANO MCHAGA NA MNYAKYUSA, SASA UNATAKA KUSEMA HARUSI IFANYIKE KWA TARATIBU ZA WAPI?

    ReplyDelete
  17. Mambo si ndo hayo! Safi sana!

    Tupende utamaduni wetu!

    ReplyDelete
  18. Duh!!! Briliiantttttt!!!! very brilliant kabisa!!!!

    beautifullll mno!!

    hongera sana mwanamke wa shoka DA MIJA kwa arusi nzuri sijapata kuona....Africa is beautiful bwana......

    Nawatakieni maisha marefu na yenye amani, wewe mwenyewe binafsi, Mume wako na hata Watoto Mungu atakaomjalieni......

    Michuzi, hizi ziende pia katika haya magazeti ya mjini, ili wengi zaidi wajifunze kupenda asili...

    je kanisani walikwenda lakini??

    mark msaki

    ReplyDelete
  19. Asemavyo Bw.Msaki ni sawa;picha za harusi ya kaka Manju na Bi.Mija ziwekwe magazetini jamani,wanastahili kuonwa na wabongo wote.
    Wamafungua njia ambayo labda wengi walikuwa hawaioni.
    Hongera sana tena sana.
    By the way hao wazungu wanaotaka kujua maana ya desturi zetu ni wa wapi?Maana muItaliano hataki kujua mambo yetu!

    ReplyDelete
  20. Acheni uharibifu wa mazingira nyie, hiyo migomba mmeitoa wapi...! Watu wanapanda Vyakula nyie mnaenda kutumia ovyo ovyo...! Ole wenu kukatokea njaa mwaka huu.

    ReplyDelete
  21. Swali langu kwa maharusi , jee hivi ndivyo wanavyoishi au ilikuwa kwa ajili ya harusi tuu . Namaanisha ya kuwa nikienda kwao leo hii watanipa maji kwenye kibuyu kama wanavyopotray hapo .

    Kama jibu ni hapana , then the all idea was just a wastage of time

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...