msome mh. zitto kabwe kwenye http://www.bongocelebrity.com/ pamoja na mengi ya miss tz 2007

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. endeleeni kuwakosesha appetite hawa watu...we need people like you brother...angalau tupige makelele tuu!...alafu usijisahau kula kamanda you are loosing weight au sijui macho yangu?...BIG UP!!!...

    ReplyDelete
  2. duuu! Zitto kakaaa upo?

    Pole na majukumu na maswaiba kaka.

    Ene wei tutafika tu ndugu yangu!

    ReplyDelete
  3. Vipi Mh. Bado unaunguruma? Lakini umepima afya? usijeuka@#%&*& hapa halafu iwe taabu....

    ReplyDelete
  4. CCM sasa yanuka rushwa

    na Mwandishi Wetu

    MWENENDO wa mambo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) sasa unaonekana kwenda kombo na unaonyesha kila dalili kwa chama hicho kutumbukia shimo katika kashfa mbaya ya rushwa.

    CCM imeingia katika kashfa kubwa ya wanachama na viongozi wake kukumbwa na tuhuma za rushwa na ubadhirifu wa mali za chama licha ya viongozi wake wakuu kutokubaliana na ukweli huu.

    Wachunguzi wa mambo, sasa wanaonyesha wasiwasi mkubwa wa kuporomoka kwa hadhi ya chama hicho huku kikitoa nafasi kwa kambi ya upinzani kuanza kujiimarisha.

    Matukio ya hivi karibuni ya kukamatwa kwa wabunge wawili wa chama hicho na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Arusha wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho yamekipaka matope na kuzipa nguvu hoja za wanasiasa wa kambi ya upinzani kuwa ushindi wa chama hicho hupatikana kwa rushwa.

    Ingawa Kamati ya Maadili ya CCM imeonyesha kukerwa na tuhuma zinazowakabili wabunge hao pamoja na viongozi wengine na kupendekeza wasiruhusiwe kugombea uongozi, kauli ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba, kwamba uchaguzi huo ulikuwa safi inazidi kutoa ujumbe kuwa bado kuna viongozi ndani ya chama hicho wanaoficha tatizo linalokitafuna chama chao.

    Kauli ya Makamba inatofautiana na malalamiko ya wanachama wake wengi kuhusu kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

    Malalamiko ya kuwepo kwa mchezo mchafu katika chaguzi mbalimbali za chama hicho sasa si geni, lakini linaonekana kuvuta hisia za wengi baada ya wanachama wake kuanza kunaswa wakihusishwa na rushwa.

    Mbali na rushwa katika uchaguzi, tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma zinazowaandama baadhi ya makada wa chama hicho ambao wana nyadhifa kubwa serikalini, nazo zinakoleza sifa mbaya ya chama hicho.

    Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni mmoja wa watu wanaotajwa kuiweka CCM katika hali mbaya ya kutoaminiwa na wananchi kwa kuhusishwa kwake na kusaini mkataba wa mgodi wa Buzwagi kinyume cha taratibu.

    Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa hatua hii ni matokeo ya kuwepo kwa makundi ndani ya chama ambapo kila kundi sasa linapambana dhidi ya kundi jingine, huku wanamtandao wakiendelea kuwa na sifa ya juu ya kuchafua wanachama wasio wanamtandao.

    Jambo jingine linalotajwa kukichafua chama hicho ni utitiri wa ndugu wa viongozi wakuu kujitumbukiza katika siasa na kunyakua baadhi ya nafasi nyeti katika chama.

    Ingawa ndani ya Bunge kuna wabunge kadhaa wa chama hicho ambao ni wanandoa huku wengine wakiwa na nyadhifa kubwa serikalini, ndani ya chama hilo linaonekana kuwa doa linalokigeuza chama hicho kuonekana kama cha familia zaidi.

    Hatua ya mke ya Rais, Salma Kikwete kugombea nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wilayani Lindi huku mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete na ndugu mwingine wa Rais, Yusuph Kikwete kuchaguliwa kuwakilisha Wilaya ya Bagamoyo, kunaacha maswali mengi.

    Ingawa si jambo baya kwa ndugu wa viongozi wakuu wa nchi kuwa wanasiasa, historia ya chama hicho inaonyesha kuwa hakijawahi kuwa na mwenyekiti ambaye mkewe na mtoto wake ni wajumbe wa vikao vya mkutano mkuu wa taifa, wakiwa na uwakilishi wa sehemu fulani ya nchi.

    Mbali na familia ya Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, mke wa Katibu Mkuu wa chama, naye amechaguliwa kuwa mjumbe wa NEC - Taifa hivyo anashiriki moja kwa moja katika maamuzi makubwa ya chama hicho.

    Vita ya kuwania madaraka miongoni mwa wananchama wa chama hicho inayoendelea sasa katika mikoa ya Mbeya na Mara, ni ishara ya chama hicho kupoteza mwelekeo.

    ReplyDelete
  5. Zitto huchoki tu acha kutafta umaarufu wa burebure fanya vitu watu wavione sio uzushi na kuropoka vitu ambavyo huwezi kuvithibitisha kama kweli unajua kilichomo kwenye mkataba toa basi huo mkataba watu wauone kijana vipi taaratibuuuuuu muhaa yatakushinda. jifunze kupangilia pointi na kufanya uchunguzi wa kina kabla hujasema mbele za watu hata kama una haki ya kuyongea kikatiba ila zingatia utaratibu wa kuongea, zingatia mahali, kitu, na uzito wa jambo lenyewe kabla hujaosha kinywa chako au na wewe muosha kinywa? anyway nimekusoma kijana unataka umaarufu wa fastafasta ila utakukosti mtu wangu kuwa mpore fuata taratibu na kanuni zilizopo. Nakupenda zitto ila hapo umeniboa unatoa kauli nzito kumbe huna ushahidi unawachokoza makada wa CC.........eeeeh utaumia! punguza kuchonga ngenga Muha wewe ubishi na malumbano sio sifa wala ujanja. Michuzi huyo mdogo wako vipi hebu mpe somo.

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaa kafumbua mengi sana, sasa hebu someni wenyewe on this link ni kiasi gani Tanzania itapata endapo mafuta yatagunduliwa(endapo!!!! ya right, why trying anyway) what will 10% do to the nation?????
    http://www.statoil.com/STATOILCOM/SVG00990.nsf?OpenDatabase&lang=en

    ReplyDelete
  7. Sorry wadau, here is the whole story. You can go to the STATOIL and click search, then type Tanzania and you will see the topic.thanks

    Awarded exploration acreage in Tanzania

    Statoil has signed a production sharing agreement (PSA) today, 18 April, for deep water Block 2 off Tanzania in the Indian Ocean. This is the first time Statoil has been awarded exploration acreage in Tanzania.



    Block 2 is located off Tanzania in the Indian Ocean.
    (Illustration: Venche Mellemstrand)

    The PSA was signed in the capital of Tanzania, Dodoma, between Statoil, the government of the United Republic of Tanzania and the Tanzanian Petroleum Development Corporation (TPDC). Statoil is operator of the block. If a commercial discovery is made, TPDC has the right to participate in joint operations with a 10% participating interest.

    "We are very pleased by today’s signing and are looking forward to start exploring for oil and gas in an area we see as very interesting," says Bill Maloney, senior vice president for global exploration (GEX) in International Exploration & Production.

    Block 2 covers an area of 11,099 square kilometres and has water depths up to 3,000 metres. The area has no previous exploration and is considered to be frontier.

    The work programme comprises of 5,800 kilometres of 2D seismic and an optional 3D in the initial four-year exploration period.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...