BURIANI MAMA SALOME JOSEPH MBATIA AMBAYE MCHANA HUU UMELAZWA KWENYE NYUMBA YAKO YA MILELE HUKO MOSHI. INGAWA KIMWEILI UMETUTOKA LAKINI UTABAKI NASI KIROHO DAIMA. MUNGU ALAZE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI - AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Huyu mama alikuwa mzuri sana du haya ulale salama.u know i always picture myself kaka michuzi imagine watu mlizoe kuhamka asubuhi mnamuona mama nyumbani akiwa anajiandaa kwenda kazini na kelele zake za asubuhi kama kawaida za mama wa kiafrika halafu ghafla kimya au partner ile routen yenu ya kila siku mmehamka mnaharakisha kwenda kazini kila kitu jukumu la mke sasa wewe ndio uanze ku run family it is so hard anyway poleni sana wadodgo zetu na matatizo yaliyowapa

    ReplyDelete
  2. jamani mama wa watu sijaona picha yake ambayo ameacha kuchela mungu wasaidie familia yake kipindi hiki.

    ReplyDelete
  3. kaka Michuzi kabla ya kuto maelezo ni bora ukasoma mwenyewe kwanza maana hii michumsho yako inazidimmkila siku ila najua na majukumu mengi pole sana

    ReplyDelete
  4. Michu!
    Hii ndio ile picha ambayo Mama Mbatia alikuomba umsafishie ukauchuna mpaka ametangulia mbele ya haki?? itabidi nakala uipeleke kwenye kaburi lake,,,ahadi ni deni mithupu

    ReplyDelete
  5. We Anony (Saturday, October 27, 2007 4:20:00 PM EAT) Hivi umeona kwanza ulichokiandika au ulikimbilia kuangalia michuzi wapi amekosea kutype na kuanza kulalamika while we mwenyewe umeandika mambo ya ajabu?
    Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndio utoe kwenye jicho la mwenzako.

    Rest in peace mama Salome Mbatia.

    ReplyDelete
  6. KWELI KIZURI HAKIDUMU.

    ReplyDelete
  7. BWANA MICHZI NACHUKUA FURSA HII KUKUPONGEZA KWA UNAVOJITOLEA KUTUFIKISHIA HABARI MUHIMU ZA YANAYOJIRI NCHINI KWETU TANZANIA. BILA KUKUFICHA NAFIKIRI TUKIO HILI NI MOJA YA MENGI AMBAYO YANAONYESHA JINSI GANI UMEIVA KATIKA FANI YA UPASHAJI HABARI. NASEMA HAYA YOTE KWA KUWA UMETUMIA BUSARA NA ETHICS KU-COVER TUKIO HILI BILA YA KUIUMIZA ZAIDI FAMILIA YA MAREHEMU. KUNA BAADHI YA BLOG ZA WATU MAARUFU KAMA CHEMI Che MPONDA AMBAO WAMEBANDIKA PICHA ZINAZOONYESHA MAREHEMU AKIWA AMEBANWA NA WANABLOG WAKIULIZA WAPI ETHICS ZA UHANDISHI WA HABARI ZIMEPOTELEA HAKUNA MAJIBU BALI MATUSI. NINA UHAKIKA UNGETAKA UNGEWEZA KUWEKA PICHA KAMA HIYO LAKINI UMETUMIA UBINAADAMU ULIO NAO KUCHUJA NI ZIPI ZA KUBANDIKA BILA KUONDOA MAUDHUI YA HABARI..HONGERA SANA BWANA MICHUZI MWENYEZI MUNGU ATAKUJALIA KWA YALE YOTE UNAYOYAOMBA..MEANWHILE MUNGU AILAZE MAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMEN

    ReplyDelete
  8. Jamani na wale wengine waliokufa kwa ajali tumewakumbukaje? Au kwavile huyu alikuwa waziri wenzake kwenye msiba huo hawatajwi na wao watazikwa kama mbwa? Mhhh...Jamani Serikali angalieni hizo barabara acheni kula mahela maana zitawamaliza ninyi wenyewe mnaokula hayo mahela...!!Sasa faida iko wapi? Barabara zisipowamaliza ninyi zitawamaliza watoto wenu...wapi na wapi? Poleni wafiwa...mimi zangu zaidi kwa yule Otingo na Dereva wa Mama Salome...nao si watu jamani?

    ReplyDelete
  9. OFF TOPIC

    Lakini kwa wadau wa ukeketaji mnaweza kujifunza hapa -
    http://www.sfgate.com/cgi-bin/article.cgi?f=/n/a/2007/10/25/national/a093521D06.DTL&type=bondage

    Wakati sis huku tunatumia a negative label (FGM = Female Genital Mutilation) wenzetu wanaita "piercing" ambayo connotation yake ni kitu stylish japokuwa madhara ni yale yale.

    Talking about double standards? Ni lini tutaamka???

    ReplyDelete
  10. KWANZA NAWAPA POLE SANA WANA FAMILIA WOTE ! INAHUZUNISHA KWA KILA MTU KWA KUONDOKEWA NA MAMA HUYU TENA YAONYESHA ALIKUWA ANA DALILI ZA UADILIFU UKIZINGATIA ALIKUWA KWENYE KAMPENI ZAKE ZA KICHAMA NA AKAWA AMEKODI GARI BINAFSI ! NI WACHACHE KATI YA VIONGOZI WETU WANATHUBUTU HIVYO ! ZAIDI TWASEMA BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA ! R I P

    Mzushi

    ReplyDelete
  11. Sunday, October 28, 2007 12:20:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous NAKUSHUKURU SANA KWA KUGUNDUA MAPUNGUFU YA CHEMI CHEMPONDA KWENYE BLOG YAKE. KWELI PICHA ZAKE HAZINA MATIKI KABISAAAAAA! LABDA AKITOA PICHA ZA WAZAZI WAKE MAAANA ANAPENDA SANA KUJIDAI NAO KILA MARA KAMA VILE AKINA MICHUZI HAWANA WAZAZI. UKIMTOLEA MAONI ANAJIDAI KUPANDISHA YAANI HATAKI KUSHAURIWA KABISA LABDA USHAURI WA RAFIKIE MICHUZI TU. UKITAKA KUTHIBITISHA HAYO ANGALIA IDADI YA COMENTS KWENYE BLOG YAKE INADHIHIRISHA WATEMBELEAJI NI WACHACHE SANA.

    ReplyDelete
  12. Bwana alitoa na sasa ametwaa jina la bwana libarikiwe, jamani inaumiza sana hasa kwa familia yake watoto na mumewe walizoea kusikia sauti yake mara kwa mara kama alivyosema anony. fulani hapo juu ni kweli kabisa mama ndiye muwajibikaji mkuu katika familia lakini kazi ya mungu haina makosa.
    Pia kaka michuzi jitaidi uwape familia yake hizo picha zake ulizonazo maana ahadi ni deni.
    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU SALOME MBATIA MAHALI PEM PEPONI-AMINA.

    ReplyDelete
  13. Kwanza poleni kwa msiba familia ya Marehemu. Lakini hii ni moja tu kati ya maelfu ya ajali za barabarani zinazotokea nchini Tanzania kila mwaka bila kuchukuliwa hatua zozote za kukomesha ajali hizo. Tunapata habari za wachache tu wanaokufa kati yao kama bibi huyu ambao ni wakubwa au ambao huripotiwa. Suala la vifo vinavyotokana na ajali za barabarani linabidi lidhibitiwe na serikali ili kukomesha mauaji hayo holela. Inashangaza serikali kukalia kimya suala hili, na watu pia kuelekea kulizoea..jamani watanzania amkeni..ajali za barabarani zinaweza kuepushwa na kupunguza vifo vya holela..tuzingatie kuendesha magari kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, kutokulewa na kuendesha na pia baada ya kutumia mihadarati..ni bora kuchelewa kuliko kutokufika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...